Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Wapiga kura walioshiriki uchaguzi walikuwa wangapi?

  Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati anaonekana kutoa taarifa za kukinzana kuhusu idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura.

  Awali, alikuwa ametangaza kuwa wanakadiria asilimia 48 ya watu waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza.

  Lakini kwenye Twitter sasa ameonekana kukiri kwamba makadirio hayo yalikuwa ya juu mno.

  Anasema idadi halisi ya wapiga kura waliojitokeza, ambayo wamebainisha kwa sasa, ni wapiga kura 6,553,858.

  View more on twitter
  View more on twitter

  Tamko la Bw Chebukati sasa linaonesha waliojitokeza kati ya jumla ya 19,611,423 waliojiandikisha kupuiga kura ni asilimia 33.4.

  Katika uchaguzi wa tarehe 8 Agosti, waliojitokeza walikuwa 15,073,662 ambao ni sawa na asilimia 78.91.

 2. Habari za hivi pundeChebukati: Waliojitokeza kupiga kura ni 48%

  Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati amesema wanakadiria kwamba idadi ya waliojitokeza kupiga kura leo kufikia wakati wa kufungwa kwa vituo saa kumi na moja jioni ni asilimia 48.

  Akihutubia wanahabari, mwenyekiti huyo amesema vituo 87 kati ya vituo vyote vya kupigia kura vilifunguliwa, ambavyo ni vituo 35,564.

  Kati ya vituo hivyo, fomu za matokeo kutoka kwa fomu za matokeo kutoka kwa fomu 27,124 zimepokelewa.

  "Vituo 5,389 ambavyo vimetapakaa kote nchini havikufunguliwa. Baadhi vimo katika kaunti nne ambazo nilitangaza awali kwamba uchaguzi umeahirishwa," amesema.

  Bw Chebukati amesema vituo kamili vilivyoathiriwa vitatangwa kesho katika gazeti rasmi la serikali.

  Baadhi ya watu wameshutumu tarehe mpya ya uchaguzi iliyotangazwa na Bw Chebukati wakisema Jumamosi ni siku ya ibada kwa waumini wa kanisa la Kiadventisti ambao ni wengi katika kaunti ambazo uchaguzi umeahirishwa.

  Bw Chebukati hata hivyo amesema walizingatia mambo mengi kabla ya kutangaza tarehe mpya.

  "Matokeo ya uchaguzi ni lazima yatangazwe katika siku saba. Lazima tujinyime baadhi ya mambo. Wasiotaka kupiga kura hawatalazimishwa," amesema.

 3. Matokeo yaanza kuingia kutoka vituoni

  Tume ya Uchaguzi imekuwa ikipakia fomu za matokeo kutoka kwenye vituo vya kupigia kura mtandaoni.

  Kinyume na awali, fomu zinawekwa zilivyo mtandaoni.

  Kufikia sasa, fomu za matokeo kutoka vituo 16,282 kati ya 40,883 zimepakiwa.

  Hapa chini ni moja ya fomu za matokeo zilizopakiwa.

  Ni fomu kutoka kituo cha kupigia kura cha Deliverance katika mtaa wa Kawangware, Nairobi.

  Matokeo

  IEBC imekuwa ikifafanua mfumo unaotumiwa wakati huu kutangaza matokeo:

  View more on twitter
 4. Tayari kupokea matokeo Eldoret

  Maafisa wa tume ya uchaguzi katika Taasisi ya Teknolojia ya Bonge la Ufa mjini Eldoret wako tayari kuanza kupokea matokeo kutoka eneo bunge la Ainabkoi.

  Eneo bunge hilo lina vituo 113.

  Maafisa
  BBC
  Image caption: Meza ya maajenti wa vyama
  Maafisa
 5. Vituo vyaanza kumaliza kuhesabu kura

  Mwandishi wetu Robert Kiptoo ambaye yupo katika kituo cha kujumlishia matokeo ya Afraha mjini Nakuru katika Bonde la Ufa anasema baadhi ya vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Nakuru vimemaliza kuhesabu kura.

  Matokeo yanatarajiwa kuanza kutangazwa vituoni lakini tume ina hadi siku saba kutangaza matokeo kamili ya uchaguzi huo.

  Hali katika shule ya upili ya Afraha
  Image caption: Hali katika shule ya upili ya Afraha
  Afraha
 6. Chiloba: Sijaingilia uchaguzi wa leo

  Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya Uchaguzi IEBC Ezra Chiloba amekuwa likizoni. Alikwenda likizo ya wiki tatu baada ya shinikizo kutoka kwa muungano wa upinzani Nasa kumtaka ajiuzulu kuzidi.

