Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Abdalla Seif Dzungu na Dinah Gahamanyi

time_stated_uk

 1. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja , shukrani tukutane tena Jumatatu

 2. Ni kwanini Taliban imepinga ndoa za wake wengi kwa makamanda wake?

  Wanawake wa Taliban

  Kiongozi wa Taliban nchini Afghanistan ametoa amri ya kuwasihi makamanda wa kundi hilo kuachana na utamaduni wa kuoa wanawake wengi, ambao unawafanya "kukosolewa na maadui wetu''.

  Bonyeza hapa kusoma taarifa hii zaidi...

 3. Matokeo ya uchaguzi Uganda 2021: Picha hii haioneshi wizi wa kura Uganda

  Mitandao ya kijamii

  Wakati matokeo ya uchaguzi wa urais yakisubiriwa nchini Uganda, baadhi ya watumiaji wa mtandao wamekuwa wakishirikishana taarifa ambayo haihusiani na uchaguzi wa Alhamisi.

  Moja ya taarifa hizo ni picha ya zamani, ambayo ni mfano wa picha ya uchaguzi uliopita ambayo imeshirikishwa sana miongoni mwa umma.

  Picha hiyo inadaiwa kumuonesha kijana akimzuia afisa wa polisi kuiba sanduku la kura.

  Katika moja ya akaunti za Twitter, picha hiyo imeshirikishwa tena zaidi ya mara 3,000.

  Hata hivyo picha hiyo imeelezewa kimakosa.

  Tumeipata picha hiyo katika taarifa ya habari iliyochapishwa kwenye mtandao mwaka 2016 wakati Uganda ilipofanya uchaguzi uliopita.

  Maelezo katika picha yanasema polisi aking’ang’ana kubeba sanduku yenye vifaa vya kupigia kura katika kituo cha polisi cha Ggaba, pembezoni mwa mji mkuu Kampala.

  Hii ni baada ya wapiga kura wenye shauku kumzingira baada kusubiri kupiga kura kwa saa kadhaa.

  Picha hiyo hiyo pia ilitumiwa kwa madai ya hitilafu katika uchaguzi uliofanyika nchini Burkina Faso mwezi Novemba mwaka jana.

 4. Matokeo ya uchaguzi uganda 2021: Bobi Wine asema kufungwa kwa Intaneti kulivuruga uchaguzi

  bobi

  Bobi Wine amewaambia waandishi wa habari kuwa anaamini intaneti na mitandao ya kijamii vilifungwa ili kuvuruga mchakato wa uhesabuji kura.

  Mgombea huyo wa upinzani amedai kuwa kulikuwa na wizi.

  Mawakala wake pamoja na wawaikilishi wameendelea kukamatwa.

  Lakini mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Simon Byabakama, amesema kuwa Bobi Wine ana jukumu la kutoa ushahidi kwamba kuna wizi.

  Amesema kuwa wagombea walikuwa na mawakala ambao walishuhudia kuhesabiwa kwa kura katika vituo vya kukusanya na kuhesabu kura.

  Ni vituo viwili tu vya upigaji kura vilivyoripoti dosari na shughuli ya kupiga kura ikasitishwa katika vituo hivyo.

  Katika kituo kimoja cha kupigia kura, mtu mmoja alitoroka na sanduku la kura.

 5. Matokeo ya uchaguzi 2021:Bobi Wine apinga matokeo rasmi

  Mgombea wa urais nchini Uganda, Bobi Wine amepinga matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa hadi sasa na kujitaja binafsi kama rais mteuli, licha ya tume ya uchaguzi kusema kuwa sio kura zote zilizokwisha hesabiwa.

  Bobi Wine anadai uchaguzi wa Alhamisi ulitawaliwa na wizi mbaya zaidi wa kura kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Uganda, lakini hakutoa ushahidi wowote kuhusu madai yake.

  Ametangaza kuwa mapambano ndio kwanza yameanza.

  Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anasema kuwa atazungumza na waandishi wa habari tena mnamo saa chache zijazo juu ya kitakachofuatia.

  Matokeo ya awali yanayotolewa na Tume ya uchaguzi yanaonesha Rais Yoweri Museveni anaongoza kwa zaidi ya 60%.

  Wakati huohuo wanajeshi wakiwa wamezingira nyumba ya Bobi Wine.

 6. Afisa wa ngazi ya juu wa Rwanda afariki dunia kutoka na corona

  Thomas Kigabo

  Mchumi wa Benki kuu ya Rwanda Thomas Kigabo amefariki dunia kutokana na Covid-19.

  Amefariki mjini Nairobi Kenya ambako alikuwa akipata matibabu.

  Bw.Kigabo amekuwa mchumi mkuu katika Benki kuu ya Rwanda kwa zaidi ya miaka 10. Alikuwa pia muhadhiri wa chuo kikuu na muhubiri.

  Ni afisa wa ngazi ya juu zaidi wa serikali ya Rwanda kufariki kutokana na Covid-19 nchini humo.

  View more on twitter

  Hadi sasa Rwanda imerekodi visa vya watu 10,000 waliopatwa na virusi vya corona na vifo 133.

  Benki Kuu ya Rwanda imetoa taarifa kuhusu kifo chake kupitia mtandao wa Twitter:

 7. Makumi wauawa mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo

  Wapiganaji wa ADF

  Afisa wa ngazi ya juu mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo amesema kuwa raia 46 wameripotiwa kuuawa katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wa kiislamu.

  Kikundi cha Uganda cha Allied Democratic Forces (ADF), kimekuwa kikilaumiwa kwa mauaji ya mamia ya watu katika eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni.

