Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Mwenyekiti wa IEBC amemtangaza Rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais
 2. Bw Kenyatta alipata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27 ya kura zilizopigwa
 3. Bw Raila Odinga alipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74 ya kura zote zilizopigwa
 4. Waliojitokeza walikuwa 15,073,662 ambayo ni asilimia 78.91 kati ya 19m waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura
 5. Upinzani ulidai Alhamisi kwamba Raila Odinga alishinda uchaguzi na kuitaka tume imtangaze kuwa mshindi wa urais

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Mzozo kuhusu gavana wa Mombasa na cheti cha ushindi

Kumekuwepo na taarifa zinazoenezwa kwamba afisa mkuu wa uchaguzi Mombasa alikataa kumpa Gavana Ali Hassan Joho cheti cha ushindi.

Lakini Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) imepuuzilia mbali taarifa hizo.

Badala yake, IEBC imesema kuna mambo fulani ambayo hayakuwa yamekamilishwa na kwamba pande zote mbili zilikubaliana kukutana tena kwa hafla ya kukabidhi rasmi cheti leo saa nane adhuhuri.

View more on twitter

Kwaheri!

Ni hayo kwa sasa. Fuatilia yanayojiri baada ya Rais Kenyatta kutangazwa mshindi wa urais hapa: Hali baada ya Kenyatta kutangazwa mshindi

Kagame na Museveni wampongeza Kenyatta

Kiongozi wa Rwanda Paul Kagame, aliyeshinda uchaguzi wa urais nchini mwake hivi majuzi, amekuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza kumpongeza Bw Kenyatta baada yake kutangazwa kuwa mshindi wa urais.

Rais wa taifa jirani la Uganda Yoweri Museveni pia amempongeza Bw Kenyatta.

View more on twitter
View more on twitter
View more on twitter

Kenyatta: Nawashukuru wananchi kwa kuwa na imani nami

Rais Kenyatta, akihutubu baada ya kutangaza mshindi wa urais amewashukuru wananchi kwa kuwa na imani naye na serikali yake.

"Nawaahidi tutaendelea na kazi tuliyoianza. Nawashukuru sana Kenya. Kadhalika, naishukuru tume ya uchaguzi kwa kazi nzuri waliyoifanya," amesema.

"Nawapongeza wote walioshinda, na kwa walioshindwa pia tutaishi kupambana siku nyingine."

Kwa upinzani amesema: "Sisi si maadui, ni raia wa nchi moja. Kila shindano, kutakuwa na washindi na wanaoshindwa, lakini tutasalia kuwa Wakenya. Nawapa moyo wa ushirikiano, twafaa kuungana pamoja. Wakenya wanataka sisi tufaulu."

"Sana kwa Raila Odinga, namuomba yeye, wafuasi wake, wote waliochaguliwa kupitia upinzani, tutafanya kazi pamoja, tutashirikiana, tutakua pamoja na kuendeleza nchi pamoja."

"Kwa Wakenya wenzangu, uchaguzi huja na kuondoka lakini Kenya itaendelea kuwepo, tukumbuke daima kwamba sisi ni ndugu na dada. Jirani yako bado ni jirani yako. Tuendelee kudumisha amani. Hakuna haja ya fujo, sisi wanasiasa pia huja na kuondoka. Lakini jirani yako atabaki."

"Mengi zaidi tutasema kesho."

Habari za hivi pundeKenyatta atangazwa mshindi wa urais Kenya

Bw Wafula Chebukati amemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne.

Bw Kenyatta alipata kura 8,203,290 na angalau asilimia 25 ya kura katika kaunti 35.

Mwenyekiti huyo amekabidhi cheti cha ushindi kwa Bw Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto.

Habari za hivi pundeMatokeo ya uchaguzi wa urais Kenya

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati ametangaza matokeo ya uchaguzi wa urais kama ifuatavyo:

Jumla ya wapiga waliojiandikisha 19,611,423

 • Ekuru Aukot 27,311 (0.18)
 • Abduba Dida 38,093 (0.25)
 • Cyrus Jirongo 11,705 (0.08)
 • Japheth Kaluyu 16,482 (0.11)
 • Uhuru Kenyatta 8,203,290 (54.27)
 • Michael Wainaina 13,257 (0.09)
 • Joseph Nyagah 42,259 (0.28)
 • Raila Odinga 6,762,224 (44.74)

Chebukati arejea kusoma matokeo ya uchaguzi

Mwenyekiti wa IEBC amerejea jukwaani baada ya matokeo kutiwa saini na maajenti. Anasoma kura alizopata kila mgombea katika kila kaunti.

Amesema hilo ni takwa la kisheria.

Ameanza kusoma matokeo ya Kaunti nambari 1: Mombasa.

