Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limethibitisha kwamba watu 32 walifariki
  2. Watu watano bado hawajulikani walipo, na sita bado wamelazwa hospitalini
  3. Bwawa lililoporomoka lilikuwa katika shamba la mfanyabiashara kwa jina Patel katika eneo la Solai, Subukia katika Kaunti ya Nakuru
  4. Kufikia sasa, watu 158 wamefariki Kenya kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha maeneo mengi, watu laki tatu wamekimbia makwao

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Video: Hali ilivyo Solai

Mwandishi wetu Victor Kenani ametutumia video ya hali ilivyo kwa sasa eneo la mkasa ambapo mvua kubwa imenyesha.

View more on facebook

Mvua kubwa yanyesha na kutatiza uokoaji

Mvua
BBC

Waandishi wa BBC Becky Lipscombe na Victor Kenani wapo eneo la mkasa.

Wanasema mvua kubwa imenyesha na kutatiza juhudi za uokoaji. Baadhi ya wakazi wamelazimika kujikinga kwa kutumia miavuli. Wengine wamelazimika kukimbilia majumba yaliyonusurika kujikinga.

Magari mengi, yakiwemo magari ya kuwabeba wagonjwa yamekwama kwenye matope barabarani.

Maafisa wa jeshi la Kenya wamo eneo hilo kusaidia juhudi za uokoaji lakini mvua inatatiza juhudi za uokoaji.

Mvua
BBC

Msemaji wa Rais: Tumesikitishwa na matukio Solai

Msemaji wa Rais Kenyatta, Manoah Esipisu, ametoa taarifa kuhusu matukio mkasa wa Solani. Amesema:

Tumesikitishwa sana na vifo na uharibifu wa mali uliotokana na bwawa katika shamba la Patel, eneo la Solai, Subukia kuvunja kingo zake. Watu wa kusaidia katika uokoaji walifika eneo la mkasa na tunawapongeza kwa juhudi zao.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Polisi wamefika eneo hilo. Idara husika zitatoa taarifa ya kina tutakapopata maelezo kamili.

Manusura wa bwawa la Solai wazungumza

Manusura wa mkasa wa bwawa la Solai ambalo limewaacha zaidi ya watu 32 wakiwa wamefariki wamezungumza kuhusu janga hilo lililowakumbuka wakati walipokuwa wakijiandaa kulala.

Usiku wa Jumatano , Pius mzee alikuwa akizungumza na mkewe na wanawe wanne baada ya chakula cha jioni wakati maji yalipovamia nyumba yao.

Alisema alijaribu kukimbia pamoja na wanawe wawili lakini akazidiwa na maji hayo yaliokuwa na kasi.

Mzee huyo alilazimika kusalimu amri baada ya mwamba mkubwa uliokuwa ukisombwa na maji kumgonga.

"Mke wangu alikuwa na watoto wawili na mara moja ikatokea, sikuwaona. Hadi sasa sijui wako wapi’’ , aliambia chombo cha habari cha Nation akiwa katika hospitali ya level 5 mjini Nakuru.

Baadhi ya Wakenya waomboleza

Picha za maeneo yalioathirika na bwawa la Patel eneo la Subukia, Nakuru

Picha za maeneo yalioathirika na bwawa la Patel eneo la Subukia, Nakuru
BBC
Picha za maeneo yalioathirika na bwawa la Patel eneo la Subukia, Nakuru
BBC
Picha za maeneo yalioathirika na bwawa la Patel eneo la Subukia, Nakuru
BBC
Picha za maeneo yalioathirika na bwawa la Patel eneo la Subukia, Nakuru
BBC

Familia 450 zimeathiriwa

Takriban familia 450 zimeathiriwa , watu 47 wakijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Nakuru/Bahati huku wengine 41 wakitibiwa nan a kwenda nyumbani.

