Mnara wa Mau Mau wazinduliwa Nairobi

Image caption Mnara wa kumbukumbu wa Mau Mau

Mnara wa kuwakumbuka wapiganaji wa Mau Mau, walioongoza vita vya ukombozi kutoka kwa utawala wa kikoloni nchini Kenya, miaka ya 50,mezinduliwa rasmi katika bustani ya Uhuru mjini Nairobi.

Image caption Mnara wa kumbukumbu wa Mau Mau

Mnara huo umefadhilia na serikali ya Uingereza, kama sehemu ya mkataba ulioafikiwa mwaka wa 2013, ambao pia uliidhinisha wapiganaji hao kulipwa fidia ya £20m, kwa wapiganaji hao wa Mau Mau ambao walidhulumiwa na kuteswa na wanajeshi wa kikoloni wa Uingereza.

Image caption Mnara wa kumbukumbu wa Mau Mau

Serikali ya Uingereza ilikubali kuwa Wakenya hao waliteswa na kuwa inajuta mateso na dhuluma waliyoyapata.