Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya yaliyokujia mubashara, tukutane tena kesho.
Mahakama yamnyima dhamana Paul Rusesabagina
ReutersCopyright: Reuters
Mahakama ya mwanzo mjini Kigali imekataa kumpa dhamana Paul Rusesabagina, ‘shujaa’ wa filamu ya mauaji ya kimbari ya
Rwanda anayeshitakiwa kwa ugaidi.
Bwana Rusesabagina alisimama mwenyewena akakata rufaa ya uamuzi huo, mwanishi wa
habari binafsi ameiambia BBC.
Jaji alisema kuwa kuna hofu kamba iwapo Bwana Rusesababgina ataachiliwa ''inaweza kuvuruga uchunguzi
unaoendelea'' .
Uamuzi wa mahakama unamaanisha kuwa, sasa Bwana Rusesabagina atahamishwa
kutoka mahabusu ya polisi na kupelekwa gerezani.
Anashitakiwa makosa 13 kuhusiana na mashambulio ya kikundi
cha waasi wa FLN yaliyowauwa raia kusini-magharibi mwa Rwanda katika miaka 2018
na 2019.
FLN kikundi cha muungano wa wapinzani MRCD-Ubumwe unaoendesha harakati zake nje na
Bwana Rusesabagina alikuwa ni Makamu
rais wa muungano huo.
Msaidizi wa Membe yuko mikononi mwa polisi, asema Mambosasa
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Membe alihoji aliko msaidizi wake Jerome LuandaImage caption: Membe alihoji aliko msaidizi wake Jerome Luanda
Baada ya mgombea wa
urais ACT Wazalendo Bernard Membe kudai msaidizi wake ametekwa na watu
wasiojulikana, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazarus
Mambosasa amesema yuko mikononi mwa polisi.
Mambosasa amesema
Jerome Luanda anashikiliwa na jeshi la polisi na anaendelea kuhojiwa kwa tuhuma
za utakatishaji wa fedha.
‘’Kimsingi tunae,
tumemkamata na amekamatwa akitoka safarini akitoka safarini pamoja na Membe
mwenyewe, na amekamatwa viwanja vya Mwalimu Nyerere Internaltonal Airport, kwa
hiyo hakukamatiwa mahali pa giza, alikamatwa mchana’’, amesema Mambosasa.
Bwana Mambosasa
amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kuwa amematwa na watu
wasiojulikana.
Jerome Luanda alikamatwa baada ya kurejea nchini akitokea Dubai katika Muungano wa nchi za kiarabu ambako aliambatana na Bwana Membe.
Membe awali alitangaza kuwa anakwenda Dubai kwa matibabu.
Kupitia ukurasa wa
twitter awali Bwana Membe alihoji ni wapi msaidizi wake alipo akielekeza hoja
yake kwa Kamanda Lazaro Mambosasa:
‘’Mpelelezi wangu mkuu akimaliza kukamilisha uchunguzi wake tutaliangalia
tulipeleke mahakamani’’ amesema Kamanda Mambosasa
Amekataa kuelezea ni
kituo gani anakoshikiliwa Luanda, lakini akasema yuko salama na anayetaka kujua
yuko wapi anaweza kuja na kuthibitisha yuko wapi.
Maya Moore aolewa na mwanaume aliyemsaidia kutoka gerezani
@MOOREMAYACopyright: @MOOREMAYA
Irons na Moore, katika picha waliyopiga baada ya kuachiliwa huru kutoka gerezani mwezi Julai mwaka huuImage caption: Irons na Moore, katika picha waliyopiga baada ya kuachiliwa huru kutoka gerezani mwezi Julai mwaka huu
Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani Maya Moore ameolewa
na Jonathan Irons manaume aliyemsaidia kumuondoajela baada ya kufungwa miaka bila hatia.
