Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji alitekwa Alhamisi alfajiri wakati alipokuwa akielekea mazoezini Dar es Salaam
 2. Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema polisi wanaendelea na operesheni ya kumtafuta
 3. Waziri wa Muungano na Mazingira Tanzania Januari Makamba amesema amezungumza na baba mzazi wa Mo ambaye amethibitisha kuwa tajiri huyo alitekwa
 4. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda amesema vyombo vyote vya usalama viko kazini

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Kutwekwa kwa Mo Dewji: Msemaji wa Simba Haji Manara akamatwa

  Msemaji wa Simba Haji Manara amekamatwa na kuzuiliwa kuhusiana na sakata la kutekwa kwa Mo Dewji.

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema Manara anashikiliwa kutokana na kusambaza taarifa za tukio hilo la kutekwa kwa Mo kwenye mitandao kwa madai ya kutumwa na familia, bila kutumwa na familia hiyo.

  “Hajatumwa na familia hivyo tunamshikilia,” amesema Mambosasa.

 2. Maswali yanayogonga vichwa kutekwa kwa Mo Dewji

  Kutekwa kwa tajiri Mo Dewji kumewaacha wengi katika lindi la mshangao na suitafahamu.

  Kuna maswali kadhaa ambayo yamekuwa yakijitokeza toka iliiporipotiwa kutokea kwa tukio hilo Alhamisi asubuhi na kupatikana kwa majibu yake kunaweza kukatoa mwangaza wa kulielewa tukio lenyewe na pengine kupelekea kupatikana kwa tajiri huyo.

  Baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa vimenukuu vyanzo kutoka jeshi la polisi Tanzania kuwa yawezekana kuwa Mo ametekwa kwa sababu za kifedha, ikihisiwa watekaji watadai komboleo ili wamuachie huru.

  Mpaka sasa si familia wala mamlaka za nchi ambazo zimeeleza sababu rasmi ya tukio hilo. Hivyo haifahamiki ni kwanini tajiri huyo ametekwa.

  Soma zaidi: Maswali yanayogonga vichwa kutekwa kwa Mo

 3. Dewji atanda katika magazeti Tanzania

  Kwa kiasi fulani taarifa kuhusu kutekwa kwa Mo Dewji zimegubika magazeti Tanzania leo

  Magazeti leo Tanzania
 4. Siku ya pili, Mo Dewji bado hajapatikana

  Watu 12 wanashikiliwa na jeshi Tanzania kutokana na tukio hilo

  Imeingia siku ya pili leo tangu tajiri mashuhuri nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla Mo Dewji atekwe nyara na watu wasiojulikana.

  Mo alitekwa jana alfajiri wakati akielekea katika ukumbi wa mazoezi katika hoteli moja ya kifahari jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa taarifa ya mwisho ya polisi jana jioni, watu 12 wanashikiliwa na jeshi hilo kutokana na tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea.

  Mamlaka zinatarajiwa kueleza umma leo Ijumaa wamefikia wapi na uchunguzi wao mpaka sasa.

  Bado haijafahamika ni akina nani wamehusika na uhalifu huo licha ya mamlaka kusema kulikuwa na wazungu wawili walioshiriki.

  Mo, mwenye miaka 43, anakisiwa na jarida la masuala ya kifedha la Forbes kuwa na utajiri wa dola bilioni 1.5 kiasi kinachomfanya kuwa tajiri namba moja Afrika Mashariki na tajiri mwenye umri mdogo zaidi Afrika nzima.

 5. Washukiwa 12 'wazuiliwa' kuhusiana na kutekwa kwa Dewji

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji wamefikia 12.

  Bw Dewji bado hajulikani alipo baada ya kutekwa mapema asubuhi jijini Dar es Salaam.

 6. Sababu iliyomfanya Mo Dewji kurejea Tanzania

  Mo Dewji alisomea Marekani na mpango wake ulikuwa kusalia na kufanya kazi huko.

  Ilikuwaje mwishowe akajipata Tanzania?

