Jopo la mjadala kuhusu ugaidi

BBC sema Kenya ni ulingo wa kuyaweka wazi maswala makubwa ya maendeleo, ambayo wananchi wanakabiliana nayo. Kazi yetu kubwa ni kuwakutanisha watawala na watawaliwa ili kutafuta ufumbuzi kupitia gumzo. Na hapa studio za washirika wetu wa KBC tumewaalika wakenya kutoka maeneo tofauti ya nchi ambao hasa wameathiriwa na swala la ugaidi – kama vile… Mombasa, Westgate Victims, victim of anti -Terror Unit, Garissa, Mandera, Nairobi, Lamu, Kwale

Mwezi wa Septemba, tarehe ishirini na moja mwaka jana, Kenya ilishuhudia kisa kibaya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea mjini Nairobi tangu kushambuliwa kwa ubalozi wa Marekani mwaka wa 98. Watu zaidi ya sitini waliuawa na wengine wengi kujeruiwa pale magaidi walipovamia jengo la maduka la Westgate. Shambulo hili liliotokea licha ya Kenya kuchukua hatua kali za kupambana na ugaidi.

Tunauliza – je, Kenya inafanikiwa katika vita dhidi ya ugaidi? Na nini hasa athari ya juhudi hizo.

Hapa studio nina jopo la wageni watatu mashuhuri:

1) Kwanza kabisa ni Bi Grace Kaindi - ambaye ni Naibu Inspector Jenerali wa Polisi.

2) Pia tunaye Mwenda Njoka - ambaye ni msemaji wa wizara ya mambo ya ndani na pia mwandishi maarufu wa siku nyingi.

3) Mwanajopo wa tatu ni Bi Kagwiria Mbogori – yeye ni Menyekiti wa tume ya taifa ya haki za binadamu.