Kenya yaupinga uchunguzi wa wizi wa fedha za Covid-19
ReutersCopyright: Reuters
Wanasiasa walihusishwa na mikataba ya kusambaza vifaa vya kujikinga na maambukizi (PPE)Image caption: Wanasiasa walihusishwa na mikataba ya kusambaza vifaa vya kujikinga na maambukizi (PPE)
Waziri wa afya nchini Kenya amepuuzilia mbali taarifa
ya uchunguzi iliyodai kuwa kulikuwa na wizi mkubwana kutoweka kwa mamilioni ya dola za msaada
kutoka kwa wahisani pamoja na vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kuisaidia nchi
kudhibiti kusambaa kwa Covid-19.
Taarifa ya uchunguzi wa televisheni nchini humo ilidai
kuwa misaada ya zaidi ya dola milioni 400 haikuweza kubainika ilitumiwa vipi, huku
visa vya maambukizi ya virusi
vya corona vikiendelea kuongezeka nchini.
Wahudumu wa afya nchini Kenya wametishia kufanya mgomo kutokana na ukosefu
wa vifaa vya kujikinga na maambukizi wawapo kazini.
Uchunguzi huoulidai kuwa watu binafsi ,wakiwemo wanasiasa,
walinufaika na mikataba ya kusambaza vifaa vya kujikinga(PPE), zikiwemo barakoa
zinazotumiwa na wahudumu wa afya na magauni.
Baadhi ya makampuni ambayo
yalizawadiwa mikataba ya mamilioni ya dola yalikuwa yameundwa tu miezi michache
ya awali, ilidai taarifa hiyo ya uchunguzi.
Makampuni mengine yaliyoshinda zabuni yalikuwa na uhusiano na maafisa wa
ngazi ya juu serikalini jambo lililoibua maswali juu ya uhalali wa kisheria wa
wao kupewa zabuni hizo.
Akiwa mbele kamati ya bunge Waziri wa afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe,
alielezea yaliyofichuliwakatika taarifa
hiyo kama uongo na akasema wizara yake inaweza kueleza matumizi ya msaada wa thamani
ya zaidi ya dola milioni 200 ilioupokea.
Lakini uchunguzi huo unadai kuwa mara
mbili ya pesa hizo haziwezi kuelezwa zilitumiwa vipi. Serikali inapinga madai
hayo.
Italia yaipatia msaada Tunisia iwazuwie wahamiaji
AFPCopyright: AFP
Meli ya wahamiajiImage caption: Meli ya wahamiaji
Serikali ya Italia inasema kuwa itatoa dola milioni 13 kwa taifa la Tunisia kulisaidia kuimarisha mpaka wake wa majini na kuwazuwia wahamiaji kuvuka bahari ya Mediterranean katika maboti madogo.
Katika ziara yake mjini Tunis, Waziri wa mambo ya nje wa Tunisia, Luigi Di Maio, alisema kuwa hakuna nafasi zaidi nchini mwake kwa ajili ya kuwapokea wahamiaji haramu waliowasili kinyume cha sheria.
Serikali ya Italia ilikuwa tayari umeishatoa mafunzo ya kijeshi kwa vikosi vya Tunisia vya majini na nchi kavu kwa ajili ya kuwazuwia wahamiaji wanaoondoka kuomba hifadhi nchini Italia.
Italia imekua ikihangaika kukabiliana na wimbi la maelfu ya wahamiaji wanaowasili nchini hkwenye fukwe za kusini mwa nchi hiyo, kazi ambayo ilikuwa ni ngumu zaidi hasa wakati huu wa mzozo wa virusi vya corona.
Post update
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Ilidaiwa kuwa watoto hao wangeenda Marekani kusomeshwaImage caption: Ilidaiwa kuwa watoto hao wangeenda Marekani kusomeshwa
Serikali ya Marekani imewasilisha kesi ya udanganyifu na
usafirishaji haramu dhidi ya wale waliohusika na mpango wa uasili wa watoto ambao
walikuwa si yatima na kuwatoa kwa
familia za Wamarekani.
Watoto wa Uganda walichukuliwa kutoka katika familia zao kwa ahadi kuwa
watasomeshwa katika shule maalumu nchini Marekani.
Badala yake walifikishwa mahakamani kama
yatima kwa ajli ya kuasiliwa na Wamarekani.
Marekani imewawekea vikwazo
raia wanne wa Uganda miongoni mwao majaji wawili kwa kuhusika katika biashara
haramu ya kimataifa ya mfumo wa uasili.
Taarifa ya
Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani iliyotolewa Jumatatu, inasema kuwa Jaji wa ngazi ya juu Wilson Musalu Musene na
Mkuu wa zamani wa kitengo cha uhalifu wa kimataifa, Jaji mstaafu Moses Mukiibi walishiriki katika njama ambapo
watoto wadogo walichukuliwa kutoka kwenye familia zao na kukabidhiwa kwa mtandao
haramu unaowaasili kwa njia za ufisadi
kwa kusaidiwa na maafisa wa Uganda.
Hongo
zinadaiwa kulipwa kwa majaji hao wawili ili wahalalishe kesi za watoto hao.
Mawakili
wawili ambao pia wamewekewa vikwazo hivyo ni , Dorah Mirembe na Patrick Ecobu ambao wanadaiwa kusaidia kutoa
hongo kwa majaji wa Uganda na maafisa wengine ili kuidhinisha mchakato wa kesi
za uasili kinyume cha sheria.
Habari za moja kwa moja
time_stated_uk
Misururu mirefu yashuhudiwa kwenye maduka ya pombe Afrika Kusini
Afrika Kusini imelegeza sheria za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona na kuweka kiwango cha piliJumanne, na kuruhusu mauzo ya pombe na sigara.
