Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Muungano wa upinzani Nasa umepinga matokeo yanayotangaza na kusema IEBC imekuwa ikitangaza matokeo bila kutoa fomu 34A
 2. Kumekuwa wagombea urais wanane, lakini ushindani mkubwa ulikuwa kati ya Rais Kenyatta na Bw Raila Odinga
 3. Matokeo yaliyotolewa kufikia sasa yanaonyesha Bw Kenyatta ana kura 7m naye Bw Odinga kura 5.6m.
 4. Bw Odinga anawania urais kwa mara ya nne.
 5. Kulikuwa na jumla ya vituo 40,883 vya kupigia kura kote nchini

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufikia sasa

Imepakiwa mnamo 21:15

Katika matokeo ya awali ya vituo 39620 out of 40883 yaliyopakiwa na IEBC mtandaoni:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 8009175 votes (54.31%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 6608405 votes (44.81%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 393969

IEBC: Mfumo wetu wa matokeo haukudukuliwa

Tume ya uchaguzi nchini Kenya imesema kuwa mfumo wake wa kutoa matokeo haukudukuliwa kama ilivyodaiwa na upinzani.

Mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba amesema kuwa madaia yaliotolkewa na mgombea wa upinzani Raila Odinga hayana msingi wowote.

Amesema kuwa tume hiyo imefanya uchunguzi kubaini hayo.

Ameongezea kuwa kufikia sasa wamepokea fomu 29,000 34A na kwamba wanatarajia fomu zote 40,000 kufikia kesho alfajiri.

Vilevile ameongezea kuwa upigaji kura umkamilika katika vituo vyote nchini

Mkurugenzi wa IEBC Ezra Chiloba
Getty Images
Mkurugenzi wa IEBC Ezra Chiloba

John Kerry na maafisa wa IEBC

Aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry akimsikiliza afisa mmoja wa uchagui nchini Kenya.

Wengine ni makamishna wa IEBC na wawakilishi wa vyama vya kisiasa.

John Kerry na maafisa wa IEBC
BBC
John Kerry na maafisa wa IEBC

AU yapongeza IEBC kwa uchaguzi Kenya

Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC inaonekana ilitekeleza majukumu yake kulingana na sheria, mkuu wa kundi la waangalizi wa Umoja wa Afrika ,Thabo Mbeki amesema.

Mbeki ambaye alikuwa rais wa Afrika Kusini aliongezea kuwa mahakama ya Kenya imejiandaa kukabiliana na mgogoro utakaozuka katika uchaguzi huo.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amedai kwamba mfumo wa kidijitali wa tume hiyo ulidukuliwa , na matokeo kuvurugwa ili kumpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Tume ya IEBC imeahidi kuchunguza madai hayo

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki
BBC
Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki

Uchaguzi Kenya: Hakuna matokeo ya mwisho usiku wa leo

Tume ya uchaguzi nchini Kenya imewashauri raia kupuuzilia mbali madai ya uwongo yanayosambazwa kupitia ujumbe kwamba matokeo ya uchaguzi huo wa urais yatachapishwa usiku wa leo

Ujumbe wa Twitter
Twitter
Ujumbe wa Twitter

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufikia sasa

Katika matokeo ya awali ya vituo 39091 kati ya 40883 yaliyopakiwa na IEBC mtandaoni:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,977,905 (54.32%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 6,578,586 (44.79%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 387,959.

Mtu mmoja afariki katika maandamano Kenya

Mtu mmoja ameuawa katika makabiliano na maafisa wa polisi katika ngome ya upinzani ya Mathare katika mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya, walioshuhudia wameambia BBC.

Risasi zilifyatuliwa wakati wa makabiliano hayo kulingana na walioshuhudia.

Kitengo cha habari cha AFP kilimnukuu afisa mmoja wa polisi aliyesema kuwa watu wawili waliuawa.

''Walikuwa miongoni mwa kundi la waandamanaji katika eneo hilo na maafisa walitumwa kuzima ghasia hizo'', afisa huyo aliambia AFP.

''Tumeambiwa kwamba wengi wao walikuwa wezi ambao walitumia fursa hiyo na hawakuweza hata kuwaheshimu polisi''.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa uchaguzi huo umefanyiwa udanganyifu ili kumpokonya ushindi.