  Mwezi Septemba, aliandika kwenye Instagram sababu iliyomfanya kurejea, ambapo anasema ni ushauri wa babake pamoja na kugundua kwamba kulikuwa na fursa nyingi Tanzania.

  Ujumbe aliouandika 10 Septemba, 2018 ndio huu:

  Quote Message: Nilipomaliza masomo yangu ya shahada nikiwa nchini Marekani niliamua kubaki huko na kufanya kazi. Nilitumia muda na nguvu nyingi kazini lakini pesa ambayo niliipata haikukidhi kufanikisha malengo yangu.
  Quote Message: Ndipo Baba yangu akanishauri nirejee nyumbani Tanzania na nilipofatilia kwa kipindi hicho niligundua kwamba Tanzania kuna fursa nyingi za kibiashara na hapo ndipo nilipoamua kurudi na kujiunga katika biashara ya familia.
  Quote Message: Muhimu kufahamu ni kwamba mafanikio sio lazima uende kuyatafuta nje ya nchi, hapa hapa nchini kwetu kuna fursa ambazo ukifanyia kazi utafanikiwa. Unafikiri kwanini baadhi ya watu wanapenda kuishi/kufanya kazi nje ya nchi?
 7. Mambosasa: Dewji bado hajapatikana, Coco Beach taarifa ni za uongo

  Mambosasa

  Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema Mo Dewji kufikia sasa bado hajapatikana.

  “Dewji bado tunaendelea kumfuatilia na kuwafuatilia watu waliofanya uhalifu huo, wa kumteka.

  “Zipo taarifa mtaani kwamba ameshapatikana, wengine wanadai kwamba amepatikana kule Coco Beach lakini taarifa kutoka meza yangu hii, na taarifa ambazo sasa ni taarifa rasmi, bado hajapatikana wala wahusika bado hawajakamatwa.

  “Jeshi la polisi linaendelea na operesheni kali kufuatia tukio hilo, mikoa yote mitatu tunaendelea na ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha kwamba tukio hili ambalo ni la aina yake na ambalo limefanywa na raia wa kigeni halipati nafasi ya kuchafua taswira nzuri ya Tanzania kwa maana ya mahali ambapo wahalifu, vinaendelea kukemewa kwa pamoja.

  “Mahali ambapo watu wameendelea kuita ni kisiwa cha amani.”

 8. Kituo cha mazoezi alikotekwa Dewji chafungwa

  Kituo cha mazoezi cha Colosseum ambako Mo Dewji alikuwa anakwenda kwa mazoezi alipotekwa kimefungwa.

  Kumebandikwa langoni kwa nia ya kuomba radhi kuwa kituo hicho kwa leo kimefungwa kwa sababu zisizozuilika na kitafunguliwa hapo kesho.

  Baadhi ya walinzi waliokuwepo eneo la tukio kwa mda huu wa mchana walizuia waandishi wa habari kuingia ndani, lakini eneo la kuegesha magari la nje lilionekana kuwa na watu wachache huku waandishi kadhaa wa habari wakiingia na wengine kuondoka.

  Walinzi waliokuwa kwenye zamu wakati wa tukio pamoja na mmiliki wa hoteli hiyo wanahojiwa na polisi.

  Colosseum
  Colosseum
  Image caption: Watu wakipiga picha langoni
  Gari la Dewji
  Bango langoni
 9. Ushabiki wa Mo Dewji kwa Simba FC

  Mohammed Dewji ni mfadhili wa klabu ya Simba inayocheza Ligi Kuu Tanzania.

  Hivi karibuni amekuwa akifurahia maendeleo kwenye klabu hizo na zaidi kujengwa kwa uwanja wa mazoezi.

