Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo ya moja kwa moja kwa leo.
BBCCopyright: BBC
Marvin na LucilleImage caption: Marvin na Lucille
Tunakuacha na picha hii ya wanandoa kutoka Nebraska, Marekani
waliosherehekea maisha yao ya ndoa kwa kupiga picha wakiwa wamevalia nguo walizovaa siku ya harusi yao mwaka 1960.
Wakazi wa Kigali kutozwa faini ya dola 10 kwa kutovalia barakoa vyema
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Mamlaka katika mji mkuu wa Kigali nchini Rwanda imetangaza
kuwapiga faini watu watakaopuuza hatua zilizowekwa kukabiliana na kuenea kwa
virusi vya corona.
Hii ni kando na wanaokiuka hatua zilizopo za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona kuzuiliwa katika viwanja vya michezo kwa saa kadhaa.
Faini hizo zitakazotozwa watu katika mji wa Kigali
zinajumuisha dola 10 kwa kutovalia barakoa vizuri, kutozingatia kanuni ya
kutokaribiana na kutoheshimu saa za kafyu itaanza kutekelezwa kuuanzia saa moja
usiku.
Tangazohilo lililotolewa Alhamisi limekosolewa vikali kwenye mitandao
ya kijamii.
“Sijui kama faini hizo kubwa zitasaidia kumaliza virusi ama
itazorotesha zaidi maisha ya watu”, mmoja ya watu waliotoa maoni yao kuhusu
hatua hiyo aliandika katika mtandao wa Twitter.
Faini hizo mpya zinajumuisha dola 200 kwa watakaoandaa hafla
itakayochangia mkusanyiko wa watu na dola 25 kwa wale watakaohudhuria hafla
hiyo.
Rwanda ambayo imesifiwa kutokana kutokana na mapambano yake
dhidi ya virusi vya corona, piani moja
ya nchi za eneoSahara ambayo raia wake
wanaruhusiwa kuingia Ulaya katika eneo la Schengen.
Kufikia sasa zaidi ya watu 4,200 ameambukizwa virusi vya
corona nchini Rwanda huku vifo 17 vikiripotiwa.
Muigizaji Dwayne 'The Rock' Johnson na familia yake waambukizwa corona
INSTAGRAMCopyright: INSTAGRAM
Muigizaji maarufu wa
Marekani Dwayne "The Rock" Johnson anasema kuwa yeye na familia yake
yote walipata ugonjwa wa Covid-19.
Mwanamieleka huyo wa zamani ambaye pia ni
muigizaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani ameelezea kuwa walishangaa
kupata virusi hivyo licha ya kuchukua tahadhari.
Johnson anaishi na familia yake Marekani ambako zaidi wa watu milioni 6.1 wameambukizwa virusi vya corona huku vifo 860,000 vikihusishwa na ugonjwa huo.
Mzozo wa mto Nile: Marekani kupunguza ufadhili kwa Ethiopia
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Marekani imetangaza kuwa imepunguza ufadhili wake kwa Ethiopia unaokisiwa kugharimu dola milioni 100 kutokana na utata wa bwawa kubwa la uzalishaji umeme linalojengwa katika mto Nile.
Wanamgambo 'wawafurusha wenyeji' maeneo ya virusi Msumbiji
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Wanamgambo wamewafurusha maelfu ya watu kutoka majumbani mwaoImage caption: Wanamgambo wamewafurusha maelfu ya watu kutoka majumbani mwao
Makabiliano kati ya vikosi vya serikali ya Msumbiji na wanamgambo wa Kiislam kaskazini mwa mkoa wa
Cabo Delgado yamewafanya wakazi kukimbilia maeneo yaliyo na viwango vya juu vya
maambukizi ya corona kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la Mslaba Mwekundu(IRCS).
Baadhi ya wakimbizi
hao wako Pemba ambako IRCS lilisaidia kujenga kituo cha matibabu ya virusi vya
corona, linasema shirika hilo.
Hali hiyo inawaweka
katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi, anasemamkuu anayesimamia shughuli za IRCS mjini
Pemba Raoul Bittel.
Wanamgambo hao
wamekuwa wakifanya mashambulio katika maeneo ya vijijini katika kipindi cha
miaka miwili iliyopita.
Kundi hilo linaloitwa
al-Shabab au vijana na wenyeji– linaendesha ajenda za kijihadi lakini limekuwa
likitumia changamoto miongo kadhaa zinazokabili jamii kama vile ukosefu wa
kazi, udanganyifu katika uchaguzi, ufisadi na ghasia kujiimarisha.
