Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Mataifa ya Marekani, Ufaransa na Uingereza yamefanya mashambulio wakilenga vituo vitatu huko Syria kama adhabu kwa madai kwamba utawala wa Rais Bashar al-Asad, ulitumia silaha za kemikali dhidi ya rai
  2. Marekani inasema kuwa ililenga maeneo matatu -Kituo cha utafiti mjini Damascus na vifaa vya uhifadhi karibu na mji wa Damascus
  3. Urusi ilisema kuwa makombora yalilenga maeneo mengine lakini mengi yalitunguliwa na vifaa vya ulinzi wa angani
  4. Rais Trump alisema kuwa washirika wake walitumia uwezo wao dhidi ya ubepari na ukatili
  5. Rais wa Urusi Vladmir Putin alishutumu mashambulio hayo na kuitisha kikao cha dharura cha Umoja wa Mataifa
  6. rais wa Syria Bashar al-Assad anasema kuwa mashambulio hayo yamemfayna kuwa jasiroi zaidi kukabiliana na ugaidi.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Habari za hivi pundeRaia wa Syria wamuunga mkono rais Assad na kumshutumu Trump

Barabara za mjini Damascus zimejaa watu kama kawaida. Wanajeshi katika vizuizi wamepumzika huku vizuizi vya usalama vikipunguza operesheni zake kali.

Maduka yako wazi na watu wanaelekea kazini kama kawaida. Makumi ya raia wa Syria yamekongamana katika bustani kubwa mjini Damascus karibu na jengo la runinga ya Syria wakiunga mkono jeshi lao, Syria na rais Assad.

Wanasema kuwa wanataka kumwambia rais Trump kwamba hawamuogopi na kwamba hakuna kitakachobadilika kwa jeshi na kwa rais Assad.

Wengi walisema kuwa walitarajia shambulio hilo na kwamba hawadhani kwamba kutakuwa na shambulio jingine.

Raia wanaomuunga mkono rais Assad nchini Syria wakiandamana na kupinga mashambulizi dhidi ya Syria
afp
Raia wanaomuunga mkono rais Assad nchini Syria wakiandamana na kupinga mashambulizi dhidi ya Syria

Picha za maeneo yalioshambuliwa Syria

Maeneo yalioshambuliwa nchini Syria
Al-Ikhbariyah al-Suriyah
Maeneo yalioshambuliwa nchini Syria
Maeneo yalioshambuliwa nchini Syria
Al-Ikhbariyah al-Suriyah
Maeneo yalioshambuliwa nchini Syria
Maeneo yalioshambuliwa nchini Syria
Al-Ikhbariyah al-Suriyah
Maeneo yalioshambuliwa nchini Syria

Uingereza: Ndege zetu zilirusha makombora 8 kwa jumla

Wizara ya ulinzi nchini Uingereza imethibitisha kuwa jumal ya makombora 8 yalirushwa .

Mawili yalirushwa kutoka kila ndege zake 4 za Tornado GR4

View more on twitter

Rais Trump apongeza mashambulio na kusema 'lengo limetimizwa'

Rais wa Marekani Donald Trump amepongeza mshambulio ya usiku kucha dhidi ya Syria kama yaliotekelezwa vizuri akiongezea kuwa , 'lengo limetimia'.

Uingereza , Marekani na Ufaransa zilishambulia maeneo matatu ya serikali zikilenga kile zilichokitaja kuwa silaha za kemikali.

Zaidi ya makombora 100 yalirushwa ili kujibu shambulio linalodaiwa kuwa la kemikali katika mji wa Douma wiki iliopita.

Rais wa Urusi Valdmir Putin ameshutumu mshambulio hayo ya magharibi.

View more on twitter
View more on twitter

Waasi wapinga shambulio la Syria

Kumekuwa na matumaini machache kutoka kwa waasi wanaopinga utawala wa Assad ndani na nje ya Syria kwamba mashambulio hayo yanaweza kuwa makubwa kudhoofisha uwezo wa kivita wa serikali ya Syria.

Lakini kutokana na kile kinachojulikana ni kwamba kiongozi mmoja wa waasi hao ametaja shambulio hilo kutokuwa na muhimu wowote kwa kuwa lilishambulia vifaa vinavyotumiwa kutekeleza uhalifu na sio muhalifu mwenyewe.

