SHERIA NA KANUNI

SHERIA NA KANUNI

1. Shindano hili linaendeshwa na BBC. 2. Shindano ni kwa ajili ya raia na wakazi wa Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Washiriki lazima wawe na umri wa kati ya miaka kumi na sita (16) na ishirini na nne (24) wakati wa shindano. Washiriki watalazimika kuonesha uthibitisho wa umri na uraia wao. 3. Mchanganuo utakaowasilishwa usizidi maneno 1,500 (Elfu moja na mia tano). Na uwasilishwe kwa lugha ya Kiswahili tu. 4. Michanganuo itakayowasilishwa haitorejeshwa, hivyo mshiriki ahakikishe anahifadhi nakala. Mchanganuo uwe kazi halisi ya aliyeuandaa, na usivuke mipaka ya hakimiliki, au kuathiri mtu yeyote na kwa njia yoyote. 5. Washiriki watambue kuwa, BBC haitahakikisha kuifanya michanganuo iliyowasilishwa kuwa siri, hivyo waandaaji hawana budi kuamua ni yapi wanataka kuyaweka katika michanganuo yao. BBC haitahusika na lolote katika hilo. 6. Mchanganuo utumwe kwa BBC kupitia anuani iliyopo kwenye wavuti bbcswahili.com/faidika, au kutumwa kwa posta au kuwasilishwa katika ofisi za BBC zilizopo katika nchi zinazoshiriki kwenye shindano hili. 7. Michanganuo yote itapitiwa kwa uangalifu na michanganuo mitatu kutoka kila nchi itachaguliwa. 8. Mchuano wa kitaifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo utafanyika mjini Bukavu, Mashariki mwa nchi hiyo. 9. Washindi watatu kutoka kila nchi watalipiwa gharama zote na BBC za kushiriki katika fainali ya nchi husika.

10. Washindi wa kitaifa, watachujwa na majaji watakaoiwakilisha BBC na jamii ya wafanyabiashara ya eneo la Afrika Mashariki katika nchi husika. Mshindi katika taifa husika, atalazimika kutetea mchanganuo wake na kuwashawishi majaji, katika matangazo ya moja kwa moja ya BBC. 11. Mshindi wa kwanza kutoka kila taifa, ataalikwa na BBC kushiriki katika fainali, itakayofanyika Mombasa, Kenya. Washiriki watapambanisha michanganuo yao mbele ya majaji, katika fainali itakayotangazwa moja kwa moja kupitia BBC Idhaa ya Kiswahili na bbcswahili.com. 12. Wafanyakazi wa BBC hawaruhusiwi kushiriki katika shindano kama washindani. Kila mshiriki awasilishe mchanganuo mmoja tu. Atakayewasilisha zaidi ya mchanganuo mmoja atakuwa amejiondoa kwenye shindano. 13. BBC ina haki ya kuondoa mshiriki yeyote, wakati wowote, iwapo itaona kanuni zimekiukwa. 14. Kila mshindi, atazawadiwa tuzo maalum. Fedha taslimu hazitatolewa. Maelezo na jinsi zawadi zitakavyotolewa yanaweza kubadilishwa wakati wowote. 15. Washindi wa pili na wa tatu, katika michuano ya kitaifa, kila mmoja, atazawadiwa cheti maalum cha kutambua ushiriki wao katika shindano hili. 16. Mshindi wa kwanza atajinyakulia zawadi ya juu kabisa katika shindano, ambayo ina thamani ya dola 5,000 za Marekani na tuzo maalum. Fedha zitakuwa zikitolewa kwa mujibu wa mahitaji ya bajeti. Maelezo na jinsi zawadi zitakavyotolewa yanaweza kubadilishwa wakati wowote. Zawadi hizo na fedha haziwezi kubadilishwa na kupewa mtu mwingine, na wala hakuna njia nyingine zaidi ya kupata zawadi, kinyume na maelekezo ya BBC. 17. Washindi katika ngazi zote, watajulishwa kupitia matangazo ya BBC ya moja kwa moja. Kuingia kwa washiriki katika shindano hili, kunamaanisha washindi katika ngazi zote watakuwa radhi kurekodiwa sauti na picha zao, na kurushwa na BBC duniani kote, bila ya kibali, na vile vile kutumia michanganuo yao kwa ajili ya kulitangaza shindano na BBC. 18. Kwa kuwasilisha michanganuo, washiriki wanathibitisha kuwepo kwao katika fainali zote katika shindano hili. BBC inahifadhi haki za kubadili au kurekebisha sheria hizi, au hata kufuta kabisa shindano hili iwapo italazimika kufanya hivyo. 19. Michanganuo itachanguliwa kwa njia ya usiri na majaji, na uamuzi wao ndio wa mwisho. Hakutakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja kuhusu matokeo kati ya washiriki na majaji. 20. Kanuni na miongozo hii inarandana na sheria za Uingereza na mahakama za Uingereza ndio mipaka ya msingi. Kwa kuingia katika shindano hili, mshiriki atakuwa amesoma na kuelewa kanuni hizi, na kukubaliana nazo, na kuzifuata kama inavyotakiwa.