Masimulizi ya washiriki

Kutokana na uhakika wa hadithi zenye uthabiti za wahusika wakuu wa kipindi chetu, wasikilizaji wameweza kwa urahisi kutambua, na kuhisi maono yao na hivyo kujifunza kutokana na simulizi ya maisha ya wahusika wakuu.

Huwa tunafanya utafiti na kuwachagua wahusika wakuu kwa misingi ya wao kuwa vijana wa kawaida wanaokabiliana na maswala ya kila aina ya afya ya uzazi.

Vijana hao kisha hurekodi hadithi zao angalau kila wiki ili kuelezea visa tofauti katika maisha yao na ambavyo wanakabiliana na maswala husika.

Baadhi ya Wahusika wakuu wa kipindi katika awamu ya pili walikuwa wafuatao.

• Esther (mwathirika wa ubakaji) Hii ni hadithi ya msichana aliye kuwa na umri wa miaka 18 alipobakwa katika party, baada ya kinywaji chake kutiwa dawa. Alipima na kupata hakupata virusi vya HIV lakini akashika mimba.

Hakuweza kujua ni vijana wangapi walimwingilia wakati huo alipokuwa bado bikira. Hakumueleza yeyote wakati huo, miezi michache baadaye akagundua kwamba alikuwa mja mzito.

• Allan (mzazi mwenye umri mdogo asiye na ajira).

• Prosper & girlfriend (wapenzi wanafunzi) – Ni hadithi ya wapenzi wachanga ambao wangali katika shule ya msingi katika kanda ya Buyenzi mjini Bujumbura, na ambao wanakumbana na maswala kama vile msukumo rika, elimu pamoja na maswala mengine ya afya ya uzazi ukizingatia kuwa wameshaanza kushiriki ngono.

• Mukasa (kijana aliye shoga) – Kijana huyu mwenye umri wa miaka 23 anaishi katika jamii yenye msimamo mkali dhidi ya ushoga huko nchini Uganda. Tunamulikia maswala ya ngono salama hasa miongoni mwa mashoga.

• Michael (kijana mdogo anaeishi na virusi vya ukimwi) – Kijana huyu alie-ambukizwa virusi akiwa na umri wa miaka 13 anahadithia jinsi anavyo-ishi kwa imani licha ya kuambukizwa kwa njia ya kusikitisha. Swala la umaskini pia linachipuza kwenye simulizi yake.

• Peris – Muelimishaji rika anayenakili vipindi vyake vyote na maisha yake kama muelimishaji rika.

Makala ilivyoendelea, watayarishi wa kipindi waliwapata wahusika wengine zaidi na kuwasiliana nao, aidha moja kwa moja au kupitia mtandao wa ripota wetu wa idhaa ya Kiswahili ya BBC katika eneo zima.

Kulikuwa na changamoto ya kuhakikisha kuwa wahusika na hadithi zimepatikana kutoka kwenye eneo lote linalofikiwa na idhaa ya BBC ikiwemo eneo la maziwa makuu na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Tanzania na Kenya.

Mbali na tatizo la kuendelea kuwasiliana na watu walioko kwenye eneo hili zima na ambao sio wataalam wa utangazaji, kipindi kilifaulu katika kuwahusisha vijana wa tabaka mbalimbali na maswala mengi kuhusu afya ya uzazi yanayowakumba vijana katika eneo la Afrika Mashariki.