Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

time_stated_uk

 1. Kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Kwaheri.

 2. Mmea unaodaiwa na Madagascar kuwa dawa ya corona

  Dawa ya corona ya Madagascar

  Madagascar iliangaziwa sana katika vyombo vya habari mwezi Aprili ilipotangaza kwamba imevumbua dawa ya corona kutoka kwa mmea wa artemisia. Kufikia sasa bado hakuna ushahidi kwamba mmea huo - ambayo kemikali yake inaweza kutibu malaria - unaweza kutibu Covid-19, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

  Tunafahamu nini kufikia sasa kuhusu mmea huu na nguvu zake?

  Maelezo zaidi:

 3. Msemaji wa waasi anataka kesi yake kuunganishwa na Rusesabagina

  Yves Bucyana

  BBC Swahili

  Sankara alipokamatwa

  Nchini Rwanda ,kesi ya aliyekuwa msemaji wa kundi la waasi dhidi ya Rwanda la FLN Callixte Nsabimana maarufu Meja Sankara imeendelea ambapo mtuhumiwa ameomba kuoanisha kesi yake na Paul Rusesabagina mpinzani mkuu wa serikali ya Rwanda ambaye sasa anazuiliwa nchini humo kwa mashitaka ya ugaidi.

  Rusesabagina bado hajafunguliwa kesi mahakamani lakini siku chache zilizopita Rais Paul Kagame alidokeza juu ya watuhumiwa kuhusika katika kesi moja.

  Mahakama imejadili maombi ya mwendesha mashitaka ya kuoanisha kesi ya waliokuwa wasemaji wa kundi hilo kwa nyakati tofauti,Callixte Nsabimana maarufu Sankara na Herman Nsengimana aliyechukua naasi ya usemani wa kundi la FLN baada ya Sankara kukamatwa.

  Alipopewa nafasi,Callixte Nsabimana Sankara amekaribisha hoja hiyo na kuongezea kwamba ingekuwa vizuri hata faili la mashtaka la Rusesabagina kuharakishwa ili kesi yake pia kuoanishwa na kesi yake.

  Sankara

  ''Nilisikia kwamba faili la mashitaka la Rusesabagina lilikabidhiwa mwendeshamashitaka.ningependelea faili la ‘Boss wangu’ kuharakishwa ili tushirikishwe katika kesi moja,kwa manufaa ya sheria'' alisema.

  Kadhalika waathiriwa wanaodai kulipwa fidia katika kesi hii wameunga mkono hoja ya kuunganisha kesi hizo katika kesi moja lakini nao pia wakasisitiza kuhusu umuhimu wa kesi dhidi ya Rusesabagina ambaye alikuwa naibu kiongonzi wa vuguvugu la MRCD lililodai kuhusika na mashambulio dhidi ya maeneo ya kusini magharibi mwa Rwanda mwaka 2018.

 4. Ndege yakatiza safari yake juu ya barakoa

  Abiria katika uwanja wa ndege

  Safari ya ndege ya Canada-WestJet ilifutwa na polisi kuitwa kisa mtoto hajavaa barakoa.

  Maelezo zaidi

 5. Wagonjwa wachangamkia fursa ya kliniki tembezi Tanzania

  Aboubakar Famau

  BBC Africa, Dar es Salaam

  Wagonjwa

  Mamia ya wakazi wa mkoa wa Singida uliopo kanda ya kati nchini Tanzania ambao wanaugua magonjwa mbalimbali, wamejitokeza katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo kwa ajili ya kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa ambao wameweka kambi katika hospitali hiyo kwa muda wa wiki moja.

  Madaktari hao wamebobea katika fani mbalimbali, ikiwemo upasuaji, macho, moyo, ubongo, watoto, uzazi na kuendelea, wanatoka katika Hospital ya Benjamen Mkapa - BMH iliyopo Jiji Dodoma, ambayo ndio hospitali kuu ya rufaa ya kanda ya kati.

  Lengo la kambi hiyo ni kusogeza huduma ya afya kwa wananchi ambao kwa kawaida hushindwa kusafiri masafa ya mbali kutafuta huduma za afya.

  Wagonjwa

  Dkt. Henry Humba, ambae ni daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kutoka BMH, anasema mwitikio umekuwa mkubwa tofauti na matarajio yao ya awali.

  ''Ndani ya siku chache, tayari tumepokea wagonjwa zaidi ya elfu moja kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida. Na wengi wanaokuja wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo, macho, koo na masikio'', anasema Dkt Henry.

  Baadhi ya wagonjwa hao wakiwa katika rika na jinsia tofauti, wamesema wamerauka hospitalini hapo kwa ajili ya kupata matibabu, hata hivyo, wengine wanasema kasi ya kuhudumiwa kidogo imepungua kutokana na wingi wa wagonjwa, ingawa matumain yao ni kupata huduma kabla siku ya mwisho ya kambi hiyo ambayo ni kesho Ijumaa ya tarehe 11.

 6. Mahakama yamuidhinisha Condé kugombea muhula wa tatu Guinea

  Alpha Conde

  Mahakama ya kikatiba nchini Guinea imemuidhinisha rais Alpha Condé mwenye umri wa miaka 82 kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu utakaoandaliwa mwezi ujao.

  Mahakama hiyo pia imewaidhinisha wagombea 11, miongoni mwao mgombea mkuu wa upinzani Cellou Dalein Diallo.

  Miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya bwana Condé baada ya kiongozi huyo kushinikiza mageuzi ya kikatiba kupitia kura ya maoni ya mwezi Maachi iliyomwezesha kugombea muhula wa tatu.

