Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Adama Barrow ndio rais mpya wa Gambia

  Adama Barrow, mtu aliyeibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Gambia ameapishwa rasmi kuwa rais wa taifa hilo.

  Alikula kiapo hicho katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal huku akiwaagiza wanajeshi wa Gambia kusalia katika kambi zao.

  Ametambuliwa kimataifa.

  Lakini aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh amekataa kujizulu na muda wake wa kuhudumu umeongezwa na bunge.

  Viongozi wa Afrika Magharibi wameshindwa kumsihi bw Jammeh kuondoka mamlakani.

  Wametishia kumuondoa kwa nguvu.

  Bw Jammeh alishindwa katika uchaguzi huo wa Disemba mosi ,kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.

   Lakini anataka matokeo ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali akidai makosa mengi katika uchaguzi huo.

   ''Mimi Adama Barrow ,naapa kwamba nitatekeleza wajibu wangu katika afisi ya urais wa taifa la Gambia kwamba nitahifadhi na kutetea katiba'' .

   Na katika hotuba yake ya kuapishwa ,aliwaagiza wanachama wote wa jeshi la gambia kusalia katika kambi zao. ''Wale watakaopatikana wakibeba silaha watachukuliwa kuwa waasi'', alionya.

  Rais mpya wa Gambia Adama Barrow
  Image caption: Rais mpya wa Gambia Adama Barrow
 2. Wasifu wa rais mpya wa Gambia Adama Barrow

  -Adama Barrow alizaliwa mwaka 1965 katika kijiji kimoja karibu na mji wa kibiashara wa Basse Mashariki mwa Gambia. 

  - Alihamia mjini London miaka ya 2000 ambapo anaripotiwa alifanya kazi kama mlinzi kwenye duka moja, Kaskazini mwa London, akiendelea pia na masomo yake. 

  - Alirejea nchini Gambia mwaka 2006 ambapo alianzisha kampuni yake ya kuwekeza. 

  -Barrow mwenye umri wa miaka 51 aliteuliwa kuongoza muungano wa vyama saba vya upinzani kumpinga Rais Yahya Jammeh. 

  -Amekosoa kutokuwepo kwa miula miwili kwa urais na pia kulaani kufungwa kwa wanasiasa wa upinzani. 

  -Anaunga mkono uhuru wa mahakama, wa vyombo vya habari na wa vyama vya umma. 

  Rais mpya wa Gambia Adama Barrow baada ya kuapishwa
  Image caption: Rais mpya wa Gambia Adama Barrow baada ya kuapishwa
 3. Adama Barrow awasili eneo la kuapishwa

  Rais mteule wa gambia tayari amefika katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal kuapishwa kuwa rais wa Gambia

  Wakati huohuo balozi wa Rwanda nchini Senegal amejiunga na wanadiplomasia wengine na maafisa katika sherehe za kuapishwa kwa Adama Barrow katika ubalozi wa Gambia mjini Dakar.

   Nje ya ubalozi huo raia wengi wa Gambia wanaofanya kazi nchini Senegal wamekongamana tayari kuhudhuria kuapishwa kwa rais mteule wa Gambia Barrow ambaye wanamuona kuwa rais wa kwanza wa Gambia katika kipindi cha miaka 22.

  Rais Mteule wa Gambia Adama Barrow
  Image caption: Rais Mteule wa Gambia Adama Barrow
 4. Wanajeshi wanaomtii Jammeh kukabiliana na uvamizi wowote

  Rais wa Gambia Yahya Jammeh kwa sasa yuko katika makao yake rasmi, kwa mujibu wa shirika la habari la AP lililomnukuu afisa mmoja nchini humo.

   Ikiwa atakamatwa na kikosi cha kanda basi atakuwa katika ikulu na wengi wa wanajeshi wanaomtii  Jammeh watapinga hilo.

   Vikosi vya kanda vinatarajiwa kuchukua hatua.

  Senegal imetuma mamia ya wanajeshi kwenye mpaka wake na Gambia huku Nigeria ikituma ndege za kivita na helikopta mjini Dakar, na pia imepeleka meli ya kivita eneo hilo.

   Ripoti ambazo hazijathibitishwa  zinasema kuwa baadhi ya wanajeshi wa kanda tayari wameingia nchini Gambia.

   Muhula wa Jammeh kama rais ulitarajiwa kumalizika siku ya Jumatano.

