Polisi wa Kenya lawamani baada ya shambulizi la Westgate

Shambulio katika maduka ya Westgate jijini Nairobi mnamo mwezi wa September limezusha mivutano nchini Kenya na sasa idara za usalama za Kenya ambazo hufadhiliwa na serikali za Uingereza na Marekani zinashtumiwa kwa kuwauwa washukiwa wenye misimamo mikali,kwa mujibu wa makala haya ya mwaandishi wa BBC Gabriel Gatehouse.

Kiunga ndio mpaka wa mwisho wa Kenya na Somalia na Superintendent Samuel Obara anakabiliwa na mojawapo wa kazi ngumu kabisa katika jeshi la polisi.

"Hata al-Shabab sasa wanatoroka kutoka Somalia na wanajaribu kujipenyeza nchini Kenya," anasema akiwa amesimama katika eneo linalozitenganisha nchi hizo mbili katika mwambao wa bahari ya Hindi.

"Tumeamua kuwafyeka. Tunakutafuta,tunakuchapa risasi mbele ya familia yako na huanzia na viongozi "

Ilipoamua kuivamia Somalia miaka miwili iliyopita ,Kenya iliwaandama wapiganaji wa al-Shabab, kundi la Waislamu wenye msimamo mkali lenye fungamano na al-Qaeda, na ambalo bado linadhibiti eneo kubwa la kusini mwa Somalia.

Uvamizi huo ulitazamiwa kuhakikisha usalama wa Kenya. Na kwa kiwango fulani imekua hivyo. Bw Obara anaonyesha maeneo ya kwa maeneo ya mwambao na vichaka ambavyo askari wake walipiga doria siku zilizopita na ambazo zilikua zikishambuliwa.

Lakini anakiri kwamba kikosi chake hakina silaha wala askari wa kutosha.

"mpaka huu unavuja na nina hakika watu hujipenyeza bila kugunduliwa. "

Na kwa kweli hili ndilo eneo ambalo maafisa wa usalama wanaamini watu wanne wanaoshukiwa kuhusika na shambulio la maduka ya Westgate mjini Nairobi walijipenyeza kuvuka mpaka wa Kenya.

Maelezo mengi kuhusu shambulio hilo bado ni kitendawili. Lakini taswira inayojiokeza ni operesheni ya usalama iliyokwenda kombo na jeshi la polisi la Kenya likiwa linalofadhiliwa na nchi za Magharibi likiwa hamkani likiwaaandama wale wanaoshukiwa kua ni tisho.

Siku yenyewe ya shambulio la Westgate ilikua vurugu tupu. Vikosi vya usalama vilichukua dakika 90 kuwasili katika eneo hilo ambapo watu 67 walipoteza maisha yao walikua wamekwishauliwa.

Lakini ilipofika alaasiri ilielekea kama askari wa kikosi cha GSU, walikuwa wamewishawaelemea washambuliaji katika sehemu ya nyuma ya majengo ya Wetgate.

Mpaka jeshi lilipowasili . Hapo ndipo mambo yakanza kwenda kombo kwa mujibu wa afisa wa zamani wa kikosi cha GSU George Musamali.

Wafu au wahai?

Image caption Jengo la Westgate baada ya opareshini

"kila kikosi kikija na amri yake.Operesheni hiyo ilikwenda kombo," anasema.

" GSU ilikua imedhibiti hali ya mambo. Lakini jshi lilipofika,kila mtu alitimliwa na hapo ndipo mambo yakaaza kwenda kombo."

Wachunguzi wanasema wameweza kupata mabaki ya wtu watatu au wanne hivi ambao wanaamini nia ya miili ya washambliaji. Mabaki hayo bado yanafanyiwa uchunguzi bila ya matokeo yoyote ya DNA.

Baada ya idara ya polisi ya jiji la New York (NYPD) Marekani kutuma maafisa wake Nairobi kusaidia katika upelelezi,ilisema inawezekana kuwa baadhi au hata washambuliaji wote waliweza kutoroka.

Bwa Musamali,ambae bado ana uhusiano wa karibu na polisi na idara za kijasusi za Kenya anasema baadhi ya wenzake wa zamani wanakubaliana na NYPD.

"pia wanaamini washambuliaji huenda waliweza kutoka nj ya jengo.. Idara za kijasusi zinaniambia walitoka Westgate na walitoroka nchini ," anasema

Hivi sasa haijulikani kama washambuliaji wamekufa ama wahai.