Baadhi ya waandamanaji wanaopinga matokeo ya uchaguzi Kenya
EPA
Baadhi ya waandamanaji wanaopinga matokeo ya uchaguzi Kenya

Je fomu 34A na 34B ni zipi?

Kukataliwa kwa matokeo ya uchaguzi katika tovuti ya tume ya uchaguzi nchini Kenya kwa mara nyengine tena kumezua majina ya fomu zinazotumiwa katika kunakili matokeo ya uchaguzi.

Fomu zilizotajwa na mgombea wa upinzani wa Nasa Raila Odinga ni zile za 34A na 34B.

Katika kuyakataa matokeo hayo ya IEBC katika mtandao wake bwana Odinga alisema kuwa fomu 34A na 34B lazima zitolewe.

IEBC imesema kuwa maajenti wa mgombea huyo wa urais wataonyeshwa fomu 34A.

Je hizi ni fomu gani?

Chini ya sheria ya uchaguzi, fomu 34A ndio fomu ya kwanza inayotumika kunakili matokeo ya uchaguzi wa urais.

Fomu hiyo hujazwa na afisa wa tume ye uchaguzi anayesimamia uchaguzi huo kwa jina la Presiding officer baada ya kuhesabiwa kwa kura katika kituo cha kupigia kura.

Fomu hiyo huwa na maelezo kuhusu kura zilizohesabiwa za kila mgombea mbali na kuwa na idadi ya wapiga kura katika kituo hicho, kura zilizoharibika, zile zilizo na utata na kura zilizokubalika.

Mgombea ama ajenti wake baadaye hutakiwa kutia saini ili kuthibitisha kwamba yaliomo ndani ya fomu hiyo ni sahihi.

Kifungu cha 39 cha uchaguzi kinasema kuwa ili kufanyika kwa uchaguzi wa urais tume ya uchaguzi itatoa matokeo hayo kielektroniki baadaye kuyasafirisha kutoka katika kituo cha kupigia kura hadi katika kituo cha kuhesabia kura cha eneo bunge na baadaye katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura.

Form 34A hupewa afisa anayesimamia uchaguzi katika eneo bunge ambaye hujaza fomu 34B.

Hutumika kuonyesha matokeo ya kura ya urais.

Fomu hiyo huonyesha nambari ya kituo cha kupigia kura, jina la kituo cha kupigia kura, idadi ya watu waliojisajiliwa kupiga kura katika kituo hicho, matokeo ya kila mgombea na idadi ya kura zilizokubalika.

Afisa anayesimamia shughuli ya uchaguzi katika eneo bunge kwa jina Returning officer humpelekea fomu hiyo mwenyekiti wa tume ya auchaguzi IEBC ambaye ndio afisa mkuu wa matokeo ya uchaguzi wa urais.

Katika mkutano na vyombo vya habari makamu wa mwenyekiti wa tume ya IEBC Consolata Maina amesema kuwa fomu hiyo ndio itabaini ni nani mshindi wa kura ya urais.

Sheria inaruhusu kuipata fomu 34B kutoka kwa kila Retuning officer kabla ya kutangaza matokeo.

''Utangazaji wa matokeo unategemea fomu 34B ambayo tutapata kutoka kwa Retuning Officers'', alisema bi Maina.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati
Getty Images
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufikia sasa

Katika matokeo ya awali ya vituo 39091 kati ya 40883 yaliyopakiwa na IEBC mtandaoni:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,915,044 (54.35%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 6,520,918 (44.78%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 387,959.

Tume ya uchaguzi yaweka wazi fomu za matokeo

Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya imekubali kutoa fomu za matokeo ya vituo vya kupigia kura maarufu kama Fomu 34A.

Muungano wa upinzani ulikuwa umelalamikia kukosekana kwa fomu hizo na kusema ilikuwa vigumu kukagua matokeo yaliyokuwa yakipeperushwa katika mtandao wa tume hiyo.

