Na huo ndio mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja, tuonane tena kesho.
WHO yaonya juu ya ‘’utaifa wa chanjo’’
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Janga linafanywa kuwa baya zaidi na nchi zinazoweka maslahi yake mbeleImage caption: Janga linafanywa kuwa baya zaidi na nchi zinazoweka maslahi yake mbele
Janga linafanywa
kuwa baya zaidi na nchi zinazoweka maslahi yake mbele ya nyingine ‘katika
kujaribu kupata kiwango kikubwa cha zinazoweza kuwa chanjo za Covid-19 , amesemaMkuu wa Shirika la afya duniani
" Utendaji
unaoaswa kuwa ni wa kimkakati na wa
kidunia kwa ujumla umegeuka kuwa ni wa maslahi ya kila nchi-hakuna aliye salama
hadi kila mmoja ni salama ," Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema katika
taarifa yake aliyoitoa kwa njia ya mtandao.
"Tunahita
kuzuwiautaifakatika suala la chanjo ya Covid-19 ," alisema.
Ameongeza kuwa amekwishawatumia barua wajumbe wote wa WHO kujiunga na juhudi za za pamoja za kutafuta chanjo. Bofya hapa kupata taarifa zaidi...
Milio ya risasi yarindima kwenye ngome ya jeshi Mali
AFPCopyright: AFP
Msemaji wa jeshi nchini Mali amethibitisha kwamba risasi
zimepigwa ndani ya ngome ya kijeshi iliyopo karibu na mji mkuu, Bamako.
Ubalozi wa Norwayu
unasema kuwa umepokea taarifa kwamba wanajeshi wanaelekea katika mji mkuu na
ubalozi wa Ufaransa umewashauri watu kukaa nyumbani.
Hii inakuja wakati rais wa nchi hiyo Ibrahim
Boubacar Keïta akikabiliwa na shinikizo kubwa la kumtaka aondoke madarakani kufuatia
maandamano makubwa ya kumpinga.
Kumekuwa na ongezeko
la ghadhabu nchini humo kutokana na kuzorota zaidi kwa hali ya usalama huku
wapiganaji wa jihadi na ghasia za kijamii vikiongezeka.
Watu pia wanalalamikia kiwango cha ufisadi na namna hali ya uchumi
inavyoshughulikiwa.
Dkt Denis Mukwege wa DRC aombewa ulinzi
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Dkt Denis Mukwege anasema anahofia maisha yakeImage caption: Dkt Denis Mukwege anasema anahofia maisha yake
Chama
cha madaktari wa kutetea haki za binadamu kinasema kuwa mmoja wa wanachama wake
Dkt
Denis Mukwege anahofia usalama wake.
Madaktari
hao wanasema kuwa Bwana Mukwege
alitishiwa kuwa atauawa kutoka na maoni yake aliyoyatoa kuhusu mauaji
yaliyofanyika mashariki mwa Kongo miaka ya nyuma katikayaliyokuwa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa 'Mapping Report'.
Dkt Mukwege
ni daktari anayefanyika kazi katika mji wa Bukavu DRC.
Alipata
Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2018 kwa "juhudi zake za kupambana na matumizi ya ubakaji
kama siraha’’ nchini humo.
Bwana Mukwege amekuwa akilaani mauji yaliyofanyika nchini
Kongo kati ya 1993 na 2003 yaliyowauwa mamilioni ya watu yaliyotajwa katika 'Mapping Report' - na mauaji ya hivi karibuni katika eneo la
mashariki mwa Kongo.
Obama atoa orodha ya nyimbo anazozisikiliza 2020, ukiwemo wa Wizkid
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ametoa orodha
ya nyimbo zake 2020.
Smile, au tabasamu wimbo ulioimbwa na mwanamuziki wa Nigeria Wizkid, ni miongoni mwa nyimbo 53 zilizomo
kwenye orodha hiyo.
Wengine ambao nyimbo zao zimo katika orodha hiyo ni Beyonce, Rihanna, Nas, J. Cole, Nina Simone na Frank Ocean.
Bwana Obama amesema kuwa baadhi ya nyimbo hizo zitachezwa wakati
wakongamano la kitaifa la chama chaDemocratic cha wiki hii ambalo
lilifunguliwa jana usiku.