   Muhula huo uliongezwa kwa siku 90 na bunge siku ya Jumanne lakini serikali zingine za magharibi mwa Afrika hazitambui hilo. 

  Rais Jammeh amedaiwa kuwa katika ikulu ya Gambia
  Image caption: Rais Jammeh amedaiwa kuwa katika ikulu ya Gambia
 5. Botswana yasema haimtambui tena Yahya Jammeh kama rais

  Botswana ndio taifa la kwanza barani Afrika kutangaza kuwa halimtambui Yahya Jammeh kuwa rais wa Gambia kufuatia hatua yake ya kukataa kuachilia mamlaka kwa Adama Barrow ambaye alimshinda katika uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba.

  Katika taarifa, serikali ya Botswana imesema: Hatua ya bw Jammeh kukataa kuheshimu uamuzi wa raia wake unakandamiza juhudu za kukuza demokrasia na uongozi bora katika taifa la Gambia na Afrika nzima kwa jumla.

   Hatua hiyo inakiuka sheria ya Umoja wa Afrika 

  Rais wa Botswana Ian Khama akiapishwa kuwa rais
  Image caption: Rais wa Botswana Ian Khama akiapishwa kuwa rais
 6. UN kupiga kura ya kuingilia kati Gambia

  Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa UN litapiga kura baadaye hii leo kuhusu uamuzi wa kuunga mkono juhudi za Muungano wa mataifa ya Afrika Magharibi kuhamisha mamlaka katika taifa la Gambia kwa Adama Barrow kulingana na kituo cha habari cha AFP.

   Muugano huo wa kiuchumi ECOWAS umeandaa kikosi cha kuingilia kati nchini Gambia iwapo Yahya Jammeh atakataa kuondoka madarakani baada ya kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu uliopita. 

   The Gambia ambalo ni taifa dogo barani Afrika ni mojawapo wa mataifa ya muungano wa ECOWAS

 7. Raia wa Gambia ''wamsubiri Jammeh kuondoka''

  Barabara za mji mkuu wa Banjul nchini Gambia zimesalia kuwa mahame. Maduka, vituo vya gesi na hata benki zimefungwa. 

   Watu wanasalia majumbani mwao wasijue kitakachofanyika baadaye.

  Watalii kutoka Ulaya wanaendelea kuondoka katika hoteli zao na wanasafirishwa kuelekea uwanja wa ndege kupanda ndege zao ambazo zitawasafirisha hadi nyumbani mapema zaidi ya walivyopanga.

   Katika maeneo mengine, wanaume wamesimama kandakando ya barabara ,wakiwa wamekunja mikono ama wakiangalia simu zao.

   Tulizungumza na baadhi yao ambao walisema walikuwa wanamsubiri Yahya Jammeh kuondoka mamlakani.

   Walisema kwamba wataandamana wakati Adama Barrow atakapoapishwa. 

   Pia wamevitaka vikosi vya mataifa ya Magharibi kuingia katika taifa hilo mara moja.

   Wengine wana wasiwasi kwamba Jammeh huenda akakabiliana na uvamizi wowote wa kijeshi dhidi yake.  

  Hatahivyo, kumekuwa na wanajeshi wachache katika mji mkuu kufikia sasa.  

  Barabara za mji mkuu wa Banjul nchini gambai zimesalia kuwa mahame
  Image caption: Barabara za mji mkuu wa Banjul nchini gambai zimesalia kuwa mahame
 8. Ubalozi wa Gambia nchini Senegal wafungwa

  Mwandishi wa BBC mjini Dakar nchini Senegal ameenda katika ubalozi wa Gambia nchini humo na kuona kwamba umefungwa bila walinzi.

  Ubalozi huo unataraijiwa kuandaa kuapishwa kwa mfanyibiashara Adama Barrow kuwa rais wa tatu wa Gambia baadaye leo. 

  Ubalozi wa Gambia nchini Senegal
  Image caption: Ubalozi wa Gambia nchini Senegal
 9. China yataka uamuzi wa ''busara'' kufanywa Gambia

  Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini China Hua Chunying amesema: Tunazitaka pande husika kutoa uamuzi mzuri na kuwapa kipao mbele raia wa taifa hilo na taifa lenyewe kwa jumla.

   Tunaowaomba watatue mzozo huo kupitia majadiliano ushauru wa kisiasa ili kukuza amani na udhabiti. 

