Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Habari za hivi pundeRais mtarajiwa wa Zimbabwe awasili mjini Harare

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerudi nchini humo kutoka Afrika Kusini.

Anatarajiwa kutoa hotuba yake katika makao makuu ya chama cha Zanu-PF mjini Harare.

Mnangagwa akutana na rais Jacob Zuma Afrika Kusini

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amekutana na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati ambapo anasubiriwa kurudi nyumbani leo.

Bwana Zuma alitarajiwa kuwasili atika mji mkuu wa Harare leo ili kuwa mpatanishi wa mgogoro uliokuwa ukiendelea lakini akafutilia mbali zaiara hiyo baada ya rais Mugabe kujiuzulu.

Afisi ya rais Zuma ilituma ujumbe wa Twitter wa picha za mkutano wao.

Mnangagwa akutana na rais Jacob Zuma Afrika Kusini
twitter
Mnangagwa akutana na rais Jacob Zuma Afrika Kusini

Wafuasi wa Emmerson Mnangagwa wakimsubiri kuwasili mjini Harare

Wafuasi wa Emmerson Mnangagwa wakimsubiri kuwasili mjini Harare
BBC
Wafuasi wa Emmerson Mnangagwa wakimsubiri kuwasili mjini Harare
Wafuasi wa Emmerson Mnangagwa wakimsubiri kuwasili mjini Harare
BBC
Wafuasi wa Emmerson Mnangagwa wakimsubiri kuwasili mjini Harare

Wachora vibonzo wa Kenya wanavyoitazama hali ya Zimbabwe

Wachora vibonzo wa Kenya
Twitter
Wachora vibonzo wa Kenya

Hivi ndivyo wachora vibonzo wa Uganda walivyotathmini hali ya Zimbabwe

Wachora vibonzo wa Uganda
Twitter
Wachora vibonzo wa Uganda

China yaheshimu uamuzi wa Mugabe

China imesema kuwa imeheshimu uamuzi wa rais Robert Mugabe wa kujiuzulu na kwamba bado atasalia kuwa rafiki wa raia wa Uchina.

Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni Lu Kang ameongezea kuwa sera za China kwa Zimbabwe hazitabadilika. Uhusiano wa China na Zimbabwe ni mkubwa tangu vita vya Rodesian vya msituni.

Bwana Mugabe alikosa kuungwa mkono na Usovieti hivyobasi akarudi China ambayo iliwapatia wapiganaji wake wa Gorila vifaa pamoja na mazoezi.

Mataifa yote mawili yaliimarisha uhusiano wao wa kidiplomasia wakati wa uhuru wa Zimbabwe 1980 na rais Mugabe alimtembelea waziri mkuu wa China mwaka uliofuata.

Bwana Mugabe na rais wa China Xi Jinping
getty images
Bwana Mugabe na rais wa China Xi Jinping

Mugabe ameondoka je Zimbabwe itabadilika?

Je umoja wa Zimbabwe , uhuru wa kutoogopa utaleta mwanzo mpya nchini Zimbabwe. Kiongozi mpya anayetarajiwa kuapishwa alishiriki pakubwa katika utawala wa Zimbabwe.

Alikuwa mwandani wa Mugabe kwa miaka mingi na alikosana naye ili kumzuia Grace Mugabe kumrithi mumewe.

Hayakuwa mapinduzi ya kuleta demorasia katika serikali bali yalikuwa mapinduzi ya mamlaka. Mbali na hayo kuna shinikizo kubwa ya kiongozi mpya kuanza mipango muhimu ya mabadiliko.

Ufisadi na uongozi mbaya wa awali hautavutia ufadhili wa kifedha na uwekezaji kutoka kwa jamii ya kimataifa na hiyo inatakikana kuokoa uchumi wa taifa hilo ulioharibika.

Bwana Mnangagwa anakabiliwa na changamoto mpya iwapo atairejesha Zimbabwe katika utawala mbaya uliopita.

Mafikira yake ni ya kiudikteta lakini hatakuwa na ukandamizaji kama ule wa Mugabe.

Wafuasi wa makamu wa rais aliyefutwa kazi Emmerson Mnangagwa wakimsubiri kiongozi huyo kuasili nchini humo
BBC
Wafuasi wa makamu wa rais aliyefutwa kazi Emmerson Mnangagwa wakimsubiri kiongozi huyo kuasili nchini humo

Kimya kirefu cha rais Jacob Zuma chawashangaza wengi

Kimya kirefu cha rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma pamoja na chama chake tawala cha ANC kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe kinashangaza.

Kinaonyesha ushawishi wa kisaikolojia aliyokuwa nao kwao na walishangazwa sana na hatua aliyochukua. Kile afisi ya rais Zuma ilichosema ni kwamba hatoweza tena kuelekea nchini Zimbabwe kama alivyokuwa amepanga ili kupatanisha kbal ya rais Mugabe kutangaza kujiuzulu.

