Muungano wa kiuchumi wa
nchi za Afrika magharibi "umedokeza" kwamba vikwazo dhidi ya Mali
"huenda ikaondolewa", ujumbe wa Twitter kutoka ofisi ya rais wa mpito
umesema.
Ecowas iliichukulia
hatua nchi hiyo kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa madarakani Rais Ibrahim
Boubacar Keïta mwezi Augosti.
Ilikuwa imeshinikiza
kurejeshwa madarakani kwa utawala wa kiraia, lakini licha ya raia wa mpito wa kiraia
Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane kuteuliwa vikwazo havijaondolewa.
Mapema wiki hii, Rais
wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema bado kuna "masuala" yanayotakiwa
kufanyiwa kazi kabla ya hali kawaida kurudiwa.
Kwa mfano makamu wa
rais mpya wa Mali ni kiongozi wa zamani wa kijeshi is the Kanali Assimi Goita, na
Ecowas anataka kuhakikisha hatakuwa rais.
Bw.
Ndaw alikuwa afisa wa zamani wa kijeshi na waziri ulinzi.
Wakenya walalamikia kuhamishwa kwa 'mti maarufu' Nairobi
Wakenya wamekuwa
wakitumia mitandao ya kijamii kulalamikia mpango wa serikali kukata kuupanda
upya mti maarufu ambao wa ‘fig tree’ ambao uko katika njia ya barabara mpya
nayoendelea kujengwa.
Baadhi yao wanasema
hatua hiyo ni uharibifu wa mazingira huku wengine wakihoji gharama yake.
Mamlaka ya ujenzi wa
barabara wamesema kuuhamishia mti huo mahali pengine ni sehemu ya juhudi za
kuhifadhi mazingira.
Wakenya wengine mtandaoni walitania ni pesa ngapi zingetumika katika uhamishaji.
"Natumai uhamishaji huo hautagharimu bilioni moja. Niliona Singapore ikihamisha miti kwa urahisi bila gharama kubwa, Mnaweza kuomba ushauriana kwa wataalam badala ya kupeana zabuni kwa Escobar wa Kemsa," Shukry aliandika akiashiria madai ya ufisadi unaokumba Mamlaka ya kununua na kusambaza dawa nchi Kenya (Kemsa).
Wengine walihoji kwanini mti huo unahamishwa na mingine inakatwa.
Covid-19: Uganda yarejelea safari za ndege za kimataifa
BBCCopyright: BBC
Uganda imefungua tena
mipaka yake ya kimataifa kwa mara ya kwanza tangu Machi, baada ya kufungwa kama
hatua ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.
Kufuatia hatua hiyo Shirika la ndege la Uganda imefanya safari ya kimataifa mapema Alhamisi kwa kutua katika mjini Nairobi na Mogadishu
kama ilivyopangwa.
Ndege
zingine za kimataifa pia zimetua nchini Uganda na pia kuanza safari.
Mamlaka ya usafiri
wa anga imetoa wito kwa wasafiri kufika katika uwanja wa ndege saa nne kabla ya
safari zao.
Maafisa wa
uhamiaji katika uwanja wa ndege wamewashauri wasafiri kutumia kufuata maagizo
waliyopewa ili kudhibiti hali ya watu kukaribiana
Wazara ya
Afya imesema wasafiri wanaozuru Uganda watatakiwa kuwasilisha cheti cha
kuonesha wamefanyiwa uchunguzi wa corona katika kipindi cha saa 72 kabla ya
kuanza safari na kwamba hawana virusivya corona.
Kenya ilipoteza mabilioni ya Covid-19 kupitia rushwa - ripoti ya ukaguzi
AFPCopyright: AFP
Kenya ilipoteza dola
milioni 21 wakati wa ununuzi wa vifaa vya kukabiliana na maradhi ya Covid- 19,
kwa mujibu wa ripoti ya uhasibu wa hivi karibuni.
Ripoti hiyo mpya inakuja baada ya ripoti ya vyombo vya habari kuangazia visa vya wizi wa misaada ya kukabiliana na Covid-19.
Mkaguzi Mkuu Nancy
Gathangu amesema wasimamizi wa bodi inayosimamia ununuzi na usambazaji wa vifaa
vya matibabu (Kemsa) ilikiukakanunu ya
ununuzi hali ambayo ilisababisha ufujaji wa fedha za umma.
Serikali iliamuru
kufanyika kwa uchunguzikufuatia
malalamishi ya umma.
