Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Jammeh "kuachia madaraka na kuondoka"

  Kiongozi wa Gambia Yahya Jammeh atawachia madaraka na kuondoka nchini Gambia, kwa mujibu wa maafisa wanaongoza mapatano. 

  Wapatanishi wa Afrika Magharibi walitumia masaa kadha wakikutana na bwana Jammeh siku ya Ijumaa kuzungumzia hatma yake. 

  Msafara wa magari uliowabeba marais wa Guinea na Mauritania, umeondoka makao ya Jammeh lakini hayaaminiwi kuondoka nchi humo. 

  Bwana Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba na mrithi wake Adama Barrow ameapishwa. 

  Wafuasi wa Barrow walishangilia katika nchi jirani ya Senegal
  Image caption: Wafuasi wa Barrow walishangilia katika nchi jirani ya Senegal
 2. Barrow: Yahya Jammeh amekubali kuachia madaraka

  Rais wa Gambia anayetambuliwa na jamii ya kimataifa Adama Barrow ameandika kwenye Twitter kwamba Yahya Jammeh amekubali kuachia madaraka na kuondoka Gambia.

  Msafara wa magari umeonekana ukiondoka ikulu, Banjul. Hata hivyo, haijathibitishwa iwapo Jammeh yupo kwenye msafara huo.

  Jammeh amekuwa akifanya mazungumzo kwa saa kadha na marais wa Guinea na Mauritania.

 3. Jammeh ataondoka?

  Mwandishi wa BBC Umaru Fofana anasema mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Rais anayetambuliwa na jamii ya kimataifa Adama Barrow amemdokezea kwamba Jammeh amekubali kung'atuka.

  Lakini habari hizo bado hazijathibitishwa.

  Awali, zulia jekundu lililokuwa limeandaliwa uwanja wa ndege wa Banjul lilikuwa limeanza kuondolewa na wanajeshi bila kuwepo kwa Jammeh.

  Ndege ya Gambia
 4. Conde na Abdel Aziz wajiandaa kuondoka Gambia

  Msafara wa magari umeonekana ukiondoka ikulu ya Gambia. Haijabainika iwapo Jammeh yumo kwenye msafara huo.

  Katika uwanja wa ndege wa Banjul, maafisa wameonekana wakijiandaa, ishara kwamba marais Alpha Conde na Mohamed Ould Abdel Aziz wanatarajiwa kuondoka wakati wowote.

  Haijabainika iwapo wataondoka na Jammeh.

 5. Barrow anajiandaa kuanza safari?

  Rais wa Gambia anayetambuliwa na jamii ya kimataifa Adama Barrow amedokeza kuwa huenda anajiandaa kuondoka Senegal.

  Amewashukuru wenyeji wake kwenye Twitter: 

 6. Jammeh 'anaandika taarifa ya kuondoka'?

    Mwanahabari wa France 24 ameandika kwenye Twitter kwamba kuna uwezekano Jammeh anaandika taarifa ya kukubali kuondoka kwenda Guinea. 

 7. Barrow na Sall waombea amani Gambia

  Rais wa Gambia anayetambuliwa na jamii ya kimataifa Adama Barrow amepakia kwenye Twitter picha yake na rais wa Senegal Macky Sall "wakiombea amani Gambia".

  Macky Sall na Adama Barrow
  Image caption: Macky Sall na Adama Barrow
 8. Muda wapita tena bila Jammeh kuondoka

  Yahya Jammeh

  Jammeh alikuwa ameomba apewe hadi saa 16:00 (saa moja jioni Afrika Mashariki) kufanya uamuzi kuhusu iwapo ataachia madaraka au la.

  Makataa ya kwanza ya kumtaka aachie madaraka kufikia saa sita mchana yalikuwa yamepita.

  Taarifa zinasema makamu wa rais wa zamani wa Gambia, Isatou Njie-Saidy, yupo ikulu ambapo anashiriki mazungumzo ya dakika za mwisho.

  Marais wa Mauritania na Guinea wanajaribu kumshawishi Jammeh kuondoka.

 9. "Tutawakaribisha wanajeshi wa Ecowas kwa chai"

  Ousman Badjie

  Mkuu wa majeshi ya Gambia Jenerali Ousman Badjie ameambia Reuters kwamba anamtambua Rais Adama Barrow kama amiri jeshi mkuu mpya amesema hatapigana vita dhidi ya wanajeshi wa kanda wanaotaka kumuondoa kwa nguvu Yahya Jammeh. 

  Quote Message: Tutawakaribisha kwa maua na kuwaandalia kikombe cha chai
  Quote Message: Huu ni mzozo wa kisiasa. Ni suitafahamu tu. Hatutapigana na wanajeshi wa Nigeria, Togo au wanajeshi wa taifa lolote lile watakaofika hapa.
 10. Jammeh aenda msikitini kwa sala

  Mazungumzo yanapoendelea ikulu kati yake Yahyah Jammeh na marais wa Guinea na Mauritania, baadhi ya wanahabari walienda msikitini wakati wa sala ya Ijumaa ulipofika.

  Lakini mwandishi wa BBC Umaru Fofana anasema katikati mwa hotuba ya imamu Alhaji Jallow, wanahabari walitakiwa kuondoka safu nne za mbele.

  Baadaye walitolewa nje. Mmoja wa walinzi wa rais alimnong'onezea kwamba bila shaka, Jammeh na wageni wake walikuwa wanatarajiwa kuingia msikitini.