  Lakini anaonekana kukerwa na tamko la mmoja wa wabunge wa Nasa Junet Mohamed kwamba bado amekuwa wakiingilia uchaguzi wa leo. Amekanusha tuhuma hizo:

  View more on twitter
 7. Gavana wa Kisumu asema uchaguzi hautarudiwa

  Anyang' Nyong'o

  Gavana wa kaunti ya Kisumu, magharibi mwa Kenya, amesema uchaguzi hautarudiwa katika jimbo hilo kama alivyotangaza mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati Jumamosi.

  Prof Anyang'a Nyong'o amesema kaunti hiyo itafanya maombolezi ya wiki moja kwa heshima ya watu wawili waliouawa leo.

  "Nimetangaza kama gavana wa hii kaunti wiki moja ya maombolezi ambapo wakati huo hakutakuwa na sherehe. Kwetu uchaguzi huwa ni sherehe," amesema.

  Amesema iwapo tume hiyo itaendelea kusisitiza uchaguzi ufanyike, basi wataenda kortini kutaka uzuiwe.

 8. Picha za ghasia kwenye mtaa wa Kibera, Nairobi

  Picha zimekuwa zikichapishwa zinazoonyesha makabiliano kati ya polisi na waandamanaji kwenye ngome ya upinzani ya Kibera, katika mji mkuu wa Kenya Nairobi:

  Kibera
  Kibera
  Kibera
  Kibera
  Kibera
  Kibera
 9. Uchaguzi waahirishwa magharibi mwa Kenya

  Wafula Chebukati

  Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imehairisha marudio ya uchaguzi wa urais katika kaunti za Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay kutokana na kile ilichokitaja kuwa hali mbaya ya usalama.

  Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, ametangaza kuwa marudio hayo ya uchaguzi sasa yataandaliwa tarehe 28 mwezi huu.

  Kaunti hizo ni ngome za upinzani na nyumbani kwa kinara wa upinzani Raila Odinga.

  Majimbo manne
 10. Ni kura moja tu kwenye sanduku la kupigia kura Kibera, Nairobi

  Mkuu wa gazeti la The New York Times kanda ya Afrika ya mashariki, amechapisha picha hii ya sanduku la kupigia kuta lililo na kura moja tu katika kituo cha kupigia kura, mtaa wa Kibera saa 9 tangu vituo vya kupigia vifunguliwe.

  Kibera ni eneo maskini lililo mji mkuu wa Nairobi ambalo ni ngome ya upinzani.

  View more on twitter
 11. Mtu mmoja auawa mjini Kisumu, ngome ya upinzani

  Takriban mtu mmoja ameuawa na wengine watano wamejeruhiwa na polisi kwenye ngome ya upinzani huko Kisumu magharibi mwa Kenya.

  Polisi wametumia vitoa machozi na risasi kutawanya waandamanaji ambao wanasusia marudio ya uchaguzi wa urais.

  George Odhiambo wa umri wa miaka 19, alipelekwa hospitali kuu ya mji wa Kisumu akitokwa damu nyingi.

  Alifariki wakati madaktari walijaribu kukoa maisha yake.

  Daktari mmoja katika hospitali hiyo aliiambia BBC kuwa Bw. Odhiambo alipoteza damu nyingi baada ya kupigwa risasi katika mtaa mmoja wa mabanda mjini Kisumu.

  Polisi wemekuwa wakikabiliana na waandamanaji mjini Kisumu tangu mapema asubuhi.

  Kenya
 12. Jaji mkuu David Maraga apiga kura

  Jaji mkuu nchini Kenya David Maraga alipiga kura yake leo kwenye shule ya msingi ya Bosose kaunti ya Nyamira.

  Mwezi Agosti Jaji Maraga aliweka historia pamoja na majaji wenzake watatu kwa kufuta matokeo ya urais.

  Jana Jumatano alifika mahakamani peke yake wakati alitangaza kuwa mahakama, haukuwa na uwezo wa kusikiliza kesi iliyokuwa imewasilishwa kwenye mahakana ya juu, kwa sababu hakukuwa na majaji wa kutosha kusikiliza kesi hiyo.

  View more on twitter
 13. Polisi wafyatua risasi kuwatawanya waandamanaji Kisumu

  Upinzani Kisumu
  Image caption: Wafuasi wa upinzani wakichoma matairi mzunguko wa barabara Kondele, Kisumu

  Polisi wamefyatua risasi halisi mjini Kisumu wakiendelea kukabiliana na wafuasi wa Bw Odinga ambao wamefunga baadhi ya barabara, mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza aliye katika mji huo wa magharibi mwa Kenya anasema.

