Sema Kenya Msimu wa Pili

Image caption Msimulizi, watayarishi na baadhi ya walioshiriki katika mjadala mmoja.

Kipindi cha Sema Kenya sasa kipo kwenye msimu wa pili.

Hiki ni kipindi cha mjadala na ambacho hupeperushwa kupitia redio, televisheni na kwenye tovuti.

Kipindi hiki kinazuru maeneo tofauti ya nchi, lengo likiwa ni kuwapa wananchi fursa ya kuelezea hoja zao, kupata taarifa na kushiriki katika mjadala wa kitaifa.

Tangu kilipozinduliwa mwaka jana, Kipindi cha Sema Kenya kimefaulu kuandaa mijadala mikali iliojumuisha wananchi ikiangazia masuala ya usalama, mihadarati, ukabila, ugatuzi, ugavi wa ardhi na marekebisho ya sheria za ugavi wa ardhi.

Watu wanaweza kushiriki katika mazungumzo haya ya kitaifa kupitia tovuti ya BBC, mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.

Aidha, njia nyingine Sema Kenya inawafikia wananchi ni kupitia mashirika ya kijamii ambayo kipindi hiki kinashirikiana nao.

Mtindo wa Sema Kenya:

• Lugha: Sema Kenya inaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili.

• Utafiti: Sema Kenya inategemea utafiti wa kina kufanikisha makala haya.

• Wanaoshiriki: Kinahusisha watu wa tabaka mbalimbali; vijana kwa wazee, wanawake na wawakilishi wa vikundi maalum.

• Huwaleta pamoja wananchi na viongozi wao: Wananchi wa kawaida na jamii zilizotengwa wanapata fursa ya kuwahoji viongozi wao.

• Mada ya mjadala huamuliwa na washiriki katika kipindi hiki.

• Haibagui, haipendelei na inashirikisha kila moja kupitia redio na kwenye tovuti.

• Mjadala huendelea kwenye mtandao wakati kipindi kikiwa hewani hata baada ya kutia tamati kwenye redio.

Sikiliza na ushiriki kwa Sema Kenya

Televisheni: KBC kila Jumapili saa kumi na mbili jioni

Redio: Idhaa ya Dunia ya BBC (Nairobi 93.9FM, Mombasa 88.1FM) kila Jumapili saa saba alasiri.

Mtandao: bbcswahili.com/semakenya

Facebook: BBCSemaKenya

Twitter: @bbcsemakenya

Sema Kenya ... Jukwaa la Wakenya.