Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Esther Namuhisa

time_stated_uk

 1. Kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Tukutane tena Ijumaa 25/09/2020

 2. Rais Ramaphosa ataka wananchi kusheherekea urithi wao kwa wimbo wa 'Jerusalema'

  Afrika
  Image caption: Rais ataka waafrika kusini kusherekea siku ya urithi kwa wimbo wa Jerusalema

  Afrika Kusini leo wakiwa wanasheherekea siku ya urithi, waandaaji filamu wameonyesha mradi mpya unaohusisha uchezaji wa wimbo maarufu wa Jerusalema.

  Abongwe Booi na Calvin Hayward ni miongoni mwa watu wanaohusika na filamu,wameiambia BBC kuwa wanasheherekea umoja ambao umeletwa na wimbo wa Jerusalema.

  Jerusalema ni wimbo wa msanii wa Afrika kusini Master KG ambao umepata umaarufu maeneo mbalimbali duniani, ukiongozwa kwa mashindano ya kucheza katika nchi mbalimbali.

  Rais Cyril Ramaphosa ametaka raia wa Afrika Kusini kutumia wimbo wa Jerusalema kusheherekea siku ya urithi.

  View more on youtube

  Siku hii ya urithi Afrika Kusini inaangazia uzuri wa taifa hilo katika utamaduni, dini na siasa .

 3. Botswana kuanza kufundisha kiswahili shuleni

  Botswana ina mpango wa kuanzisha somo la kiswahili shuleni,mamlaka ya nchi hiyo imeeleza kwa mujibu wa mtandao wa Nation Africa.

  Waziri wa elimu wa Botswana bwana Fidelis Molao amesema lugha ya kiswahili itaanzishwa nchini humo siku zijazo.

  Kiswahili ni lugha yenye asili ya kibantu inayozungumzwa zaidi katika mataifa ya Afrika mashariki Kenya, Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda na mataifa mengine kama DRC na baadhi ya maeneo ya Malawi.

  Kama lugha ya Kiswahili itaanza kufundishwa nchini humo basi lugha hiyo itakuwa ya kwanza kutoka barani Afrika kuzungumzwa na mataifa mengi zaidi duniani.

  Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakuwa ukanda ambao washirika wake wengi wanazungumza lugha ya kiswahili na Botswana ikiwa miongoni mwa mataifa hayo , bwana Molao amesema.

  Aidha wakati rais Magufuli akimaliza muda wake kama mwenyekiti wa SADC, alisema baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chake cha uenyekiti ni pamoja na Kiswahili kufanywa kuwa lugha ya nne rasmi katika Jumuiya hiyo.

 4. Wafahamu waafrika waliopo kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi duniani

  afrika
  Image caption: Tony Elumelu ambaye ni tajiri mkubwa mjasiriamali Nigeria

  Orodha ya watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani kwa mwaka 2020, kwa mujibu wa jarida la Times imetolewa Jumanne ikiwa imejumuisha watu wanaoshughulika na sekta mbalimbali kama biashara , Sanaa, michezo, muziki na nyingine nyingi.

  Na wafuatao ni miongoni mwa waafrika ambao wako kwenye orodha hiyo.

  Tony Elumelu ni miongoni mwa watu watano wa Afrika wenye ushawishi duniani, yeye ni tajiri mkubwa mjasiriamali Nigeria, anafahamika pia kwa kutoa ufadhili katika kijamiii.

  Wapili ni mwendesha mashtaka na mwanasheria mkuu wa zamani wa Gambia Abubacarr Tambadou.

  kitabu

  Mwandishi wa kitabu cha "Children of Blood and Bones" bi.Tomi Adeyemi mwenye umri wa miaka 27-ni mwandishi wa vitabu vya simulizi na mkufunzi wa uandishi wa vitabu mwenye asili ya Nigeria.

  Wanne akiwa Jean-Jacques Muyembe ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya kitaifa ya utafiti wa sayansi nchini DRC.

  Pamoja na Dkt Tunji Funsho ni mtaalamu wa magonjwa ya moyo nchini Nigeria na mwenyekiti wa mpango wa kutokomeza polio wa shirika la kimataifa la Rotary.

 5. Elimu ya jinsia ya UN yakabiliwa na upinzani Zambia

  Mradi wa elimu ya jinsia nchini Zambia ambao unafadhiliwa na shirika la kimataifa la idadi ya watu (UNFPA) umekataliwa na waziri wa masuala ya dini nchini humo.

  Godfridah Sumaili alinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo akisema mradi huo unahamasisha kujitambua kijinsia, mapenzi ya jinsia moja na haki za kigeni za afya ya uzazi.

  “Zambia ni taifa linalofuata mlengo wa kikristo na hivyo tunapaswa kulinda maadili yetu ya kikristo,” alisema.

  Kanisa la kiinjili la kikristo pia lilipinga mradi huo lakini kulikuwa na mvutano mkubwa kutoka katika makundi mbalimbali ambayo yalionesha kuunga mkono.

  Tovuti ya Umoja wa mataifa imesema mradi huo unajumuisha taarifa sahihi kuhusu maendeleo ya binadamu na afya ya uzazi, pamoja na taarifa za mpango wa uzazi na magonjwa yanayoambukiza kupitia ngono.

 6. Yemi Alade kuwawakilisha wanawake UN

  Yemi

  Mwanamuziki wa Nigerian, Yemi Alade amehaidi kutumia sauti yake kwa ajili ya wahitaji wakiwemo wanawake, mara baada ya Umoja wa mataifa kumtangaza kuwa balozi wao.