Kemsa imepinga madai
kwamba fedha ziliibiwa katika mchakato wa ununuzi wa vifaa vya kukabiliana na
corona.
Ripoti ya ukaguzi
inasema wasimamizi wa Kemsa walikula njama na makampuni yaliyopewa zabuni
kufuja fedha za umma. Baadhi ya kampuni hizo zilisajiliwa wakati Kenya
ilipothibitisha mgonjwa wa kwanza wa Covid-19.
Vifaa vya matibabu
vilinunuliwa kwa bei ya juu zaidi na
baadhi ya bidhaa hizo bado zimekwama katika bohari ya Kemsa.
Ripoti hiyo pia
inasema fedha zilizokuwa zimetengewa bima ya afya ya umma zilitumiwa kununua vifaa vya kukabiliana na Covid-19 bila idhini ya Wizara ya Afya.
Wabunge wa Malawi wakataa msaada wa kondomu
Bunge MalawiCopyright: Bunge Malawi
Kiongozi wa wengi amesema wabunge wanaweza kumudu bei ya kondomuImage caption: Kiongozi wa wengi amesema wabunge wanaweza kumudu bei ya kondomu
Wabunge nchini Malawi wamekataa kupokea msaada wa mipira ya kondomu
zaidi ya 200,000 waliyopewa na shirika
moja la kutoa misaada.
Mipira hiyo ilikuwa iwekwe katika vyoo vya majengo ya bunge.
Kiongozi wa wengi bungeni, Richard Chimwendo, amesema wabunge hawahitaji msaada huo
kwasababu wana uwezo wa kumudu bei ya kondomu.
Msaada huo ulipewa mwenyekiti wa kamati ya,
Maggie Chinsinga.
Bw. Chimwendo alisema ripoti iliyochapishwa na
gazeti moja nchini humo kwamba msaada huo umewadhalilisha wabunge.
Ripoti hiyo ilimnukuu Bi Chinsinga akisema
kuwa bunge hutumia karibu mipira 10,000 ya kondomu kila mwezi na kwamba wakati mwingine "zinaisha", iliandika
gazeti la Nation nchini Malawi.
Naibu wa Spika, Madaliotso Kazombo, amekanusha
madai haya na kutaka gazeti hilo kuomba radhi.
Mkuu wa WHO Afrika alaani 'unyanyasaji wa kingono' uliofanywa na maafisa wake
Mkurugenzi wa Shirika
la Afya Duniani, barani Afrika Matshidiso Moeti, amesema madai kwamba wafanyakazi wa kutoa
misaada waliwanyanyasakingono wanawake
Wakati walipokuwa
wakishughulikia mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo "inavunja
moyo ".
Amesema atahakikisha uchunguzi
unafanywa kwa "haraka na njia ya uwazi bila kuegemea upande wowote" na
wale watakaopatikanakuhusika na uovu
huo watachukuliwa hatua kali.
Dk. Moeti amesema
atahakikisha njia za kuripote vitendo kama hivyo inafaimarishwa:
Uchunguzi wa mwaka mmoja uliofanywa na mashirika mawili umebaini kuwa wafanyakazi waliojitambulisha kama maafisa wa WHO waliwanyanyasa kingono wanawake nchini DR- Congo.
Afrika Kusini
imefungua mipaka yake kwa wasafiri kutoka nchi za Afrika, lakini imedumisha
vikwazo dhidi ya nchi ambazo zina viwango vya juu vya maambukizi ya corona
ikiwa ni pamoja na Uingereza, Marekani na Urusi.
Nchi hiyo ilifunga
mipaka yakemwezi Machi mwaka huu katika
juhudi za kuzuia kuenea kwa virusi.
Kuanzia leo Alhamisi
Afrika Kusini itafungua baadhi ya mipaka yake ya ardhini viwanja vyake vikuu
vya ndege Cape Town, Durban na Johannesburg.
Waziri wa mambo ya nje,
Naledi Pandor, amesema wasafiri wote watakaowasili watalazimika kuonesha cheti
cha kuthibitisha wamefanyiwa vipimo vya Covid-19 kutoka nchi zao na pia watafanyiwa
ukaguzi watakapofika nchini humo.
Nchi ambazo viwango
vya maambukizi ya virusi na vifo viko juu kuliko Afrika Kusini hawataruhusiwa
kuzuru nchi hiyo kwa shughuli za utalii.
