Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Dinah Gahamanyi

time_stated_uk

 1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena kesho.

 2. Rais Kenyatta aongeza muda wa marufuku ya kutotembea usiku Kenya

  Uhuru Kenyatta

  Akihutubia taifa juu ya mkakati wa taifa wa kudhibiti maambukizi ya Covid-19 Rais Uhuru amesema amri ya kutotembea kati ya saa tatu usiku na saa kumi alfajiri itaendelea kwa siku 30.

  " Hakutakua na mauzo ya pombe katika baa au katika migahawa " kwa kipindi hicho.

  Rais Kenyatta. amewataka wamiliki wa vilabu vya pombe kuunda mbinu za udhibiti wa shughuli yao kama sehemu ya wajibu wao kama raia kwa wateja wao ili kusaidia mchakato wa kufunguliwa kwa biashara yao.

  Hotuba hii imetolewa kufutia kikao cha kamati ya taifa ya dharura.

  Amesema masharti ya uuzaji wa mitumba yametolewa na mwongozo utatolewa juu ya biashara hiyo na serikali yake.

  Bwana Kenyatta pia amesema pia amewapongeza Wakenya kwa kufuata masharti ya kukabiliana na Covid-19, akisema kuwa kwasasa kiwango cha maambukizi nchini humo kimeshuka kutoka asilimia 13 mwezi Juni hadi asilimia 8 mwezi wa Agosti.

  Baadhi ya wakenya wameeleza hisia zao juu ya hotuba ya rais:

  View more on twitter
  View more on twitter

  Hotuba ya rais inatolewa huku maambukizi mapya ya virusi yakiripotiwa kufikia 213 katika kipindi cha saa 24 na kulifanya taifa hilo kuwa na jumla ya visa 33,016. Vifo 5 pia vimeripotiwa leo na hivyo jumla ya watu waliokufa kufikia 564. Waliopona virusi vya corona ni zaidi ya 19,000.

 3. Maelfu ya simu za China zilizo na programu za kulaghai zauzwa Afrika.

  Programu ambayo inawasajili kisiri watumiaji wa simu katika huduma zinazotoza ada imepatikana katika maelfu ya simu zinazouzwa Afrika.

  Kampuni ya Upstream ambayo hukabiliana na ulaghai wa kiteknolojia imepata nambari maalum 53,000 katika simu za Tecno, zilizouzwa Ethiopia, Cameroon, Misri, Ghana na Afrika Kusini.

  Unaweza kusoma kwa kina taarifa hii kwenye mtandao wetu

 4. Huenda Kenya ikafungua shule

  Shule

  Waziri wa elimu amedokeza juu ya kufunguliwa kwa shule mapema zaidi ya muda uliokua umependekezwa wa Januari 2021 iwapo idadi ya maambukizi itaendelea kupungua.

  George Magoha amesema kuwa taasisi za elimu ya juu zinaweza kufungua mapema kuliko ilivyopangwa.

  Kenya ilifuta muhula wa masomo wa mwaka 2020 mwezi Machi kwasababu ya janga la corona.

  Waziri alisema kuwa itakuwa ni faida kwa wanafunzi kufungua tena shule mapema kama viwango vya maambukizi vitaendela kupungua kama ilivyo sasa.

  Wizara ya afya imekua ikiripoti idadi ya chini ya maambukizi hivi karibuni huku Mkurugenzi Mkuu akisema kuwa viwango hivyo vinahitaji kufikia chini ya 5% kwa kipindi cha wiki mbili ndipo itakapofahamika kuwa viwango vya maambukizi vimepungua.

  Wiki iliyopita Shirika la afya duniani -WHO pamoja na Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicefyaliyataka mataifa ya Afrika kufikiria kufungua tena shule lakini yawe na miongozo thabiti ya kuzuwia maambukizi.

 5. Mahakama yaahirisha kesi ya Tundu Lissu

  Tundu Lissu

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jiji Dar es Salaam Tanzania imeahirisha kesi inayomkabili Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu hadi tarehe 24 Septemba 2020.

