Mazoezi makali yaongezea umri?

Image caption Kunyanya uzito

Wewe ni mkimbiaji au muinua vyuma? Wakimbia katika mbio za masafa marefu au katika mashindano ya michezo mitatu tofauti - triathlon?

Ni mazoezi yapi ambayo unaweza kufanya ikiwa unataka kujiongezea umri? Je, ni vyema zaidi kufanya mazoezi mafupi na makali, au marefu zaidi lakini ya taratibu?

Kwa mujibu wa Daktari Jamie Timmons, Profesa wa masomo ya bayologia ya uzee katika Chuo Kikuu cha Birmingham, dakika tatu za mazoezi makali kila juma kwa majuma manne kunaweza kukaboresha, kwa kiwango kikubwa, afya ya mtu.

Mazoezi haya makali yanaweza kusaidia moyo na mapafu yako kusambaza hewa mwilini vyema zaidi.

Pia yanaboresha ifanyavyokazi insulini, ambayo inaondoa sukari mwilini na kudhibiti mafuta.

Image caption Mtu akinyananyua uzito kama sehemu ya mazoezi

Nao utafiti wa Daktari Stuart Gray wa Chuo Kikuu cha Aberdeen unadhihirisha kwamba mazoezi makali na mafupi, kama kukimbia kwa kasi kwa masafa mafupi, au kuendesha baiskeli kwa sekunde 30 tu, kunaufanya mwili uondoe mafuta kutoka kwenye damu haraka zaidi kuliko kufanya mazoezi ya wastani, kama kutembea harakaharaka.

Kuondolewa kwa mafuta kutoka kwenye damu ni muhimu kwa vile kunapunguza uwezekano wa kukumbwa na tukio la mshtuko wa moyo.

Alisema Bwana Alwyn Cosgrove, “Kufanya utafiti wa namna hii ni ili kujaribu ushauriwatu kuwa na afya nzuri hata mpaka uzeenii.”

"Labda nikiweza kuboresha maisha yangu kila siku kwa kula lishe bora, kwa kufanya mazoezi na kuujenga mwili wangu, basi labda nitaweza kujiongezea miaka."