Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Asante!

  Ni hayo tu katika taarifa za moja kwa moja leo kuhusu Kimbunga Kenneth.

  Unaweza hatahivyo kufuatilia taarifa zaidi kuhusu haya na mengine mengi zaidi katika mtandao wetu wa BBC Swahili.

 2. Je unafahamu lini mwisho Kimbunga kilishuhudiwa Tanzania?

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imebainisha kuwa kimbunga cha mwisho kuikumba nchi hiyo kilikuwa mwaka 1952 mkoani Lindi.

  Kipindi hicho nchi ilikuwa chini ya ukoloni wa Mwingereza na ilikuwa bado ikiitwa Tanganyika.

  "Wakati ule Lindi haikuwa na watu wengi, na wala hakukuwa na miundombinu mingi ya kuharibiwa kama ilivyo kwa sasa," amesema Agness Kijazi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA.

  Soma Zaidi

  Ramani Kimbunga
 3. Watu 3 wafariki katika kimbunga Kenneth

  Kimbunga hicho kilichotuwa kwa upepo mkali wa kasi ya 220km/h kimesababisha vifo vya watu watatu katika visiwa vya Comoro.

  Idara ya kitaifa ya kukabiliana na majanga nchini Msumbiji, inaeleza kwamba takriban watu 30,000 wamehamishwa kutoka maeneo ambayo yalitarajiwa kuathirika na kimbunga hicho.

  View more on twitter
 4. Kimbunga Kenneth chafifia

  Mtandao mmoja wa habari Afrika kusini umeeleza katika Twitter kwamba kimbunga Kenneth kimepungua kasi na upepo unatulia, lakini mvua kubwa bado zinatabiriwa katika siku nne zijazo kaskazini mashariki mwa Msumbiji.

  View more on twitter
 5. Kumekucha Mtwara

  Wakaazi wa Mtwara wameamkia siku nyingine, na hali ni kama kawaida.

  Wafanyabiashara wanaendelea na shughuli, baadhi ya maduka yamefungulia na mengine kadhaa yakisalia kufungwa.

  Mkaazi mmoja kwa jina Pius Mkamare ameieleza BBC kwamba walikuwa na wasiwasi,

  'Tangu jana nilikuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na hali mbaya ya hewa, ki ukweli kwasababu tahadhari lazima tuchukuwe.

  'Lakini nimshukuru Mungu kwasababu hali ilivyo sasa ni hali ya shwari amani inaonekana na watu wanaendelea na shughuli zao'.

  Mtwara
  Mtwara
 6. Kimbunga Kenneth: Kinaweza kurudia kupiga tena Msumbiji?

  Comoros

  Kimbunga Kenneth tayari kimefanya uharibifu kaskazini mwa Msumbiji, huku bado nchi hiyo inatarajia dhoruba nyingine kubwa.

  Kimbunga hicho kimepungua katika saa chache zilizopita lakini utabiri wa hali ya hewa unategemea kuwa kutakuwa na mvua kubwa ambayo itasababisha mafuriko.

  Idara ya kuthibiti majanga nchini Msumbiji imesema watu elfu thelathini wamehamishwa katika makaazi yao ambapo dhoruba ya kimbunga inaweza kupiga tena.

  Kwa mengi zaidi: Bonyeza Hapa

 7. Dhoruba imekuwaje baada ya Kimbunga Kenneth kutuwa?

  Visiwa vya Comoro vimekabiliwa na uharibifu uliotokana na kimbunga Kenneth, kilichotuwa kwa upepo mkali katika visiwa hivyo ulioambatana na mvua kubwa. Upepo mkali umesababisha umeme kupotea, na pia uharibifu katika baadhi ya makaazi ya watu. Wakaazi huko kusini mwa Tanzania Mtwara waliarifiwa kuelekea katika maeneo ya juu, lakini baadhi wamekiuka agizo hilo.

  View more on twitter
 8. Shuka chini kusoma hali ilivyokuwa Alhamisi

  Pata kufahamu taarifa zaidi kuhusu mambo yanavyojiri baada ya kimbunga Kenneth kutuwa kupitia

  BBC Swahili

 9. Hofu ya Kimbunga Kenneth: Zanzibar yasitisha safari za baharini

  Mamlaka ya baharini kisiwani zanzibar ZMA imesitisha kwa muda uchukuzi wa baharini kuelekea na kutoka kisiwani humo kufuatia habari kwamba kimbunga Kenneth kinakaribia eneo la kusini mwa pwani ya Tanzania.

  Naibu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Ramadhan Hussein alisema kuwa mamlaka hiyo imelazimishwa kusitisha safari zote za baharini hadi ilani nyengine itakapotolewa ili kuzuia maafa yoyote.

  Aidha amewataka wavuvi kusitisha uvuvi hadi pale kimbunga hicho kitakapopita.