  Hii ni baada ya Rose Moshi, Mdhamini wake kuielezea mahakama kuwa mshitakiwa ameshindwa kuhudhuria kutokana na kuchelewa kukamilisha urejeshaji wa fomu za uteuzi wa kugombea urais. Miongoni mwa mashitaka anayoshitakiwa ni pamoja na kutoa maneno ya uchochezi, tuhuma ambazo anazikana.

  Bwana Lissu ambaye anawania urais na kesi za jinai sita katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. .

 6. Waendeshamashitaka wa kimataifa watafuta ushahidi Rwanda dhidi ya Felicien Kabuga

  Yves Bucyana

  BBC Swahili

  Felicienn Kabuga

  Waendeshamashitaka wa mahakamaya kimataifa ya uhalifu wa Rwanda ICTR wahamishia kazi zao nchini Rwanda kwa lengo la kukusanya ushahidi zaidi na kuandaa faili la mashitaka la mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya kimbari Felicien Kabuga kabla ya kesi yake kuanza kusikilizwa rasmi.

  Kabuga alikamatwa nchini Ufaransa mwezi Machi mwaka huu baada ya kuwa mafichoni kwa miaka 26.

  Mwendeshamashtaka mkuu wa ICTR Serge Brammertz kushoto na mwendesha mashitaka Mkuu wa Rwanda, Aimable Havugiyaremye
  Image caption: Mwendeshamashtaka mkuu wa ICTR Serge Brammertz kushoto na mwendesha mashitaka Mkuu wa Rwanda, Aimable Havugiyaremye

  Mwendeshamashitaka Mkuu wa mahakama maalum iliyochukua nafasi ya ICTRSERGE Brammertz amesema walilazimika kuongeza idadi ya waendeshamashitaka katika kesi hiyo ili kufanyia kazi faili la mashitaka la Kabugakwa kufanya uchunguzi zaidi wa mashtaka dhidi ya mtuhumiwa huyo:

  ‘’ Niliongeza idadi ya wapelelezi na waendeshamashtaka ili kuweza kufanya kazi na Rwanda sababu hata kama tunafurahia kukamatwa kwa Bwana Kabuga ni lazima faili la mashitaka dhidi yake ifanyiwe kazi ipasavyo. Lazima tutafute tena mashahidi na waathiriwa waliokuwa wameishatoa ushahidi. Tutakuna na mashirika ya manusura wa mauaji ya kimbari kwa sababu tunataka kuoanisha ushahidi wa awali na ushahidimpyana kwa kipindi kifupi’’

  Waendesha mashitaka hao wanatarajiwa kukamilisha uchunguzi wao Rwanda katika kipindi cha wiki mbili.

 7. Coast Laurent Gbagbo azuiwa kushiriki uchaguzi

  Laurent Bagbo

  Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amezuiwa kugombea urais katika uchaguzi ujao baada ya mahakama kuidhinisha uamuzi wa tume ya uchaguzi.

  Wakili wake Claude Mentenon amelimbia shirika la habari la AFP kuwa kuna matatizo mengine zaidi ya kisheria ndani ya Ivory coast dhidi yake.

  Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ilimuondoa katika orodha ya wagombea kwasababu alipatikana na hatia ya uhalifu.

  Rais wa tume ya uchaguzi , Ibrahime Coulibaly-Kuibiert, alisema mwezi Agosti kwamba yeyote anayepatikana na hatia ya uhalifu ataondolewa kwenye orodha ya wagombea.

  Alitoa tangazo hilo wakati alipokua akitangaza orodha mpya ya wagombea.

  Wagombea wanne akiwemo kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro waliondolewa kwenye orodha ya wagombea wa urais.

  Bwana Gbagbo aliondolewa mashitaka mwezi Januari 2019 baada ya kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu uliohusiana na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

 8. Mwili wa Mwanamke Mganda aliyepatikana amekufa Uingereza kurejeshwa nyumbani

  Mercy Baguma alipoteza kazi nchini Uingereza kabla ya kifo chake
  Image caption: Mercy Baguma alipoteza kazi nchini Uingereza kabla ya kifo chake

  Maandalizi yafanyika kurejesha mwili wa Mwanamke Mganda aliyepatikana amekufa Uingereza yanafanyika nchini Uganda.

