Siri ya Ushindi

Faidika na BBC
Image caption Faidika na BBC

Unatakiwa kupanga mchanganuo wako kwa usahihi na maneno yanayoeleweka vyema kwa lugha ya Kiswahili. Kwa maelezo na usaidizi, jiunge nasi kwenye kipindi chetu cha 'Biashara Yako' kila wiki.

Mchanganuo wako usizidi maneno 1,500.

Mchanganuo wako uwiane vyema na zawadi ya kwanza ambayo ni dola 5,000 za Marekani. Fedha hizo zitakuwa mtaji wa kuanzishia biashara.

Jaribu kubuni mradi ulio na tofauti na wenye mtazamo wa kipekee. Epuka kuandika mchanganuo wa miradi ambayo ni imezoeleka sana. Kwa mfano mradi wa duka la rejareja, au mradi wa matatu / daladala.

Lakini iwapo una wazo la kuendesha biashara ya kawaida, lakini kwa njia ya kipekee na ya aina yake, mchanganuo huo unaweza kutazamwa.

Kumbuka mchanganuo wa biashara ulenge maslahi ya nchi na wananchi wa Afrika Mashariki na Kati.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuandika mchanganuo.

JINA LA MRADI

Andika bayana jina la mradi wako.

UTANGULIZI/ MAELEZO MUHIMU

Andika kwa muhtasari maelezo juu ya wazo lako, na kwa nini unadhani ni linafaa.

BAJETI

Eleza matumizi ya mradi wako kwa kutumia kigezo cha zawadi ya kwanza ya dola elfu tano.

MALENGO

Mbali na kuonesha faida ya biashara, ainisha mipango ya sasa na ya baadaye ya mradi..

MIKAKATI

Je kuna jambo gani la kuhatarisha mradi wako? Umejitayarisha vipi na hilo?

KUMBUKA!!

Kabla ya kuandika mchanganuo jiulize kwanza.

NANI:

Je nani atafanya nini katika mradi? Nani anahusika wapi na vipi?

NINI:

Je nini kinatakiwa au kitatakiwa kufanyika? Je kitagharimu kiasi gani?

WAPI:

Je mradi huo utafanyika wapi?

VIPI:

Je mradi huo utafanyika vipi? Utaendeshwa vipi? Utawala utakuwaje? Utachukua muda gani?

LINI:

Je lini utaanza mradi? Ni wakati gani utapiga hatua kubwa za kibiashara?

KWA NINI: Je kwa nini umechangua mradi na njia ulizoainisha?

USISITE: Kuomba ushauri kutoka kwa wataalam.

Usiandike mchanganuo kama unaandika insha, na vilevile usisahau kutuandikia jina lako, anuani na namba ya simu.