Chebukati: Nitarejea kutangaza matokeo

Bw Chebukati amesema mgombea anayetangazwa mshindi anafaa kuwa amepata asilimia 50 ya kura zilizopigwa na kura moja zaidi, na pia awe amepata asilimia 25 ya kura katika angalau nusu ya kaunti kote nchini, ambazo ni kaunti 24.

Kabla ya kutangaza matokeo, Bw Chebukati amesema sharti yatiwe saini na maajenti, na hapo ameahidi kurejea baadaye kutangaza matokeo.

Chebukati: Mpiga kura wa kawaida alipata usemi

Bw Chebukati amesema siku ya uchaguzi huwa muhimu sana, kwani ni dakika tano, ambazo mpiga kura wa kawaida hupata kupaza sauti usemi wake.

Amesema hilo lilifanyika siku ya uchaguzi.

Amewashukuru waangalizi wa uchaguzi ambao waliridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika, pamoja na wanahabari wa nchini na kimataifa.

Chebukati: Waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 78.91

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Wafula Chebukati kwa sasa anahutubu ukumbi wa Bomas.

Amesema tume ya uchaguzi imejifunza mengi sana.

Amesema idadi ya waliojitokeza kupiga kura Jumanne walikuwa 15,073,662 ambao sawa na asilimia 78.91 ya wapiga kura 19 milioni waliojiandikisha.

Habari za hivi pundeUpinzani wakosa kuafikiana na tume ya uchaguzi

Muungano wa upinzani umesema hauungi mkono tangazo ambalo litafanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Kenya.

Ajenti mkuu wa muungano huo Musalia Mudavadi amesema malalamiko yaliyowasilishwa na muungano huo kwa tume hayajashughulikiwa ipasavyo.

Bw Mudavadi amesema baada ya kukutana na tume hiyo, walifahamishwa kwamba baadhi ya mambo yao yatashughulikiwa baada ya matokeo kutangazwa.

"Mikutano ilikuwa kama shughuli ya uhusiano mwema tu," amesema.

Tume ilikuwa imewaalika maajenti wakuu kwa mkutano kabla ya kutoa tangazo saa moja unusu.

Lakini upinzani umesema hautashiriki katika kukubaliana na tangazo la tume hiyo.

Naibu ajenti wa muungano huo James Orengo ametilia shaka waangilizi ambao walikuwa wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Amesema waangalizi hao walifaa kuchunguzwa kwanza.

Bw Orengo amesema pia kwamba muungano huo haupangi kwenda kortini kupinga matokeo.

Ufafanuzi kuhusu Fomu 34A na Fomu 34B

Tangu kuanza kutangazwa kwa matokeo, kumekuwepo na mjadala kuhusu fomu za matokeo ya uchaguzi.

Kumekuwa na Fomu 34A na Fomu 34B na sasa kuna Fomu34C.

Tume ya uchaguzi imejaribu kufafanua. Fomu 34A ni ya matokeo ya vituoni, 34B ya matokeo katika ngazi ya eneo bunge na 34C katika ngazi ya taifa.

View more on twitter

Kenyatta kuhutubu moja kwa moja kupitia runinga

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutoa hotuba itakayopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga akiwa jumba la KICC, Nairobi.

Bw Kenyatta atatoa hotuba yake muda mfupi baada ya tangazo la IEBC, ambalo linatarajiwa kuwa la mshindi wa uchaguzi wa urais.

View more on twitter

Habari za hivi pundeTume ya uchaguzi kutoa tangazo saa moja unusu

Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Uchaguzi IEBC amesema maafisa wa tume hiyo watakutana na maajenti wakuu wa wagombea katika muda wa dakika 15 zijazo.

Ametangaza kwamba mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati atatoa tangazo saa moja unusu leo jioni.

Ingawa hajaeleza tangazo la Bw Wabukati litahusu nini, kumekuwa na matarajio kwamba huenda tume hiyo ikamtangaza mshindi wa urais leo.

Habari za hivi pundeRais Kenyatta awasili ukumbi wa KICC

Rais Uhuru Kenyatta ambaye aliwania urais kupitia chama cha Jubilee uchaguzi mkuu Jumanne amewasili katika jumba la KICC kwa mkutano wa chama hicho.

Polisi wakabiliana na wafuasi wa Odinga Kisumu

Polisi wa kukabiliana na ghasia wamekabiliana na vijana waliokuwa wameandamana na kufunga barabara katika mtaa wa Kondele mjini Kisumu.

Maeneo mengine ya mji huo ambao ni ngome ya mgombea wa upinzani Raila Odinga hayakuwa na watu wengi huku biashara nyingi zikifungwa.

Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema polisi walifyatua risasi halisi hewani kujaribu kuwatawanya waandamanaji.

Maafisa wameingia pia katika baadhi ya mitaa kushika doria.

