Huwezi kusikiliza tena

Kenya inauwezo kukabiliana na majanga?

Tangu kujipatia uhuru wake, Kenya imekumbwa na majanga kadhaa, mengine yakibinadamu na mengine yakitokana na hali ya anga.

Image caption Uokoaji katika Shambulizi la kigaidi katika Maduka ya Westgate

Majanga ambayo yamewahi kutoka hivi karibuni ni , Shambulizi la kigaidi la katika Maduka ya Westgate, Moto katika mtaa wa Sinai uliosababishwa na kuvuja kwa mafuta na wenyeji kuyachota hivyo kusababisha vifo vya watu wengi, Kisa cha Sachang'any ambapo wanakijiji walichomeka moto baada ya kutaka kuchota mafuta kutoka trela lililokuwa na mafuta kuanza kuvuja.

majanga ambayo yanatoka na hali ya ngala ni kama vile ukame huko kaskazini mashariki mwa Kenya, sehemu fulani sa Pwani ya Kenya na eneo la Rift Valley.

Katika Mjadala huu BBC Sema Kenya inauliza, Je Kenya iko tayari kukabiliana na majanga yanapotokea?