Na hadi kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa hii leo. Kwaheri.
Mkuu mpya wa jeshi nchini Msumbiji afariki dunia kwa corona
Mkuu wa jeshi nchini
Msumbiji aliyeteuliwa hivi karibuni, Eugénio Ussene Mussa, amefariki dunia
Jumatatu baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Aliaga dunia wakati
anapata matibabu katika moja ya hospitali kubwa nchini Msumbiji, kwa jina Maputo
Central Hospital.
Ni chini ya mwezi mmoja
tangu alipoapishwa kama Mkuu wa jeshi Januari 20 na kuchukua usukani.
Kabla ya kushika
hatamu alikuwa anahusika na oparesheni za kubabiliana na wanamgambo wa Kiislamu
katika eneo lenye utajiri mkubwa wa gesi mkoa wa Cabo Delgado.
Mwezi uliopita, aliwaambia
wanajeshi waliokuwa wamekusanyika kwamba 2021 utakuwa mwaka muhimu katika
kukabiliana na ugaidi.
Mjumbe wa kibinafsi wa
Umoja wa Mataifa nchini Msumbiji, Mirko Manzoni, ametuma risala za rambirambi
kwa Rais Filipe Nyusi na watu wa msumbiji.
Virusi vya Corona: Chuo Kikuu Huria Tanzania chatahadharisha wanafunzi, wafanyakazi
BBCCopyright: BBC
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimetoa tahadhari kwa wanafunzi na wafanyakazi wake juu ya hatari ya maambukizi ya virusi vya corona na kuwataka kuchukua hatua zote za kujilinda.
Tahadhari hiyo imetolewa kupitia waraka wa Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Elifas Tozo Bisanda wa jana Februari 8, 2020. Waraka amabao hii leo umekuwa ukisambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Tanzania.
Awali BBC ilizungumza na Profesa Tozo ambaye amesisitiza kuwa: "taarifa hii ni ya ndani kwa wafanyakazi pamoja na wanafunzi...wengine haiwahusu."
Waraka huo unawataka wanafunzi na wafanyakazi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kuwa tishio la maambukizi "linashamiri".
"Kwa upande wa wanafunzi tunasisitiza
wakae nyumbani na kusoma kwa njia ya mtandao, hatutaruhusu wanafunzi na wageni
kuingia kwenye kampasi zetu bila sababu maalumu’’ inasema taarifa hiyo.
Kwa upande wa wafanyakazi wao wataendesha mikutano yao kwa
njia ya mtandao.
Aidha taarifa hiyo pia imesisitiza umuhimu wa kujifukiza na
kutumia dawa asili, lakini pia kujilinda kwa kuvaa barakoa na kuepuka
misongamano.
"Inakua ngumu sana kuepuka maambukizi kama hatuzingatii
masharti ya kujikinga. Hata hivyo imethibitishwa kuwa taratibu za kujifukiza
(Nyungu) zinaleta ahueni lakini haimaiinishi kwamba virusi vile vitakufa’’
inasema taarifa hiyo.
Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) halijathibitisha dawa yeyote ya mitishamba kutibu virusi vya corona na pia imetahadharisha juu ya kujifukiza.
Mwezi uliopita Kanisa Katoliki nchini Tanzania lilitoa
tahadhari juu ya wimbi jipya la maambukizi ya corona na kuwataka wananchi
kuchukua hatua zote za kujikinga.
Tahadhari hiyo ilitolewa kupitia waraka ulioandikwa na Rais
wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas Nyaisonga.
Hata hivyo Wizara ya afya nchini humo bado haijathibitisha
taarifa za uwepo wa wagonjwa au vifo vinavyo sababishwa na wimbi jipya la virusi vya corona.
Mara ya mwisho kutolewa kwa taarifa za mwenendo wa maambukizi
ya virusi vya corona ilikua mwezi Aprili mwaka jana.
Ethiopia yapanga kufunga kambi za wakimbizi Tigray
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Ethiopia inapanga kufunga kambi mbili za wakimbizi zilizopio kaskazini mwa
jimbo la Tigray ambalo lilikumbwa na vita kati ya waliokuwa watawala (TPLF) na
serikali kuu, kwa mujibu wa shirika la wakimbizi nchini humo.
Akizungumza na wanahabari Jumanne, mkuu wa Shirika la
Wakimbizi na Wanaorejea nchini Ethiopia, Tesfaye Gobezay, amesema ukaribu na
mipaka ya Eritrea na hali mbaya ya kijiographia ndizo sababu zilizopeekea kufungwa kwa
kambi hizo.
Karibu wakimbizi 100,000 kutoka Eritrea walikuwa wanaishi
kambini huko Tigray kabla ya kuanza kwa mapigano mapema mwezi Novemba.
Kambi mbili - Shimbela na Hitsats – ambazo zilikuwa na
zaidi ya wakimbizi 20,000 hazijaweza kufikiwa kwa ajili ya kupewa misaada siku
za hivi karibuni.
Bwana Tesfaye aliongeza kuwa wakimbizi watapelekwa
katika kambi zingine au kurejeshwa wenye jamii.