Chini ya sheria mpya, mauzo ya pombe yanaruhusiwa kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi kati ya saa tatu za aubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Misururu imekuwa ikionekana nje ya maduka ya pombe katika miji mikubwa nchini humo.
Watu pia wanaruhusiwa kusafiri baina ya mikoa. Imeruhusiwa Kuwatembelea watu wa familia na marafiki lakini kwa makundi mawili.
Mbuga za wanyama na fukwe zimeefunguliwa ili kuwaruhusu watu kujivinjari na matukio yamichezo ili kuruhusu watu kuyatembelea
Uvaaji wa barakoa kwenye maeneo ya umma ni lazima.
Kenya yaupinga uchunguzi wa wizi wa fedha za Covid-19
Waziri wa afya nchini Kenya amepuuzilia mbali taarifa ya uchunguzi iliyodai kuwa kulikuwa na wizi mkubwana kutoweka kwa mamilioni ya dola za msaada kutoka kwa wahisani pamoja na vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kuisaidia nchi kudhibiti kusambaa kwa Covid-19.
Taarifa ya uchunguzi wa televisheni nchini humo ilidai kuwa misaada ya zaidi ya dola milioni 400 haikuweza kubainika ilitumiwa vipi, huku visa vya maambukizi ya virusi vya corona vikiendelea kuongezeka nchini.
Wahudumu wa afya nchini Kenya wametishia kufanya mgomo kutokana na ukosefu wa vifaa vya kujikinga na maambukizi wawapo kazini.
Uchunguzi huoulidai kuwa watu binafsi ,wakiwemo wanasiasa, walinufaika na mikataba ya kusambaza vifaa vya kujikinga(PPE), zikiwemo barakoa zinazotumiwa na wahudumu wa afya na magauni.
Baadhi ya makampuni ambayo yalizawadiwa mikataba ya mamilioni ya dola yalikuwa yameundwa tu miezi michache ya awali, ilidai taarifa hiyo ya uchunguzi.
Makampuni mengine yaliyoshinda zabuni yalikuwa na uhusiano na maafisa wa ngazi ya juu serikalini jambo lililoibua maswali juu ya uhalali wa kisheria wa wao kupewa zabuni hizo.
Akiwa mbele kamati ya bunge Waziri wa afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe, alielezea yaliyofichuliwakatika taarifa hiyo kama uongo na akasema wizara yake inaweza kueleza matumizi ya msaada wa thamani ya zaidi ya dola milioni 200 ilioupokea.
Lakini uchunguzi huo unadai kuwa mara mbili ya pesa hizo haziwezi kuelezwa zilitumiwa vipi. Serikali inapinga madai hayo.
Italia yaipatia msaada Tunisia iwazuwie wahamiaji
Serikali ya Italia inasema kuwa itatoa dola milioni 13 kwa taifa la Tunisia kulisaidia kuimarisha mpaka wake wa majini na kuwazuwia wahamiaji kuvuka bahari ya Mediterranean katika maboti madogo.
Katika ziara yake mjini Tunis, Waziri wa mambo ya nje wa Tunisia, Luigi Di Maio, alisema kuwa hakuna nafasi zaidi nchini mwake kwa ajili ya kuwapokea wahamiaji haramu waliowasili kinyume cha sheria.
Serikali ya Italia ilikuwa tayari umeishatoa mafunzo ya kijeshi kwa vikosi vya Tunisia vya majini na nchi kavu kwa ajili ya kuwazuwia wahamiaji wanaoondoka kuomba hifadhi nchini Italia.
Italia imekua ikihangaika kukabiliana na wimbi la maelfu ya wahamiaji wanaowasili nchini hkwenye fukwe za kusini mwa nchi hiyo, kazi ambayo ilikuwa ni ngumu zaidi hasa wakati huu wa mzozo wa virusi vya corona.
Post update
Serikali ya Marekani imewasilisha kesi ya udanganyifu na usafirishaji haramu dhidi ya wale waliohusika na mpango wa uasili wa watoto ambao walikuwa si yatima na kuwatoa kwa familia za Wamarekani.
Watoto wa Uganda walichukuliwa kutoka katika familia zao kwa ahadi kuwa watasomeshwa katika shule maalumu nchini Marekani.
Badala yake walifikishwa mahakamani kama yatima kwa ajli ya kuasiliwa na Wamarekani.
Marekani imewawekea vikwazo raia wanne wa Uganda miongoni mwao majaji wawili kwa kuhusika katika biashara haramu ya kimataifa ya mfumo wa uasili.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani iliyotolewa Jumatatu, inasema kuwa Jaji wa ngazi ya juu Wilson Musalu Musene na Mkuu wa zamani wa kitengo cha uhalifu wa kimataifa, Jaji mstaafu Moses Mukiibi walishiriki katika njama ambapo watoto wadogo walichukuliwa kutoka kwenye familia zao na kukabidhiwa kwa mtandao haramu unaowaasili kwa njia za ufisadi kwa kusaidiwa na maafisa wa Uganda.
Hongo zinadaiwa kulipwa kwa majaji hao wawili ili wahalalishe kesi za watoto hao.
Mawakili wawili ambao pia wamewekewa vikwazo hivyo ni , Dorah Mirembe na Patrick Ecobu ambao wanadaiwa kusaidia kutoa hongo kwa majaji wa Uganda na maafisa wengine ili kuidhinisha mchakato wa kesi za uasili kinyume cha sheria.
Vikwazo hivyo ni vya kifedha pamoja na kusafiri.