Alloush ni mwanachama wa jaish al-Islam-basi la mwisho la wapiganaji wanaondoka mjini Douma limeondoka.

Baada ya ushindi mashariki mwa Ghouta vikosi vya serikali vimekuwa vikielekea katika maeneo mengine, ikiwemo eneo linalokaliwa na wanajihad kusini mwa mji wa Damascus.

Urusi: Shambulio la Syria litaathiri mazungumzo ya amani

Shambulio la angani dhidi ya Syria litaathiri mazungumzo ya amani , msemaji wa Urusi amesema kulingana na chombo cha hanbari nchini humo RIA.

Maria Zakahrova alisema: Kitendo hiki kinatoa ishara kali kwa watu walio na itikadi kali na wapiganaji kwamba wanatekeleza vitendo vya sawa.

Iran: Majeshi ya Magharibi yanataka kuthibitisha uwepo wao mashariki ya kati

Rais wa Iran Hassan Rouhani ameshutumu uvamizi wa mashambulizi yalioongozwa na Marekani nchini Syria akisema kuwa mashambulio ya Marekani katika mashariki ya kati hayana athari zozote bali ni 'kuangamiza na kuharibu'.

Katika mkutano siku ya Jumamaosi, kiongozi wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei, alisema kwamba majeshi ya magharibi yanataka kuthibitisha uwepo wao katika eneo la mashariki ya kati kutokana na shambulio hilo.

Rais wa Iran Hassan Rouhani katika mkutano
EPA
Rais wa Iran Hassan Rouhani katika mkutano

Seneta John McCain apongeza shambulio la Trump

Seneta wa chama cha Republican nchini Marekani John McCain alipongeza hatua ya rais Donald Trump.

Lakini alionya kuwa mkakati wa muda mrefu ulihitajika na kumtaka kamanda huyo mkuu kuweka malengo yake.

Matamshi kama hayo yalitolewa na seneta wa chama cha Democrat Bob Menendez aliyesema kuwa :

Mashambulio ya kijeshi sio suluhu ya mkakati mwafaka.

View more on twitter

Kanda ya video inaonyesha kifaa cha kutungua makombora

Mzalishaji vipindi wa BBC Riam Dalati anasema kuwa kanda hii ya video ilirekodiwa katika mji mkuu wa Syria Damascus, mapema siku ya Jumamosi

View more on twitter

Trump ajipata mashakani kwa kutoshauri bunge

Baada ya dakika chache za kutangaza kuhusu shambulio la Syria , rais Trump alijipata mashakani kutoka kwa wabunge wa Republican na Democrat kwa kuagiza mashambulio nchini Syria bila ya kuwashauri.

Seneti wa chama cha Democrat Tim Kaine alitaja kuwa 'makosa na haramu' na kuonyesha wasiwasi wake kwamba hatua hiyo inaweza kumshawishi bwana Trump akaishambulia Iran ama hata Korea Kaskazini.

Mbunge wa chama cha Republican hakumsaza bwana Trump kwani alisema kwamba hatua hiyo ni kinyume na katiba.

Wataalam wa kisheria hatahivyo wametofautiana na mjadala huo uliokuwepo mwaka mmoja uliopita wakati Trump alipochukua hatua dhidi ya Syria mwezi Aprili uliopita kufuatia shambulio katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Khan Sheikhoun ambalo Umoja wa Mataifa na wataalam wa OPCW wanasema kuwa gesi ya neva kwa jina Sarin ilitumika.

View more on twitter
View more on twitter

Tazama ndege za kijeshi zikiondoka

Rais wa Ufaransa alituma video katika mtandao wa Twitter ambayo inaonyesha ndege za kivita zikiondoka kabla ya kufanya mamshambulio nchini Syria

View more on twitter

Habari za hivi pundeUrusi yaonya kulipiza shambulio la Marekani Syria

Urusi imeionya Marekani kwamba isubiri matokeo ya athari za mashambulio yake .

