Je,Kenya inashinda vita dhidi ya ugaidi?

Mwezi huu, tarehe ishirini na moja mwaka jana, Kenya ilishuhudia kisa kibaya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea mjini Nairobi tangu kushambuliwa kwa ubalozi wa Marekani mwaka wa 98. Watu zaidi ya sitini waliuawa na wengine wengi kujeruiwa pale magaidi walipovamia jengo la maduka la Westgate. Shambulo hili liliotokea licha ya Kenya kuchukua hatua kali za kupambana na ugaidi.

Basi leo tunauliza – je, Kenya inafanikiwa katika vita dhidi ya ugaidi? Na nini hasa athari ya juhudi hizo.

Hapa studio nina jopo la wageni watatu mashuhuri:

Maelezo ya picha,

Kwanza kabisa ni Bi Grace Kaindi - Naibu Mkuu wa Polisi Kenya, Mwenda Njoka - ambaye ni msemaji wa wizara ya mambo ya ndani , Bi Kagwiria Mbogori – Menyekiti wa tume ya taifa ya haki za binadamu. na Pia Khelef Khalifa , Mwenyekiti Bodi ya MUHURI