Burundi yataka ilipwe mabilioni ya pesa za fidia na lililokua koloni lake
RÉVÉRIEN NDIKURIYOCopyright: RÉVÉRIEN NDIKURIYO
Maafisa nchini Burundi wanasema kuwa Burundi haitaki tu fidia ya pesa tasilimu tu,
bali zaidi inataka kujua ukweli kuhusu maasi yaliyofanywa na wakoloni nchini humo.
Bunge la seneti nchini Burundi linaongoza mchakato ulioanza mwaka 2016 wa "kutafuta sababu ya nchi hiyo kuwa na ubaguzi wa kikabila uliosababisha mauaji
makubwa ".
Mwishoni mwa wiki
iliyopita ilidaiwa kuwa Burundi iliidai Ujerumani ambayo ilikuwa koloni lake dola bilioni 43
kama fidia.
Misururu mirefu yashuhudi wa kwenye maduka ya pombe Afrika Kusini
ReutersCopyright: Reuters
Afrika Kusini imelegeza sheria za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona na kuweka kiwango cha piliJumanne, na kuruhusu mauzo ya pombe na sigara.
Chini ya sheria mpya, mauzo ya pombe yanaruhusiwa kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi kati ya saa tatu za aubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Misururu imekuwa ikionekana nje ya maduka ya pombe katika miji mikubwa nchini humo.
Watu pia wanaruhusiwa kusafiri baina ya mikoa. Imeruhusiwa Kuwatembelea watu wa familia na marafiki lakini kwa makundi mawili.
Mbuga za wanyama na fukwe zimeefunguliwa ili kuwaruhusu watu kujivinjari na matukio yamichezo ili kuruhusu watu kuyatembelea
Uvaaji wa barakoa kwenye maeneo ya umma ni lazima.
Kenya yapuuzilia mbali uchunguzi wa wizi wa fedha za Covid-19
ReutersCopyright: Reuters
Wanasiasa walihusishwa na madai ya kusambaza vifaa vya kujikinga na maambukiziImage caption: Wanasiasa walihusishwa na madai ya kusambaza vifaa vya kujikinga na maambukizi
Waziri wa afya nchini Kenya amepuuzilia mbali taarifa
ya uchunguzi iliyodai kuwa kulikuwa na wizi mkubwana kutoweka kwa mamilioni ya dola za msaada
kutoka kwa wahisani pamoja na vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kuisaidia nchi
kudhibiti kusambaa kwa Covid-19.
Taarifa ya uchunguzi wa televisheni nchini humo ilidai
kuwa misaada ya zaidi ya dola milioni 400 haikuweza kubainika ilitumiwa vipi, huku
visa vya maambukizi ya virusi
vya corona vikiendelea kuongezeka nchini.
Wahudumu wa afya nchini Kenya wametishia kufanya mgomo kutokana na ukosefu
wa vifaa vya kujikinga na maambukizi wawapo kazini.
Uchunguzi huoulidai kuwa watu binafsi ,wakiwemo wanasiasa,
walinufaika na mikataba ya kusambaza vifaa vya kujikinga(PPE), zikiwemo barakoa
zinazotumiwa na wahudumu wa afya na magauni.
Baadhi ya makampuni ambayo
yalizawadiwa mikataba ya mamilioni ya dola yalikuwa yameundwa tu miezi michache
ya awali, ilidai taarifa hiyo ya uchunguzi.
Makampuni mengine yaliyoshinda zabuni yalikuwa na uhusiano na maafisa wa
ngazi ya juu serikalini jambo lililoibua maswali juu ya uhalali wa kisheria wa
wao kupewa zabuni hizo.
Akiwa mbele kamati ya bunge Waziri wa afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe,
alielezea yaliyofichuliwa katika taarifa
hiyo kama uongo na akasema wizara yake inaweza kueleza matumizi ya msaada wa thamani
ya zaidi ya dola milioni 200 ilioupokea.
Lakini uchunguzi huo unada imara
mbili ya pesa hizo haziwezi kuelezwa zilitumiwa vipi. Serikali inapinga madai
hayo.
Italia yatoa msaada wa dola milioni 13 kwa Tunisia iwazuwie wahamiaji
AFPCopyright: AFP
Boti la wahamiajiImage caption: Boti la wahamiaji
Serikali ya Italia inasema kuwa itatoa dola milioni 13 kwa taifa la Tunisia kulisaidia kuimarisha mpaka wake wa majini na kuwazuwia wahamiaji kuvuka bahari ya Mediterranean katika maboti madogo.
