Mtu mweusi aliyebaguliwa ataka haki

Haki miliki ya picha AFP GETTY IMAGES
Image caption Mtu aliyebaguliwa na mashabiki wa Chelsea alilia haki

Mtu aliyezuiliwa kuingia Paris Metro train na mashabiki wa timu ya mpira ya Chelsea kwa sababu ya ubaguzi wa rangi ametaka waadhibiwe.

Mtu huyo mwenye miaka 33 anayeitwa Souleymane S aliambia gazeti la Le Parisien: “Hawa watu, hawa mashabiki wanapaswa kufungwa".

Video ilionyesha mtu huyo akizuiliwa kuingia kwenye Metro na akisukumwa na mashabiki hao.

Watu walisikika wakiimba: "Sisi ni wabaguzi wa rangi na hivyo ndivyo tupendavyo".

Kanda hiyo ya video ilitolewa na gazeti la the Guardian lililotoa ripoti kuwa tokeo hilo lilifanyika Richelieu-Drouot katika mji mkuu wa Fance siku ya Jumanne kabla mechi ya Champions Legue.