Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Mchezaji wa asili ya Tanzania Yusuf Poulsen amewafungia Denmark bao dakika ya 59
 2. Argentina walitoka sare na Iceland mechi iliyochezwa awali 1-1, Ufaransa wakashinda 2-1 dhidi ya Australia
 3. Nigeria wamefungwa 2-0 na Croatia, bao moja likiwa la kujifunga
 4. Lionel Messi alipoteza penalti mechi yao dhidi ya Iceland

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Nigeria walazwa 2-0 na Croatia, Denmark 1-0 Peru, Argentina 1-1 Iceland, Ufaransa 2-1 Australia

Messi ashindwa kufunga penalti dhidi ya Iceland, mchezaji ambaye babake ni Mtanzania Yusuf Poulsen afungia Denmark

Imekuwa siku nyingine ya masikitiko kwa Afrika baada ya mwakilishi mwingine Nigeria kulazwa 2-0 na Croatia katika mechi ya Kundi D.

Misri na Morocco walikuwa Ijumaa wamechapwa 1-0 na Uruguay na Iran.

Matumaini sasa ni kwa Tunisia watakaokutana na England Jumatatu saa tatu usiku na Senegal watakaokutana na Poland Jumanne saa kumi na mbili usiku.

Misri watakuwa tena uwanjani saa tatu usiku siku hiyo dhidi ya wenyeji Urusi.

Siku ilianza kwa mechi za Kundi C katika ya Ufaransa na Australia. Pande zote zilikabidhiwa penalti baada ya refa kushauriana na waamuzi wenzake upande wa teknolojia wa VAR.

Pande zote zilifunga penalti zao, lakini mwishowe Ufaransa iliilaza Australia 2-1 baada ya bao la Paul Pogba kuvuka mstari.

Aidha, kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia mwaka huu, Penalti tano zilitolewa huku mbili kati yao zikipotezwa na wachezaji katika muda wa kawaida wa mchezo.

Katika uwanja wa Spartak mjini Moscow, taifa ndogo la Iceland liliwashangaza wengi baada ya kujitetea dhidi ya Ajentina.

Lionel Messi alinyimwa bao la penalti na kipa wa Iceland Hannes Halldórsson ambaye aliishia kutuzwa mchezaji bora wa mechi. Refa kutoka Poland Szymon Marciniak aliipa Argentina penalti dakika ya 63 baada ya Maximiliano Meza kulazwa na Rurik Gislason.

Ingawa Aguero ailiiweka Argentina kifua mbele dakika ya 19, bao lake lilifutwa na Alfred Finnbogason dakika chache baadaye.

Mchuano huo ulifuatwa na ule wa Denmark na Peru ambapo Denmark ilijinyakulia ushindi kupitia mshambulizi mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen.

Licha ya kupoteza mechi na fursa ya kuongoza kupitia penalti, kikosi cha Peru kiliweka historia kwa kuliwakilisha taifa hilo katika kombe la dunia tangu 1982. Christian Cueva alipoteza mkwaju wake dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika. Shuti lake lilipaa angani.

Kocha wa Denmark Age Hareide amemtaja kipa wake Kasper Schmeichel na mabeki kwa kuchangia ushindi huo.

Siku iliisha na mechi ya Kundi D kati ya Croatia na Nigeria. Makosa ya mabeki yalipelekea Nigeria kulazwa 2-0 na kuninginia mkiani.

Timu hiyo imesalia na kibarua kigumu kwani ndio timu pekee bila alama lkatika kundi hilo

Habari za hivi pundeMechi imemalizika Croatia 2-0 Nigeria

Muda wa ziada Croatia bado kifua mbele

Croatia 2-0 Nigeria

Mashabiki wa Nigeria wana matumaini makubwa lakini muda hauna huruma.

Zimeongezwa dakika 4 za zaida, lakini Croatia ndio inakaribia kuondoka na ushindi.

Kombe la - mikwaju ya penalti?

Penalti tano ndani ya siku moja.

Mechi za kombe la dunia leo zimekaribia kuvunja rekodi ya idadi ya Penalti kutolewa.

Mkwaju wa dakika chache zilizopita uliotiwa kimiani na Luka Modric ni wa tano kukabidhiwa timu.

Rekodi ya Kombe la dunia ni penalti sita ndani ya siku moja.

Habari za hivi pundeCroatia wafunga bao la pili

Luka Modric amewafungia Croatia bao la pili, kupitia mkwaju wa penalti baada ya William Ekong kumuangusha Mario Mandzukic kwenye sanduku.

Modric akifunga
Getty Images

Croatia na Nigeria wafanya mabadiliko

Croatia imeanza kufanya mabadiliko.