Marekani yaomba Rwanda 'kutoa mazingira ya kiutu' kwa Rusesabagina
RIBCopyright: RIB
Paul Rusesabagina alipokamatwaImage caption: Paul Rusesabagina alipokamatwa
Naibu wa waziri wa mbambo ya nje wa Marekani kuhusu masuala ya
Afrika Tibor Nagy, amefanya mazungumzo na balozi wa Rwanda nchini Marekani kujadili kukamatwa kwa Paul Rusesabagina ''shujaa'' aliyeangaziwa katika filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.
“Marekani inatarajia serikali ya Rwanda itatoa mazingira ya kiutu, kwa kuzingatia utawala wa sheria, kwa kuendesha machakato wa kisheria ulio wazi na usio na upendelea dhidi ya bwana Rusesabagina, bwana Nagy aliandika kwenye Twitter yake baada ya kukutana na balozi wa Rwanda.
Maafisa wa Rwanda
wanasema bwana Rusesabagina, 66, alikamatwa kupitia waranti ya kimataifa kwa kuongoza ''vuguvugu la kigaidi''
Lakini binti yake
ameiambia BBC kwamba madai hayo si ya kweli.
Rusesabagina,66, mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rwanda amabaye anaishi ughaibuni aliangaziwa katika filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Alisimamishwakwa muda mfupi mbele ya wanahabari mjini Kigali siku ya Jumatatu.
Maafisa hawakuelezea mazingira ya kukamatwa, lakini walisema alikamatwa kupitia kibali cha kimataifa kwa kuongoza "vuguvugu la kigaidi".
Bwana Rusesabagina, Mnyarwanda mwenye uraia wa Ubelgiji na makazi ya kudumu ya kiushi nchini Marekani alikuwa amesafiri kutoka San Antonio, Texas kwenda Dubai Alhamisi iliyopita,familia na chama chake kiliambia BBC.
Serikali ya Rwanda haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai ya kutekwa kwake.
Mamlaka ya wanyamapori nchini Zimbabwe imepata
mizoga zaidi ya tembo na kufikisha 22 jumla ya wanyama waliokufa.
Tembo hao wanashukuwa huenda walipata maambukizi ya bakteria kwa mujibu wa
mamlaka.
Wengi wa tembo waliokufa ni wadogo, mkubwa akiwa na miaka 18.
Mamlaka aidha inashuku huenda tembo wadogo walikufa baada ya kula nyasi
zilizokua na sumu.
Inasemekana kumekuwa na uhaba wa lishe na tembo wadogo walikuwa na
changamoto ya kufikia majani ya miti mirefu.
Ethiopia kutoa bure maelfu ya mikate kwa wakazi wa Addis Ababa
Mamalaka
katika mji mkuu wa Addis Ababa,Ethiopia unapanga kutoa bure maelfu ya
mikate kwa wakazi kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha mwaka mpya wa Ethiopia
2013.
Ruzuku
hiyo ya siku moja itakayotolewa Jumatatu ya tarehe saba Septemba, itaakuwa
mwanzo wa siku tano za sherehe za kuadhimisha mwezi wa mwishokatika kalenda ya
Ethiopia.
Mnamo
mwezi Juni serikali ilizindua kiwanda kikubwa cha uoka mikate viungani mwa mji
mkue.
Maafisa
wanasema unauwezo wa kuoka mikate milioni mbili ya wastani kwa siku.
Afisa
wa serikali alioweka mtandaoni video ya mtambo wa kuoka mkate wa Sheger ukiwa
unafanya kazi wakati wa uzinduzi huo.
UN kuweka kambi mpya Sudan Kusini
Getty ImagesCopyright: Getty Images
David Shearer anasema uwepo wa UN utatoa ulinzi katika eneo hiloImage caption: David Shearer anasema uwepo wa UN utatoa ulinzi katika eneo hilo
Ujumbe wa UN nchini Sudan Kusini imesema
utaweka kambi mpya ya walinda amani katika eneo la Lobonok baada ya walinzi sita wa makamu wa rais Wani Igga kuuawa mwezi uliopita.
Ujumbe huo ulitaja mashambulio mengine dhidi ya raia na misafara ya kibinadamu katika eneo hilo kama sababu ya kuanzisha kambi hiyo mpya.