Mwenyekiti wa tume hiyo Bw Wafula Chebukati amewaambia wanahabari kwamba meza maalum itatengwa katika kituo kikuu cha kujumlishia matokeo ukumbi wa Bomas, Nairobi kwa ajili ya maajenti wa vyama ambao wangependa kukagua fomu hizo

Aidha, ameongeza kwamba fomu hizo zitapakiwa kwenye tovuti ya tume hiyo. Tayari baadhi zimeshapakiwa.

View more on twitter

Polisi wakabiliana na waandamanaji Mathare

Tumepokea picha za polisi wa kupambana na fujo wakijaribu kuzima maandamano katika ngome ya upinzani katika mtaa wa Mathare, Nairobi.

Mathare
Reuters
Mathare
Reuters
Mathare
Reuters

Polisi wamekuwa wakisaidia pia kuzima maandamano mjini Kisumu ambapo baadhi ya wakazi walikuwa wamefunga barabara na kuwasha moto matairi.

Maandamano Kisumu
Reuters
Kisumu
Reuters
Kisumu
Reuters

Waziri apuuzilia mbali madai ya maandamano na fujo

Kaimu waziri wa usalama Dkt Fred Matiang'i amepuuzilia mbali taarifa ambazo amesema zinaenezwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna maandamano na fujo katika baadhi ya maeneo Kenya.

Amesema taarifa hizo hazina msingi wowote.

"Iwapo kungekuwa na jambo, mkuu wa polisi ndiye huyu hapa angekuwa wa kwanza kujua," amesema Dkt Matiang'i.

Mwandishi wa BBC Odeo Sirari aliyepo mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya hata hivyo anasema muda mfupi uliopita polisi wamekabiliana na vijana waliokuwa wakiandamana katika barabara ya Manyatta katika mtaa wa Kondele na eneo la Kibos.

Amepiga picha hizi:

Kondele
BBC
Moto
BBC
Maji
BBC

Chebukati: Tutachunguza madai ya Nasa kuhusu udukuzi

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amewaambia wanahabari baadaye kwamba wamepata habari kuhusu tuhuma za muungano huo wa upinzani kwamba mitambo yao ya uchaguzi ilidukuliwa.

Amesema tume haiwezi kupuuza tuhuma kama hizo na kwamba maafisa wake watafanya uchunguzi kubaini iwapo kuna ukweli wowote katika madai hayo.

Hata hivyo alieleza imani yake kwamba mfumo wa uchaguzi unaotumiwa na tume hiyo ni imara na kwamba ulitumiwa na shughuli zote za awali, na sasa "imesalia shughuli ya mwisho" ya kupeperusha na kutangaza matokeo ya kura.

Matokeo ya urais ya hivi punde zaidi Kenya

Katika matokeo ya vituo 38249 kati ya 40883:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,757,201 (54.4%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 6,380,316 (44.74%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 353,389.

Odinga: Mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa

Mgombea urais wa muungano wa upinzani Nasa Raila Odinga amewaambia wanahabari kwamba wamepata habari kwamba mitambo ya Tume ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo halisi kufanyiwa ukarabati.

Bw Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, amesema wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya IEBC.

Waziri huyo mkuu wa zamani amesema baada ya kuingia, wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na kupunguza matokeo yake.

Amesema anaamini hilo lilifanyika katika kaunti zote na kwamba wagombea wa NASA katika nyadhifa nyingine waliathirika pia.

Bw Odinga, amesema huo ulikuwa "ulaghai wa hali ya juu".

Hata hivyo, ametoa wito kwa wafuasi wa muungano huo waendelee kuwa watulivu.

Bw Musyoka amesema anawashauri wafuasi wa muungano huo waendelee na shughuli zao za kawaida, ingawa huenda karibuni wakatakiwa kuchukua hatua.

Bw Odinga na Kalonzo wamekataa kusema ni hatua gani zaidi watachukua na badala yake wakasema wanasubiri kusikia ufafanuzi kutoka kwa IEBC kuhusu yaliyotokea.

Jubilee yasema madai ya upinzani hayana ukweli

Raphael Tuju
BBC

Katibu mkuu wa chama cha Jubilee chake Rais Uhuru Kenyatta, Bw Raphael Tuju, ameambia wanahabari kwamba madai ya muungano wa upinzani Nasa kwamba matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi IEBC hayaeleweki si ya kweli.

