Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Obama ampongeza Trump, amwalika White House

  Rais Obama amempigia simu Donald Trump kumpongeza kwa ushindi uchaguzi wa urais ambapo pia amemwalika ikulu ya White House mnamo Alhamisi wajadiliane kuhusu shughuli ya mpito.

  Obama pia amempigia Hillary Clinton na kumpongeza kutokana na alivyofanya kampeni.

  Rais Obama atatoa taarifa zaidi Jumatano kutoka White House kujadili matokeo ya uchaguzi na hatua ambazo tunaweza kuchukua kama taifa kuungana tena pamoja baada ya kipindi cha uchaguzi huu uliokuwa na ushindani mkali", katibu wa ikulu amesema kupitia taarifa.

  Taarifa kamili hii hapa:

  Obama
 2. Wafuasi wa Trump washerehekea

  Wafuasi wa Donald Trump wamekuwa wakisherehekea maeneo mbalimbali Marekani.

  Hizi hapa ni baadhi ya picha:

  Trump
  Trump
  Trump
  Trump
 3. Putin atuma pongezi kwa Donald Trump

   Kiongozi wa Urusi Vladimir Putin ametuma ujumbe wa telegramu kumpongeza Donald Trump kwa kushinda urais Marekani.

  Amesema ni matumaini yake kwamba uhusiano kati ya Urusi na Marekani "utaondolewa kutoka hali ya mzozo".

  Bw Trump alimsifu Bw Putin wakati wa kampeni, hatua iliyomfanya kushutumiwa na mgombea wa Democratic Hillary Clinton na wakuu wengine wa Democratic.

  Soma zaidi hapa: Trump asema Putin 'ni kiongozi bora kuliko Obama'false

 4. EU yampongeza Trump na kumpa mwaliko

  Wakuu wa Umoja wa Ulaya  Donald Tusk na Jean-Claude Juncker wameandika barua kumpongeza rais mteule wa Marekani Donald Trump na kusisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na EU.

  Wamempa mwaliko wa kuzuru Ulaya.

 5. Waziri mkuu wa Uingereza ampongeza Trump

  Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amempongeza Trump kufuatia ushindi wake uchaguzi wa urais Marekani.

  Amesema Marekani na Uingereza zina uhusiano maalum na wa muda mrefu na ambao msingi wake ni "uhuru, demokrasia na ujasiriamali."

  Ameeleza matumaini yake kwamba Marekani na Uingereza zitasalia kuwa washirika wakuu.

  "Nasubiri kufanya kazi na Rais mteule Donald Trump," amesema kupitia taarifa.

  Trump
 6. Museveni, Kenyatta, Kagame wampongeza Donald Trump

  Rais wa Uganda Yoweri Museveni amejiunga na viongozi mbalimbali duniani wanaompongeza Donald Trump kwa kushinda urais Marekani.

  Bw Museveni, kupitia ujumbe kwenye Twitter, amesema anasubiri kufanya kazi na Trump kama alivyofanya kazi na marais wengine waliomtangulia.

  Wengine waliompongeza ni Dkt John Magufuli wa Tanzania, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Ali Bongo wa Gabon, Rais Abdul Fattah al-Sisi wa Misri, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

  Makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini Dkt Riek Machar pia amempongeza Bw Trump na kueleza matumaini kwamba ushindi wake utakuwa "mwisho wa watawala wa kiimla Afrika".

 7. Ni vigumu kujua mshindi majimbo manne

  ABC News wanasema itakuwa vigumu kufanya makadirio zaidi ya matokeo ya uchaguzi katika majimbo yaliyosalia Marekani.

  Wamesema majimbo ya New Hampshire, Arizona, Michigan na Minnesota ushindani ni mkali sana hivyo itakuwa vigumu kukadiria.

  Trump tayari ameshinda.

 8. Korea Kusini 'kudumisha uhusiano na Trump'

  Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Yun Byung-se amesema anaamini Donald Trump ataendeleza msimamo wa sasa wa Marekani wa kutoivumilia Korea Kaskazini.

  "Trump ameashiria kwamba tatizo kubwa linalokabili dunia ni silaha za nyuklia na wanachama wa kundi lake la wataalamu wa usalama wa taifa wana msimamo huo ambao unahusisha kuishinikiza vikali Korea Kaskazini," Yun amesema, akilihutubia bunge.