Urusi imeitaka Marekani kutarajia uwezekano wa majibu ya shambulio hilo Balozi wake nchini Marekani

Anatoly Antononov alisema katika taarifa kwamba kitendo hicho hakutakubaliwa bila mupata majibu.

Rais Vladmir Putin wa Urusi
BBC
Rais Vladmir Putin wa Urusi

Ufaransa: Utawala wa Syria 'ulivuka mstari mwekundu'

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kuwa ameagiza mashambulio dhidi ya Syria kwa sababu makumi ya wanaume wanawake na watoto waliuawa kinyama na silaha za kemikali.

Aliongezea: Mstari mwekundi ulivukwa

"The red line had been crossed," he added.

View more on twitter

Theresa May: Hatuna lengo jingine bali kuangamizi silaha za kemikali

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amezungumza kwa mara ya kwanza tangu tangazo la shambulio la pamoja nchini Syria .

Bi May alisema kuwa kulikuwa na muhimu kuangamiza silaha za kemikali za utawala wa Syria na kuzuia utumizi wake.

Lakini alisisitiza: Hatutaki kubadilisha uatawala wa taifa hilo wala kuingilia vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Waziri mkuuwa Uingereza kushoto, rais wa Marekani Donald Trump katikati na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Kulia
Getty Images
Waziri mkuuwa Uingereza kushoto, rais wa Marekani Donald Trump katikati na waziri mkuu wa Ufaransa Macron Kulia

Shambulio ni onyo kwa utawala wa Asaad

Shambulio lililotekelezwa na Marekani pamoja na washirika wake lilikuwa muhimu zaidi ya shambulio la Marekani dhidi ya kambi za kijeshi za Syria mwaka mmoja ulioipita , lakini kwanza lilionekana kuwa mchezo wa maneno wa rais Trump.

Mwaka uliopita makombora 59 yalirushwa lakini mara hii makombora yaliorushwa ni mara mbili ya makombora yaliotumika awali.

Mashambulio hayo yamesitishwa kwa sasa lakini kuna onyo kwamba iwapo utawala wa rais Assad utaendelea kutumia silaha za kemikali basi mashambulio zaidi yatatekelezwa.

Makombora yalirushwa na ndege aina ya RAF Tornado
PA
Makombora yalirushwa na ndege aina ya RAF Tornado

Trump: Hatutakubali ukatili dhidi ya raia wa Syria

Taarifa zinasema milio ya milipuko imesikika katika maeneo kadhaa ya miji wa Damascus na Homs.

Katika taarifa yake rais Trump amedai kwamba vituo vilivyolengwa vinahusiana na utafiti wa uhifadhi na utengenezaji wa silaha za kemikali.

Rais Trump ameongeza kusema kwamba Marekani iko tayari kuendeleza mashambulio hayo hadi utawala huo wa Syria utakapokoma kabisa kutumia silaha za kemikali.

Rais Donald Trump baada ya kuagiza mashambulio dhidi ya viwanda na hifadhi za silaha za kemikali Syria
BBC
Rais Donald Trump baada ya kuagiza mashambulio dhidi ya viwanda na hifadhi za silaha za kemikali Syria

Shambulio limetufanya kuwa 'majasiri' zaidi

Rais wa Syria Bashar al-Asaad anasema kuwa mashambulio yaliotekelezwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa yamemfanya kuwa jasiri zaidi ya alivyokuwa awali kukabiliana na wapinzani wake.

Katika matamshi ya kwanza tangu tangu shambulio hilo la alfajiri , bwana Asaad pia aliishutumu Marekani kwa kupoteza uaminifu .

Mapema rais Trump alisema kuwa mashambulio hayo yalikuwa yakilenga viwanda vya kutengeza silaha za kemikali vinavyolaumiwa kwa shambulio la kemikali kwa raia wanaoishi mjini Douma wiki moja iliopita.

Bwana Trump alisema kuwa Marekani na washirika wake walikuwa wakitumia uwezo wao dhidi ya ubepari na ukatili.

Pia alilaumu Urusi kwa kushindwa kuweka ahadi ya kukabiliana na silaha za kemikali nchini Syria.

Rais wa Syria Bashar Al Asaad
Ronald Grant
Rais wa Syria Bashar Al Asaad

Natumai hamjambo...