  Mwanamke huyo anatoka katika jimbo la Busoga, anasema mwandishi wa BBC mjini Kampala.

  Mercy Baguma, aligunduliwa katika nyumba ya gorofa mjini Glasgow Jumamosi iliyopita baada ya watu kusikia kelele ya kilio cha mtoto wake.

  Msemaji wa polisi wa eneo hilo amesema kuwa kifo chake kinachukuliwa kama kisichoelezeka, lakini hakuna anayeshukiwa.

  Shirika la misaada la wakimbizi Refugee charity Positive Action in Housing linasema kuwa Bi Baguma aliomba uhamiaji na kuishi katika "umasikini mkubwa".

  Linasema kuwa alpoteza kazi yake baada ya haki yake ya kufanya kazi nchini Uingereza kuisha.

  Mtoto wake wa kiume alipatikana kando yake akilia na "akiwa mdhaifu baada ya kuwa na njaa kwa siku kadhaa " kwa mujibu wa Robina Qureshi, mkurugenzi wa Positive Action in Housing.

  Mtoto huyo alilazwa hospitalini na kutolewa tarehe 24 Agosti, na sasa anaishi na baba yake.

 9. Walioambukia virusi vya corona Afrika ni karibu milioni 1.2

  Mataifa ya Afrika yanashauriwa kupima virusi vya corona zaidi
  Image caption: Mataifa ya Afrika yanashauriwa kupima virusi vya corona zaidi

  Watu waliopatikana na maambukizi ya virusi vya corona wanakaribia kufikia milioni 2.1 , barani Afrika kwa mujibu wa taarifa za hivi punde zilizotolewa na kituo cha udhibiti na uzuwiaji wa magonjwa (CDC).

  Kituo hicho kimetuma ujumbe wake wa Twitter kwamba idadi ya maambukizi sasa imefikia watu 1,196,710, vifo 28, 014 huku idadi ya waliopona ikiwa ni 922, 833.

  Afrika Kusini ndiyo inayoongoza kwa maambukizi ikiwa na 611,450 waliopatwa na virusi, ikifuatiwa na Misri 97,478, Morocco 53,252, Nigeria 52,548, Ghana 43,622, Algeria 42,302, Ethiopia 42,143 na Kenya watu 32,803.

  Kituo cha CDC kimekuwa kikiyataka mataifa kuweka mikakati ya haraka za kukabiliana na janga kwa kuwapima watu zaidi na kutafuta watu waliokutana na wenye maambukizi ili wapimwe.

  Hivi karibuni kituo hicho kilizindua upimaji wa kinga ya mwili ili kutambua makali ya maambukizi ya virusi hivyo barani Afrika.

 10. Kampeni za uchaguzi zaanza rasmi leo Tanzania

  Rais John Pombe Magufuli
  Image caption: Rais John Magufuli anawania kiti hicho kwa muhula wa pili

  Kampeni za uchaguzi zimeanza rasmi nchini Tanzania kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba.

  Rais John Magufuli, ambaye anawania kuchaguliwa kwa muhula wa pili, anakabiliana na wagombea 14 wa kiti hicho .

  Chama tawala cha CCM kimetawala siasa za Tanzania tangu nchi hiyo ipate Uhuru.

  Lakini idadi kubwa ya wagombea wa urais mara hii inaweza kuwa ni faida kwake.

  Bwana Magufuli alisifiwa sana alipoingia madarakani miaka mitano iliyopita, lakini baadhi wamekuwa wakimtuhumu kuongoza kwa ukandamizaji.

  Mwezi Juni alitangaza kuwa virusi vya corona vimeshindwa nchini Tanzania kutokana na maombi.

  Tangu wakati huo Watanzania wengi wamekua wakiendelea na shughuli zao kama kawaida licha ya hofu zinazoelezewa na wakosoaji wake ndani na nje ya nchi hiyo.

  Uchaguzi wa mwaka huu unatarajiwa kuwa wenye ushindani zaidi.

 11. Hujambo na karibu kwa matangazo mubashara leo Jumatano tarehe 26.08.2020