  Wiki iliyopita, aliandika kwenye Twitter: "Kwa miaka mingi nimekuwa nikiota na sisi tuwe na uwanja wetu wa mazoezi, na ninafurahi sasa ninawezesha ndoto hii baada ya miaka 82 tangu kuanzishwa kwa klabu ya SIMBA. Nimeanza kukamilisha ahadi ya uwanja wa Bunju. Insha'Allah kazi ya ujenzi itakamilika kabla ya mwezi wa 2, 2019"

  View more on twitter
  View more on twitter
 10. Simba FC washtushwa na kutwekwa kwa Dewji

  Klabu ya kandanda ya Simba ambayo Mohammed Dewji amewekeza kwa asilimia 49 imesema imeshtushwa na taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo tajiri.

  Ofisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema pamoja na mshtuko walionao, wanaaminini litafanya kazi yake na na kuhakikisha kuwa mfanyabiashara huyo maarufu kama Mo anapatikana.

  Manara ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa uongozi wa klabu hiyo upo katika huzuni kubwa kwa kuwa ni jana tu walikuwa naye tajiri huyo katika kikao cha bodi ya wadhamini wa klabu hiyo na alikuwa na furaha wakati wote.

  Amewataka wapenzi na mashabiki wa Simba wawe watulivu wakiliachia jeshi la polisi kufanya kazi yake na kwamba wanaamini Mo Dewji atapatikana akiwa hai.

 11. Busara ya Mo Dewji na kauli yake kuhusu watoto na wanawake

  Mfanyabiashara aliyetekwa Mo Dewji ni mtu aliyefanikiwa sana kibiashara na watu wengi humfuatilia katika mtandao wa Twitter.

  Mara kwa mara, hutoa ushauri, na pia huwa hafichi upendo wake kwa klabu ya Simba FC ambayo ndiye mdhamini wake mkuu.

  Ijumaa wiki iliyopita, aliandika: "Kila jambo unaloogopa, Mungu ana mpango wake. Mungu ni mkuu kuliko hofu uliyonayo. Ana mamlaka na maisha yako ya baadae. Kuwa na imani."

  View more on twitter

  Kuhusu urafiki na mikopo, kauli yake hii:

  View more on twitter

  Kuhusu utajiri na umaskini, aliweka nukuu hii aliyoitoa kwingine pengine: "Walio fukara hujaribiwa kwa umaskini, sisi nao hujaribiwa kwa kupewa zaidi ya tunavyovihitaji."

  View more on twitter

  Ana ushauri pia kuhusu kufanikiwa maishani:

  View more on twitter

  Kuhusu kuwezeshwa kwa wanawake:

  View more on twitter

  Kuhusu kuwa mfano bora kwa watoto: "Hata tunapofikiri hawatuoni, wanatuona. Hata tunapofikiri hatulei, tunalea"

  View more on twitter
 12. Watanzania washangazwa na kutekwa kwa Mo Dewji

  Watanzania mtandaoni wamekuwa wakieleza kushangazwa na kusikitishwa kwao na kisa cha kutekwa kwa tajiri Mo Dewji mapema leo.

  Baadhi wameeleza wasiwasi kwamba visa kama hivi vinavyowahusisha 'watu wasiojulikana' vimekuwa vingi mno na mara nyingi havipati ufumbuzi.

  Mbunge wa upinzani Zitto Kabwe amesema:

  View more on twitter

  Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amesema:

  View more on twitter

  Ubalozi wa Italia nchini Tanzania pia umeshtushwa na kisa hicho.

  View more on twitter

  Hilda Newton kwenye Twitter anasema kisa hicho kinaonesha hakuna aliye salama lakini Ali Kibao anamjibu kwamba "ni tukio la kawaida tu".

  View more on twitter
 13. Mo Dewji ni nani hasa na mbona ni maarufu?

  Kwa mujibu wa jarida maarufu la masuala ya fedha la Forbes, ana utajiri wa dola bilioni 1.5.

  Mo mwenye umri wa miaka 43 ndiyo tajiri namba moja Afrika Mashariki, na pia miongoni ma matajiri wa umri mdogo zaidi Afrika.

  "Alinunua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti," inaongeza ripoti hiyo.

  Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na baba yake miaka ya 1970.

  Soma zaidi: Kumfahamu Mo Dewji

 14. Taarifa ya Makonda kuhusu Mo Dewji ilivyozua utata

  Bw Makonda baada ya kikao chake na wanahabari
  Image caption: Bw Makonda baada ya kikao chake na wanahabari

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekanusha taarifa za kupatikana kwa mfanyabishara Mohammed Dewji.

  Amesema kwamba taarifa zilizosambaa kuwa amepatikana sio za kweli.

  Taarifa hizo zilikuwa zinamnukuu Bw Makonda.

  Hata hivyo, alikuwa amenukuliwa visivyo.

  Bw makonda alikuwa amewaambia wanahabari kwamba habari sahihi au ambazo wengi wanazisubiri ni kwamba "Mo amepatikana, na wahalifu wametiwa mikononi mwa vyombo vyetu vya dola."

  Wengi walichukulia hilo kuwa tangazo la kupatikana kwa Mo Dewji.

  "Ninayo matumaini ya weledi na ukubwa wa jeshi letu la polisi na vyombo vyengine tutahakikisha ndugu tumepata akiwa salama.

  "Naomba kuwatoa hofu wanahnchi, mkoa wa Dar es salaam bado ni shwari na wa amani. Tusiwepo na taarifa za kuchanganyana na kupeana maneno ya kutishana watu wakaogopa hata kwenda kufanya kazi.

  Na ndio maana hata Mo mwenyewe angeweza kuwa na mabodyguard (walinzi) lakini kwa sababu ya amani iliyoko katika mkoa wetu, anatembea peke yake," amesema Bw Makonda.

 15. Polisi: Mo Dewji alitekwa na Wazungu wawili

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameambia wanahabari kwamba waliomteka Mohamed Dewji ‘Mo’ ni wazungu wawili.

  Akizungumza na wanahabari nje ya hoteli ya Colosseum, amesema kufikia sasa watu wawili wanazuiliwa.

  "Asubuhi ya leo Wazungu wawili walikuwa na gari aina ya Surf. Kulikuwa na magari mawili, moja lilikuwa ndani na lingine nje, gari la ndani liliwasha taa ghafla na lile lililokuwa nje likaingia na kwenda kupaki karibu na gari la Mo Dewji lililokuwa limepaki,” amenukuliwa na gazeti la Mwananchi.

  “Na Mo akiwa ndani ya gari hilo Wazungu wawili wakatoka na kumbana MO Dewji baada ya kutoka ndani ya gari lake na kisha kumpakia katika gari lao aina ya Surf kisha wakaondoka naye kusikojulikana.”.

 16. Makamba: Nimesikitishwa na taarifa za kutekwa kwa Mo Dewji

  Waziri wa Muungano na Mazingira Tanzania Januari Makamba ambaye ni rafiki wa karibu wa Mo Dewji ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa amezungumza na baba mzazi wa Mo ambaye amethibitisha kuwa mfanyabiashara huyo ametekwa.

  Amesema amesikitishwa sana na kisa hicho.

  View more on twitter
 17. Mo Dewji alitekwa eneo la Oyster Bay

  Mo Dewji

  Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio hilo, Mo alifika katika hoteli moja ya kifahari katika eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam kama ilivyo ada yake kila siku alfajiri kwa ajili ya kufanya mazoezi ya viungo.

  Hatahivyo, punde aliposhuka tu kwenye gari yake, watu wasiofahamika walijitokeza na kufyatua risasi hewani kisha kumnyakua mfanyabiashara huyo na kutokomea nae kwenye gari lao.

  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema taarifa za awali zinazonesha waliohusika katika utekaji wa mfanyabiashara huyo ni watu wawili ambao ni raia wa kigeni.

 18. Mo Dewji atekwa nyara Dar es Salaam

  Mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji alitekwa leo alfajiri wakati alipokuwa akielekea mazoezini, vyombo vya usalama nchini Tanzania vimethibitisha.