Tazama hali ilivyokuwa kupitia picha za Peter Njoroge.

Kisumu
BBC
Kisumu
BBC
Kisumu
BBC
Kisumu
BBC
Kisumu
BBC
Makabiliano Kisumu
BBC

Habari za hivi pundeIEBC: Twasubiri fomu za maeneo bunge mawili

Ezra Chiloba
Getty Images

Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Uchaguzi Ezra Chiloba amesema tume hiyo sasa imefanikiwa kupata fomu za matokeo kutoka maeneo bunge 288.

Amesema Fomu 34B za maeneo mawili bado haziko tayari. Hata hivyo amesema wameziona fomu hizo na wamewasiliana na wasimamizi wa uchaguzi maeneo hayo mawili.

Hata hivyo, kulikuwa na mambo yaliyofaa kufafanuliwa kwenye fomu hizo.

Bw Chiloba amewaomba Wakenya kuwa na subira.

"Ni muhimu zaidi tuwe sahihi kuliko kuharakisha," amesema.

Ameeleza kuwa tume itafanya kikao baadaye kikiongozwa na mwenyekiti Wafula Chebukati kutoa maelezo zaidi.

Taarifa ya IEBC yasubiriwa, Jubilee wajiandaa KICC

Tume ya uchaguzi ilikuwa imeahidi kutoa taarifa zaidi kuhusu fomu za matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo bunge ambazo zilikuwa bado hazijapokelewa kufikia sasa.

Hayo yakijiri, chama cha Jubilee kimeendelea kuandaa ukumbi wa mikutano wa KICC.

Wafuasi wa Jubilee wanaendelea kufika, na wengine wanatumia fursa hiyo kuuza bendera.

Jubilee
BBC
Bendera
BBC
Usalama umeimarishwa karibu na KICC
BBC
Usalama umeimarishwa karibu na KICC

Habari za hivi pundeNaibu Rais William Ruto awasili Bomas

Naibu Rais William Ruto, ambaye ni mgombea mwenza wa Rais Uhuru Kenyatta amewasili katika ukumbi wa Bomas.

Kalonzo Musyoka awasili Bomas

Kalonzo
BBC

Mgombea mwenza wa urais wa Bw Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, amewasili katika ukumbi wa Bomas of Kenya unaotumiwa kujumlishia matokeo.

Taarifa zinasema pia kwamba Bw Odinga yuko Bomas ingawa hajaonekana.

Upinzani wasisitiza hawakubali matokeo ya IEBC

Oburu
BBC

Viongozi wa muungano wa upinzani Nasa, wakiwemo kakake mgombea urais Raila Odinga, Oburu Oginga, wamewahutubia wanahabari na kusisitiza kwamba hawayakubali matokeo ya awali yanayotangazwa na IEBC katika mtandao wake.

Habari za hivi pundeChebukati: Bado hatujatokea fomu kutoka maeneo 17

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Wafula Chebukati amesema tume hiyo kufikia sasa imepokea Fomu 34B, fomu za matokeo kutoka maeneo bunge kutoka maeneo 273.

Tume hiyo ilikuwa imetarajia kupokea fomu hizo kufikia saa sita leo mchana.

Matokeo kutoka kwa maeneo 17 bado yanasubiriwa, amesema akihutubia wanahabari Bomas.

Miongoni mwa maeneo ambayo matokeo hayajafika kwa tume ni Nyali, Mvita, Lagdera, Wajir Mashariki, Mandera Magharibi, Imenti Kaskazini, Kiminini, Kitui Mashariki, Ndaragwa, Mathira, Turkana Kaskazini, Kasipul, Ndhiwa, Mogirango Kaskazini na Embakasi Mashariki.

"Tutawapasha kuhusu hatua tulizopiga saa nane unusu adhuhuri.

Kwa sasa, tutarudi faraghani na kushauriana na maajenti waangalizi na maafisa wengine,” amesema.

"Nawaomba Wakenya kuwa na subira, tafadhali rejeeni kazini tukiendelea kukamilisha kazi hii.”

'Wanawake walifanya vyema sana uchaguzini

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Jinsia Wilfred Lichuma amesema tume hiyo imefurahishwa sana na idadi ya wanawake walioshinda nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi uliofanyika Jumanne.

Kwa mara ya kwanza kuna magavana watatu waliochaguliwa ikilinganishwa na mwaka 2013 ambapo hakuna mwanamke hata mmoja aliyechaguliwa gavana.

Wanwake 3 pia wamechaguliwa kuwa maseneta na 23 kama wabunge.

Kuna wanawake 97 waliochaguliwa kuwa wawakilishi wa wadi.