Mkuu wa ujunbe huo , David Shearer, amesema kambi hiyo mpya itasaidia kutoa ulinzi katika eneo hilo.
Kumeshuhudiwa mashambulio kadhaa dhidi ya wafanyakazi wa
kutoa misaaada katika siku chache zilizopita ,kwa mijibu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo.
Waasi wa kundi la National Salvation Front (Nas) ambalo linaongozwa na jenerali wa zamani wa
jeshi Thomas Cirillo Swaka, limekiri kuhusika na shambulio la mwezi uliopita
dhidi ya msafara wa makamu wa rais.
Kundi hilo halikuwa sehemu ya mkataba amani uliotiwa saini kati ya
serikali na makundi ya upinzani yaliyojihami mwaka 2018 kukomesha papigano
yaliyodumu kwa miaka kadhaa
Kenya yazuia mali ya 'wafadhili' wa Al Shabab
BBCCopyright: BBC
Kenya imezuilia mali ya watu tisa
wanaotuhumiwa kufadhili kundi la wanamgambo wa Al Shabab nchini Somalia.
Wizara ya mambo ya ndani imesemahatua hiyo ni sehemu yajuhudi mpya za kukabiliana na ugaidina kudibiti ‘’ ugaidi nyumbani’’
Katika taarifa yake waziri wa usalama wa
kitaifa Fred Matiangi amesemakuzuiliwa
kwamali ya Wakenya hao tisakutahakikishahawawezi tena kufadhili kundi la Al Shabab ‘’ ndani ya mipaka yetu’’.
Pia ameonya kuwa kundi hilo lilikuwa
likiwasajili ,kuwapa mafuzo na kuwawekamiongoni mwa raia‘’ ili
waendeleze ajenda yao ya misimamo mikali na ugaidi.''
Tangazo hilo linajiri wakati ambapo Rais
Uhuru Kenyatta amewaambia viongozi wa kimataifa kwamba janga la Covid 19
limechangia vitendo vya kigaidi, kuzidisha mzozo wa wakimbizi na kuongezeka kwa
silaha ndogo ndogo katika eneo la Pembe ya Afrika.
Kenya imekabiliwa na mashambulio kadhaa
kutoka kwa Al Shabab tangu ilipowapeleka wanajeshi wake Somalia 2011
kukabiliana na kundi hilo
Rais
Kenyatta ailikuwa akizungumza katika mkutano wa Aqaba kuhusu Covi-19
uliandaliwa kupitia mfumo wa kidijitali na Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan ambao pia
ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Rais Rodrigo
Duterte wa Ufilipino na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress
kujadili jannga la corona na usalama wa kimataifa.
Habari za moja kwa moja
Na Ambia Hirsi
time_stated_uk
Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo ya moja kwa moja kwa leo.
Tunakuacha na picha hii ya wanandoa kutoka Nebraska, Marekani waliosherehekea maisha yao ya ndoa kwa kupiga picha wakiwa wamevalia nguo walizovaa siku ya harusi yao mwaka 1960.
Wakazi wa Kigali kutozwa faini ya dola 10 kwa kutovalia barakoa vyema
Mamlaka katika mji mkuu wa Kigali nchini Rwanda imetangaza kuwapiga faini watu watakaopuuza hatua zilizowekwa kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona.
Hii ni kando na wanaokiuka hatua zilizopo za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona kuzuiliwa katika viwanja vya michezo kwa saa kadhaa.
Faini hizo zitakazotozwa watu katika mji wa Kigali zinajumuisha dola 10 kwa kutovalia barakoa vizuri, kutozingatia kanuni ya kutokaribiana na kutoheshimu saa za kafyu itaanza kutekelezwa kuuanzia saa moja usiku.
Tangazohilo lililotolewa Alhamisi limekosolewa vikali kwenye mitandao ya kijamii.
“Sijui kama faini hizo kubwa zitasaidia kumaliza virusi ama itazorotesha zaidi maisha ya watu”, mmoja ya watu waliotoa maoni yao kuhusu hatua hiyo aliandika katika mtandao wa Twitter.
Faini hizo mpya zinajumuisha dola 200 kwa watakaoandaa hafla itakayochangia mkusanyiko wa watu na dola 25 kwa wale watakaohudhuria hafla hiyo.
Rwanda ambayo imesifiwa kutokana kutokana na mapambano yake dhidi ya virusi vya corona, piani moja ya nchi za eneoSahara ambayo raia wake wanaruhusiwa kuingia Ulaya katika eneo la Schengen.
