David Ssegawa, mshindi wa 2007

Image caption David Ssegawa

Mshindi wetu wa kwanza katika shindano la faidika na BBC alikuwa ni David Ssengwa kutoka Uganda.

David aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na miwili aliwashinda zaidi ya washindani wengine elfu tano. Alipokea tuzo ya kitita cha dola elfu mbili za Marekani kutoka kwa Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Majaji walipendezwa sana na wazo lake la kutengeneza mishumaa. Katika mahojiano David alielezea Faidika jinsi shida ya kukosekana umeme nchini Uganda ilimvuta kufikiria wazo hilo la kutengeneza mishumaa. ‘‘ Uganda imekuwa ikikumbwa na tatizo la kupotea kwa umeme kila mara. Bei ya mafuta imepanda kufuatia mpango wa serikali kujaribu kuhifadi kiwango cha vile watu wanatumia nguvu za umeme. Hii imesababisha mahitaji ya mishumaa kuongezeka. Kwa sasa mishumaa inaletwa nchini Uganda kutoka Uchina , lakini mimi ninajaribu kuanzisha biashara hiyo hapa nchini Uganda ili iwafaidi jamii.’’

David alipokea pia tuzo ya kompyuta ya laptop, na nafasi ya kuhutubia wajumbe katika kungomano la Commonwealth Youth Forum wakati wa mkutano wa wakuu wa serikali umaarufu Commonwealth Heads of Government Meeting uliofanya mjini Kampala Uganda mwaka alfu mbili na saba. David alinuia kutumia fedha alizotuzwa kununua machine ya kuyeyusha na kutangeza mishumaa. Alinuia pia kukodi mahala atakapofanyia kazi hiyo kwa miezi mitatu na kuajiri wafanyikazi kadha.

Kwa bahati mbaya , David hakuweza kuanzisha biashara Yake,. Katika mahojiano David anaeleza safari yake na msimamo aliyonayo kwa sasa.