Andrej Kramaric amempisha mwenzake Marcelo Brozovic.

Kwa upande mwingine, Nigeria wameamua kujaribu bahati langoni kwa kumleta mchezaji wa Leicester Ahmed Musa, kuchukua nafasi ya kiungo wa Arsenal, Alex Iwobi.

Habari za hivi pundeCroatia wapewa penalti

Croatia 1-0 Nigeria

Croatia wamepewa penalti baada ya William Ekong kumkatalia mchezaji wa Croatia eneo la hatari.

Ekong
Getty Images

Croatia waongoza Kundi D

Iwapo hali itasalia kuwa hivi, timu ya Croatia huenda ikachukua uongozi wa Kundi hilo baada ya Ajentina kutoka sare na Iceland hapo awali.

Croatia inaiongoza Nigeria zikiwa zimekatika zaidi ya dakika 50 kwenye mchuano.

Nigeria waimarika lakini bahati bado haijasimama

Kipindi cha Pili Croatia 1-0 Nigeria

Ni dakika ya 52 sasa. Kipindi cha pili kinaendelea uwanja wa Kaliningrad huku Nigeria ikitawala mchezo dakika za kwanza.

Wanasaka bao la kusawazisha mambo kwa udi na uvumba.

Croatia bado yaongoza.

Kunayo matumaini Nigeria?

Safu ya mashambulizi ya Nigeria inaonekana kuwa butu.

Ighalo na Iwobi wanajitahidi, lakini juhudi hizo hazijaleta mchango mkubwa.

Kulingana na orodha ya wachezaji walioko benchi ya timu hiyo, Ahmed Musa na Kelechi Iheanacho ndio wafungaji wa kutegemewa.

Kazi kwa kocha wa Nigeria Mjerumani Gernot Rohr.

Nigeria
Reuters
Wachezaji wa Nigeria

Mechi yaingia mapumzikoni

Croatia 1-0 Nigeria

Nigeria imesalia na dakika 45 kujinusuru baaada ya awamu ya kwanza kukamilika.

Timu hiyo imebeba matumanini ya raia Milioni 18 pamoja na mashabiki wa Afrika kutoka kila pembe ya dunia.

Tayari wawakilishi wengine kutoka AFrika, Misri na Morocco wamepoteza mechi zao za kwanza.

Nigeria ni timu ya kwanza kutoka AFrika kufungwa katika kipindi cha kwanza katika Kombe la Dunia mwaka huu.

Nigeria na mabao ya kujifunga!

Mabao mawili ya karibuni zaidi waliyofungwa Nigeria Kombe la Dunia ni ya kujifunga.

Mbali na mechi hii dhidi ya Croatia, goli jingine walilojifunga lilikuja kati ya timu hiyo na Ufaransa mnamo 2014 wakati Joseph Yobo alipoelekeza boli kwenye lango lake.

Croatia yakita kambi Nigeria

Winga Ante Rebic, wakishirikiana na mfungaji Mario Mandzukic wamekita kambi eneo la Nigeria.

Wanamuandalia pasi Ivan Perisic, lakini mkwaju wake unapaa.

Kona kwa Croatia lakini refa anaagiza mechi uendelee.

Habari za hivi pundeCroatia wajipatia bao dhidi ya Nigeria

Croatia 1-0 Nigeria

Croatia imechukua uongozi kufuatia kichwa cha Mario Mandzukic kilichoelekezwa langoni na mchezaji wa Nigeria na Peter Etebo.

Jezi za Nigeria ziko wapi?

Nigeria 0-0 Croatia

Ingawa jezi za Nigeria zilizokuwa na mchanganyiko wa rangi nyeupe na njano, zimezua gumzo kutokana na miundo yao, timu hiyo leo imelazimika kutumia jezi za kijani kibichi.

Hii ni kwa sababu Croatia ndio inatambulika kuwa timu iliyoko nyumbani na hivyo basi kutumia jezi nyeupe.

Hata hivyo, mashabiki wa Nigeria uwanjani Kaliningrad wanajivunia kuvaa sare hizo.

Soma zaidi: Jezi za Nigeria zauzwa zote baada ya watu milioni 3 kuagiza

Tazama jezi za nyumbani za mataifa hapa: Jezi za mataifa yanayocheza Kombe la Dunia 2018 urusi

Croatia 0-0 Nigeria

Mchuano unaelekea dakika kumi za kwanza lakini mechi bado ni 0-0.

Baada ya Iceland Kutoka sare na Argentina, atakayepata ushindi kati ya timu hizi atakuwa na nafasi ya kuongoza kundi lao.

Nigeria ilipata mkwaju wa ikabu lakini shuti ya Victor Moses iliondolewa na mabeki wa Croatia.