Kufikia sasa zaidi ya watu 4,200 ameambukizwa virusi vya corona nchini Rwanda huku vifo 17 vikiripotiwa.
Muigizaji Dwayne 'The Rock' Johnson na familia yake waambukizwa corona
Muigizaji maarufu wa Marekani Dwayne "The Rock" Johnson anasema kuwa yeye na familia yake yote walipata ugonjwa wa Covid-19.
Mwanamieleka huyo wa zamani ambaye pia ni muigizaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani ameelezea kuwa walishangaa kupata virusi hivyo licha ya kuchukua tahadhari.
Johnson anaishi na familia yake Marekani ambako zaidi wa watu milioni 6.1 wameambukizwa virusi vya corona huku vifo 860,000 vikihusishwa na ugonjwa huo.
Mzozo wa mto Nile: Marekani kupunguza ufadhili kwa Ethiopia
Marekani imetangaza kuwa imepunguza ufadhili wake kwa Ethiopia unaokisiwa kugharimu dola milioni 100 kutokana na utata wa bwawa kubwa la uzalishaji umeme linalojengwa katika mto Nile.
Maelezo zaidi hapa
Wanamgambo 'wawafurusha wenyeji' maeneo ya virusi Msumbiji
Makabiliano kati ya vikosi vya serikali ya Msumbiji na wanamgambo wa Kiislam kaskazini mwa mkoa wa Cabo Delgado yamewafanya wakazi kukimbilia maeneo yaliyo na viwango vya juu vya maambukizi ya corona kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la Mslaba Mwekundu(IRCS).
Baadhi ya wakimbizi hao wako Pemba ambako IRCS lilisaidia kujenga kituo cha matibabu ya virusi vya corona, linasema shirika hilo.
Hali hiyo inawaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi, anasemamkuu anayesimamia shughuli za IRCS mjini Pemba Raoul Bittel.
Wanamgambo hao wamekuwa wakifanya mashambulio katika maeneo ya vijijini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Kundi hilo linaloitwa al-Shabab au vijana na wenyeji– linaendesha ajenda za kijihadi lakini limekuwa likitumia changamoto miongo kadhaa zinazokabili jamii kama vile ukosefu wa kazi, udanganyifu katika uchaguzi, ufisadi na ghasia kujiimarisha.
Marekani yaomba Rwanda 'kutoa mazingira ya kiutu' kwa Rusesabagina
Naibu wa waziri wa mbambo ya nje wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika Tibor Nagy, amefanya mazungumzo na balozi wa Rwanda nchini Marekani kujadili kukamatwa kwa Paul Rusesabagina ''shujaa'' aliyeangaziwa katika filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.
“Marekani inatarajia serikali ya Rwanda itatoa mazingira ya kiutu, kwa kuzingatia utawala wa sheria, kwa kuendesha machakato wa kisheria ulio wazi na usio na upendelea dhidi ya bwana Rusesabagina, bwana Nagy aliandika kwenye Twitter yake baada ya kukutana na balozi wa Rwanda.
Maafisa wa Rwanda wanasema bwana Rusesabagina, 66, alikamatwa kupitia waranti ya kimataifa kwa kuongoza ''vuguvugu la kigaidi''
Lakini binti yake ameiambia BBC kwamba madai hayo si ya kweli.
"Tunaamini alitekwa nyara kwasababu hawezi kuenda Rwanda kwa hiari yake." aliambia BBC.
Rusesabagina,66, mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rwanda amabaye anaishi ughaibuni aliangaziwa katika filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Alisimamishwakwa muda mfupi mbele ya wanahabari mjini Kigali siku ya Jumatatu.
Maafisa hawakuelezea mazingira ya kukamatwa, lakini walisema alikamatwa kupitia kibali cha kimataifa kwa kuongoza "vuguvugu la kigaidi".
Bwana Rusesabagina, Mnyarwanda mwenye uraia wa Ubelgiji na makazi ya kudumu ya kiushi nchini Marekani alikuwa amesafiri kutoka San Antonio, Texas kwenda Dubai Alhamisi iliyopita,familia na chama chake kiliambia BBC.
Serikali ya Rwanda haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai ya kutekwa kwake.
Maelezo zaidi:
Utata juu kukamatwa kwa 'shujaa' wa filamu ya mauaji ya Rwanda.