 9. Waziri mkuu wa Singapore asema Trump amerudia Brexit

  Waziri mkuu wa Singapore, mshirika mkuu wa Marekani barani Asia, amempongeza Donald Trump na anasema nchi yake itafanya kazi naye.

  Lee Hsien Loong amesema: "Sawa na Brexit mwezi Juni, ushindi wa Bw Trump ni mtindo unaofanyika katika mataifa yaliyoendelea - kuonesha kusikitishwa kwa watu na jinsi mambo yalivyo."

  Bw Trump majuzi alitaja Singapore, pamoja na China na India, kama nchi za bara Asia 'zinazoiba' nafasi za kazi kutoka Marekani.

 10. Modi ampongeza Trump, afurahia 'urafiki'

  Waziri mkuu wa India Narendra Modi amempongeza Donald Trump kupitia msururu wa ujumbe kwenye Twitter.

  Amesema anafurahia urafiki ambao Bw Trump ameonyesha kwa India wakati wa kampeni.  

 11. Kiongozi wa EU asikitishwa na ushindi wa Trump

  Rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya Martin Schulz amesema ushindi wa Donald Trump ni "kura ya uasi" ambayo inafanana na Brexit (kura ya Waingereza kujitoa EU).

  Ameambia redio ya Europe 1 kwamba ameshangazwa na kusikitishwa na kwamba anatarajia iwe vigumu zaidi kufanya kazi na utawala wa Bw Trump kuliko utawala wa Rais Obama.

  Amemtaka Bw Trump "aheshimu maadili muhimu na uhuru wa mataifa."

 12. Kiongozi wa zamani wa Ku Klux Klan ampongeza Trump

    David Duke, kiongozi wa zamani wa kundi la Ku Klux Klan, amempongeza Trump kupitia Twitter na pia akawapongeza "watu wetu" waliompigia kura.

 13. Mambo ambayo Trump yakuyazungumzia

  Hakuzungumza kuhusu ukuta aliosema atajenga katika mpaka wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji.

  Aidha, hakuzungumzia vitisho vyake kwamba atamfunga jela  Hillary Clinton, na pia kwamba atahakikisha Waislamu wanakaguliwa sana kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

 14. Ukurasa wa kwanza wa gazeti la New York Times

  Gazeti la New York Times ambalo lilikuwa linamuunga mkono Bi Clinton.

  Donald Trump
 15. Trump: "Nitakuwa rais wa kila Mmarekani'

  Akihutubu baada ya ushindi, Trump amesema: "Naahidi kila raia wa taifa hili letu kwamba nitakuwa rais wa kila Mmarekani. Na hilo ni muhimu sana kwangu.

  "Kwenu ambao mliamua kutoniunga mkono siku za nyuma, na kulikuwa na watu kadha, ninaomba ushauri wanu na nitamuomba tusaidiane ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kuunganisha taifa hili letu tukufu."

 16. Trump ashinda jimbo la Alaska

  Donald Trump ameshinda jimbo la Alaska na kuchukua kura zote tatu za wajumbe kutoka jimbo hilo, kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Sasa ana wajumbe 278 naye Bi Clinton kura 218.

  Mgombea huhitaji kura 270 kushinda.

 17. Nkurunziza ampongeza Trump

  Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ni miongoni mwa viongozi waliompongeza Donald Trump kupitia Twitter. Amesema ushindi wa Trump ni ushindi wa Wamarekani wote.

 18. Magufuli ampongeza Trump kwa ushindi Marekani

  Rais wa Tanzania John Magufuli ameandika ujumbe kwenye Twitter akimpongeza rais mteule wa Marekani.

  Ameahidi kwamba Watanzania wataendeleza urafiki na Marekani.

 19. Trump ashinda jimbo la Wisconsin

  Trump ameshinda jimbo la Wisconsin na kujishindia kura 10 za wajumbe. Hilo limemuwezesha kufikisha kura 275 za wajumbe, Clinton akiwa na kura 218.

  Mshindi alihitaji kura 270.

  Trump Clinton
 20. Trump ashinda jimbo la Pennsylvania

  Makadirio ya ABC News yanaonesha Trump ameshinda Pennsylvania. Jimbo hilo lina kura 20 za wajumbe. Sasa Trump ana kura 265 za wajumbe na Clinton kura 218. Mshindi alihitajiwa kupata kura 270 za wajumbe.