Maswali yenu ya afya ya uzazi

Daktari William Obwaka akihojiwa katika kipindi
Image caption Daktari William Obwaka akihojiwa katika kipindi

Kila wiki ya nne ya makala ya Kimasomaso tunawaalika wataalamu kuchambua maswali yenu na pia kuvunja dhana nyingi zilizoko kuhusu afya ya uzazi. Wiki hii tumewaalika daktari William Obwaka kutoka hospitali ya Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Silas Kishaluli kutoka hospitali ya Muhimbili jijini Dar- es Salam, Tanzania kujibu maswali yenu.

Mojawapo ya maswali ambayo madaktari watafafanua kwa undani zaidi ni hili la Mwanaidi kutoka Tanzania anasema,'Mimi nina ndugu yangu alitoa mimba miezi kama sita iliyopita lakini cha kushangaza ni mpaka sasa matiti yake yanatoa maziwa na pia tumbo linamsumbua sana, je hii inasababishwa na nini?' Anne Mwajuma kutoka Nairobi anauliza, 'Je, kuna hatari gani ya kufanya mapenzi wakati mwanamke anaugua kutoka na yeast infection?'

Image caption Kenzo Msanii kutoka Nairobi, Kenya

Basi usikose kujiunga nasi kufafanuliwa haya na mengine mengi. Katika upande wa wasanii wiki hii uwanjani tunampisha msanii Kennedy Omondi a.k.a Kenzo kutoka Kenya, akituburudisha kwa kibao chake kipya 'Jiwachilie'.

Basi ikiwa ulikuwa umeuliza swali kwa daktari jiunge nasi katika kipindi jumapili hii upate jawabu na iwapo utakuwa na swali au maoni mengine usisite kutuandikia: kimasomaso@bbc.co.uk au unaweza kututumia ujumbe mfupi kwa nambari hii +447786202005, unaweza pia kututumia barua kwa sanduku la posta 58621-00100, Nairobi. Tuko pia katika mtandao wa Facebook, group yetu ni, “KIMASOMASO”