  Meli
  Image caption: Meli
 10. Tanesco yawatahadharisha wateja wake Lindi na Mtwara

  Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetaka wateja wake wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuendelea kuchukua tahadhari ya uwezekano wa kuwepo kwa Kimbunga ikiwemo kutojikinga na mvua chini ya nguzo zilizobeba transfoma.

  Taarifa iliyotolewa na Tanesco imeeleza kuwa wananchi wanatakiwa kuwa mbali na miundombinu ya umeme na kutokaa chini ya nguzo zote zenye nyaya.

  Tanesco imeshauri pia iwapo kimbunga kitaambatana na radi, upepo mkali au umeme kupungua nguvu na kuongezeka nyumbani, wanatakiwa kuuzima kwenye kifaa cha 'main switch'.

  Taarifa za uwezekano wa kuwepo kimbunga kilichopewa jina Keneth mikoa ya kusini zinaendelea kutolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

 11. Kimbunga Kenneth chawasili Msumbiji kikiwa na kasi ya kilomita 220 kwa saa

  Maelfu ya watu wameondolewa na kupelekwa katika maeneo mengine nchini Msumbiji huku kimbunga Kenneth chenye nguvu kikiwasili katika eneo la kadskazini ya Msumbiji.

  Kimbunga hicho kilikuwa na upepo wenye kasi ya kilimota 220 kwa saa sawa na tufani ya awamu ya nne.

 12. Utulivu washuhudiwa Mtwara na Lindi

  Utulivu unaendelea kushuhudiwa katika eneo la Mtwara mjini pamoja na Lindi.

  Mjini Mtwara watu wanaoenakana wakiendelea na shughuli zao za kawaida lakini sio wengi kama ilivyo kawaida.

  Maduka yamefungwa mapema.

 13. Kimbunga Kenneth kusomba maji ya bahari hadi nchi kavu

  Kimbunga hicho kinatarajiwa kusomba maji ya bahari hadi ufukweni kwa urefu wa mita kadhaa.

  Wiki sita zilizopita , kimbunga kama hicho kilipiga eneo la katikati la msumbiji na kuwawau takriban watu elfu moja huku kikiathiri mamilioni ya watu.

 14. Habari za hivi pundeKimbunga Kenneth kufanya uharibifu mkubwa Msumbiji

  Kimbunga Kenneth ni cha kwanza katika eneo la Tropiki kikiwa na uwezo wa tufani baada ya kupiga mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji wa Cabo Delgado .

  Kimbunga hicho kilipata nguvu katikati ya wiki hii na kuwa sawa na tufani ya awamu ya nne katika bahari ya Atlantic mashariki mwa bahari ya Pacific kabla ya kuwasili.

  Kimewasili katika mkoa wa Cabo Delgado kati ya Palma na Pemba siku ya Alhamisi jioni.

  Kabla ya kuwasili Msumbiji , Kenneth kiliwaua watu watatu katika taifa la kisiwani la Comoros siku ya Jumatano usiku.

  Maeneo ya eneo ambalo kimewasili kimbunga hicho yanakabiliwa na uharibifu mkubwa kutokana na upepo wenye kasi kubwa , mafuriko na maporomoko ya udongo.

  Hatari hiyo itaongezeka wakati kimbunga hicho kitakapoingia katika nchi kavu.

 15. Kimbunga cha mwisho Tanzania kilipiga 1952

  Wakati upwa wa kusini mwa Tanzania ukijiandaa na makali ya Kimbunga Kenneth kinachotarajiwa muda wowote kuanzia leo usiku mpaka Ijumaa alfajiri, mamlaka nchini humu zimebainisha kuwa mara ya mwisho kwa wnwo hilo kupigwa na tufani ilikuwa takribani miongo saba iliyopita.

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imebainisha kuwa kimbunga cha mwisho kuikumba nchi hiyo kilikuwa mwaka 1952 mkoani Lindi.

  Kipindi hicho nchi ilikuwa chini ya ukoloni wa Mwingereza na ilikuwa bado ikiitwa Tanganyika.

  "Wakati ule Lindi haikuwa na watu wengi, na wala hakukuwa na miundombinu mingi ya kuharibiwa kama ilivyo kwa sasa," amesema Agness Kijazi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA.

  Taarifa zaidi: Bonyeza

 16. Kimbunga Kenneth hakitotua Pwani ya Kenya

  Idara ya hali ya hewa nchini kenya imekanusha taarifa amabzo zimekuwa zikisambaa kwamba Kimbunga Kenneth kitapita katika pwani ya Kenya.

  Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii Twitter, idara hiyo imeeleza kwamba kwa ufafanuzi wa kifisikia, vimbunga haviwezi kukaribia kiasi hicho karibu na ikweta. Hatahivyo imeeleza kwamba athari za kimbunga hicho huenda zikadhihirika kwa mfumo wa mvua nyingi katika maeneo ya Isiolo, magharibi mwa nchi, Samburu na ikiwemo Nairobi.

  View more on twitter