Vikosi vya Nigeria na Croatia

Croatia:Subasic, Vrsaljko, Lovren, Vida, Strinic, Rakitic, Modric, Rebic, Kramaric, Perisic, Mandzukic.

Wachezaji wa akiba: Livakovic, Corluka, Kovacic, Brozovic, Jedvaj, Bradaric, Caleta-Car, Nikola Kalinic, Badelj, Pjaca, Pivaric, Lovre Kalinic.

Nigeria:Uzoho, Abdullahi, Troost-Ekong, Balogun, Idowu, Ndidi, Etebo, Moses, Mikel, Iwobi, Ighalo.

Wachezaji wa akiba: Ezenwa, Echiejile, Musa, Simy, Iheanacho, Obi, Ogu, Onazi, Awaziem, Ebuehi, Omeruo, Akpeyi.

Refa:Sandro Ricci (Brazil)

Mechi imeanza: Nigeria v Croatia

Nigeria wameanzisha mchezo.

Wachezaji wameingia uwanjani, mechi inaanza saa nne

Nigeria wamesifiwa sana kutokana na mavazi na sare yao.

Nigeria
Nike

Mashabiki wa Nigeria na Croatia uwanjani

Nigeria
EPA
Croatia
Getty Images

Uwanja unaochezewa mechi ya Nigeria v Croatia

Uwanja wa Kaliningrad mjini Kaliningrad ndio unaochezewa mechi ya Nigeria na Croatia.

Uwanja huu ulizinduliwa mwaka huu na una uwezo wa kuwapokea mashabiki 35,212*

Uwanja huu ulio na umbali wa maili 770 kutoka Moscow, uko katikati ya mataifa ya Poland na Lithuania.

Kimuundo, unafanana na uwanja wa Bayern Munich wa Allianz Arena. Uwanja huu mpya ulikumbwa na sakata mbalimbali ikiwemo kusambaratika kwa kampuni iliyokabidhiwa kandarasi ya kwanza.

Awali ulitarajiwa kuwalaki mashabiki 45,000 kabla ya kupunguzwa hadi mashabiki 35,000.

Baada ya kombe la mwaka huu 2018, viti 10,000 vitaondolewa ili kutumika na klabu inayoshiriki daraja la pili ya ligi ya Urusi, Baltika Kaliningrad. Hii ni kwa kuwa ni jumla ya mashabiki 3,500 tu waliohudhuria mechi za klabu hiyo msimu uliopita.

Takwimu muhimu kuhusu Nigeria na Croatia

Mataifa hayo mawili yalipokutana

 • Croatia na Nigeria wanakutana kwa mara ya kwanza
 • Croatia imewahi kuonana na timu moja tu kutoka Afrika kwenye Kombe la Dunia mwezi Juni 2014 ambayo ni Cameroon. Croatia ilishinda 4-0.
 • Nigeria wamewahi kushinda mechi moja tu katika ya sita walizocheza dhidi ya wapinzani kutoka Ulaya walipoilaza Bosnia-Herzegovina mnamo 2014. (Imepoteza 4, ikatoka sare mechi 1).

Croatia

 • Croatia imeandikisha ushindi mechi moja tu kati ya mechi zake saba za mwisho Kombe la dunia. (4-0) dhidi ya Cameroon 2014. (Sare mbili , imepoteza nne).
 • Imekosa kufungwa goli mechi mbili tu kati ya mechi 11 zake za mwisho.
 • Kunzia 2006, Croatia haijawahi kushinda mechi yake ya kwanza kombe la dunia.
 • Mechi zilizoshirkisha Croatia katika makala manne ya kombe la dunia zimeshuhudia kadi nyekundu tano. (tatu kwa Croatia, mbili kwa wapinzani wake).
 • Ivan Perisic amehusika kwenye nusu ya magoli ya Croatia katika Kombe la dunia lililotangulia (mabao mawili na mchango moja).
 • Kocha Zlatko Dalic aliyeajiriwa kuiongoza Croatia Oktoba 2017, wanashiriki shindano kubwa kwa mara ya kwanza akiwa mkufunzi. Timu yake iliifunga Ukraine kwnye mechi yake ya mwisho ya kufuzu kwa kombe la dunia kabla ya Ugiriki kwenye mchujo.