  China ina maslahi chungu nzima ya kidiplomasia na kibiashara barani Afrika na imeshirikishwa sana katika juhudi za kuleta amani nchini Sudan Kusini kulingana na ripoti za Reuters.

   China iliendelea na ushirikiano wa kidiplomasia na Gambia mnamo mwezi Machi mwaka jana.

   Taifa hilo lilikuwa mshirika mkubwa wa kidiplomasia na Taiwan ,ambayo China inaichukulia kama mkoa unaotaka kujitenga na kwamba hauna haki rasmi ya kushirikiana na mataifa mengine ya kigeni.

   The Gambia limekuwa taifa mojawapo ya mataifa machache barani Afrika ,pamoja na Burkina fasso ,Swaziland na Sao Tome na Principe kutambua Taiwan.

   Sao Tome ilianza ushirikiano na China mwezi uliopita. 

  Viongozi wa muungano wa mataifa ya Magharibi ECOWAS ndio waliongoza majadiliano Gambia
  Image caption: Viongozi wa muungano wa mataifa ya Magharibi ECOWAS ndio waliongoza majadiliano Gambia
 10. Wakili wa Yahya Jammeh atorokea Senegal

  Wakili wa rais Yahya Jammeh ametorokea nchini Senegal baada ya kumuandikia barua rais Jammeh akimtaka kuachilia mamlaka gazeti la Nigeria Primium times limesema.

  Edu Gomez alisema kuwa amemfanyia kazi Jammeh chini ya shinikizo chungu nzima.

  Gazeti hilo pia limenukuu barua hiyo ikisema: Siku ya Jumanne tarehe 17 mwezi Januari 2017, mwanangu na mimi tulifanya uamuzi muhimu kutafuta hifadhi katika taifa jirani la Senegal.

  Hatua hii tuliona ni muhimu kutokana hofu inayoendelea kutanda na wasiwasi kila wakati.

   BBC hatahivyo haijapata uthibitisho huru wa ripoti hiyo.

   Bw Gomez alimwakilisha Jammeh katika harakati za kufutilia mbali ushindi wa kiongozi wa upinzani Adama Barrow katika uchaguzi wa tarehe mosi Disemba.

  Barua alioandika wakili wa Yahya Jammeh baada ya kutorokea Senegal
  Image caption: Barua alioandika wakili wa Yahya Jammeh baada ya kutorokea Senegal
 11. Adama Barrow kuapishwa ubalozini Senegal

  Mtu ambaye alishinda uchaguzi unaokumbwa na utata nchini Gambia anasema kwa ataapishwa kama rais wa anchi kwenye ubalozi wa Gambia ulio kwenye nchi jirani ya Senegal.

  Ujumbe ulioandikwa kwenye akaunti za Adama Barrow za mitandao ya kijamii uliiwaalika watu kuhudhuria sherehe hiyo.

  Jitihada za mwisho za viongozi wa kanda za kumshawisha Yahya Jammeh kuondoka madarakani kama rais zimeshindwa. Alishindwa uchaguzi mwezi uliopita lakini anataka matokeo hayo kufutwa akidai kuwepo itilafu.

   Vikosi vya wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi viko tayari kushinikiza mabadiliko ya mamlaka nchini Gambia, nchi ambayo ni maarufu kwa watalii.

  Rais mteule wa Gambia muda mfupi baada ya kushinda uchaguzi
  Image caption: Rais mteule wa Gambia muda mfupi baada ya kushinda uchaguzi
 12. Makamu wa rais wa Gambia ang'atuka

  Makamu wa rais nchini Gambia Isatou Njie-Saidy amejiuzulu saa chache kabla ya muda wake wa kuongoza kutimia ,AFP imenukuu duru za familia yake.

  Waziri wa mazingiura na elimu ya juu pia alijiuzulu,ikiwa ni msururu wa mawazuri kumtoroka bw Jammeh kufuatia hatua yake ya kukataa kujiuzulu baada ya zaidi ya miongo miwili afisini AfP imeripoti.

  Makamu wa rais nchini Gambia Isatou Njie-Saidy
  Image caption: Makamu wa rais nchini Gambia Isatou Njie-Saidy
 13. Hujambo

    Karibu katika ukurasa wetu wa habari za moja kwa moja kutoka Gambia ambapo tunakupasha matokeo mbali mbali kutoka taifa hilo pamoja na taarifa zinazogonga vichwa vya habari barani Afrika