Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai amemtaka Rais Robert Mugabe kujiuzulu
  2. Siku ya Jumatano wanajeshi walilizingira bunge na majengo mengine makuu ya serikali.
  3. Saa kadha baadaye wakatangaza kuwa walikuwa wanawalenga waalifu wanamzunguka Rais Mugabe.
  4. Rais Robert Mugabe yuko katika kizuizi cha nyumbani mjini Harare lakini mke wake Grace anaripotiwa kukimbia kwenda Namibia
  5. Mzozo kuhusu ni nani anaweza kumrithi Mugabe kati ya Bi Grace Mugabe na Bw. Mnangagwa umekigawanya chama cha Zanu-PF.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Picha za kwanza za mkutano wa mkuu wa jeshi na Mugabe

Picha za kwanza za mkutano kati ya Rais Robert Mugabe na mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Jen Constantino Chiwenga pamoja na wajumbe kutoka Afrika Kusini katika ikulu ya rais Harare zimetolewa.

Gazeti la Serikali la Herald limepakia picha hii kwenye Twitter:

View more on twitter

Mugabe ashiriki mazungumzo ikulu Harare

Mugabe amekuwa akizuiliwa na wanajeshi nyumbani kwake Harare
Reuters
Mugabe amekuwa akizuiliwa na wanajeshi nyumbani kwake Harare

Serikali ya Afrika Kusini imesema Rais Robert Mugabe anakutana na wajumbe kutoka nchi za kanda ya kusini mwa Afrika katika juhudi za kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Alisafiri hadi kwenye ikulu kutoka makao yake ya kibinafsi ambako amekuwa akizuiliwa na jeshi.

Wanajeshi waliingilia kati na kutangaza kudhibiti serikali Jumatano katika kinachoonekana kuwa juhudi za kumzuia mke wa Mugabe, Grace, asitwae madaraka.

Duru zinadokeza wkamba Bw Mugabe anataka kusalia madarakani hadi wakati wa kufanyika wka uchaguzi mwaka ujao.

Lakini mpinzani wake wa muda mrefu Morgan Tsvangirai amemtaka ajiuzulu mara moja kwa maslahi ya raia.

Makamu wake wa zamani Joice Mujuru pia ametaka kuwe na serikali ya mpito na pia uchaguzi huru na wa kuaminika.

Mzozo wa Zimbabwe pia unajadiliwa katika mkutano wa jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC, nchini Botswana.

Joice Mujuru: Tunahitaji serikali ya mpito

Joice Mujuru
AFP/Getty

Joice Mujru, makamu wa rais wa zamani na kiongozi wa muungano wa upinzani wa People's Rainbow Coalition (PRC), ameomba kuwepo na mazungumzo yanayoshirikisha wahusika wote nchini humo.

Amesema matokeo ya mazungumzo hayo inafaa kuwa uchaguzi huru na wa haki Zimbabwe.

Amani inaweza tu kupatikana kwa kuvumiliana na kubadilishana mawazo kwa Wazimbabwe wenyewe. Tukisonga mbele … matukio ya kisiasa yanahitaji kuhusisha wadau wote muhimu humu nchini.

Shughuli ya kujenga upya nchi yetu na kuhakikisha maridhiano ya taifa inaweza tu kutokea iwapo kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, ambao utafanyika kwa kipindi kifaacho na kitakachoafikiwa wakati wa kuunda serikali ya mpito.

Kabla ya kufutwa kazi kwake mwaka 2014, Bi Mujuru alitazamwa na wengi kama mrithi mtarajiwa wa Bw Mugabe.

Hata hivyo alifukuzwa kutoka kwenye chama tawala mwaka 2015.

Mwezi uliopita, alichaguliwa kuwa kiongozi wa muungano wa vyama sita vya upinzani kwa jina People's Rainbow Coalition.

Habari za hivi pundeTsvangirai amtaka Mugabe ajiuzulu

Tsvangirai
EPA

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe Morgan Tsvangirai amesema Rais Robert Mugabe anafaa kujiuzulu mara moja na kupisha serikali ya mpito ambayo itafanikisha kuandaliwa kwa uchaguzi huru na wa kidemokrasia.

Tsvangirai amesema hayo akihutubia wanahabari mjini Harare.

Mkuu wa AU asema hawatakubali mapinduzi

Conde
EPA

Rais wa Guinea ambaye kwa sasa ndiye mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) amekariri msimamo wa muungano huo na kusema hautakubali "mapinduzi ya kijeshi" Zimbabwe, shirika la habari la AFP limemnukuu akisema.