Ziara hiyo sasa imeahirishwa hadi tyangazo jingine , taarifa ilisema. Lakini badala yake chma cha upinzani nchini Afrika Kusini DA kilijibu na hivyobasi kuungwa mkono na raia weusi pamoja na wazungu kiliposema:

Huu ni ushindi wa raia wa Zimbabwe ambao wametaabika chini ya uongozi wa Mugabe .Habari ya bwana Mugabe sio geni na kwamba inaendelea katika bara la Afrika.Mtu aliyekuwa shujaa wa taifa lake , Mugabe alisababisha migawanyiko, ukosefu wa udhabiti na kuharibika kwa uchumi wakati alipobadilika kutoka kuwa mpiganiaji wa uhuru hadi kuwa dikteta.Hilo sio tu kwa Mugabe bali hata Zanu -PF chama ambacho amekitawala kwa kutumia nguvu kwa kuchukua mamlaka tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.Chama cha ANC kinaonyesha ishara kama zile za Zanu-PF, kimekumbwa na ufisadi mkubwa na ghasia huku pande pinzani zikipigania madaraka katika serikali kwa lengo la kujitajirisha badala ya kuwahudumia wananchi.Baada ya kuchukua madaraka miaka 23 kutoka kwa wazungu ,ANC sasa kinakabiliwa na changamoto ya kujiimarisha au tishio la kuangamiza uchumi wa Afrika kusini kama Zanu-Pf kilivyofanya kwa miaka 37.

Robert Mugabe na rafiiye wa Afrika Kusini rais Jacob Zuma
afp
Robert Mugabe na rafiiye wa Afrika Kusini rais Jacob Zuma

Makundi ya raia wa Zimbabwe kumlaki Mnangagwa

Makundi ya raia wa Zimbabwe yameanza kuwasili katika uwanja wa ndege wa kijeshi mjini Harare ambapo Emmerson Mnangagwa anayetarajiwa kumrithi rais Robert Mugabe anatarajiwa kuwasili baadaye leo.

Chombo kimoja cha habari nchini Zimbabwe kimechapisha picha za makundi hayo.

Makundi ya raia wa Zimbabwe kumlaki Mnangagwa
Twitter
Makundi ya raia wa Zimbabwe kumlaki Mnangagwa

''Grace Mugabe hafai kubebeshwa msalaba wa Mugabe''

Hatua ya rais Robert Mugabe ya kumfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa ililifanya jeshi kuingilia kati siasa za Zimbabwe.

Kufutwa kwake kulionekana kumrahisishia mkewe raia Grace Mugabe kumrithi mumewe kwa kuwa alikuwa katika harakati za kupewa wadhfa wa makamu wa rais.

Hatahivyo mbunge wa upinzani Priscilla Mushonga ameambia BBC kwamba kumlaumu Mugabe kwa mgogoro huo ni sawa na kumuondolea lawama Mugabe.

''Nadhani ni rahisi sana kumlaumu mwanamke huyo.Nadhani Mugabe amekuwa kiongozi mbaya tanngu 1983 alipowaua watu 20,000 katika eneo la Matabeleland.Wakati huo bi Mugabe pengine alikuwa katika kidato cha kwanza katika shule ya upili.Ni kweli kwamba huenda alihusika na mabo mengi lakini huenda alikuwa kifaa tu cha kutumia kwa yeye kuendelea kusalia madarakani.Kwa hivyo kumlaumu Grace kwa yote yaliofanyika nadhani sio sawa''.

Raia wa Zimbabwe wakibeba bango la Grace Mugabe wakati wa maandamano nchini humo
afp
Raia wa Zimbabwe wakibeba bango la Grace Mugabe wakati wa maandamano nchini humo

Makamu wa rais wa Zimbabwe akataa kurudi nyumbani

Wakati Emmerson Mnangagwa alipofutwa kazi wiki mbili zilizopita hakuwa makamu wa raius wa Zimbabwe pekee.

Phelekezela Mphoko ni makamu wa rais mwengine ambaye anajuliakana kwa kumuunga mkono mkewe rais Mugabe na kulingana na sheria anapaswa kumrithi Mugabe.

Hatahivyo chama cha Zanu PF kimsema kuwa Mnangagwa ataapishwa kufuatia uamuzi uliochukuliwa na kamati yake kuu siku ya Jumapili.

Bwana Mphoko alikuwa ameondoka katika taifa hilo wakati Jeshi lilipochukua mamlaka wiki moja iliopita, na kulingana na gazeti la NewsDay hajarudi nyumbani kwa kuwa anahofia kukamatwa.

Gazeti hilo limenukuu duru akisema kuwa amebadilisha mipango yake ya usafiri. Alitarajiwa kurudi nchini zimbabwe kufikia siku ya Ijumaa , kutoka Tokyo Japan.