  Afisa wa Congo alisema kuwa wanajeshi wamepelekwa katika kijiji ambacho kilishambuliwa ili kusaidia katika mchakato wa kutafuta miili ya watu waliouawa.

 8. Lady Gaga, Jennifer Lopez kutumbuiza wakati wa kuapishwa kwa Joe Biden.

  Jennifer Lopez na Lady Gaga
  Image caption: Jennifer Lopez na Lady Gaga walimuunga mkono Joe Biden katika kampeni za uchaguzi mwaka jana

  Lady Gaga alimfanyia kampeni Bw Biden wakati wa uchaguzi, ambapo alionekana nae katika mkesha wa siku ya uchaguzi mwezi Novemba mwaka jana.

  Ataimba wimbo wa taifa katika sherehe za kuapishwa kwa Bw Biden tarehe 20 Januari. Lopez ambaye pia alimuunga mkono Bw Biden mwaka jana, atafanya onyesho la muziki siku hiyo.

  Lady Gaga alijiunga na Biden katika kampeni
  Image caption: Lady Gaga alijiunga na Biden katika kampeni siku moja kabla ya uchaguzi wa rais mwaka jana

  Baada ya sherehe hizo, Tom Hanks ataonesha kipindi maalumu cha nyota wa muziki cha tevisheni.

  Kipindi hicho maalumu kilichoitwa - Celebrating America, cha dakika 90 pia kitawashirikisha wanamuziki Warekani Jon Bon Jovi, Demi Lovato, Justin Timberlake na Ant Clemons, na kitatangazwa moja kwa moja katika vituo vya habari vya ABC, CBS, CNN, NBC and MSNBC.

  Kamati ya maandalizi ya kuapishwa kwa Bw Biden imesema kuwa "itasherehekea mwanzo wa safari mpya ya taifa kuelekea umoja wa Marekani" na kuonesha uvumilivu, ushujaa na utashi wao wa kuungana na kuwa pamoja kama taifa katika kupona na kujijenga upya ".

 9. Habari za hivi pundeMatokeo ya uchaguzi Uganda 2021: Rais Museveni aongoza katika kura zilizohesabiwa

  Rais Yoweri Museveni
  Image caption: Rais Yoweri Museveni anawania muhula wa sita

  Rais wa Uganda Yoweri Museveni anaongoza kwa kura nyingi katika matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Ijumaa asubuhi.

  Bw Museveni amepata kura 1,536,205 sawa na (65.02%), huku mshindani wake mkuu Robert Kyagulanyi,maarufu kama Bobi Wine, akipata kura 647,146(27.39%) kutoka vituo 8,310 vya kupigia kura.

  Uganda ina jumla ya vituo 34, 684 vya kupigia kura.

 10. Polisi Uganda wavamia kituo cha ukusanyaji wa kura kisicho cha serikali

  Fred Enganga

  Polisi nchini Uganda wamevamia hoteli moja ambako kikundi cha wanaharakati wa mashirika ya kiraia na wakaguzi wa uchaguzi walikuwa wamekusanya taarifa kutoka kwa waangalizi wengine wa uchaguzi tofauti na Tume ya Uchaguzi.

  Msemaji wa polisi nchini humo, Bw Fred Enanga amesema kuwa walipata taarifa za ujasusi kwamba baadhi ya wanaharakati wa kiraia walikua wameweka kituo chao cha ukusanyaji wa matokeo ya kura katika Hoteli Africana iliyopo mjini Kampala , kando na kituo cha taifa kinachokusanya matokeo ya uchaguzi wa rais na wabunge.

  “ Tulituma watu wetu katika Hoteli Africana. Watu wenye jukumu la kudhibiti uchaguzi ni Tume ya uchaguzi. Huwezi kujua ni nini kilicho nyuma ya kituo hiki cha ukusanyaji wa matokeo ya kura. Huenda wana nia mbaya ambayo inaweza kuchochea ghasia . Sheria inaruhusu Tume ya uchaguzi tu kutangaza mataokeo. Kuwa na kituo cha kukusanya matokeo kando kunashusha hadhi ya uchaguzi na tume ya uchaguzi,” Bw Enanga aliiambia NTV Uganda.

 11. Tume ya Uchaguzi Uganda kupeperusha matokeo licha ya kufungwa kwa intaneti

  Matokeo ya uchaguzi Uganda
  Image caption: Matokeo ya uchaguzi Uganda

  Tume ya Uchaguzi nchini Uganda siku ya Alhamisi ilihakikisha kwamba matokeo ya moja kwa moja ya Uchaguzi katika kituo kikuu cha kujumlisha kura cha kitaifa yataendelea licha ya kufungwa kwa intaneti nchini humo.

  Mkuu wa Tume ya Uchguzi Simon Byabakama alisema kwamba wanatumia mbinu fulani kurusha matokeo hayo lakini haikutoa maelezo zaidi.

  ‘’ Hatutumii intaneti ya nchini kurusha matangazo . Tunatumia mfumo wetu . Msijali, matokeo yatapeperushwa licha ya kwamba mtandao umefungwa’’ , aliwambia waandishi.

  Ilitoa matokeo ya awali siku ya Ijumaa kutoka vituo 330 ambayo yalimuonesha rais Yoweri Museveni akichukua uongozi wa mapema kulingana na gazeti la Daily Monitor.

  Taifa hilo lina jumla ya vituo vya kupigia kura 34,684

  Sheria ya Uganda inaipatia uwezo Tume hiyo kupokea matokeo kutoka wilaya zote na kuyatangaza katika muda was saa 48 baada ya shughuli ya kupiga kura kukamilika.

 12. Natumai hujambo na karibu katika matangazo yetu mubashara kuhusu matokeo ya Uchaguzi wa Uganda