Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Maandamano yafanyika kote Marekani

   Maandamano ya kumpinga Trump yamefanyika kote nchini Marekani

  Huko San Francisco, waandamanaji waliunda minyororo ya watu kwenye daraja la Golden Gate.
  Huko Seattle, wanafunzi waliandamana barabarani .
  Waandamanaji walibeba mabango Los Angeles
 2. Gari lachomwa Washington

  Gari ambalo lilihariwa mapema na waandamanaji sasa limechomwa moto Washington.

  Kwa sasa wazima moto wanauzima moto huo. Moto umewashwa sehemu tofauti kote mjini humo wakati Rais Trump anaelekea Ikulu ya White House

 3. Rais Trump na mkewe watembea kwa miguu

  Rais mpya wa Marekani Donald Trump na mkewe Melanie wanatembea kwa miguu wakielekea kazi yao mapywa katika barabara ya Pennsylvania . 

   Kama ilivyo ada wakati wa kuapishwa kwa marais nchini Marekani, hutembea katika barabara hiyo wakiwa na mwana wao Barron kutoka katika gari la the Beast.

  Donald Trump mkewe Melnaie na mwana wao barron wakitembea katika barabara ya Pennsylvania
  Image caption: Donald Trump mkewe Melnaie na mwana wao barron wakitembea katika barabara ya Pennsylvania
 4. Msafara wa Trump waelekea Ikulu ya Whitehouse

  Msafara wa rais Donald Trump's presidential motorcade unaelekea katika ikulu ya rais ukishangiliwa na idadi kubwa ya wafuasi wake waliosimama kandakando ya barabara.

  Trump yuko ndani ya gari lake la The Beast.

  Msafara wa Donald Trump
  Image caption: Msafara wa Donald Trump
  Gari la The beast
  Image caption: Gari la The beast
 5. Maandamano ya kumpinga Trump yafanyika duniani

  Maafisa wa polisi mjini Washington DC wameambia BBC kwamba takriban waandamanji 95 wanaopinga kuapishwa kwa Donald Trump wamekamatwa kufikia sasa.

  Maafisa wawili wa polisi wamejeruhiwa lakini hawana majeraha mabaya.

  Maafisa wote wawili wamesafrishwa katika eneo la matibabu ,lakini afisa anayezungumza na vyombo vya habari hajui ni wapi. 

  Katika mji mkuu wa Uhispania Madrid, waandamanaji walibeba mabango wakimtaja barrack Obama kama 'matumaini na Donald Trump ''Chuki.

  Katika mji mkuu wa Peru ,Lima ,waandamanaji walimshutumu msimamo wa Trump kuhusu haki za wanawake.

   Mjini Hong Kong , mwanadamanji mmoja alijifunga kwa nyororo katika lango kuu la ubalozi wa Marekani lakini akaondolewa na polisi.

  takriban waandamanji 95 wanaopinga kuapishwa kwa Donald Trump wamekamatwa
  Image caption: Takriban waandamanji 95 wanaopinga kuapishwa kwa Donald Trump wamekamatwa
  Katika mji mkuu wa Uhispania Madrid, waandamanaji walibeba mabango wakimtaja barrack Obama kama 'matumaini na Donald Trump ''Chuki.
  Image caption: Katika mji mkuu wa Uhispania Madrid, waandamanaji walibeba mabango wakimtaja barrack Obama kama 'matumaini na Donald Trump ''Chuki.
  Katika mji mkuu wa Peru ,Lima ,waandamanaji walimshutumu msimamo wa Trump kuhusu haki za wanawake.
  Image caption: Katika mji mkuu wa Peru ,Lima ,waandamanaji walimshutumu msimamo wa Trump kuhusu haki za wanawake.
  Mjini Hong Kong , mwanadamanaji mmoja alijifunga kwa nyororo katika lango kuu la ubalozi wa Marekani lakini akaondolewa na polisi.
  Image caption: Mjini Hong Kong , mwanadamanaji mmoja alijifunga kwa nyororo katika lango kuu la ubalozi wa Marekani lakini akaondolewa na polisi.
 6. Ushauri wa Papa kwa Donald Trump

  Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis alisema katika ujumbe wake kwa rais mpya wa Marekani Donald Trump baada ya kuapishwa kwamba anafaa kuwahudumia masikini na aongozwe na maadili mema.

   ''Chini ya uongozi wako, naomba heshima ya Marekani iimarishwe kwa kuwaangazia masikini , wakiwa na wale wanaohitaji hudumu''. Mnamo mwezi Febnruari 2016 Trump alimuita Pope mwenye aibu baada ya kiongozi huyo wa dini kusema kuwa kujenga ukuta sio Ukristo.

  Matamshi hayo yalionekana kama pingamizi ya hatua ya Trump kutka kujenga ukutaka kati ya mpaka wa Marekani na Mexico.

  Kiongozi wa kanisa katoliki katika ujumbe wake kwa Donald Trump
  Image caption: Kiongozi wa kanisa katoliki katika ujumbe wake kwa Donald Trump
 7. Trump amshukuru Clinton

  Wengine wamelalama kwamba Trump alifaa kumtaja mpinzani wake Hillary Clinton katika hotuba yake , kufuatia hatua yake ya kuhudhuria kuapishwa kwake.

   Lakini kulingana na gazeti la Washinton Post ,wakati yeye na rais Bill Clinton walipowasili katika eneo hilo la kuapishwa kwa Trump,Trump alienda hadi katika meza ya familia ya Clinton na kumsalimia kwa mkono.  

  Ahsante kwa kuhudhuria,Trump anadaiwa kumnong'onezea.

