Mhariri wa Sema Kenya anasema...

Image caption Wanyama Chebusiri, Mhariri wa Sema Kenya

Kipindi chako maarufu, BBC Sema Kenya kimeshika kasi! Kinatamba kote nchini Kenya kuwapa fursa wananchi wa kawaida na viongozi wao kujadili uajibikaji na maendeleo.

Kaunti ya Pokot Magharibi inasifa zinazo kata mbele, nyuma na pia katikati- utajiri wa mila, kiangazi cha kupindukia na wizi wa mifugo. Kwa hivyo, wiki jana tulikuwa katika kaunti ya Pokot Magahribi karibu na mpaka wa Kenya na Uganda, ambako tulijadili kwa kiina athari za utamaduni katika ustawi wa eneo hilo.

Ukeketaji wa wasichana bado ni tatizo kubwa licha ya juhudi mahsusi zinazoedelezwa kwa ushirikiano wa serikali, kanisa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Kwa kauli moja, gavana, seneta pamoja na viongozi wengine waliahidi kujitolea kwao kuimarisha vita dhidi ya tohara ya wasichana na kutokomeza utamaduni huo kutoka kaunti ya Pokot Magharibi.

Jumapili hii tunarudi jijini Nairobi kupiga darubini swala linalozungmziwa sana nchini kenya kwa sasa-ONGEZEKO LA USHURU WA THAMANI. Wengi, hasa walala hoi wanalalamika vikali kwamba ongezeko hilo limesababisha bei ya bidhaa muhimu kwenda juu na hivyo kufanya gharama ya maisha kuwa ghali mno. Kwa upande wake, serikali inatetea hatua hiyo ikisema hela zinazotokana na ongezeko hilo zitafadhili miradi ya maendeleo bila kutegemea misaada kutoka nje.

Sasa je, ni yapi maoni yako kuhusu swala hili?

Wanyama wa Chebusiri,

Mhariri, BBC Sema Kenya