Tunataka katiba iheshimiwe na mfumo wa utawala wa kikatiba urejeshwe. Hatutakubali mapinduzi ya kijeshi.

Tunafahamu kwmaba kuna matatizo ya ndani. Haya yanafaa kutatuliwa kisiasa ndani ya chama cha Zanu-PF na si kwa uingiliaji wa jeshi."

Anaonekana kuchukua msimamo mkali kuliko Tume ya AU ambayo kupitia taarifa usiku wa kuamkia leo ilisema mzozo huo unafaa kutatuliwa "kwa njia ambayo itaendeleza demokrasia na kuheshimiwa kwa haki za kbinadamu".

Lakini tume hiyo haikutaja kilichotokea huko kuwa mapinduzi ya kijeshi.

Majenerali ambao wametwaa madaraka wanasisitiza kwamba hawajafanya mapinduzi ya kijeshi bali wanataka kuwakabili "wahalifu" ambao wanamzingira Rais Robert Mugabe.

Bw Conde aliingia madarakani Guinea mwaka 2010 baada ya kukabiliana na watawala wa kiimla na kijeshi kwa muda mrefu. Aliwahi kwenda uhamishoni na wakati mwingine kufungwa jela.

Kiongozi wa vijana Zanu-PF aomba jeshi msamaha

Kiongozi wa muungano wa vijana wa chama tawala Zanu-PF Kudzai Chipanga, ambaye amekuwa muungani mkono wa Rais Robert Mugabe na mkewe Grace ameomba radhi kutokana na hatua yake ya kulishutumu na kulionya jeshi dhidi ya kuchukua mamlaka nchini humo.

Jumanne, alikuwa amemwambia mkuu wa majeshi Jen Constantino Chiwenga anafaa “kusalia kwenye kambi za jeshi”.

Alisema wanachama wake hawatakubali wanajeshi wakiuke katiba na kwamba yeye na wafuasi wake walikuwa tayari kufariki wakimtetea Mugabe.

Lakini usiku wa kuamkia leo, alisoma taarifa kwenye runinga ya taifa ZBC, akisema kwamba alikuwa amekosea.

Tangu wakati huo nimetafakari na kutambua binafsi kwamba nilikosea, pamoja na wakuu wenzangu kwa kudunisha afisi yako yenye heshima.

Sisi bado ni wadogo na hufanya makossa na tumejifunza mengi kutokana na makosa haya.

Kasisi anayefanikisha mazungumzo Zimbabwe

Fidelis Mukonori
AFP

Padri wa kanisa Katoliki ambaye ana urafiki wa karibu na familia ya Mugabe anahusika katika mazungumzo kati ya Rais Robert Mugabe na jeshi nchini humo – duru nchini humo zinasema – kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Kasisi Fidelis Mukonori amekuwa rafiki wa rais huyo tangu miaka ya 1970, kwa mujibu wa makala kwenye gazeti la serikali la Herald iliyochapishwa miaka michache iliyopita.

Anachukuliwa kama “kiongozi wa kiroho” wa Mugabe.

Je, Mugabe atakubali kufanya mazungumzo?

Mugabe atakubali mazungumzo?
EPA
Mugabe atakubali mazungumzo?

Afrika Kusini imetuma ujumbe kwa mazungumzo ya dharura na rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na makanda wa jeshi wanamweka chini ya kizuizi cha nyumbani.

Waziri wa ulinzi Nosiviwe Maphisa-Nqakula, na waziri wa usalama wa kitaifa Bongani Bongo waliwazili kwenyr mji mkuu wa Zimbabwe Harare jana usiku.

Lakini Mugabe anasisitizia kuwa yenye bado ni raia wa Zimbabwe kwa mujibu wa mtandao wa Times Live nchini Afrika Kusini.

Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai arejea Harare

Tsvangirai
AFP

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) Morgan Tsvangirai amerejea nchini Zimbabwe.

Bw Tsvangirai amekwua akipokea matibabu ya saratani nje ya nchi hiyo.

Msemaji wa chama hicho amesema kiongozi huyo alirejea Harare Jumatano jioni. Kurejea kwake kunazidisha uvumi wa kuafikiwa kwa makubaliano ya hali ya kisiasa baada ya Mugabe.

Tendai Biti ataka kuwe na serikali ya mpito

Mwanasiasa wa upinzani Tendai Biti, ambaye alihudumu kama waziri wa fedha wakati wa serikali ya umoja nchini Zimbabwe kuanzia mwaka 2009 hadi 2013, anasema kuwa nchi inahitaji kwa dharura utawala wa mpito ili iweze kuendelea kidemokrasia.