  Jumatano, Yemi alitajwa kuwa balozi wa nia njema na shirika la kimataifa la maendeleo (UNDP).

  Katika ujumbe wake kwenye video, alisema atawaangazia wale wanaoangaika kiuchumi na kijamii kutokana na athari za mlipuko wa corona.

  Yemi amesema yuko tayari kutoa suluhu ya changamoto nyingi kupitia ubunifu wake.

  Wanawake ni miongoni mwa watu bilioni 4 ambao wanajaribu kukabiliana na corona bila ya kupata usaidizi wowote.

 7. Gambia yalaumiwa kukataa rasimu ya katiba

  Gambia

  Kiongozi wa upinzani nchini Gambia ameilaumu serikali kwa kukataa rasimu ya katiba inayoainisha ukomo wa urais.

  Bunge lilikataa katiba hiyo Jumanne.

  Kipengele kinachomzuia rais Adama Barrow kuweka muda wa ukomo wa utawala kwa mihula mingine miwili kunaonekana kuwa hatua kubwa ya mshikamano.

  Kiongozi wa chama cha 'United Democratic Party '(UDP), Ousainou Darboe, alisema mapendekezo hayo yalikuwa sio dalili nzuri ya demokrasia.

  Uchaguzi mkuu ujao unapangwa kufanyika mwakani.

  Bwana Darboe ameapa kuitambulisha tena rasimu hiyo ya katiba kama upande wa upinzani ukishinda uchaguzi.

  Rais Barrow aliingia madarakani mwaka 2016 - baada ya kumalizika kwa utawala wa kimabavu wa ending Yahya Jammeh uliodumu miaka 22.

 8. Ni sharti upime Corona kabla ya kufunga ndoa Rwanda

  Yves Bucyana

  BBC Swahili

  Manzi Jules &Solange

  Suala la kuwataka wanandoa na wageni wao kupima Covid-19 kwa gharama zao ili kuwaruhusu kufanya sherehe za baada ya kufunga ndoa ,linaendelea kuzua mjadala mkali nchini Rwanda.

  Wakati huu wa Covid-19, ni wageni 30 tu wanaoruhusiwa kuhudhuria sherehe za harusi kulingana na hatua iliyowekwa na serikali ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona nchini humo.

  Huku gharama za vipimo vya Covid-19 kwa mtu mmoja ni dolla 50.

  Jambo ambalo linawafanya baadhi kuamua kufanya hafla ya kanisani tu pasipo kusherehehekea harusi kwa kuhofia gharama hizo,huku wengine wakiahirisha kabisa harusi zao.

  Manzi Jules &Solange
  Image caption: Manzi Jules na mke wake Solange

  Manzi Jules na mkewe Solange ambao wamefunga pingu za maisha katika kanisa la Mtakatifu Bosco mjini Kigali hawakuwa na sherehe zozote baada ya ibada ya ndoa.

  Na si kwamba sherehe zimekatazwa,la hasha ni kuambatana na maagizo yaliyopo ya kuzuia maambukizi ya Covid-19. Agizo la serikali linahitaji kwamba kufanya sherehe yoyote ya harusi, wanandoa na wageni wao lazima wawe na uthibitisho kuwa walipima Covid-19 na hawana virusi hivyo.

  ‘’Tuliamua kuja kanisani kupata baraka za Mwenyezimungu tu,haingewezekana kupima waalikwa wote 30,ingenigharimu franga milioni moja unusu($ 1500) tutafanya sherehe muda utakaporuhusu,’’Manzi Jules alisema.

  Manzi Jules &Solange

  Aidha hatua hiyo ya kupima covid 19 imewalazimu wengine kuhairisha kufunga ndoa.

  ‘’Masharti haya yalitolewa siku chache kabla ya harusi yangu .niliamua kuahirisha harusi na sherehe zake kwani unajua siku ya harusi hutokea mara moja katika maisha ya mtu .tunaomba serikali kuturahisishia kwa kupima watu kama ilivyofanya tangu mwanzoni mwa Covid-19 au kupunguza gharama ya vipimo’’

  Waziri wa mambo ya ndani Anastase Shyaka amesema serikali iliweka masharti hayo ili kuokoa maisha ya wananchi.

  Awali Mashirika yasiyo ya kiserikali yaliiandikia serikali kulalamikia hatua zinazochukuliwa zikiwemo hizi za kuwataka watu kugharamia wenyewe vipimo vya covid19 kutokana na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu kwa wananchi.

 9. Je Ecowas itaiondolea Mali vikwazo ?

  Mali

  Viongozi wa Afrika Magharibi wameonesha kuwa wanaweza kuongeza vikwazo dhidi ya Mali kufuatia mapinduzi yaliyofanyika mwezi uliopita.

  Mwakilishi wao, rais wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan,alipowasili Mali alisema kuwa maofisa wa jeshi ambao wamemuondoa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keïta walikubali wito wa kimataifa wa kuruhusu uongozi wa mpito utoke kwa raia.

  Maelezo yake yamependekeza kuwa Jumuiya ya kiuchumi ya ukanda wa Afrika magharibi , Ecowas, inaweza kukubali uteuzi wa aliyekuwa waziri wa ulinzi wa zamani, Bah Ndaw, kama rais wa mpito huku makamu wake akiwa anatoka upande wa jeshi, kaneli Assimi Goita.

  Uagizaji wa bidhaa nchini Mali tangu taifa hilo liwekewe vikwazo vya kibiashara.

 10. Karibu katika matangazo mubashara