Miaka 50 ya Idhaa

mkuu wa idhaa
Image caption Solomon Mugera, mkuu wa idhaa ya Kiswahili

Ni miaka 50 tangu mwanafunzi wa Tanzania aliyekuwa akisoma Uingereza kujipatia kazi ya kufana-kuzindua kwa mara ya kwanza kabisa matangazo ya kwanza kabisa ya idhaa ya kiswahili ya BBC.

''Hii ni London.Leo kwa mara ya kwanza kabisa BBC inawapa salamu wakaazi wa Afrika mashariki kwa lugha yao. Asalaam Aleikum''.

Kwa sauti tulivu,Oscar Kambona akazindua idhaa ambayo miaka mingi baadaye bado inaaminika kama miongoni mwa mamilioni ya wasikilizaji Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.

Mwaka 1957 kulishuhudiwa mabadiliko makubwa ya kisiasa katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.Ghana ikawa nchi ya kwanza kujipatia uhuru na kutoa mwelekeo kwa nchi zingine za eneo hilo.

Tangu kuzunduliwa tarehe 27 mwezi Juni mwaka 1957,Idhaa ya kiswahili ya BBC ilitangaza habari kuhusu vita vya kujitafutia uhuru na pia sherehe baada ya kujipatia uhuru Tanganyika, Uganda, Kenya, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Rwanda na Burundi.

Idhaa ya Kiswahili ya BBC iliwapa fursa waasisi kama Mwalimu Julius Nyerere wa tanzania,Rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta na Milton Obote wa Uganda fursa ya kuendeleza itikadi zao.

Idhaa hii ilijipatia sifa ya ujasiri kwa jinsi ilivyotangaza uvamizi wa Tanzania nchini Uganda ili kumaliza utawala wa kiimla wa Idi Amin mwaka 1972 na pia hatua ya Rwanda na Uganda kutimua dikteta mwingine Mobutu Sese Seko wa Zaire ambayo sasa inajulikana kama jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kwa miaka mingi Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilitawala masafa ya utangazaji Afrika Mashariki na |kati kwani ilikuwa njia mbadala ya kupata habari kwa vyombo vilivyomilikiwa na serikali.

Na huku idhaa ya Kiswahili ya BBC ikitimiza miaka 50,inakabiliwa na changamoto nyingi. Ushindani kutoka stesheni za Fm,mahitaji ya wasikilizaji yamebadilika na ni wachache tu wanaosikiliza masafa mafupi.

Kari Blackburn ambaye alikuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC mwaka 1996 hadi 1999 anakumbuka baadhi ya matukio muhimu wakati huo.

''Ulikuwa wakati wa mabadiliko makubwa kwa utanagazaji wa radio Afrika Mashariki na tulifahamu tosha kuwa hata mashabik wetu hawangevumilia matangazo ya masafa mafupi baada ya kusikiliza matangazo ya FM ambayo yalisikika vizuri zaidi.''

Kwahivyo pamoja na Barry Langridge, Michel Lobelle na Tido Mhando tukaanzisha ushirikiano na vyombo vikubwa vya habari nchini Tanzania kama IPP na Radio Free Africa.

''Wakati wa maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Idhaa ya Kiswahili ya BBC aliyekuwa Rais wakati huo Daniel arap Moi akatupa idhini ya kutangaza kwa vipimo vya FM Naironi na Mombasa."

''Wakati huo tulifanya mabadiliko makubwa katika vipindi vyetu na kuvipa majina kwa mara ya kwanza-Amka na BBC,Dira ya Dunia na Leo Afrika.''

''Kama mwanamke wa kwanza kuongoza Idhaa hii nilijitahidi sana kuwavutia wanahabari mashuhuri wa kike kama Mariam Omar, Suzanne Mungy na Vicky Ntetema."

Mrithi wa Kari Blackburn, Tido Mhando alikuwa mwenye bidii ya aina yake.Alifanikisha idadi ya wasikilizaji kuongezeka kutoka milioni 9 hadi milioni 18.

Hadi leo idadi ya wasikilizaji imeongezeka na kufikia milioni 21.3. Hii imetokana na ongezeko la wasikilizaji katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Kenya baada ya kuwa na radio washirika ambazo hutangaza kwa masafa ya FM.

Tido Mhando alifanya mahojiano na marias wengi. Daniel arap Moi wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, aliyekuwa Rais wa Tanzanian Benjamin Mkapa na mrithi wake Jakaya Kikwete, Paul Kagame wa Rwanda, aliyekuwa Rais wa Msumbiji Joachim Chissano na Joseph Kabila wa DRC ambaye alimrithi babake Laurent Kabila.

Tido alikuwa mwandishi wa habari wa mwisho kumhoji Laurent Kabila siku chache kabla ya kuuawa.

''Kwa kuwa marais wengi walikubali tuwahoji ni hiyo ilikuwa ishara kwamba waliiamini BBC''

''Tulipata mafanikio makubwa. Tulifungua ofisi katika eneo letu na tukahakikisha waandishi wetu wamepata vifaa vya kufanya kazi''.

''Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilikuwa idhaa ya kwanza ambayo sio ya kiingereza kutangaza Ligi ya Premier ya Uingereza kwa wasikilizaji wa Kiswahili.''

''Huenda hatua kubwa tuliopiga ni kuhamisha matangazo yetu ya asubuhi ,amka na BBC kutoka London hadi Nairobi. Tulitaka kuwa karibu na wasikilizaji wetu.''

Kwa Tido,maisha katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC yalikuwa ya kuchangamsha. ''Kila mwaka tulikuwa tukishugulikia mambo mapya. Tulitaka kutimiza mahitaji ya wasikilizaji.''

Na hadi sasa hamu ni hiyo hiyo. Enzi ya utangazahi inakabiliwa na changamoto nyingi kutoka platforms such as mobile phones and ipods.

Wasikilazaji wetu hawataki tu kusikiliza wanataka kushiriki na pia kuamua ajenda.

Wakati tunaposherehekea miaka 50 tutawekeza zaidi kwa wasikilizaji wetu. Tumeanzisha shindano la biashara vijana wenye umri wa miaka 16 hadi 24 ambapo kijana anayetoa wazo nzuri zaidi la biashara hujipatia $2000 na lap top.

Nia ya shindano la Faidika na BBC ni kutafuta wazo la kuvutia la biashara ambalo litasaidia kuimarisha maisha ya kijana na jamii yake.

Maelfu ya vijana hufuzu katika shule,taasisi mbalimbali na viuo vikuu kila mwaka. Sio wote ambao hufanikiwa kujipatia kazi katika sekta za umma na kibinafsi. Wengi wao hulazimika kuanzisha biashara ndogondogo au or simply waste away on the streets and in villages.

Faidika na BBC inatuma ujumbe kwa vijana kuwa mawazo yao yanaweza kuwa ya kweli. Ni ishara kwamba Bbc inawajali na pia inajali hali ya baadaye ya maisha yao.

Shindano hilo lilivutia zaidi ya vijana 5,000. Vijana watatu waliofika fainali walipambana nchini Tanzania katika hafla iliyotangazwa moja kwa moja kwa radio na Televisheni.

Ilikuwa hafla ya kwanza kabisa ya idhaa ya BBC isiyo ya kiingereza kutangazwa mojamoja kwa njia ya televisheni.

Mshindi alipata fursa ya kuwasilisha mawazo yake katika kikao cha vijana wakati wa mkutano wa Marais wa Jumuiya ya Madola mjini Kampala Uganda.

Na Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda kilijitolea kumpa ushauri wa kibiashara kabla ya kunzisha biashara yake.