Operesheni ya uokoaji inayohusisha maafisa wa KDF na vijana wa huduma za kitaifa NYS inaongozwa na Kamishna wa bonde la ufa

View more on twitter

Miili ya waathiriwa ilipatikana katika matope

Mmoja ya walioshuhudia maafa ya kupasuka kwa bwawa nchini Kenya anasema kuwa wamepata miili iliofukiwa katika matope.

‘’Tulipata miili 11 iliokuwa imefukiwa na matope katika shamba moja la kahawa na hawa ni watu ambao huenda walikuwa wakitoroka lakini hawakufanikiwa kutokana na nguvu na kasi ya maji kutoka kwa bwawa hilo’’ ,alisema.

Wengi wao ni wawawake na watoto ambao hawakuweza kukimbia kwa kasi pamoja na wazee.

Hii ni kwa niaba ya afisa mkuu wa polisi katika eneo la ajali ambaye alizungumza na chombo cha habari cha AFP..

Afisa huyo aliongezea kuwa wafanyikazi wa kukabiliana na dharura walitumia wakati wao mwingi nyaki za usiku miili na kufikia sasa wamefanikiwa kufikia nusu ya eneo hilo.

Badhi ya raia wakiwatafuta wapendwa wao kufuatia mkasa wa kupasuka kwa bwawa mjini Nakuru nchini Kenya
Reuters
Badhi ya raia wakiwatafuta wapendwa wao kufuatia mkasa wa kupasuka kwa bwawa mjini Nakuru nchini Kenya

Wenyeji wa Solai kuandamana

Mlolongo mrefu wa magari unatarajiwa katika barabara kuu ya Nakuru-Nairobi nchini Kenya baada ya wakaazi wa eneo la Reroni kupanga kufunga barabara hiyo kwa kufanya maandamano kuhusu vifo vya Solai

Juhudi za uokoaji zinavyoendelea

Baadhi ya maafisa wa msalaba mwekundu wakisaidiana na vijana wa huduma za kitaifa , wanabeba miili ya walioathirika
BBC
Baadhi ya maafisa wa msalaba mwekundu wakisaidiana na vijana wa huduma za kitaifa , wanabeba miili ya walioathirika
Baadhi ya maafisa wa serikali pamoj na wale wa msalaba mwekundi wakiwatafuta manusura
BBC
Baadhi ya maafisa wa serikali pamoj na wale wa msalaba mwekundi wakiwatafuta manusura

Habari za hivi pundeWatu 27 wafariki baada ya bwawa kuvunja kuta zake

Watu 27 wamefariki na maelfu wengine wameachwa bila ya makaazi wakati bwawa moja mjini Nakuru nchini Kenya lilipovunja kuta zake Jumatano usiku.

Wakaazi wanasema watu wengine zaidi hawajulikani waliko.

Bwawa la Patel mjini Nakuru katika mkoa wa bonde la ufa lilivunja kuta zake jana usiku na kusomba mamia ya nyumba za wakaazi waliokuwa karibu na eneo hilo.

Waziri wa mambo ya ndani Kenya Fred Matiangi amewasili katika eneo hilo.

Bwawa lasababisha vifo vya watu 27 baada ya kuvunja kingo zake
BBC
Bwawa lasababisha vifo vya watu 27 baada ya kuvunja kingo zake
Takriban watu 2500 wameachwa bila makao baada ya bwana kuvunja kingo zake Kenya
BBC
Takriban watu 2500 wameachwa bila makao baada ya bwana kuvunja kingo zake Kenya
Raia wa eneo la Nakuru nchini Kenya wakitazama kwa mshangao baada ya bwawa kuvunja kingo zake kutokana na vua kubwa inayoendelea kunysha nchini humo
BBC
Raia wa eneo la Nakuru nchini Kenya wakitazama kwa mshangao baada ya bwawa kuvunja kingo zake kutokana na vua kubwa inayoendelea kunysha nchini humo

Natumai hamjambo..