'Wakati wa kufungua shule ni sasa', asema Waziri wa Elimu Kenya
Twitter/Wizara ya ElimuCopyright: Twitter/Wizara ya Elimu
Waziri wa Elimu Kenya George MagohaImage caption: Waziri wa Elimu Kenya George Magoha
Waziri wa
Elimu wa Kenya George Magoha kwa mara nyiingine amesema shule zinastahili
kufunguliwa sasa na wala sio mwezi Januari mwaka ujao.
Akizungumza
na kamati ya bunge kuhusu elimu siku ya Jumanne Bw. Magoha alisema hata kama
serikali itasubiri hadi Januari mwaka 2021, mwenendo wa ugonjwa wa Covid -19
huenda usibadilike akiongeza kwamba watoto ''wako salama'' zaidi shuleni kuliko
nyumbani.
“Lazima
tufanye maamuzi magumu.Wakati wa
kufungua shule ni sasa,” Waziri Magoha aliiambia kamati ya bunge.
Amesema wizara yake inafanya kazi na wadau wa sekta ya elimu kujadili “jinsi” shule zitakavyofunguliwa “hivi
karibuni ”, huku akifuchua kuwa mapendekezo yaliyotolewa na jopokazi la elimu
kuhusu mwenendo wa Covid 19 yalijumuisha changamoto zote zinazokabili ufunguzi wa
shule wakati huu wa janga la corona.
Jopokazi hilo lilikuwa
limependekeza shule za msingi na za upili kufunguli wakati ya tarehe 5 na 19 Oktoba 2020. Alisema kalenda hiyo mpya ya ufunguzi wa shule ilikuwa imepangwa kwa njia ambayo ingehakikisha hakuna mwanafunzi angerudia darasa.
Watu 50 wauawa katika maandamano Guinea
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Vikosi vya uslama vyalaumiwa kwa kutekeleza mauaji GuineaImage caption: Vikosi vya uslama vyalaumiwa kwa kutekeleza mauaji Guinea
Shirika la kutetea haki la Amnesty
International limesema karibu watu 50 wameuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano
ya kupinga serikali nchini Guinea mwaka jana.
Ripoti mpya ya shirika hilo limelaumu vikosi
vya usalama kwa kutekeleza mauaji ya kiholela.
Baadhi ya waandamanaji walipigwa risasi wakiandamana dhidi ya hatua ya Rais Alpha Condé
kutaka kusalia madarakani kwa muhula wa tatu.
Ripoti hiyo pia imeangazia jinsi watu 200 walivyojeruhiwa na wengine 70 kuzuiliwa kinyume cha sheria.
Uchaguzi wa urais utafanyika nchi humo baadaye
mwezi Oktoba.
Karibu katika matangazo mubashara Alhamisi 01.10.2020
Habari za moja kwa moja
Na Ambia Hirsi
time_stated_uk
Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.
Fahamu majumba 10 marefu zaidi barani Afrika 2020
Historia ya majumba marefu zaidi barani Afrika ilianza mwaka 1973 kufuatia ujenzi wa jumba refu la Carlton Centers mjini Johannesburg.
Orodha kamili hapa:
Ecowas 'yadokeza' kuondolea Mali vikwazo
Muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika magharibi "umedokeza" kwamba vikwazo dhidi ya Mali "huenda ikaondolewa", ujumbe wa Twitter kutoka ofisi ya rais wa mpito umesema.
Ecowas iliichukulia hatua nchi hiyo kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta mwezi Augosti.
Ilikuwa imeshinikiza kurejeshwa madarakani kwa utawala wa kiraia, lakini licha ya raia wa mpito wa kiraia Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane kuteuliwa vikwazo havijaondolewa.
Mapema wiki hii, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema bado kuna "masuala" yanayotakiwa kufanyiwa kazi kabla ya hali kawaida kurudiwa.
Kwa mfano makamu wa rais mpya wa Mali ni kiongozi wa zamani wa kijeshi is the Kanali Assimi Goita, na Ecowas anataka kuhakikisha hatakuwa rais.
Bw. Ndaw alikuwa afisa wa zamani wa kijeshi na waziri ulinzi.
Wakenya walalamikia kuhamishwa kwa 'mti maarufu' Nairobi
Wakenya wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kulalamikia mpango wa serikali kukata kuupanda upya mti maarufu ambao wa ‘fig tree’ ambao uko katika njia ya barabara mpya nayoendelea kujengwa.
Baadhi yao wanasema hatua hiyo ni uharibifu wa mazingira huku wengine wakihoji gharama yake.
Mamlaka ya ujenzi wa barabara wamesema kuuhamishia mti huo mahali pengine ni sehemu ya juhudi za kuhifadhi mazingira.