Soma zaidi: Wanawake washinda nyadhfa za Ugavana Kenya

Hali ukumbi wa Bomas yabadilika matokeo yakisubiriwa

Maafisa wakuu wa serikali pamoja na mabalozi wameanza kuwasili ukumbi wa Bomas ambako kuna kituo cha taifa cha kujumlishia na kutangazia matokeo ya urais, ishara kwamba tangazo muhimu linasubiriwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed na washirika wengine wakuu wa Rais Uhuru Kenyatta wamewasili Bomas.

Mabalozi wa Marekani na Uingereza pia wamewasili.

Kunashuhudiwa shughuli nyingi na usalama umeimarishwa pamoja na hali kuonekana kubadilika katika ukumbi huo.

Tume ya uchaguzi IEBC ilikuwa imetangaza kwamba inatarajia kupokea matokeo yote kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana.

Mwenyekiti wa tume hiyo anatarajiwa kutangaza matokeo baadaye baada ya kuhakikiwa kwa fomu za matokeo.

Matokeo ya awali kwenye tovuti ya tume hiyo yanaonesha Rais Kenyatta akiongoza kwa takriban asilimia 10 ya kura zilizohesabiwa dhidi ya Bw Odinga.

Tume ya uchaguzi ina siku saba kisheria kutangaza matokeo ya urais.

Godec
BBC
Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec amewasili Bomas
Gari la zulia
BBC
Gari likiwa linabeba zulia jekundu
Magari yakifika Bomas
BBC

Hali ilivyo KICC ukumbi wa mkutano wa Jubilee

Hivi ndivyo hali ilivyo ukumbi wa Jumba la Kimataifa la Mikutano la Jomo Kenyatta (KICC) ambako chama cha Jubilee kinatarajiwa kuwa na mkutano baadaye leo.

KICC
BBC
KICC
BBC

Ni maeneo bunge 20 pekee hayajawasilisha matokeo

Tume ya uchaguzi imetangaza kwamba kufikia sasa imepokea fomu za matokeo ya jumla kutoka maeneo bunge 270 kati ya 290 kote nchini humo.

Tume hiyo ilisema jana jioni kwamba inatarajia kupata Fomu 34B za matokeo kutoka maeneo yote kufikia saa sita mchana.

View more on twitter

Mabaki ya soko lililoteketea Garissa

Bashkas Jugsooday

BBC Swahili, Garissa

Wachuuzi katika soko la Garissa ambalo liliteketezwa moto Alhamisi baada ya makabiliano kati ya wafuasi wa wagombea wawili wa ugavana wamefika subuhi kujaribu kuokoa mali iliyosalia.

Sehemu kubwa ya soko hilo iliteketezwa.

Fujo zilizuka baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne kutangazwa.

Ali Bunow Korane wa chama cha Jubilee chake Rais Kenyatta alitangazwa mshindi.

Taarifa zinasema watu wasioridhishwa na matokeo hayo walichoma moto sehemu za soko hilo.

Hali ya utulivu imerejea lakini wazima moto wameendelea kukabiliana na moto huo.

Korane alipata kura 55 335 (51,48%) naye mpinzani wake wa karibu Nathif Jama Adan wa chama cha Wiper akapata kura 50 471 (46,95%).

Bw Adan ndiye gavana anayeondoka.

Garissa After
BBC
Garissa after
BBC
Garissa after
BBC
Garissa after
BBC

Chebukati: Matokeo ya upinzani hayaeleweki

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya amesema tume hiyo ilipokea barua kutoka kwa muungano wa upinzani NASA ambapo wanadai mgombea wao Raila Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne.

Bw Wafula Chebukati amesema matokeo hayo hayaeleweki kwa sababu muungano huo haukuambatanisha Fomu 34A za matokeo vituoni ambazo walitumia kufanya hesabu yao.

Aidha, ameonga muungano huo kwamba ni kinyume cha sheria kwao kujitangazia matokeo.

Bw Chebukati alizungumza na mwandishi wa BBC Anne Soy, msikilize:

Chebukati: Hatujui upinzani ulitoa matokeo yao wapi

Kenyatta aendelea kuongoza matokeo ya awali

Matokeo ya awali yanaonesha Bw Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee anaongoza akiwa na kura 8 163 572 naye Bw Raila Odinga wa chama cha ODM kilicho katika muungano wa National Super Alliance ana kura 6 747 099.

Matokeo yaliyotangazwa ni ya vituo 40489 kati ya vituo 40883.

Kura zilizoharibika zimeendelea kuwa nyingi, na kufikia sasa ni kura 399 935.

Hujambo!

Karibu kwa siku nyingine ya taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika Jumanne. Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kenya (IEBC) inatarajia kupokea fomu zote za matokeo kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana. Tangazo la mshindi wa urais linatarajiwa kutolewa baada ya tume hiyo kuhakiki fomu hizo.