Alfajiri ya Octoba 4, kasoro ya wiki mbili baada ya shambulio la Westgate , mhubiri mwenye msimamo mkali Ibrahim "Rogo" Omar alipigwa risasi na kuuwawa alipokua akisafiri na gari katika vitongoji vya mji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya Mombasa.

Yeye hakuhusishwa rasmi na Westgate lakini wafuasi wake wanaamini aliuliwa na kikosi cha polisi cha kupambana na ugaidi,Anti-Terror Police Unit (ATPU).

Usumbufu mahakamani

Rasmi polisi ya Kenya inakanusha kuhusika na mauaji yake lakini akiongea bila kutaka kutajwa jina lake.Afisa wa kikosi hicho anasema , ATPU waluhusika na muaji hayo.

"mfumo wa mahakama nchini Kenya hausaidii kazi ya polisi ," alisema.

"kwa hiyo tunaamua kuwaaangamiza,tunakutafuta,tunakupiga risasi mbele ya familia yako na huanzia na viongozi ."

Kilichomfika Bw Omar kimelezwa katika ripoti ya shirika la Waislamu la kutetea haki za binaadamu Muslims for Human Rights, inayoorodhesha mauaji kadhaa yasio halali ,watu kutoweka ,mateso na utekaji nyara vitendo vinavyodaiwa kutekelezwa na ATPU, kikosi kinachofadhiliwa kifedha na kimafunzo na Marekani na Uingereza.

"wanataka kuwafurahisha Waingereza na Wamarekani ,kwa sababu wanafadhiliwa kifedha," anasema Francis Auma, aliyetayarisha ripoti hiyo .

ATPU haikujibu maombi ya kuhojiwa na BBC . Katika taarifa yake,Wizara ya mambo ya je ya Uingereza ilisema inachukulia vibaya sana madai ya ukiukwaji wa haki binaadamu.

Taarifa hiyo iliongeza kusema kwamba "uingereza ina maslahi muhimu sana nchini Kenya. Tunachukulia kwamba maslahi haya yanahatarishwa kama ilivyobainishwa na shambulio la hivi karibuni katika maduka ya Westgate,na kwa Uingereza -hasa kutoka wapiganaji raia wa kigeni katika kanda ya Afrika ya Mashariki -ambao idadi yao kubwa wana fungamano na Uingereza.

"Tunashirikiana na serikali kupambana na tishio hili na kusaidia kuhakikisha utawala wa sheria nchini Kenya."

Bw Musamali anasema wengi wanaohusika na kupambana na ugaidi nchini Kenya wanahisi mfumo wa sheria nchini unazuia juhudi zao.

"Ikiwa polisi wanahusika basi ni kutokana na kuchoshwa.

"watakua na maelzo fulani na pengine wanajua fulani anahusika na ugaidi. Lakini unampeleka mahakamani na kesho anaachiwa kwa dhamana na kuendelea na vitendo vile vile ."

Ni watu wachache sana wasioamini kwamba Kenya ina tatizo la misimamo mikali.

Mwaalimu wa kiislamu Abubakar Shariff Ahmed, anaejulikana kwa jina Makaburi na anaetajwa katika orodha ya vikwazo vya Marekani na Umoja wa Mataifa na Marekani akishtumiwa kwa kuwaandikisha vijana wa Kiiislamu wa Kenya kushiriki katika harakati za utumiaji nguvu za siasa kali nchini Somalia - mashtaka anayoyakanusha anasema idara za kijasusi za Kenya zinawalenga moja kwa moja wale wanaowachukulia kua ni tisho.

Lakini jee idara za ujasusi zinawalenga watu wanaohusika hasa?

"labda ni hivyo,lakini aghlabu hapana ," anahisi Makaburi .

"najua wataniua.Lakini mimi siogopi usalama wangu. Mimi ni Muislamu halisi. Naamini maisha na kifo changu yako mikononi mwa Allah."

Na juhudi za polisi za kupambana na siasa kali zinaonekana kua na matoeko tofauti katika eneo la mtaa wa vibanda wa Majengo mjini Nairobi.

"Wanatuuwa ," kijana mmoja aliniambia ambae pamoja na wengine wamelalamika kwamba yeyote mwenye asili ya Kisomali au wa imani ya Kiislamu anashukiwa kuwa mfuasi wa al-Shabab. Wote walikanusha kumjua yeyote aliyejiunga na kundi hilo la msimamo mkali.

"Lakini hakuna tatizo ikiwa watajiunga na al-Shabab ama al-Qaeda," alisema Ahmed Abdurahman, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 20, akiongeza kwamba hii ni njia mojawapo ya kuzipatia fedha familia zao ikiwa hawana ajira.