Wakenya wengine mtandaoni walitania ni pesa ngapi zingetumika katika uhamishaji. "Natumai uhamishaji huo hautagharimu bilioni moja. Niliona Singapore ikihamisha miti kwa urahisi bila gharama kubwa, Mnaweza kuomba ushauriana kwa wataalam badala ya kupeana zabuni kwa Escobar wa Kemsa," Shukry aliandika akiashiria madai ya ufisadi unaokumba Mamlaka ya kununua na kusambaza dawa nchi Kenya (Kemsa).
Wengine walihoji kwanini mti huo unahamishwa na mingine inakatwa.
Covid-19: Uganda yarejelea safari za ndege za kimataifa
Uganda imefungua tena mipaka yake ya kimataifa kwa mara ya kwanza tangu Machi, baada ya kufungwa kama hatua ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.
Kufuatia hatua hiyo Shirika la ndege la Uganda imefanya safari ya kimataifa mapema Alhamisi kwa kutua katika mjini Nairobi na Mogadishu kama ilivyopangwa.
Ndege zingine za kimataifa pia zimetua nchini Uganda na pia kuanza safari.
Mamlaka ya usafiri wa anga imetoa wito kwa wasafiri kufika katika uwanja wa ndege saa nne kabla ya safari zao.
Maafisa wa uhamiaji katika uwanja wa ndege wamewashauri wasafiri kutumia kufuata maagizo waliyopewa ili kudhibiti hali ya watu kukaribiana
Wazara ya Afya imesema wasafiri wanaozuru Uganda watatakiwa kuwasilisha cheti cha kuonesha wamefanyiwa uchunguzi wa corona katika kipindi cha saa 72 kabla ya kuanza safari na kwamba hawana virusivya corona.
Kenya ilipoteza mabilioni ya Covid-19 kupitia rushwa - ripoti ya ukaguzi
Kenya ilipoteza dola milioni 21 wakati wa ununuzi wa vifaa vya kukabiliana na maradhi ya Covid- 19, kwa mujibu wa ripoti ya uhasibu wa hivi karibuni.
Ripoti hiyo mpya inakuja baada ya ripoti ya vyombo vya habari kuangazia visa vya wizi wa misaada ya kukabiliana na Covid-19.
Mkaguzi Mkuu Nancy Gathangu amesema wasimamizi wa bodi inayosimamia ununuzi na usambazaji wa vifaa vya matibabu (Kemsa) ilikiukakanunu ya ununuzi hali ambayo ilisababisha ufujaji wa fedha za umma.
Serikali iliamuru kufanyika kwa uchunguzikufuatia malalamishi ya umma.
Kemsa imepinga madai kwamba fedha ziliibiwa katika mchakato wa ununuzi wa vifaa vya kukabiliana na corona.
Ripoti ya ukaguzi inasema wasimamizi wa Kemsa walikula njama na makampuni yaliyopewa zabuni kufuja fedha za umma. Baadhi ya kampuni hizo zilisajiliwa wakati Kenya ilipothibitisha mgonjwa wa kwanza wa Covid-19.
Vifaa vya matibabu vilinunuliwa kwa bei ya juu zaidi na baadhi ya bidhaa hizo bado zimekwama katika bohari ya Kemsa.
Ripoti hiyo pia inasema fedha zilizokuwa zimetengewa bima ya afya ya umma zilitumiwa kununua vifaa vya kukabiliana na Covid-19 bila idhini ya Wizara ya Afya.
Wabunge wa Malawi wakataa msaada wa kondomu
Wabunge nchini Malawi wamekataa kupokea msaada wa mipira ya kondomu zaidi ya 200,000 waliyopewa na shirika moja la kutoa misaada.
Mipira hiyo ilikuwa iwekwe katika vyoo vya majengo ya bunge.
Kiongozi wa wengi bungeni, Richard Chimwendo, amesema wabunge hawahitaji msaada huo kwasababu wana uwezo wa kumudu bei ya kondomu.
Msaada huo ulipewa mwenyekiti wa kamati ya, Maggie Chinsinga.
Bw. Chimwendo alisema ripoti iliyochapishwa na gazeti moja nchini humo kwamba msaada huo umewadhalilisha wabunge.
Ripoti hiyo ilimnukuu Bi Chinsinga akisema kuwa bunge hutumia karibu mipira 10,000 ya kondomu kila mwezi na kwamba wakati mwingine "zinaisha", iliandika gazeti la Nation nchini Malawi.