Katika ziara yake mjini Tunis, Waziri wa mambo ya nje wa Tunisia, Luigi Di Maio, alisema kuwa hakuna nafasi zaidi nchini mwake kwa ajili ya kuwapokea wahamiaji haramu waliowasili kinyume cha sheria.
Serikali ya Italia ilikuwa tayari umeishatoa mafunzo ya kijeshi kwa vikosi vya Tunisia vya majini na nchi kavu kwa ajili ya kuwazuwia wahamiaji wanaoondoka kuomba hifadhi nchini Italia.
Italia imekua ikihangaika kukabiliana na wimbi la maelfu ya wahamiaji wanaowasili nchini kwenye fukwe za kusini mwa nchi hiyo, kazi ambayo ilikuwa ni ngumu zaidi hasa wakati huu wa mzozo wa virusi vya corona.
Marekani yawawawekea vikwazo raia wanne wa Uganda
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Wazazi waliambiwa watoto watasomeshwa katika shule maalumuImage caption: Wazazi waliambiwa watoto watasomeshwa katika shule maalumu
Serikali ya Marekani imewasilisha kesi ya udanganyifu na
usafirishaji haramu dhidi ya wale waliohusika mpango wa uasili wa watoto ambao
walikuwa si yatima na kuwatoa kwa
familia za Wamarekani.
kuwa
Watoto wa Uganda walichukuliwa kutoka aktika familia zao kwa ahadi kuwa
watasomeshwa katika shule maalumu nchini Marekani.
Badala yake walifikishwa mahakamani kama
yatima kwa ajli ya kuasiliwa na Wamarekani.
Marekani imewawekea vikwazo
raia wanne wa Uganda miongoni mwao majaji wawili kwa kuhusika katika biashara
haramu ya kimataifa ya mfumo wa uasili.
Taarifa ya
Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani iliyotolewa Jumatatu, inasema kuwa Jaji ya
ngazi ya juu Wilson Musalu Musene na
Mkuu wa zamani wa kitengo cha uhalifu wa kimataifa, Jaji mstaafu Moses Mukiibi walishiriki katika njama ambapo
watoto wadogo walichukuliwa kutoka kwa familia zao na kukabidhiwa kwa mtandao
haramu unaowaasili kwa njia za ufisadi
kwa kusaidiwa na maafisa wa Uganda.
Hongo
zinadaiwa kulipwa kwa majaji hao wawili ili wahalalishe kesi za watoto hao.
Mawakili
wawili ambao pia wamewekewa vikwazo hivyoni , Dorah Mirembe na Patrick Ecobu ambao wanadaiwa kusaidia kutoa
hongo kwa majaji wa Uganda na maafisa wengineili kuidhinisha mchakato wa kesi
za uasili kinyume cha sheria. Vikwazo
hivyo ni vya kifedha pamoja na kusafiri.
Karibu katika matangazo mubashara Jumanne 18.08.2020
Habari za moja kwa moja
time_stated_uk
Post update
Na huo ndio mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja, tuonane tena kesho.
WHO yaonya juu ya ‘’utaifa wa chanjo’’
Janga linafanywa kuwa baya zaidi na nchi zinazoweka maslahi yake mbele ya nyingine ‘katika kujaribu kupata kiwango kikubwa cha zinazoweza kuwa chanjo za Covid-19 , amesemaMkuu wa Shirika la afya duniani
" Utendaji unaoaswa kuwa ni wa kimkakati na wa kidunia kwa ujumla umegeuka kuwa ni wa maslahi ya kila nchi-hakuna aliye salama hadi kila mmoja ni salama ," Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema katika taarifa yake aliyoitoa kwa njia ya mtandao.
"Tunahita kuzuwiautaifakatika suala la chanjo ya Covid-19 ," alisema.
Ameongeza kuwa amekwishawatumia barua wajumbe wote wa WHO kujiunga na juhudi za za pamoja za kutafuta chanjo. Bofya hapa kupata taarifa zaidi...
Milio ya risasi yarindima kwenye ngome ya jeshi Mali
Msemaji wa jeshi nchini Mali amethibitisha kwamba risasi zimepigwa ndani ya ngome ya kijeshi iliyopo karibu na mji mkuu, Bamako.
Ubalozi wa Norwayu unasema kuwa umepokea taarifa kwamba wanajeshi wanaelekea katika mji mkuu na ubalozi wa Ufaransa umewashauri watu kukaa nyumbani.