Lakini duru zimesema kuwa anataka tiketi zake za usafiri kubadilishwa ili aelekee Zambia au Msumbiji .

Anajua anaogopa kukamatwa kwa sababu anatakikana kwa kuzuia haki na kufanya ufisadi.

Makamu wa rais wa Zimbabwe akataa kurudi nyumbani
BBC
Makamu wa rais wa Zimbabwe akataa kurudi nyumbani

Matamshi ya Mugabe alipokuwa akijiuzulu

Alivyosema Mugabe katika barua yake ya kujiuzulu

Matamshi ya Mugabe alipokuwa akijiuzulu
Getty Images
Matamshi ya Mugabe alipokuwa akijiuzulu

Rais mpya wa Zimbabwe kuhudumu hadi 'uchaguzi wa 2018'

Kufuatia ripoti kwamba aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangangwa huenda akaapishwa kuwa rais , shirika la habari la reuters sasa linasema kuwa atahudumu hadi 2018.

Kiranja wa Chama cha Zanu-Pf, Lovemore Matuke aliambia vyombo vya habari kwamba Mnangagwa atahudumu kipindi kiliochosalia cha rais Mugabe.

Chini ya sheria za sasa uchaguzi mkuu ujao unaweza kufanyika mnamo mwezi Septemba 2018.

Rais wa Guinea ataka uchaguzi wa urais Zimbabwe kufanywa 2018

Rais wa Guinea na mwenyekiti wa Umoja wa bara Afrika Alpha Conde amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya rais Robert Mugabe kujiuzulu.

Bwana Conde pia alimtaja Mugabe kuwa shujaa wa Afrika. ''Ni makosa kwamba anaondoka kupitia mlango wa nyuma''.

Bwana Conde amesema kuwa uchaguzi wa urais nchini Zimbabwe unafaa kutekelezwa mwaka 2018 na kwamba Umoja wa Afrika utalisaidia taifa hilo.

Rais Alpha Conde wa Guinea
EPA
Rais Alpha Conde wa Guinea

Emmerson Mnangagwa anayetarajiwa kumrithi Mugabe ataapishwa Ijumaa

Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, ambaye kufutwa kwake kazi kulisababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, anatarajiwa nchiuni humo siku ya Jumatano.

KIongozi huyo baadaye anatarajiwa kuapishwa rasmi Ijumaa, kulingana na shirika la utangazaji la Zimbabwe (ZBC).

Emmerson Mnangagwa, aliyetorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini , kulingana na Zanu-PF.

Kuondoshwa kwake madarakani kulisababisha chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala wa miaka 37 wa Bwana Mugabe.

Taarifa kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amejiuzulu zilikuja kwa njia ya barua iliyosomwa bungeni Jumanne , bunge likalazimika kuahirisha mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa dhidi yake.

Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane

Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuwasili nchini Zimbabwe
BBC
Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuwasili nchini Zimbabwe

Picha za Mugabe zaondolewa ukutani Zimbabwe

Shule moja ya Zimbabwe imesambaza kanda ya video iliokuwa ikionyesha mtu mmoja akiondosha picha ya Mugabe katika ukuta wa shule hiyo.

Hatahivyo hakusema kule kanda hiyo ya video ilikochukuliwa.

Watu wakiondoka picha ya Mugabe katiuka ukuta wa shule moja
Twitter
Watu wakiondoka picha ya Mugabe katiuka ukuta wa shule moja

Magari ya kijeshi yaanza kuondoka mjini Harare

Magari ya kijeshi yaliokuwa yameshika doria katika kila kona ya mji wa Harare yameanza kuondoka kulingana na mtandao mmoja ambao umekuwa ukichapisha maswala ya kisiasa ya taifa hilo la Afrika ya kusini.

Jeshi lilichukua mamlaka siku ya Jumatano iliopita na kusababisha kujiuzulu kwa rais Mugabe.

Magari ya Kijeshi yaliokuwa yameshikilia doria katika mji mkuu Harare
Reuters
Magari ya Kijeshi yaliokuwa yameshikilia doria katika mji mkuu Harare

Marekani yapongeza kujiuzulu kwa Mugabe

Ubalozi wa Marekani mjini Harare umesema kuwa ni hatua ya kihistoria na kuwapongeza raia wa Zimbabwe kwa kutoa sauti zao na kusema kwa njia ya amani kwamba ni wakati wa mabadiliko.

Uingereza: Tutaisaidia Zimbabwe kuwa na uchaguzi ulio huru na haki

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa kujiuzulu kwa Mugabe kunaipatia Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala uongozi wa Mugabe.

Amesema kuwa Uingereza ambaye ni rafiki wa zamani wa Zimbabwe atafanya kila awezalo kusaidia kufanyika kwa uchaguzi ulio huru na haki na kujenga uchumi wa Zimbabwe.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May
BBC
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Natumai hamjambo