  Watu wawili wamejeruhiwa - wote wawili wakiwa na majeraha ya risasi kwenye mapaja.

  Waliojeruhiwa ni mvulana wa miaka 15 na mwanamume wa miaka 21.

  Wawili hao wanapokea matibabu hospitalini.

  Mwandishi wetu anasema mabomu ya kutoa machozi pamoja na maji ya kuwasha yametumiwa kuwatawanya watu waliokuwa wamekusanyika katika uwanja mkuu wa mji huo ambao ni ngome ya Bw Odinga.

 14. Wakenya wachache wajitokeza Dar es Salaam na Arusha

  Upigaji kura katika uchaguzi wa urais wa marudio Kenya unafanyika katika katika balozi na afisi za kibalozi za nchi hiyo mataifa ya Afrika Mashariki na Afrika Kusini.

  Nchini Tanzania, ni wachache waliojitokeza kupiga kura asubuhi ubalozi wa Kenya Dar es Salaam na mjini Arusha.

  Faith Wambui Njogu, mmoja wa waliofika kupiga kura ameambia BBC ana furaha kwamba ametekeleza wajibu wake.

  "Nawaambia tu (Wakenya) wapige kura kuwe na amani, cha muhimu amani. Tupendane sote," amesema.

  Jijini Dar es Salaam, hali imekuwa hivi:

  Wambui Njogu amewahimiza Wakenya kudumisha amani
  Image caption: Wambui Njogu amepigia kura yake Dar na amewahimiza Wakenya kudumisha amani
  Dar es Salaam
  Dar es Salaam
  Dar es Salaam

  Mjini Arusha

  Arusha
  Arusha
  Arusha
 15. Wafuasi wa Odinga wachoma matairi Kisumu

  Katika maeneo mengi Kisumu, mji ambao ni ngome ya Raila Odinga, wakazi wamefunga barabara na kuchoma matairi.

  Mwandishi wa BBC Alistair Leithead anasema hajashuhudia kituo chochote ambapo upigaji kura unaendelea.

  Ametutumia picha hii:

  Kisumu
 16. Habari za hivi pundeKenyatta apiga kura Kiambu

  Kenyatta

  Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee amepiga kura yake katika eneo la Mutomo, Gatundu katika kaundi ya Kiambu.

  Amesema amefurahia kwamba raia wanajitokeza kupiga kura.

  "Tumechoshwa na uchaguzi na sasa ni wakati wa kusonga mbele. Uchaguzi ni fursa kwa raia kuwachagua viongozi kama ilivyosema Mahakama ya Juu. Hebu tuwachague viongozi na tusonge mbele," amesema.

 17. Wakazi wafunga barabara Bangladesh, Mombasa

  Wakazi katika mtaa wa Bangladesh eneo la Jomvu mjini Mombasa wamefunga barabara za kuelekea kwenye vituo vya kupigia kura.

  Wamekabiliana na polisi waliokuwa wakijaribu kuwatawanya.

  Bangla
  Bangla
  Bangla
 18. Heri ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Kenyatta

  Rais Kenyatta anatimiza miaka 56 hivi leo. Alizaliwa siku sawa na ya leo mwaka 1961.

  Watoto hawa wamekuwa kwenye kituo cha kupigia kura cha Mutomo, ambacho ndicho Bw Kenyatta, wakiwa na fulana zenye ujumbe wa kumtakia heri siku ya kuzaliwa kwake.

  Mama yao Joan Wamaitha amemwambia mwandishi wa BBC Anthony Irungu kuwa: "Walitazama video ya heri ya siku ya kuzaliwa ya rais na wakasisitiza wapate fulana hizi na wamsalimie Rais Kenyatta."

  Heri ya siku ya kuzaliwa
 19. Mavazi ya bendera Gatundu

  Familia hii imefika katika kituo cha kupigia kura cha Mutomo, Gatundu katika jimbo la Kiambu na mavazi ya kipekee - mavazi ya rangi za bendera ya Kenya.

  Rais Kenyatta amejiandikisha kupigia kura katika kituo hicho na anatarajiwa kupiga kura baadaye leo.

  Bendera
 20. Naibu Rais William Ruto apiga kura Eldoret

  Naibu Rais William Ruto, ambaye ni mgombea mwenza wa Rais Uhuru Kenyatta, amepiga kura yake katika kituo cha shule ya msingi ya Kosachei eneo la Turbo mjini Eldoret magharibi mwa Kenya.

  Ruto akipiga kura
  Ruto foleni
  Image caption: Ruto akiwa kwenye foleni
  Kituo hicho watu wamejitokeza kwa wingi
  Image caption: Kituo hicho watu wamejitokeza kwa wingi