Mtayarishi "Mambo ni moto sana!"

Tunaendelea kukuletea Mjidala mtoto moto.....

Shabiki mpendwa , BBC Sema Kenya inazidi kukupa fursa ya kukutanisha ana kwa ana na kiongozi wako ili umweze kumuuliza maswali magumu yanayokukera.

Mbali na kukutana na Kiongozi wako wakati wa mjadala pia unaweza kutoa maoni yako kupitia nambari 22340 ukianza na neno SEMA. Kumbuka huduma hii hatozwi malipo yeyote. Hii nikukurahisishia njia ya kuwasiliana na kiongozi wako.

Vile Vile tunakupa fursa ya kuwasiliana na na kiongozi wako kupitia mtandao wetu wa kijamii.

Nakukumbusha tu kuwa msimu huu wa tatu kipindi chako cha BBC Sema Kenya kimenga!

Kukukumbusha tu ili kufanuikisdha kipindi chako cha BBC Sema Kenya tunalenga watazamaji wa tabaka mbali mbali, kutumia mbinu tofauti tukiwa watangazaji wa kisasa.

Tunao wana jopo ambao ni wataalam katika sekta tofauti na washiriki wengi kwenye studio. Mbali na hawa, baadhi ya watarihi wetu wanazunguka sehemu tofauti, pamoja sehemu zilizotengwa nchini wakiandaa mijadala midogo ambayo inaunganishwa na mjadala wa studio. Muundo huu mpya unahakikisha kwamba sauti za wanyonge na waliotengwa, zote zinasikika. Kwa kweli msimu huu wa tatu utafana sana.

Utafiti unaashiria kwamba vipindi vinavyolenga usahii wa masuala, vinashawishi utawala bora katika jamii na pia katika mazingira tofauti. Sema Kenya ni mojawapo wa vipindi kama hivi, na kinawapa wananchi jukwaa la kushiriki katika mazungumzo yanayolenga sera mbadala.

Shabiki mpendwa, tunakualika kushirki katika mijadala kwenye kurasa zetu za kijamii za Twitter na Facebook. Vipindi vyote pia vinapatikana katika mtandao wetu BBC Sema Kenya.

Kipindi kitapeperushwa hewani kupitia KBC Channel 1 kila Jumapili saa kumi na mbili jioni, na kurudiwa kila Jumatano saa nne usiku. BBC Swahili, KBC Idhaa ya taifa na redio washirika kumi na wanne pia watakipeperusha kipindi. Hivi, sio rahisi kwamba utapitwa na kipindi!

Sema Kenya ni nafasi yako ya kujiunga na mazungumzo ya kitaifa ukiwa unaijenga nchi ya Kenya kama unaivyoipenda.

Mtayarishi MKuu

JB Ohaga