Irons aliachiliwa huru tarehe 23 Julai baada ya kufungwagerezani kwa miaka 23, na baadaye kubainika
kuwa hakutekeleza makossa ya wizi na ghasia, na hivyo hukumu yake kufutwa mwezi Machi.
Moore alikuwa
amesitishakucheza katika WNBA mwaka 2019 ili aweze kuhakikisha anaachiliwa huru .
"Tulioana miezi
kadhaa iliyopita na tunafurahia kuendelea na ukurasa huu mpya wa maisha pamoja," Moore
mwenye umri wa miaka 31, alikiambia kipindi cha Good Morning America.
Moore alichaguliwa
awali katika awamu ya kwanza ya mchezo kuchezea timu yaMinnesota Lynx mnamo mwaka 2011, akawasaidia kushinda
vikombe vinne vya Championi na kutangazwa kama mchezaji bora zaidi au MVP mwaka
2014.
Mchezaji huyo, ambaye
ni mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya WNBA pia ana medali ya dhahabu za Olympiki na
medali mbili za Shindano la dunia.
Rais wa Afrika Kusini aomba wimbo wa Jerusalema uchezwe katika sikukuu
Rais wa Afrika Kusini Cyril
Ramaphosa amewaombaraia wa nchi yake kusherehekea siku ya Urithi
yam waka huu -Heritage Day kwa kufanya shindano ladensi ya wimbo wa Jerusalema.
Jerusalema ni wimbo wa
mwanamuziki wa Afrika Ksuinina mzalishaji
KG ambao umevuma na kusambaa kote duniani. Wimbo huo ulinadi densi ya aina yake
inayochezwa na makundi ya watu kote dunianiambayo inasambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii.
Heritage Day ni
sikukuu inayosherehekewa kila mwaka
tarehe 24 Septemba kwa ajili ya maadhimisho ya utamaduni na utofauti wa watu wa nchi hiyo.
"Hapawezi kuwa
na njia nyingine nzuri ya kusherehekea utaifa wetu kuliko kujiunga na jambo
ambalo linasambaakote duniani ambalo
nidensi ya Jerusalema challenge," Bwana Ramaphosa alisema
katika hotuba yake ya televisheni.
"Kwahiyo ,
ninawaomba nyote kushiriki hili katika shindano la Siku ya urithi- Heritage Day na muoneshe dunia kile tunachoweza kukifanya ."
Virusi vya corona: Hatua za udhibiti zalegezwa Afrika kusini, huku maambukizi yakipungua
ReutersCopyright: Reuters
Afrika Kusini ilitekeleza amri ya kutotoka nje tarehe tarehe 27 MachiImage caption: Afrika Kusini ilitekeleza amri ya kutotoka nje tarehe tarehe 27 Machi
Afrika Kusini , ambayo ilikuwa ni moja ya nchi
zilizochukua hatua kali mapema zaidi duniani za kukabiliana na kusambaa ka
virusi vya corona, imetangaza kulegeza zaidi hatua hizo dhidi ya viusi hivyo.
Kuanzia tarehe 20 Septemba amri ya kutotembea nje usiku
itapunguzwa, mikusanyiko itaruhusiwa kwa 50% ya uwezo wa maeneo ya mikusanyiko , na pombe zitauzwa tena.
"Tumevuka dhoruba la
virusi vya corona," alisema Rais Cyril Ramaphosa katika hotuba yake ya televisheni.
Lakini sharia za kukaa
mbali na uvaji wa barakoa zitaendelea.
Afrika Kusini ambayo
iliingia katika kipindi cha sheria ya kukaa nyumbani tarehe 27 Machi – hadi sasa
imeripoti zaidi ya maambukizi 650,000, ikiwa na vifo zaidi ya 15,000.
Hatahivyo, idadi ya
maambukizi mapya imepungua hadi 12,000 kwa
siku katika mwezi wa Julai walikuwa
chini ya 2,000.
