
Ziara ya Magufuli Kenya
Hujambo! Fuatilia habari za moja kwa moja kuhusu ziara ya Rais wa Tanzania John Magufuli katika nchi jirani ya Kenya hapa. Rais Magufuli anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais Kenyatta kuzindua pia barabara wakati wa ziara hiyo ya siku mbili.
Habari za moja kwa moja
time_stated_uk
Magufuli alivyopokelewa na Kenyatta ikulu Nairobi
Maafisa wa Rais Uhuru Kenyatta, kwenye akaunti yake ya Twitter, wamepakia picha za jinsi Rais wa Tanzania John Magufuli alivyolakiwa ikulu, Nairobi.
Magufuli: Kenya ni mshirika wetu mkubwa Afrika
Magufuli: Kenya ni mshirika wetu mkubwa kibiashara Afrika
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa Kenya ndio mshirika nambari moja wa Tanzania katika uwekezaji na biashara barani Afrika.
Akizungumza katika ikulu ya rais jijini Nairobi mda mfupi baada ya kuwasili nchini Kenya,Rais Magufuli amesisitiza kuwa hakuna taifa jingine ambalo limewekeza nchini mwake kama Kenya.
Amesema kuwa kulingana na rekodi za uwekezaji nchini Tanzania kuna takriban kampuni 529 nchini humo kutoka Kenya ambazo zinaingiza takriban dola bilioni 1.7 kila mwaka huku takriban Watanzania 57,260 wakiwa wameajiriwa.
Rais huyo vilevile ametoa wito kwa Wakenya wanaotaka kuwekeza nchini Tanzania kuharakisha hatua hiyo.
Aidha ameongezea kuwa amekuwa akiwasiliana na rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara na kiwakosoa wale wanaodhani kwamba uhusiano wake na rais wa Kenya una utata.
Magufuli alakiwa na waziri wa mambo ya nje
Wizara ya mambo ya nje Kenya imepakia picha za Rais Magufulia kilakiwa uwanja wa ndege na waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohamed. Bi Mohamed anawania wadhifa wa rais wa tume ya Umoja wa Afrika (AU).
Kenya inataka nini ziara ya Magufuli?
Msemaji wa Rais Kenyatta, Manoah Esipisu, Jumapili aligusia baadhi ya mambo ambayo Kenya inatarajia kutoka kwa ziara ya Rais Magufuli nchini Kenya.
Alisema: “Ziara ya Rais huyu inatupatia fursa ya kufanya upya na kukoleza uhusiano wetu katika nyanja mbalimbali. Viongozi wa nchi hizi watashauriana kuhusu masuala mbalimbali ya pamoja katika ngazi ya taifa kwa taifa na kanda. Wataangazia sana masuala ambayo tayari kumekuwa na mazungumzo, na tunatarajia matokeo ya mazungumzo hayo kutangazwa.
“Masuala kadha yatajadiliwa, ikiwemo ada ya vibali vya kufanyia kazi ambayo raia wa Kenya hutozwa, pamoja na karo ya juu ambayo Wakenya hutozwa vyuo vikuu (Tanzania). Mashauriano kuhusu kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi hizi mbili pia yatafanyika. Kadhalika, na muhimu sana katika mazungumzo hayo ni shughuli za magari ya kusafirisha watalii yanayovuka mipaka.
“Muhimu katika mashauriano haya itakuwa pia kufufuliwa kwa Tume ya Ushirikiano wa Pamoja na Tanzania (JCC) ambayo ni jukwaa ambalo linaweza kutumiwa kutangaza biashara na uwekezaji baina ya nchi zote mbili.
“Rais Kenyatta pia atazungumza na Rais Magufuli kumhusu Bi Amina Mohammed (waziri wa mambo ya nje wa Kenya) anayewania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Magufuli awasili ikulu, Nairobi
Rais Magufuli amewasili katika ikulu ya Nairobi ambapo amekagua gwaride la heshima. Pia amepigiwa mizinga 21 kama ilivyo ada kwa viongozi wa mataifa wanapozuru Kenya.
Mambo matano atakayoyafanya Magufuli akiwa Kenya
Wakati wa ziara yake ya siku mbili Kenya Rais Magufuli, kwa mujibu wa ikulu ya Tanzania, anatarajiwa:
Magufuli amewasili 'mapema'
Mwandishi wa gazeti la kibinafsi la Nation, Kenya ameandika kwenye Twitter kwamba Rais Magufuli tayari amewasili uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta. Mwandishi huyo anasema huenda kiongozi huyo amewasili mapema kuliko ilivyotarajiwa.
Ziara ya Magufuli kwa kibonzo
Mchoraji vibonzo mashuhuri Afrika Mashariki, Godfrey Mwapembwa maarufu kama Gado amepakia kwenye Twitter kibonzo kuhusu ziara ya Rais Magufuli Kenya.
Viongozi wamuaga Magufuli JNIA
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na viongozi wengine wakipunga mikono kumuaga Rais Magufuli katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akianza safari ya kwenda Nairobi.
Magufuli aabiri ndege kwenda Kenya
Ikulu ya Rais Tanzania imepakia picha hii mtandaoni, ya Rais Dkt John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akipanda ndege kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya. Ziara hiyo ni ya siku mbili.
Rais Magufuli aanza ziara ya kwanza Kenya
Magufuli kushauriana na Kenyatta na kuzindua barabara
Rais wa Tanzania John Magufuli anatarajiwa kuanza ziara yake ya kikazi katika nchi jirani ya Kenya leo.
Kwenye ziara hiyo ya siku mbili, Rais Magufuli anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake na pia kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.
Barabara hiyo, ambayo inaunganisha maeneo mbalimbali ya jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini, ni moja kati ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara ambayo imekuwa ikitekelezwa na serikali ya Kenya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kuu.