Huwezi kusikiliza tena

Mjadala wa Muhtasari wa Msimu wa Pili

Ugatuzi Kenya

Je, baada ya Mwaka mmoja wa ugatuzi Kenya, mfumo huu wa utawala umefikia wapi? Huu ndio ulikuwa swali kuu katika mjadala huu. Sikiliza maoni ya wana jopo ambao walizungumzia maswala yaliyotokana na mijadala yafuatayo.

Kwanza kabisa, katika kaunti ya Kakamega, mgogoro kati ya viongozi wa kaunti ulionekana wazi tulipokuwa huko. Tazama Mjadala huu hapa:

Sema Kenya Kakamega

Migororo pia ilionekana wazi katika kaunti ya Machakos ambapo Seneta na Gavana hawasikilizani kwa mambo mengi. Mvutano huu ulionekana haswa ambapo Gavana hakukubali kuwa katika meza moja na Seneta.

Sema Kenya Machakos

Baadaye katika kaunti ya Murang'a, wakazi walisema kwamba hawajajumuishwa katika mipango kuu ya kaunti. Tazama mjadala hapa:

Sema Kenya Murang'a

Msimu mpya wa Sema Kenya unaanza Aprili 2014. Usipitwe!