Hii inakuja wakati rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keïta akikabiliwa na shinikizo kubwa la kumtaka aondoke madarakani kufuatia maandamano makubwa ya kumpinga.
Kumekuwa na ongezeko la ghadhabu nchini humo kutokana na kuzorota zaidi kwa hali ya usalama huku wapiganaji wa jihadi na ghasia za kijamii vikiongezeka.
Watu pia wanalalamikia kiwango cha ufisadi na namna hali ya uchumi inavyoshughulikiwa.
Dkt Denis Mukwege wa DRC aombewa ulinzi
Chama cha madaktari wa kutetea haki za binadamu kinasema kuwa mmoja wa wanachama wake Dkt Denis Mukwege anahofia usalama wake.
Madaktari hao wanasema kuwa Bwana Mukwege alitishiwa kuwa atauawa kutoka na maoni yake aliyoyatoa kuhusu mauaji yaliyofanyika mashariki mwa Kongo miaka ya nyuma katikayaliyokuwa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa 'Mapping Report'.
Dkt Mukwege ni daktari anayefanyika kazi katika mji wa Bukavu DRC.
Alipata Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2018 kwa "juhudi zake za kupambana na matumizi ya ubakaji kama siraha’’ nchini humo.
Bwana Mukwege amekuwa akilaani mauji yaliyofanyika nchini Kongo kati ya 1993 na 2003 yaliyowauwa mamilioni ya watu yaliyotajwa katika 'Mapping Report' - na mauaji ya hivi karibuni katika eneo la mashariki mwa Kongo.
Obama atoa orodha ya nyimbo anazozisikiliza 2020, ukiwemo wa Wizkid
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ametoa orodha ya nyimbo zake 2020.
Smile, au tabasamu wimbo ulioimbwa na mwanamuziki wa Nigeria Wizkid, ni miongoni mwa nyimbo 53 zilizomo kwenye orodha hiyo.
Wengine ambao nyimbo zao zimo katika orodha hiyo ni Beyonce, Rihanna, Nas, J. Cole, Nina Simone na Frank Ocean.
Bwana Obama amesema kuwa baadhi ya nyimbo hizo zitachezwa wakati wakongamano la kitaifa la chama chaDemocratic cha wiki hii ambalo lilifunguliwa jana usiku.
Burundi yataka ilipwe mabilioni ya pesa za fidia na lililokua koloni lake
Maafisa nchini Burundi wanasema kuwa Burundi haitaki tu fidia ya pesa tasilimu tu, bali zaidi inataka kujua ukweli kuhusu maasi yaliyofanywa na wakoloni nchini humo.
Bunge la seneti nchini Burundi linaongoza mchakato ulioanza mwaka 2016 wa "kutafuta sababu ya nchi hiyo kuwa na ubaguzi wa kikabila uliosababisha mauaji makubwa ".
Mwishoni mwa wiki iliyopita ilidaiwa kuwa Burundi iliidai Ujerumani ambayo ilikuwa koloni lake dola bilioni 43 kama fidia.
Misururu mirefu yashuhudi wa kwenye maduka ya pombe Afrika Kusini
Afrika Kusini imelegeza sheria za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona na kuweka kiwango cha piliJumanne, na kuruhusu mauzo ya pombe na sigara.
Chini ya sheria mpya, mauzo ya pombe yanaruhusiwa kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi kati ya saa tatu za aubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Misururu imekuwa ikionekana nje ya maduka ya pombe katika miji mikubwa nchini humo.
Watu pia wanaruhusiwa kusafiri baina ya mikoa. Imeruhusiwa Kuwatembelea watu wa familia na marafiki lakini kwa makundi mawili.
Mbuga za wanyama na fukwe zimeefunguliwa ili kuwaruhusu watu kujivinjari na matukio yamichezo ili kuruhusu watu kuyatembelea
Uvaaji wa barakoa kwenye maeneo ya umma ni lazima.
Kenya yapuuzilia mbali uchunguzi wa wizi wa fedha za Covid-19
Waziri wa afya nchini Kenya amepuuzilia mbali taarifa ya uchunguzi iliyodai kuwa kulikuwa na wizi mkubwana kutoweka kwa mamilioni ya dola za msaada kutoka kwa wahisani pamoja na vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kuisaidia nchi kudhibiti kusambaa kwa Covid-19.
Taarifa ya uchunguzi wa televisheni nchini humo ilidai kuwa misaada ya zaidi ya dola milioni 400 haikuweza kubainika ilitumiwa vipi, huku visa vya maambukizi ya virusi vya corona vikiendelea kuongezeka nchini.