 11. Barrow: Jammeh anafaa kuondoka Gambia

  Mwanahabari mwenye makao yake Dakar Nicolas Haque anasema amezungumza na Rais wa Gambia anayetambuliwa na jamii ya kimataifa Adama Barrow ambaye amemwambia Yahya Jammeh anafaa kuondoka nchini humo.

  WIki iliyopita, Barrow alisema hakukuwa na haja kwa Jammeh kwenda uhamishoni.

  Aliahidi kwamba hatashtakiwa na serikali mpya.

 12. Habari za hivi pundeJammeh aomba muda zaidi Gambia

  Mwandishi wa BBC Thomas Fessy, ambaye yupo Banjul, anasema Yahya Jammeh, ambaye alikuwa amepewa hadi saa sita mchana (saa tisa Afrika Mashariki) kuachia madaraka, ameomba aongezewe muda. Ameomba apewe hadi saa kumi alasiri saa za Gambia (16:00 GMT).  

 13. Jammeh 'huenda akenda Guinea'

  Mwandishi wa BBC Umaru Fofana anasema amewasili ikulu ya Gambia akiandamana na marais wa Guinea na Mauritania.

  Muda wa mwisho uliotolewa na Ecowas kwa Jammeh kuondoka madarakani umeongezwa kutoa fursa ya kufanyika kwa mazungumzo.

  Fofana amesema duru zinadokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Jammeh kuondoka na kwenda Conakry, Guinea leo. Watu wamejitokeza barabarani na wanainua mikono na kuimba "amani".

 14. Jammeh hajafika kumlaki Abdul Aziz

  Yahya Jammeh hajafika uwanja wa ndege kumlaki Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdul Aziz. Aidha, hakumlaki mjumbe wa UN Afrika Magharibi.

 15. Ndege ya rais wa Mauritania ikitua Banjul

 16. Habari za hivi pundeWanajeshi wa Ecowas kusubiri mazungumzo

  Muda wa Yahya Jammeh kuachia madaraka kwa Amani umepita.

  Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba wanajeshi wa Ecowas watasubiri mazungumzo yafanyike kati ya Yahya Jammeh na marais wa Mauritania na Guinea.

  Mwandishi wa BBC anasema ndege ya rais wa Mauritania imetua Banjul.

 17. Jammeh ataongezewa muda?

  Marais wa Mauritania na Guinea, ambao wanatarajiwa kujaribu kumshawishi, kwa mara ya mwisho, Rais Yahya Jammeh kuondoka kwa amani, wanatarajiwa kuwasili Banjul.

  Hii ina maana huenda muda aliopewa Jammeh kuondoka madarakani ukaondoka kutoa fursa kwa mashauriano kufanyika.

  Kuna zulia jekundu na magari ya kirais ya Rolls Royce uwanjani Banjul kuwasubiri marais hao, kama unavyoona pichani.

  Banjul
  Gari
  Gari
 18. Habari za hivi pundeNdege ya rais wa Mauritania yatua Banjul

  Ndege ambayo inatumiwa na rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz imewasili uwanja wa ndege wa Banjul. Tayari ni saa sita nchini Gambia, muda wa mwisho uliotolewa kwa Rais Yahya Jammeh kung'atuka.

 19. Marais wanataka kuondoka na Jammeh

  Jammeh

  Wanahabari mjini Banjul wanaripoti kuwa marais wa Mauritania na Guinea watamwambia Yahya Jammeh kwamba lazima aondoke nao kwa ndege watakayokuwa wanatumia, la sivyo aondolewa kwa nguvu.

  Mwenyekiti wa tume ya Ecowas Marcel de Souza, amesema majeshi ya muungano huo yataingilia kati “asipokubali kuondoka Gambia”.

  Jammeh ameahidiwa hifadhi Nigeria na Morocco.

  Mke wa Jammeh, Zineb alizaliwa nchini Morocco – babake ni mzaliwa wa Guinea na mamake raia wa Morocco.

  Jammeh anadaiwa kuwa bado ikulu na mkewe na mwana wao wa kiume.

  Haijabainika hatima ya Jammeh itakuwa gani iwapo atakamatwa na wanajeshi wan chi jirani.

  Wiki iliyopita, Barrow aliambia BBC kwamba hakuna haja ya Jammeh kutafuta hifadhi nje ya nchi.

  „Twamtaka Jammeh awe Gambia, sidhani anahitaji kwenda nchi nyingine,” alisema.

  Alhamisi, msemaji wa Barrow, Halifa Sallah, alisema Jammeh hafai kushtakiwa kwa makosa aliyotekeleza tangu achukue madaraka kupitia mapinduzi yasiyokuwa na umwagikaji wa damu mwaka 1994.

  Bw Sallah alisema pia kuwa Jammeh atajivunia hadhi inayopewa viongozi wa zamani.

 20. Jina na sifa nyingi za Yahya Jammeh

  Yahya Jammeh anafahamika sana kwa kujilimbikizia sifa. Amekuwa akijiongezea sifa hizo kwenye jina lake rasmi.

  Mwaka 2015, alijiongezea  Babili Mansa kwenye jina lake rasmi.

  Kulingana na kabila la Mandika jina hilo lina maana ya 'mjenzi daraja mkuu' ama 'mshindi wa mito'.

  Jina lake kamili likawa Mtukufu Sheikh Profesa Alhaji daktari Yahya AJJ Jammeh Babili Mansa.

  Soma zaidi: Rais wa Gambia aongezewa jina jingine