Tembo zaidi wafa Zimbabwe
Mamlaka ya wanyamapori nchini Zimbabwe imepata mizoga zaidi ya tembo na kufikisha 22 jumla ya wanyama waliokufa.
Tembo hao wanashukuwa huenda walipata maambukizi ya bakteria kwa mujibu wa mamlaka.
Wengi wa tembo waliokufa ni wadogo, mkubwa akiwa na miaka 18.
Mamlaka aidha inashuku huenda tembo wadogo walikufa baada ya kula nyasi zilizokua na sumu.
Inasemekana kumekuwa na uhaba wa lishe na tembo wadogo walikuwa na changamoto ya kufikia majani ya miti mirefu.
Ethiopia kutoa bure maelfu ya mikate kwa wakazi wa Addis Ababa
Mamalaka katika mji mkuu wa Addis Ababa,Ethiopia unapanga kutoa bure maelfu ya mikate kwa wakazi kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha mwaka mpya wa Ethiopia 2013.
Ruzuku hiyo ya siku moja itakayotolewa Jumatatu ya tarehe saba Septemba, itaakuwa mwanzo wa siku tano za sherehe za kuadhimisha mwezi wa mwishokatika kalenda ya Ethiopia.
Mnamo mwezi Juni serikali ilizindua kiwanda kikubwa cha uoka mikate viungani mwa mji mkue.
Maafisa wanasema unauwezo wa kuoka mikate milioni mbili ya wastani kwa siku.
Afisa wa serikali alioweka mtandaoni video ya mtambo wa kuoka mkate wa Sheger ukiwa unafanya kazi wakati wa uzinduzi huo.
UN kuweka kambi mpya Sudan Kusini
Ujumbe wa UN nchini Sudan Kusini imesema utaweka kambi mpya ya walinda amani katika eneo la Lobonok baada ya walinzi sita wa makamu wa rais Wani Igga kuuawa mwezi uliopita.
Ujumbe huo ulitaja mashambulio mengine dhidi ya raia na misafara ya kibinadamu katika eneo hilo kama sababu ya kuanzisha kambi hiyo mpya.
Mkuu wa ujunbe huo , David Shearer, amesema kambi hiyo mpya itasaidia kutoa ulinzi katika eneo hilo.
Kumeshuhudiwa mashambulio kadhaa dhidi ya wafanyakazi wa kutoa misaaada katika siku chache zilizopita ,kwa mijibu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo.
Waasi wa kundi la National Salvation Front (Nas) ambalo linaongozwa na jenerali wa zamani wa jeshi Thomas Cirillo Swaka, limekiri kuhusika na shambulio la mwezi uliopita dhidi ya msafara wa makamu wa rais.
Kundi hilo halikuwa sehemu ya mkataba amani uliotiwa saini kati ya serikali na makundi ya upinzani yaliyojihami mwaka 2018 kukomesha papigano yaliyodumu kwa miaka kadhaa
Kenya yazuia mali ya 'wafadhili' wa Al Shabab
Kenya imezuilia mali ya watu tisa wanaotuhumiwa kufadhili kundi la wanamgambo wa Al Shabab nchini Somalia.
Wizara ya mambo ya ndani imesemahatua hiyo ni sehemu yajuhudi mpya za kukabiliana na ugaidina kudibiti ‘’ ugaidi nyumbani’’
Katika taarifa yake waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiangi amesemakuzuiliwa kwamali ya Wakenya hao tisakutahakikishahawawezi tena kufadhili kundi la Al Shabab ‘’ ndani ya mipaka yetu’’.
Pia ameonya kuwa kundi hilo lilikuwa likiwasajili ,kuwapa mafuzo na kuwawekamiongoni mwa raia‘’ ili waendeleze ajenda yao ya misimamo mikali na ugaidi.''
Tangazo hilo linajiri wakati ambapo Rais Uhuru Kenyatta amewaambia viongozi wa kimataifa kwamba janga la Covid 19 limechangia vitendo vya kigaidi, kuzidisha mzozo wa wakimbizi na kuongezeka kwa silaha ndogo ndogo katika eneo la Pembe ya Afrika.
Kenya imekabiliwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa Al Shabab tangu ilipowapeleka wanajeshi wake Somalia 2011 kukabiliana na kundi hilo
Rais Kenyatta ailikuwa akizungumza katika mkutano wa Aqaba kuhusu Covi-19 uliandaliwa kupitia mfumo wa kidijitali na Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan ambao pia ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress kujadili jannga la corona na usalama wa kimataifa.