Msumbiji yaripoti kupungua kwa uwindaji haramu wa ndovu
Martin Harvey/WWFCopyright: Martin Harvey/WWF
Msumbiji imerekodi kushuka kwa 70% kwa uwindaji haramu wa ndovu, kwa mujibu wa
waziri wa ardhi na mazingira, Ivete Maibasse.
Amesema kupungua
huko kwa vitendo vya uwindaji haramu kumetokana na juhudi za vikosi vya usalama
za kulinda maeneo ya uhifadhi a wanyama hao.
"Hadi mwaka 2014,
tulikuwa tunarekodi kupotea kwa tembo 1,200 kwa mwaka ," alisema, na
kuongeza kuwa idadiimepungua na kufikia
hadi ndovu 360 kwa mwaka kati yam waka 2015 na 2019.
Waziri huyo amesema
kwamba hoifadhi ya mbuga za wanyama ya Niassa, eneo kubwa linalolindwa zaidi nchini ,
limepoteza ndovu mmoja kwa uwindaji haramu katika kipindi cha miaka miwili
iliyopita.
Jimbo la Kaduna laidhinisha sheria ya kuwahasi wabakaji watoto
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Kumekuwa na malalamiko makubwa juu ya ubakaji kote nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuniImage caption: Kumekuwa na malalamiko makubwa juu ya ubakaji kote nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuni
Gavana wa jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Kaduna, Nasir Ahmad el-Rufai, amesaini sheria inayotoa
adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya ubakaji wa watoto.
Kulingana na sheria hiyo wanaopatikana na hatia ya ubakaji wa watoto walio chini ya umri
wa miaka 14 watapewa hukumu ya kufanyiwa upasuaji wa kuwahasi na kifo
Pale ambapo muathiriwa
atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 14, sharia inasema muhalifu atahukumiwakuhasiwa na kifungo cha maisha.
Wahalifu wa kike
watu wazima watakaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto watahukumiwa kuondolewa
mishipa ya uzazi (fallopian tubes) na kifo.
Katika kesi za ubakaji ambapomuathiriwa ana umri wa miaka 14 , ripoti ya
kimatibabu itakuwa muhimu katika kuthibitisha madai.
Wabakaji wa watoto
pia wataorodheshwa katika kumbukumbu ya watu wenye makossa ya ngono
itakayochapishwa katika vyombo vya habari.
Gavana wa Kaduna
alithibitisha kuwa amesaini sheria hiyo katika tweet aliyoituma Jumatano jioni.
Wabunge wa jimbo
hilo waliidhinisha muswada wa sharia hiyo wiki iliyopita.
Kaduna ni jimbo
pekee nchini Nigeria lenye kipengele cha aina hiyo katika sharia yake ya
ubakaji.
Kumekuwa na malalamiko makubwa ya umma dhidi
ya ubakajikote nchini Nigeria katika
miezi ya hivi karibuni. Licha ya kwamba watu kadhaa wamekuwa wakikamatwa,
inaaminiwa kuwa idadi ya wanaopatikana na hatia ni ya chini.
Wafungwa saba kati ya 219 waliotoroka gerezani Uganda wakamatwa
GoogleCopyright: Google
Wafungwa walikimbilia katika milima ya MorotoImage caption: Wafungwa walikimbilia katika milima ya Moroto
Wafungwa saba kati ya 219 waliotoroka kutoka katika gereza kaskazini-mashariki mwa Uganda wamekamatwa.
Wafungwa hao walimpiga risasi na kumuua askazi ambaye alijaribu kuwazuwia kutoroka, kabla ya kukimbilia kwenye mlima wa Moroto-Mount Moroto Jumatano mchana.
Msemaji wa hudma za magereza nchini humo amesema wamepeleka helikopta tatu na askari wanaotembea kwa miguu kuwasaka wafungwa hao. Wawili kati yao wamepigwa risasi na kufa.
Inasemekana wafungwa hao walitoroka na
bunduki 15 pamoja na risasi.
