Shabiki wa Sema Kenya

Mjadala wa Uwekezaji - Murang'a

Image caption Rose Gitau

Mjadala wa Murang’a uliangazia uwekezaji katika kaunti. Wakazi wa Murang’a walikaribishwa kuwauliza viongozi wao maswali hata kwenye mtandao. Rose Gitau alikuwa na haya ya kusema:

“Je, viongozi wanafanya nini kuharakisha mradi wa kuajiri walimu? Wana mipango ipi ambayo itafanisisha mkakati huo? Kuajiri walimu kulingana na wakati ambao walimaliza masomo sio nzuri hata kidogo. Tunashangaa! Nimejiuliza sana hili swali. Kiongozi wetu labda anaweza kutupa jibu mwafaka. Asante.”