Wahudumu wa afya nchini Kenya wametishia kufanya mgomo kutokana na ukosefu wa vifaa vya kujikinga na maambukizi wawapo kazini.
Uchunguzi huoulidai kuwa watu binafsi ,wakiwemo wanasiasa, walinufaika na mikataba ya kusambaza vifaa vya kujikinga(PPE), zikiwemo barakoa zinazotumiwa na wahudumu wa afya na magauni.
Baadhi ya makampuni ambayo yalizawadiwa mikataba ya mamilioni ya dola yalikuwa yameundwa tu miezi michache ya awali, ilidai taarifa hiyo ya uchunguzi.
Makampuni mengine yaliyoshinda zabuni yalikuwa na uhusiano na maafisa wa ngazi ya juu serikalini jambo lililoibua maswali juu ya uhalali wa kisheria wa wao kupewa zabuni hizo.
Akiwa mbele kamati ya bunge Waziri wa afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe, alielezea yaliyofichuliwa katika taarifa hiyo kama uongo na akasema wizara yake inaweza kueleza matumizi ya msaada wa thamani ya zaidi ya dola milioni 200 ilioupokea.
Lakini uchunguzi huo unada imara mbili ya pesa hizo haziwezi kuelezwa zilitumiwa vipi. Serikali inapinga madai hayo.
Italia yatoa msaada wa dola milioni 13 kwa Tunisia iwazuwie wahamiaji
Serikali ya Italia inasema kuwa itatoa dola milioni 13 kwa taifa la Tunisia kulisaidia kuimarisha mpaka wake wa majini na kuwazuwia wahamiaji kuvuka bahari ya Mediterranean katika maboti madogo.
Katika ziara yake mjini Tunis, Waziri wa mambo ya nje wa Tunisia, Luigi Di Maio, alisema kuwa hakuna nafasi zaidi nchini mwake kwa ajili ya kuwapokea wahamiaji haramu waliowasili kinyume cha sheria.
Serikali ya Italia ilikuwa tayari umeishatoa mafunzo ya kijeshi kwa vikosi vya Tunisia vya majini na nchi kavu kwa ajili ya kuwazuwia wahamiaji wanaoondoka kuomba hifadhi nchini Italia.
Italia imekua ikihangaika kukabiliana na wimbi la maelfu ya wahamiaji wanaowasili nchini kwenye fukwe za kusini mwa nchi hiyo, kazi ambayo ilikuwa ni ngumu zaidi hasa wakati huu wa mzozo wa virusi vya corona.
Marekani yawawawekea vikwazo raia wanne wa Uganda
Serikali ya Marekani imewasilisha kesi ya udanganyifu na usafirishaji haramu dhidi ya wale waliohusika mpango wa uasili wa watoto ambao walikuwa si yatima na kuwatoa kwa familia za Wamarekani.
kuwa Watoto wa Uganda walichukuliwa kutoka aktika familia zao kwa ahadi kuwa watasomeshwa katika shule maalumu nchini Marekani.
Badala yake walifikishwa mahakamani kama yatima kwa ajli ya kuasiliwa na Wamarekani.
Marekani imewawekea vikwazo raia wanne wa Uganda miongoni mwao majaji wawili kwa kuhusika katika biashara haramu ya kimataifa ya mfumo wa uasili.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani iliyotolewa Jumatatu, inasema kuwa Jaji ya ngazi ya juu Wilson Musalu Musene na Mkuu wa zamani wa kitengo cha uhalifu wa kimataifa, Jaji mstaafu Moses Mukiibi walishiriki katika njama ambapo watoto wadogo walichukuliwa kutoka kwa familia zao na kukabidhiwa kwa mtandao haramu unaowaasili kwa njia za ufisadi kwa kusaidiwa na maafisa wa Uganda.
Hongo zinadaiwa kulipwa kwa majaji hao wawili ili wahalalishe kesi za watoto hao.
Mawakili wawili ambao pia wamewekewa vikwazo hivyoni , Dorah Mirembe na Patrick Ecobu ambao wanadaiwa kusaidia kutoa hongo kwa majaji wa Uganda na maafisa wengineili kuidhinisha mchakato wa kesi za uasili kinyume cha sheria. Vikwazo hivyo ni vya kifedha pamoja na kusafiri.
Karibu katika matangazo mubashara Jumanne 18.08.2020