Jengo la gereza hilo liko
kwenye eneo la mlima Moroto- Mount Moroto, pembeni mwa mji huo.
Kwa mujibu wa shirika la
habari la Associated Press, wafungwa walivua
sare zao za jela za rangi ya manjano na
kukimbia uchi milimani kuepuka kubainika.
Inaaminia kuwa wafungwa hao walikuwa wakijaribu kutumia njia ya milimani kuvuka ili waweze kuvuka mpaka waingie Kenya
Gereza hilo ambao kwa kawaida huwahifadhi wafungwa 600, kwa sasa limefungwa huku uchunguzi ukiendelea kubaini ni vipi wafungwa hao walivunja gereza na kutoroka.
Jeshi limetuma picha ya msako wao dhidi ya wafungwa:
Habari za moja kwa moja
Na Dinah Gahamanyi
time_stated_uk
Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya yaliyokujia mubashara, tukutane tena kesho.
Mahakama yamnyima dhamana Paul Rusesabagina
Mahakama ya mwanzo mjini Kigali imekataa kumpa dhamana Paul Rusesabagina, ‘shujaa’ wa filamu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda anayeshitakiwa kwa ugaidi.
Bwana Rusesabagina alisimama mwenyewena akakata rufaa ya uamuzi huo, mwanishi wa habari binafsi ameiambia BBC.
Jaji alisema kuwa kuna hofu kamba iwapo Bwana Rusesababgina ataachiliwa ''inaweza kuvuruga uchunguzi unaoendelea'' .
Uamuzi wa mahakama unamaanisha kuwa, sasa Bwana Rusesabagina atahamishwa kutoka mahabusu ya polisi na kupelekwa gerezani.
Anashitakiwa makosa 13 kuhusiana na mashambulio ya kikundi cha waasi wa FLN yaliyowauwa raia kusini-magharibi mwa Rwanda katika miaka 2018 na 2019.
FLN kikundi cha muungano wa wapinzani MRCD-Ubumwe unaoendesha harakati zake nje na Bwana Rusesabagina alikuwa ni Makamu rais wa muungano huo.
Msaidizi wa Membe yuko mikononi mwa polisi, asema Mambosasa
Baada ya mgombea wa urais ACT Wazalendo Bernard Membe kudai msaidizi wake ametekwa na watu wasiojulikana, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazarus Mambosasa amesema yuko mikononi mwa polisi.
Mambosasa amesema Jerome Luanda anashikiliwa na jeshi la polisi na anaendelea kuhojiwa kwa tuhuma za utakatishaji wa fedha.
‘’Kimsingi tunae, tumemkamata na amekamatwa akitoka safarini akitoka safarini pamoja na Membe mwenyewe, na amekamatwa viwanja vya Mwalimu Nyerere Internaltonal Airport, kwa hiyo hakukamatiwa mahali pa giza, alikamatwa mchana’’, amesema Mambosasa.
Bwana Mambosasa amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kuwa amematwa na watu wasiojulikana.
Jerome Luanda alikamatwa baada ya kurejea nchini akitokea Dubai katika Muungano wa nchi za kiarabu ambako aliambatana na Bwana Membe.
Membe awali alitangaza kuwa anakwenda Dubai kwa matibabu.
Kupitia ukurasa wa twitter awali Bwana Membe alihoji ni wapi msaidizi wake alipo akielekeza hoja yake kwa Kamanda Lazaro Mambosasa:
‘’Mpelelezi wangu mkuu akimaliza kukamilisha uchunguzi wake tutaliangalia tulipeleke mahakamani’’ amesema Kamanda Mambosasa
Amekataa kuelezea ni kituo gani anakoshikiliwa Luanda, lakini akasema yuko salama na anayetaka kujua yuko wapi anaweza kuja na kuthibitisha yuko wapi.