Bw Tuju amesema upinzani unafaa kukubali kwamba haukufanya vyema katika uchaguzi uliofanyika Jumanne.

Amesema katika kaunti zote ambazo Bw Kenyatta alishinda mwaka 2013, hakuna kaunti hata moja ambayo ameipoteza kwa upinzani.

Badala yake, amesema chama hicho kilifanikiwa kupata uungwaji mkono maeneo ambayo hakikufanya vyema uchaguzi uliopita mfano Nyamira na Kisii, wakati huu Jubilee walifanya vyema.

Upinzani ulikuwa umelalamika kwamba IEBC imekataa kutoa Fomu 34A za kuthibitisha matokeo ya urais kutoka vituo vya kupigia kura.

Lakini Bw Tuju amesema: "IEBC wamewezesha maafisa wetu wa kiufundi kupata Fomu 34A. Wanazichunguza kwa makini. sible for our technical team to access Form 34A. Fomu hizo ambazo tunazo, Nasa wanazo na IEBC wanazo zinafaa kuwa na maelezo sawa."

Matokeo ya urais ya hivi punde zaidi Kenya

Katika matokeo ya vituo 36659 kati ya 40883:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,461,933 (54.64%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 6,079,136 (44.51%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 353,389.

Yasemavyo magazeti nchini Kenya

Wakenya wanapoendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumanne, hivi ndivyo vichwa vya habari vya magazeti vinavyosema:

Magazeti Kenya
BBC

Matokeo ya urais ya sasa hivi

Katika matokeo ya vituo 35095 kati ya 40883:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,163,684 (54.82%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 5,794,443 (44.34%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 338,584

Wasimamizi wa uchaguzi wasubiri kuwasilisha matokeo Kisumu

Mwandishi wa BBC Odeo Sirari, ambaye amekuwa katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya anasema wasimamizi wa uchaguzi katika eneo bunge la Kisumu ya Kati bado wanasubiri kupeperusha matokeo ya kura kutoka eneo hilo.

Pichani hapa chini ni masanduku ya kupigia kura yakiwa katika kituo cha kujumlishia matokeo cha eneo bunge hilo katika shule ya upili ya Lions High.

Lions High
BBC

Kenyatta afikisha kura 7 milioni uchaguzi wa urais Kenya

Katika matokeo ya vituo 34713 kati ya 40883:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,092,508 (54.89%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 5,721,889 (44.28%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 331,846.

Matokeo ya uchaguzi wa urais Kenya kufikia sasa

Tume ya uchaguzi imetangaza matokeo kutoka kwa vituo 34,180 kati ya jumla ya vituo 40883 ambapo:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 6,998,750 (55.01%)
 • Raila Odinga wa ODM kura 5,619,817 (44.17%)
 • Joseph Nyagah (huru) 31,107 (0.24%)
 • Abduba Dida wa ARK 26,000 (0.2%)
 • Ekuru Aukot wa Thirdway Alliance 22,101 (0.17%)
 • Japheth Kaluyu (huru) 9,445 (0.07%)
 • Cyrus Jirongo wa UDP 9,129 (0.07%)
 • Michael Wainaina (huru) 6,967 (0.05%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 326,001

Matokeo ya hivi punde ya urais Kenya

Matokeo yaliyotolewa kwa sasa ni kutoka vituo 34016 kati ya jumla ya vituo 40883.

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 6,971,985 (55.05%)
 • Raila Odinga wa ODM kura 5,589,069 (44.13%)

Matokeo ya urais Kenya yaliyotangazwa hivi punde

Matokeo ya vituo 33274 kati ya 40883 yanaonesha:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 6,828,935 (55.14%)
 • Raila Odinga wa ODM kura 5,454,180 (44.04%)

Matokeo ya urais ya sasa hivi

Katika matokeo ya vituo 32218 kati ya 40883:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 6627485 (55.21%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 5279763 (43.98%)