  Trump amshukuru Clinton
  Image caption: Trump amshukuru Clinton
 8. Trump atumia akaunti rasmi ya Twitter @POTUS

  Trump hatimaye amechapisha ujumbe wake wa kwanza kwa kutumia akaunti rasmi ya rais wa Marekani @POTUS.

  Hii ni mara ya kwanza kwa akaunti hiyo kuhamishwa rasmi kwa kuwa hakuna rais kabla ya Obama aliyekuwa na uwepo wake katika mitandao ya kijamii.

  Trump hatimaye amechapisha ujumbe wake wa kwanza kwa kutumia akaunti rasmi ya rais wa Marekani
  Image caption: Trump hatimaye amechapisha ujumbe wake wa kwanza kwa kutumia akaunti rasmi ya rais wa Marekani
 9. Vifo vyaripotiwa katika mkutano wa Trump Nigeria

  Polisi walirusha vitoa machozi katika mkutano nchini Nigeria ulioandaliwa kuonyesha uungaji mkono wa rais mpya wa Marekani Donald Trump.

   Kundi moja linalotaka kujitenga limesema kuwa watu 11 wamefariki lakini polisi wamekana kwamba hakuna mtu aliyefariki.

   Maandamano hayo yaliandaliwa katika jimbo la Southern River na wanaharakati ambao wanamtaka Trump kuunga mkono uanzilishi wa jimbo huru la Biafra kwa watu wa Igbo.

  Maandamano katika mkutano wa Trump Nigeria
  Image caption: Maandamano katika mkutano wa Trump Nigeria
 10. Trump achukua afisi na kuanza kusaini maagizo ya rais

  Huku aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama akiendelea kuzungumza na wafuasi wake ,rais mpya Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais ,baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale yalioafikiwa na rais Obama.

  Video content

  Video caption: Trump atia saini maagizo rasmi Marekani
 11. Obama awashukuru wafuasi wake

  "Tulipoanza safari hii ,tulifanya hivyo kwa imani ya raia wa Marekani  uwezo wao, uwezo wetu wa kuungana na kulibadilisha taifa hili.

  Tulijua kwamba mabadiliko hayakufanyika kutoka juu kwenda chini bali chini kwenda juu''.

 12. Trump atumia akaunti binafsi ya Twitter

  Badala ya kutumia akaunti yake mpya ya mtandao wa Twitter ya @POTUS ,rais mpya wa Marekani Donald Trump ametumia akaunti yake binafsi ya @DonaldTrump kuchapisha baadhi ya vipande vya hotuba yake.

  Twitter
  Image caption: Twitter
 13. Sanamu ya Trump yachomwa Canada

  Maandamano ya umoja dhidi ya Donald Trump yaendelea nchini Canada.

   Hii hapa picha kutoka Montreal

  sanamu ya Trump yachomwa na waandamanaji Canada
  Image caption: Sanamu ya Trump yachomwa na waandamanaji Canada
 14. Kwaheri Obama

  Obama na mkewe tayari wamepanda ndege ya kijeshi ambayo inawapeleka hadi katika kambi ya kijeshi ya Andrew Air base.

   Wakiwa huko watapanda ndege inayoelekea California kwa likizo.

   Huku Obama akiondoka ,alisalimiana kwa mkono na rais Donald Trump na mkewe na pia kuwashukuru walinzi wake. 

  Joe Biden na mkewe watapanda treni ambayo itawapaleka nyumbani kwao Delaware ambako ni umbali wa saa mbili.

  Ndege iliombeba Obama yaondoka
  Image caption: Ndege iliombeba Obama yaondoka
 15. Trump: Uwe mweupe au mweusi sote ni watu wamoja

  'Uwe mweusi, mweupe ama udhurungi sote hutokwa na damu nyenkundu' 

 16. Melania akabidhiwa @FLOTUS

  Melania Trump amekabidhiwa ukurasa rasmi wa mke wa rais @FLOTUS ambao umekuwa ukitumiwa na Michelle Obamap.

  Michelle Obama sasa atakuwa anatumia @FLOTUS44

  FLOTUS
 17. Trump: Nitaunganisha dunia dhidi ya ugaidi

  "Tutaunganisha ulimwengu dhidi ya ugaidi ,ambao tutauangamiza kabisa duniani.

 18. Trump: 'Wakati wa maneno matupu umekwisha'

  "Ni lazima tufikiri sana na kuwa na ndoto kubwa.

   Sitakubali wanasiasa amba huzungumza sana bila kuwatendea . 

   Wakati wa mazungumzo matupu umekwisha ,masaa ya kufanya vitendo yamewadia.

   Usikubali mtu akwambia kwamba haiwezi kufanyika''.

  Hotuba ya Trump
  Image caption: Hotuba ya Trump
 19. Trump: kuanzia leo itakuwa Marekani kwanza ,Marekani kwanza

  Trump ameahidi kwamba  kazi na elimu zitapatiwa kipau mbele katika utawala wake.

  "Tumeyafanya mataifa maengine kuwa tajiri,dhabiti .Moja baada ya nyengine viwanda vyetu vimeondoka 

  Kutoka siku hii ya leo itakuwa Marekani  kwanza ,Marekani Kwanza

  Donald Trump akitoa hotuba baada ya kuapishwa
  Image caption: Donald Trump akitoa hotuba baada ya kuapishwa
 20. Tutaifanya Marekani kuwa taifa kuu tena

  Pamoja, tutaifanya Marekani kuwa taifa kuu tena. Tutaifanya kuwa taifa tajiri tena. Ijionee fahari tena, tutaifanya salama tena. Na ndio, pamoja, tutaifanya Amerika kuwa taifa kuu tena.