  Karibu wa 30 wameripotiwa kuuawa katika maandamano hayo.

  Bwana Condé alichaguliwa mara ya kwanza 2010 na kisha kuchaguliwa tena kwa mara ya pili 2015.

  Siku ya Jumanne, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alitoa wito kwa viongozi wa Afrika Magharibi kuzingatia ukomo wa mihula yao madarakani kwa mujibu wa katiba -ambayo alitaja kuwa chanzo cha mizozo ya kisiasa katika eneo hilo.

 7. Mshindi wa Tuzo ya Nobel 2018 awekwa chini ya ulinzi wa UN DR-Congo

  Dennis Mukwege

  Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Denis Mukwege amewekwa chini ya ulinzi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo baada ya vitisho vya kuuawa kutolewa dhidi yake.

  Dkt Mukwege alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2018 kutokana na juhudi zake za kutibu wahanga wa ubakaji katika mzozo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo.

  Mnamo mwenzi Julai Dkt Mukwege alisema kwamba alikuwa akitishiwa baada ya kuangazia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

  Ameandika kwenye Twitter yake kuhusu kupelekwa kwa vikosi vya usalama vya Umoja wa Mataifa katika hospitali ya Panzi iliyopo mjiwa Bukavu ambako anaendesha shughuli zake:

  View more on twitter

  Vita Mashariki mwa DRC vimewalazimisha mamia kutoroka makwao hali inayohatarisha maisha yao.

 8. Kambi ya watalii Kenya inayovuruga uhamaji wa nyumbu kufungwa

  Nyumbu

  Kambi ya watalii iliyojengwa karibu na Mto Mara nchini Kenya na ambayo ilizuia nyumbu wanaohama njia ya kupita itabolewa Alhamisi, kulingana na Seneta wa eneo hilo Ledama Ole Kina.

  Seneta huyo aliambia BBC kuwa inasikitisha kambi hiyo ilivuruga uhamiaji huo wa kila mwaka kwa muda mfupi lakini nyumbu hao waliendelea mbele na safari yao.

  "Kambi hiyo ilijengwa kinyemela kando ya mto na imekuwa hupo kwa zaidi ya siku 10, na ilijengwa katika njia ambayo haijawahi kupitiwa na nyumbu hao lakini mara hii kutokana na mvua inayonyesha kupitia hapo'' alisema bwana Ole Kina.

  Siku ya Jumatano Waziri wa Utalii wa Kenya Najib Balala, aliweka kwenye mtandao wa Twitter video inayoonesha jinsi mamia ya nyunbu hao ambao huwa kivutio kikubwa cha watalii wakijaribu kuvuka mto Mara, lakini wakarudishwa nyuma na watu walipokaribia kambi hiyo.

  View more on twitter

  Bw. Balala aliandika katika Twitter kwamba amezungumza na Gavana wa eneo hilo kuomba kambi hiyo ya watalii ‘’kuondolewa’’ kando ya mto huo ili kutoa njia ya wanyama hao kupita.

  Hatua hiyo imezua gumzo kali mitandaoni huku watu wakitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kuelezea ghadhabu zao.

  Mmoja wao aliita ‘’chukizo’’ na mwengine kusema ni ‘’uharibifu mkubwa wa turathi yetu ".

  Uhamaji mkubwa wa nyumbu ni moja wapo ya Maajabu Saba mpya duniani.

 9. Mhadhiri wa Marekani aliyedanganya kuhusu utambulisho wake ajiuzulu

  Jessica Krug

  Mhadhiri wa chuo kikuu nchini Marekani ambaye anachunguzwa baada ya kukiri kwamba alidanganya yeye ni mweusi amejiuzulu , Chuo kikuu cha George Washington kimethibitisha.

  Jessica Krug, profesa mshiriki wa Chuo Kikuu cha George Washington, alikiri kwamba yeye ni ''mzungu mwenye asili ya kiyahudi'' na mwanamke kutoka mji wa Kansas.

  Ujumbe huo ulisema: "Nimejijengea maisha ya uongo kwamba mimi ni mtu mweusi, na kudanganya katika kila hatua ya maisha yangu,"

  Kulingana na makala iliyochapishwa Alhamisi, Jessica Krug alisema aliamini visivyo kuhusu utambulisho, " kwamba sikuwa na haki ya kudai: Ni mwafrika wa kwanza kutoka Afrika Kaskazini, ni mtu mweusi mwenye asili ya Marekani, kisha mwenye asili ya Carribean kutoka Bronx".

 10. Museveni: 'Mkakati ninaotumia kuwashawishi vijana'

  Rais Yoweri Museveni

  Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amekuwa akizungumzia mkakati anaotumia kuwavutia vijana katika mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na wale ambao "wananitukana ,wakisema, wewe ni mjinga sana".

  Alisema mkakati wake ni kufanya mijadala thabiti ili kuwashawishi wakosoaji wake.

  "Sihitaji kulumbana na hawa watoto ili kuwashawishi, nikituma ujumbe kuwajibu kumi waliokuwa wakinishambulia, sita pekee wanabakia na wane wananijibu wakisema mzee ametoa hojanzuri."

  View more on twitter

  Bwana Museveni ameongoza Uganda tangu 1986 na atagombea urais kwa muhula wa sita katika uchaguzi mkuu ujao.

  Miongoni mwa wale wanapanga kumpinga katika kinyang’anyiro hicho ni msanii aliyegeuka mwanasiasa Bobi Wine, 38, wambaye ni maarufu kwa vijana.

 11. Karibu kwa matangazo mubashara