Aliiambia BBC kuwa ana matumania kuwa sasa mazungumzo yanaweza kuanza kati ya jeshi, watu wa Zimbabwe na wapatanishi wa eneo hilo.

Kiongozi huyo wa People's Democratic Party, alisema kuwa hatua kijeshi zilipata zimbabwe kwa ghafla akisema kuwa hakufikiria kuwa rais Mugabe anaweza kupitia hayo.

Tendai Biti
AFP
Tendai Biti

Mkuu wa UN ahimiza utulivu Zimbabwe

Guterres
Getty Images

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameomba kuwe na utulivu na kuvumiliana nchini Zimbabwe.

Msemaji wake, Farhan Haq, samesema Guterres anafuatilia kwa karibu yanayojiri Zimbabwe.

Ameongeza kuwa: "Kulindwa kwa haki za kimsingi, zikiwemo uhuru wa kujieleza na kutangamana, ni muhimu sana."

Kwa mujibu wa shirika la AFP, Bw Guterres pia amesema jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika, Sadc, inafanya juhudi kutanzua mzozo huo.

Waziri akamatwa akitorokea Afrika Kusini

Mbunge ambaye pia ni waziri wa serikali Paul Chimedza, amekamatwa katika kizuizi cha barabarani alijaribu kukimbia kwenda Afrika Kusini, gazeti moja linasema nchini Zimbabwe.

Gazeti hilo linasema kwa alimatwa eneo la Bubi kusini mwa nchi

Yeye ni waziri katika mkoa wa Masvingo na alihudumu kama daktari kabla ya kujiunga na siasa,.

Maafisa kadha wa Zanu-PF wanaripotiwa kuwa kizuizini akiwemo aliyekuwa mshirika mkuu wa Rais Robert Mugabe Jonathan Moyo na waziri wa fedha Ignatius Chombo.

Raia wa Zimbabwe nchini Uingereza washerehekea

Wapinzani wa Mugabe
BBC

Raia wa Zimbabwe wanaoishi uhamishoni London walikusanyika nje ya ubalozi wa taifa hilo nchini Uingereza, kusherehekea kinachoonekana kuwa kusambaratika wka utawala wa Mugabe.

Wengi ni wanachama wa shirika ambalo limekuwa likiandaa maandamano mara kwa mara dhidi ya serikali ya Mugabe.

"Leo si kituo bali ni kikomo. Tunahitaji mabadiliko kamili," alisema Chipo Parirenyatwa, mwenyekiti wa Shirika la Haki za Kibinadamu la Zimbabwe.

"Sifahamu ni vipi jeshi litaendesha mambo, lakini nina matumaini. Kuna haja ya kuwepo wka uchaguzi kwa njia ya amani na jamii ya kimataifa kushirikishwa.

"Nafikiri kuna uwezekano wa 50-50 kwamba hilo litatokea."

Namibia: Grace Mugabe hayuko hapa

Grace Mugabe
AFP
Grace Mugabe

Naibu waziri mku nchini Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah, amekana uvumi kuwa nchi yake inamhifadhi mke wa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Grace Mugabe.

"Sijapokea taarifa kama hiyo. Kile ambacho tumejulishwa ni kuwa mke wa rais na familia yake wako salama nchini mwao," alisema Nandi-Ndaitwah.

Bi Nandi-Ndaitwah ambaye pia anahudumu kama waziri wa mashauri ya nchi za kigeni, alinukuliwa akisema kuwa yale yanayoendelea katika taifa jirani wao la Zimbabwe yanaleta wasiwasi mkubwa.

Soma zaidi: Grace Mugabe anaweza kuwa ametorokea Namibia?

Hatma ya Rais Robert Mugabe bado haijulikani

Rais Robert Mugabe bado yuko katika kuzuizi cha nyumbani na hatma yake haijulikani.

Alipo mke wake Grace, ambaye alikuwa na nia ya kumrithi kama rais na kuchangia hali iliyo sasa hapajulikani.

Baadhi ya ripoti zinasema kuwa amekimbia kwenda Namibia.

Baadhi ya wanajeshi wako kwenye mitaa ya mji mkuu Harare na gari hili la wanajeshi hapo chini lilipigwa picha nje ya majengo ya bunge mapema leo:

Harare
Reuters
Harare

Karibu kwenye taarifa za Moja kwa Moja za BBC

Karibu kwenye taarifa za Moja kwa Moja za BBC tunapoendelea kufuatilia hatua za jeshi za kuchukua madaraka nchini Zimbabwe