Maya Moore aolewa na mwanaume aliyemsaidia kutoka gerezani
Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani Maya Moore ameolewa na Jonathan Irons manaume aliyemsaidia kumuondoajela baada ya kufungwa miaka bila hatia.
Irons aliachiliwa huru tarehe 23 Julai baada ya kufungwagerezani kwa miaka 23, na baadaye kubainika kuwa hakutekeleza makossa ya wizi na ghasia, na hivyo hukumu yake kufutwa mwezi Machi.
Moore alikuwa amesitishakucheza katika WNBA mwaka 2019 ili aweze kuhakikisha anaachiliwa huru .
"Tulioana miezi kadhaa iliyopita na tunafurahia kuendelea na ukurasa huu mpya wa maisha pamoja," Moore mwenye umri wa miaka 31, alikiambia kipindi cha Good Morning America.
Moore alichaguliwa awali katika awamu ya kwanza ya mchezo kuchezea timu yaMinnesota Lynx mnamo mwaka 2011, akawasaidia kushinda vikombe vinne vya Championi na kutangazwa kama mchezaji bora zaidi au MVP mwaka 2014.
Mchezaji huyo, ambaye ni mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya WNBA pia ana medali ya dhahabu za Olympiki na medali mbili za Shindano la dunia.
Rais wa Afrika Kusini aomba wimbo wa Jerusalema uchezwe katika sikukuu
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewaombaraia wa nchi yake kusherehekea siku ya Urithi yam waka huu -Heritage Day kwa kufanya shindano ladensi ya wimbo wa Jerusalema.
Jerusalema ni wimbo wa mwanamuziki wa Afrika Ksuinina mzalishaji KG ambao umevuma na kusambaa kote duniani. Wimbo huo ulinadi densi ya aina yake inayochezwa na makundi ya watu kote dunianiambayo inasambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii.
Heritage Day ni sikukuu inayosherehekewa kila mwaka tarehe 24 Septemba kwa ajili ya maadhimisho ya utamaduni na utofauti wa watu wa nchi hiyo.
"Hapawezi kuwa na njia nyingine nzuri ya kusherehekea utaifa wetu kuliko kujiunga na jambo ambalo linasambaakote duniani ambalo nidensi ya Jerusalema challenge," Bwana Ramaphosa alisema katika hotuba yake ya televisheni.
"Kwahiyo , ninawaomba nyote kushiriki hili katika shindano la Siku ya urithi- Heritage Day na muoneshe dunia kile tunachoweza kukifanya ."
Virusi vya corona: Hatua za udhibiti zalegezwa Afrika kusini, huku maambukizi yakipungua
Afrika Kusini , ambayo ilikuwa ni moja ya nchi zilizochukua hatua kali mapema zaidi duniani za kukabiliana na kusambaa ka virusi vya corona, imetangaza kulegeza zaidi hatua hizo dhidi ya viusi hivyo.
Kuanzia tarehe 20 Septemba amri ya kutotembea nje usiku itapunguzwa, mikusanyiko itaruhusiwa kwa 50% ya uwezo wa maeneo ya mikusanyiko , na pombe zitauzwa tena.
"Tumevuka dhoruba la virusi vya corona," alisema Rais Cyril Ramaphosa katika hotuba yake ya televisheni.
Lakini sharia za kukaa mbali na uvaji wa barakoa zitaendelea.
Afrika Kusini ambayo iliingia katika kipindi cha sheria ya kukaa nyumbani tarehe 27 Machi – hadi sasa imeripoti zaidi ya maambukizi 650,000, ikiwa na vifo zaidi ya 15,000.
Hatahivyo, idadi ya maambukizi mapya imepungua hadi 12,000 kwa siku katika mwezi wa Julai walikuwa chini ya 2,000.
Msumbiji yaripoti kupungua kwa uwindaji haramu wa ndovu
Msumbiji imerekodi kushuka kwa 70% kwa uwindaji haramu wa ndovu, kwa mujibu wa waziri wa ardhi na mazingira, Ivete Maibasse.