Naibu wa Spika, Madaliotso Kazombo, amekanusha madai haya na kutaka gazeti hilo kuomba radhi.
Mkuu wa WHO Afrika alaani 'unyanyasaji wa kingono' uliofanywa na maafisa wake
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, barani Afrika Matshidiso Moeti, amesema madai kwamba wafanyakazi wa kutoa misaada waliwanyanyasakingono wanawake
Wakati walipokuwa wakishughulikia mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo "inavunja moyo ".
Amesema atahakikisha uchunguzi unafanywa kwa "haraka na njia ya uwazi bila kuegemea upande wowote" na wale watakaopatikanakuhusika na uovu huo watachukuliwa hatua kali.
Dk. Moeti amesema atahakikisha njia za kuripote vitendo kama hivyo inafaimarishwa:
Uchunguzi wa mwaka mmoja uliofanywa na mashirika mawili umebaini kuwa wafanyakazi waliojitambulisha kama maafisa wa WHO waliwanyanyasa kingono wanawake nchini DR- Congo.
Maelezo zaidi:
Afrika Kusini yafungua mipaka kwa nchi za Afrika
Afrika Kusini imefungua mipaka yake kwa wasafiri kutoka nchi za Afrika, lakini imedumisha vikwazo dhidi ya nchi ambazo zina viwango vya juu vya maambukizi ya corona ikiwa ni pamoja na Uingereza, Marekani na Urusi.
Nchi hiyo ilifunga mipaka yakemwezi Machi mwaka huu katika juhudi za kuzuia kuenea kwa virusi.
Kuanzia leo Alhamisi Afrika Kusini itafungua baadhi ya mipaka yake ya ardhini viwanja vyake vikuu vya ndege Cape Town, Durban na Johannesburg.
Waziri wa mambo ya nje, Naledi Pandor, amesema wasafiri wote watakaowasili watalazimika kuonesha cheti cha kuthibitisha wamefanyiwa vipimo vya Covid-19 kutoka nchi zao na pia watafanyiwa ukaguzi watakapofika nchini humo.
Nchi ambazo viwango vya maambukizi ya virusi na vifo viko juu kuliko Afrika Kusini hawataruhusiwa kuzuru nchi hiyo kwa shughuli za utalii.
'Wakati wa kufungua shule ni sasa', asema Waziri wa Elimu Kenya
Waziri wa Elimu wa Kenya George Magoha kwa mara nyiingine amesema shule zinastahili kufunguliwa sasa na wala sio mwezi Januari mwaka ujao.
Akizungumza na kamati ya bunge kuhusu elimu siku ya Jumanne Bw. Magoha alisema hata kama serikali itasubiri hadi Januari mwaka 2021, mwenendo wa ugonjwa wa Covid -19 huenda usibadilike akiongeza kwamba watoto ''wako salama'' zaidi shuleni kuliko nyumbani.
“Lazima tufanye maamuzi magumu.Wakati wa kufungua shule ni sasa,” Waziri Magoha aliiambia kamati ya bunge.
Amesema wizara yake inafanya kazi na wadau wa sekta ya elimu kujadili “jinsi” shule zitakavyofunguliwa “hivi karibuni ”, huku akifuchua kuwa mapendekezo yaliyotolewa na jopokazi la elimu kuhusu mwenendo wa Covid 19 yalijumuisha changamoto zote zinazokabili ufunguzi wa shule wakati huu wa janga la corona.
Jopokazi hilo lilikuwa limependekeza shule za msingi na za upili kufunguli wakati ya tarehe 5 na 19 Oktoba 2020. Alisema kalenda hiyo mpya ya ufunguzi wa shule ilikuwa imepangwa kwa njia ambayo ingehakikisha hakuna mwanafunzi angerudia darasa.
Watu 50 wauawa katika maandamano Guinea
Shirika la kutetea haki la Amnesty International limesema karibu watu 50 wameuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya kupinga serikali nchini Guinea mwaka jana.
Ripoti mpya ya shirika hilo limelaumu vikosi vya usalama kwa kutekeleza mauaji ya kiholela.
Baadhi ya waandamanaji walipigwa risasi wakiandamana dhidi ya hatua ya Rais Alpha Condé kutaka kusalia madarakani kwa muhula wa tatu.
Ripoti hiyo pia imeangazia jinsi watu 200 walivyojeruhiwa na wengine 70 kuzuiliwa kinyume cha sheria.
Uchaguzi wa urais utafanyika nchi humo baadaye mwezi Oktoba.
Karibu katika matangazo mubashara Alhamisi 01.10.2020