Matokeo ya uchaguzi wa urais Kenya kufikia sasa

Tume ya uchaguzi imetangaza matokeo kutoka kwa vituo 31947 kati ya jumla ya vituo 40883 ambapo:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 6,574,087 (55.21%)
 • Raila Odinga wa ODM kura 5236724 (43.98%)
 • Joseph Nyagah (huru) 29163 (0.24%)
 • Abduba Dida wa ARK 23318 (0.2%)
 • Ekuru Aukot wa Thirdway Alliance 20700 (0.17%)
 • Japheth Kaluyu (huru) 8806 (0.07%)
 • Cyrus Jirongo wa UDP 8521 (0.07%)
 • Michael Wainaina (huru) 6519 (0.05%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 307,252

IEBC: Changamoto za kupeperusha matokeo zimetatuliwa

Afisa mkuu mtendaji wa IEBC amesema matatizo yaliyoshuhudiwa mwanzoni wakati wa kupeperushwa kwa matokeo yalitokana na kufurika kwa matokeo kutoka vituoni.

“Kulikuwa na vituo 28,000 vilivyokuwa vinawasilisha matokeo kutoka nyanjani. Upande wa kuonesha matokeo kukawa na tatizo. Lakini sasa tatizo hilo limetatuliwa kwa kiasi kikubwa. Baada ya muda, hilo halitakuwa tatizo tena,” alisema Bw Chiloba.

Afisa huyo alisema pia kwamba baada ya vituo vyenye huduma ya simu ya 3G kumaliza kutuma matokeo, vituo ambavyo vitakuwa vikituma matokeo baadaye sana itakuwa ni maandishi pekee pia Fomu za matokeo, ingawa fomu hizo zitapakiwa mtandaoni baadaye.

Alisema hata hivyo, kwa sababu maafisa wa uchaguzi huenda wakalazimika kusafiri hadi maeneo yenye huduma nzuri ya simu, upeperushaji wa matokeo hayo huenda ukachukua muda kidogo.

Tume hiyo imesema itasubiri matokeo yote, kabla ya kutangaza mshindi wa urais.

Aidha, matokeo hayo yatatangazwa kwa kufuata fomu za matokeo kutoka kwa wasimamizi wa matokeo.

Matokeo ya karibuni zaidi ya urais Kenya

Matokeo ya tume ya uchaguzi ya vituo 30937 kati ya 40883 yanaonesha:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 6,381,173 (55.26%)
 • Raila Odinga wa ODM (Muungano wa Nasa) ana 5,072,881 (43.93%)

Odinga ayatakaa matokeo ya urais yaliyotangazwa na tume

Raila odinga
BBC
Odinga alipokuwa akipiga kura mtaa wa Kibera, Nairobi

Mgombea urais wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) Raila Odinga amepinga matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo, IEBC.

Bw Odinga amewaambia wanahabari kwamba tume hiyo imekuwa ikitangaza matokeo kwenye tovuti yake bila kufuata utaratibu ufaao.

Waziri mkuu huyo wa zamani amesema kabla ya matokeo yoyote kutangazwa, IEBC inafaa kuwapa maajenti wa vyama Fomu 34A kutoka vituoni.

Amesema kwa sasa, bila kuwepo kwa fomu hizo, ni vigumu kubaini matokeo yanayopeperushwa yanatoka wapi.

"Mfumo umeacha kufanya kazi. Sasa ni mitambo inayopiga kura. IEBC wamesema kwamba hakuna chama chochote kilichopinga matokeo. Lakini vyama vitapingaje matokeo bila kujua asili yake? Ni fomu 34A pekee zinazoonesha chanzo cha matokeo," amesema.

Soma zaidi hapa: Odinga apinga matokeo ya urais

Upinzani wapinga matokeo yanayotangazwa Kenya

Mudavadi
BBC

Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) umesema haujafurahishwa na matokeo ambayo yanaendelea kupeperushwa na tume ya uchaguzi IEBC kwa umma.

Mmoja wa viongozi wa muungano huo Musalia Mudavadi amewaambia wanahabari kwamba tume hiyo haifai kupeperusha matokeo ya uchaguzi wa urais bila kuwepo kwa Fomu 34A.

Matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa kutoka vituo 29209 kati ya 40883 yanaonesha Uhuru kenyatta anaongoza akiwa na kura 6044745 (55.27%) naye Bw Raila Odinga wa chama cha ODM anayeungwa mkono na Nasa wa pili akiwa na kura 4805159 (43.93%).