Amesema kupungua huko kwa vitendo vya uwindaji haramu kumetokana na juhudi za vikosi vya usalama za kulinda maeneo ya uhifadhi a wanyama hao.
"Hadi mwaka 2014, tulikuwa tunarekodi kupotea kwa tembo 1,200 kwa mwaka ," alisema, na kuongeza kuwa idadiimepungua na kufikia hadi ndovu 360 kwa mwaka kati yam waka 2015 na 2019.
Waziri huyo amesema kwamba hoifadhi ya mbuga za wanyama ya Niassa, eneo kubwa linalolindwa zaidi nchini , limepoteza ndovu mmoja kwa uwindaji haramu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Jimbo la Kaduna laidhinisha sheria ya kuwahasi wabakaji watoto
Gavana wa jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Kaduna, Nasir Ahmad el-Rufai, amesaini sheria inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya ubakaji wa watoto.
Kulingana na sheria hiyo wanaopatikana na hatia ya ubakaji wa watoto walio chini ya umri wa miaka 14 watapewa hukumu ya kufanyiwa upasuaji wa kuwahasi na kifo
Pale ambapo muathiriwa atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 14, sharia inasema muhalifu atahukumiwakuhasiwa na kifungo cha maisha.
Wahalifu wa kike watu wazima watakaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto watahukumiwa kuondolewa mishipa ya uzazi (fallopian tubes) na kifo.
Katika kesi za ubakaji ambapomuathiriwa ana umri wa miaka 14 , ripoti ya kimatibabu itakuwa muhimu katika kuthibitisha madai.
Wabakaji wa watoto pia wataorodheshwa katika kumbukumbu ya watu wenye makossa ya ngono itakayochapishwa katika vyombo vya habari.
Gavana wa Kaduna alithibitisha kuwa amesaini sheria hiyo katika tweet aliyoituma Jumatano jioni.
Wabunge wa jimbo hilo waliidhinisha muswada wa sharia hiyo wiki iliyopita.
Kaduna ni jimbo pekee nchini Nigeria lenye kipengele cha aina hiyo katika sharia yake ya ubakaji.
Kumekuwa na malalamiko makubwa ya umma dhidi ya ubakajikote nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuni. Licha ya kwamba watu kadhaa wamekuwa wakikamatwa, inaaminiwa kuwa idadi ya wanaopatikana na hatia ni ya chini.
Wafungwa saba kati ya 219 waliotoroka gerezani Uganda wakamatwa
Wafungwa saba kati ya 219 waliotoroka kutoka katika gereza kaskazini-mashariki mwa Uganda wamekamatwa.
Wafungwa hao walimpiga risasi na kumuua askazi ambaye alijaribu kuwazuwia kutoroka, kabla ya kukimbilia kwenye mlima wa Moroto-Mount Moroto Jumatano mchana.
Msemaji wa hudma za magereza nchini humo amesema wamepeleka helikopta tatu na askari wanaotembea kwa miguu kuwasaka wafungwa hao. Wawili kati yao wamepigwa risasi na kufa.
Inasemekana wafungwa hao walitoroka na bunduki 15 pamoja na risasi.
Jengo la gereza hilo liko kwenye eneo la mlima Moroto- Mount Moroto, pembeni mwa mji huo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, wafungwa walivua sare zao za jela za rangi ya manjano na kukimbia uchi milimani kuepuka kubainika.
Inaaminia kuwa wafungwa hao walikuwa wakijaribu kutumia njia ya milimani kuvuka ili waweze kuvuka mpaka waingie Kenya
Gereza hilo ambao kwa kawaida huwahifadhi wafungwa 600, kwa sasa limefungwa huku uchunguzi ukiendelea kubaini ni vipi wafungwa hao walivunja gereza na kutoroka.
Jeshi limetuma picha ya msako wao dhidi ya wafungwa:
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Alhamisi tarehe 17.09.2020