Nigeria

 • Tangu ilipofuzu kwa makala ya 1994, Nigeria imeshiriki kombe la dunia kila wakati isipokuwa mwaka wa 2006.
 • Hakuna timu ya Afrika ambayo imefuzu kwa Kombe la Dunia kuliko Nigeria. Nigeria imeshiriki mara sita ikiwemo 2018.
 • Kati ya mechi zake 12 zilizopita katika Kombe la Dunia, Nigeria imeshinda tu mara moja (imepoteza mechi nane na kutoka sare mechi mbili mbili).
 • Ushindi wao pekee umekuja dhidi ya Bosnia-Herzegovina 2014 (1-0).
 • Meneja wao, Gernot Rohr, aliyekabidhiwa kikosi Agosti 2016 anashiriki kombe la dunia akiwa mkufunzi kwa mara ya kwanza.
 • Nigeria ni timu yake ya nne kutoka Afrika anayoinoa baada ya kuzifunza Gabon, Niger na Burkina Faso.
 • Nigeria ndio timu yenye umri mdogo zaidi katika Kombe la Dunia mwaka huu. Kwa kadiri, mchezaji wa Nigeria ana umri wa miaka 25 na siku 336.

Wachezaji watakaoanza mechi wametangazwa

Nigeria
BBC
Croatia
BBC

Sokwe mtabiri aibuka Croatia v Nigeria

Pweza Paul alipata umaarufu sana kwa utabiri wake wa matokeo ya mechi Kombe la Dunia 2010. Mwaka huu Urusi alitokea paka kwa jina Achilles aliyetabiri matokeo mechi ya Urusi na Saudi Arabia, kwamba wangeshinda.

Walishinda 5-0.

Sasa, Croatia mjini Zagreb kuna sokwe ambaye anafanya utabiri.

Ndiye huyu kazi. Hatujabaini hata hivyo matokeo ya ubashiri wake.

Soma zaidi kuhusu paka Achilles hapa: Paka mtabiri anayetaka kumrithi Paul the Octopus atabiri mshindi mechi ya Urusi na Saudi Arabia

Sokwe mtabiri
Rex Features

Furaha ya kufunga: Yusuf Poulsen alivyosherehekea

Mchezaji ambaye babake ni Mtanzania Yusuf Yurary Poulsen ndiye aliyefunga bao pekee mechi kati ya Denmark na Peru.

Alifunga dakika ya 59.

Soma zaidi kumhusu hapa:Mchezaji wa asili ya Tanzania kucheza Kombe la Dunia

Tazama alivyosherehekea:

Poulsen akisherehekea kufunga
AFP/Getty
Poulsen akisherehekea kufunga
Poulsen kisherehekea na wenzake
AFP/Getty Images
Akisherehekea na wenzake

Mechi yamalizika Denmark 1-0 Peru

Mechi imemalizika Peru wakiwa na mpira wa kurusha. Walikuwa wamezidisha mashambulizi.

Poulsen alishwa kadi ya manjano

Poulsen ameoneshwa kadi ya manjano, akijaribu kuvuruga shambulizi la Peru dakika za mwisho. Ni dakika ya 90+3 sasa.

Dakika ya 89, Peru wanazidi kushambulia Denmark

Peru wanaendeleza mashambulizi huku muda ukiyoyoma. Mechi imeongezwa dakika tano.

Poulsen afanya kazi ya ziada kwenye lango

Baadaya kipa wa Denmark kubwagwa na mpira wa juu, Poulsen ameruka juu langoni na kuupiga mpira, ukirejea chini tena kipa wao akawa amejiweka sawa na kuudaka.

Peru wameanza kushambulia zaidi baada yao kuufngwa.

Habari za hivi pundePoulsen awafungia Denmark

Denmark 1-0 Peru

Ni bao lake la tano akichezea timu ya taifa ya Denmark

Amepata pasi kutoka kwa Christian Eriksen.

Denmark walianza mechi bila kasi lakini kadiri mechi ilivyoendelea ndivyo walivyozidi kuimarika.

Soma zaidi kumhusu hapa: Mchezaji wa asili ya Tanzania kucheza Kombe la Dunia

Mchezaji wa asili ya Tanzania Yusuf Poulsen asababisha penalti

Yussuf Yurary Poulsen ambaye babake alitoka Tanga amesababisha penalti. Lakini Peru wameshindwa kufunga, Sasa ni wakati wa mapumziko.

Poulsen
FIFA/Getty Images

Peru inaonyesha mchezo mzuri dhidi ya Denmark

Peru inatawala mchezo
BBC Sport

Christian Ericksen akabwa

Nyota wa klabu ya Tottenham nchini Uingereza Christian Ericksen akabwa na wachezaji wa Peru.

Denmark inachezewa hapa na kulazimika kufukuzia vivuli

Vikosi vya timu zote mbili

Kikosi cha Peru
BBC Sport
Kikosi cha Denmark
BBC Sport

Mechi inaanza

Kombe la Dunia 2018: Denmark 0-0 Peru

Argentina 1-1 Iceland

Argentina wapata mkwaju wa adhabu

Na mechi inakamilika