Tume ya uchaguzi ya Kenya muda mfupi awali, kwenye kikao na wanahabari, imesema baada ya kukutana na wadau wa vyama, iliamua kwamba itaendelea kuonesha matokeo yanavyopokelewa kutoka vituoni.

Maafisa wa tume hiyo wamesema kufikia sasa hakuna aliyepinga matokeo ambayo yamekuwa yakipeperushwa na tume hiyo.

Matokeo ya urais yaendelea kutolewa

Matokeo yanatolewa kwa kasi kiasi sasa, tayari yamebadilika sasa na hali ni kama ilivyo hapa chini. Haya ni matokeo ya vituo 29209 kati ya jumla ya vituo 40883

Matokeo
IEBC

Kenyatta akaribia kutimiza kura 6m

Kutoka kwa kura 10 840 719 zilizohesabiwa na kukubalika kufikia sasa, Uhuru Kenyatta anaendelea kuongoza kinyang'anyiro cha urais akiwa na kura 5,989,509 (55,25%) dhidi ya mpinzani wake wa karibu Raila Odinga aliye na kura 4,764,577 kufikia sasa (43,95%).

Matokeo
IEBC

Kinyang'anyiro cha urais kufikia sasa Kenya

Tume imetangaza matokeo ya vituo 28172 kati ya jumla ya vituo 40883.

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 5,832,837 (55.18%)
 • Raila Odinga wa ODM 4,652,710 (44.02%)
 • Abduba Dida wa ARK 18,924 (0.18%)
 • Japheth Kaluyu (huru) 7,834 (0.07%)
 • Michael Wainaina (huru) 5,789 (0.05%)
 • Joseph Nyagah (huru) 26,069 (0.25%)
 • Ekuru Aukot wa Thirdway Alliance 18,373 (0.17%)
 • Cyrus Jirongo wa UDP 7,520 (0.07%)

Kenyatta aendelea kupanua uongozi Kenya

Katika matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa, Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee anaongoza akiwa na kura 5,743,793 (55.25%).

Mpinzani wake mkuu Raila Odinga wa muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) ana kura 4,568,561 (43.95%).

Matokeo hayo ni ya vituo 27683 kati ya 40,883. Kura zilizoharibika zimeongezeka pakubwa na kufikia 260588.

.

Matokeo ya urais kufikia sasa

Matokeo ya vituo 27016 kati ya jumla ya vituo 40883

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 5,602,722 (55.22%)
 • Raila Odinga wa ODM ana 4,462,244 (43.98%)

Matokeo ya karibuni zaidi uchaguzi wa urais Kenya

Baada ya matokeo ya vituo 26279 kati ya vituo 40883 kutangazwa:

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 5,447,235 (55.21%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 4,340,806 (44%)

Habari za hivi pundeMatokeo ya punde zaidi kutoka IEBC

Matokeo ya vituo 17051 kati ya 40883.

Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 3,336,790 (54.86%)

Raila Odinga wa ODM 2,699,908 (44.39%)

Kura ambazo zilikuwa zimeharibika kufikia sasa ni 149, 634.

Matokeo ya punde zaidi uchaguzi wa urais kenya

Matokeo ya vituo 9,405 kati ya 40,883

 • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 1,665,740 (55.39%)
 • Raila Odinga wa ODM ana kura 1,319,200 (43.87%)

Matokeo ya karibuni zaidi: Odinga na Kenyatta

Matokeo ya vituo 5455 kati ya jumla ya vituo 40883

 • Uhuru Kenyatta 904,477 (57.54%)
 • Raila Odinga 656293 (41.75%)

Habari za hivi pundeOdinga aongoza matokeo ya urais Arusha

Shughuli ya kuhesabu kura za Wakenya wanaoishi nje ya nchi, ambao wamepigia kura mjini Arusha, Tanzania imekamilika.

Raila Odinga amepata kura 92, naye Uhuru Kenyatta 68.

Ekuru Aukot wa Thirdway Alliance amepata kura 2.

Upigaji kura umekuwa ukifanyika Arusha, katika katika balozi za Kenya miji ya Dar es Salaam, Kigali, Kampala na Pretoria.