Hivi karibuni, shirika la UN lilisema kwamba karibu
wakimbizi 20,000 wa Eritrea hawajulikani walipo.
Kulingana na Bwana Tesfaye kumekuwa na majaribio ya
awali ya kufunga kambi za Hitsats, lakini juhudi hizo zikashindikana kwasababu chama
cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kilipinga mpango huo na pia janga
la corona likachangia.
“Kulikuwa na mapigano haswa
katika kambi hizo” na wakimbizi “walijikuta katika njia panda”,Bwana Tesfaye alisema.
Hata hivyo uchunguzi
zaidi unahitajika kubaini taarifa za kina na ikiwa kuna waliopoteza maisha yao.
WHO yaonya kuhusu kusitishwa kwa chanjo ya corona Afrika Kusini
BBCCopyright: BBC
Afrika Kusini imerekodi maambukizi milioni 1.4 ya ugonjwa wa coronaImage caption: Afrika Kusini imerekodi maambukizi milioni 1.4 ya ugonjwa wa corona
Shirika la Afya Dunia (WHO) limeonya dhidi ya maamuzi
ya haraka kuhusu ufanisi wa chanjo ya kukabiliana na virusi vya corona.
Hii ni baada ya utafiti uliofanywa Afrika Kusini
kuonesha kuwa chanjo ya AstraZeneca haitakuwa na ufanisi mkubwa dhidi ya virusi
vipya vya corona vilivyokumba nchi hiyo.
Lakini wataalamu wana matumaini kuwa chanjo hiyo bado
itakuwa na ufanisi katika kuzuia maambukizi makali.
Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kuwa
data iliyotumiwa kwenye utafiti huo, ilikuwa ni "majaribio ya
watu kidogo tu" na walioshirikishwa walikuwa "vijana wenye afya
zao".
"Ni muhimu kubaini ikiwa chanjo hiyo ina ufanisi
au la katika kuzuia watu kuwa wagonjwa zaidi," amesema katika
taarifa.
Lakini pia ametambua kuwa watengenezaji wa chanjo
watahitajika kuiboresha ili kukabiliana na virusi hivyo.
"Ni wazi kwamba watengenezaji wa chanjo
watalazimika kuiimarisha zaidi ili kwendana na virusi vipya, hasa uzingatia
virusi vya sasa kwa ajili ya siku za baadaye.
"Tunajua virusi hubadilika na tunajua tunastahili
kuwa tayari kuboresha chanjo ili ziendelee kuwa na ufanisi,"
amesema.
Polepole: Magufuli hana mpango wa kuongeza muhula mwingine
Munira Hussein
BBC Africa
BBCCopyright: BBC
Katibu wa Itikadi
na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa kuteuliwa Humphrey
Polepole amesema kuwa Rais wa Tanzania John Magufuli hana mpango wa kuongeza
muda wa kukaa madarakani.
Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji kupitia chama cha ACT-Wazalendo bungeni leo aliibua suala hilo
akikosoa wabunge wawili wa CCM ambao walitoa hoja ya kutaka Rais Magufuli
kuongezewa muda na Polepole kujibu hoja zao.
Akitoa taarifa kwa
mbunge huyo wa ACT, Polepole amesema kuwa Rais hataongeza muda wowote.
“Masuala ya Chama
cha mapinduzi hujadiliwa kwenye vikao vya chama , hapa bungeni
wabunge wana uhuru wa kuzungumza lakini kinachozungumzwa humu ndani
hakiathiri msimamo wa Chama cha Mapinduzi ambao tumeshautoa, Rais hataongeza
muda,” ameeleza Polepole.
Mjadala wa kuongeza
muda wa rais madarakani umerejea tena hivi karibuni baada ya wabunge wawili wa
CCM kuchangia Bungeni.
Awali, katika muhula wake wa kwanza, Rais Magufuli
alipuuzia mapendekezo hayo kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge lililopita akiahidi
kutoongeza hata dakika moja muda wake wa kuondoka madarakani utakapofika.
Tanzania:Deni la Taifa laongezeka kwa asilimia 7.6
BUNGECopyright: BUNGE
Ongezeko la deni la Taifa nchini
Tanzania limefikia kiasi cha trilioni 59 hadi kufikia mwaka 2020 ambayo ni sawa
na ongezeko la asilimia 7.6 ikilinganishwa na shilingi trilioni 54.8 kwa kipindi kama hicho mwaka
2019, huku Bunge likitoa ushauri liwe himilivu.
Kati ya kiasi hicho deni la ndani
limefikia sh trilioni 16.2 na deni la nje sh. Trilioni 42.8.
Ongezeko la deni limetokana na
ukopaji kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. Gazeti la Nipashe nchini Tanzania limeripoti
Hayo yamebainishwa na Sillo Baran
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti alipokuwa akiwasilisha
taarifa kuhusu tathimini ya utekelezajiwa mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2017 mpaka 2020/2021.
Ingawa deni hilo ni himilivu kwa viashiria vyote muhimu serikali imeshauriwa ione haja ya kujipima uhimilivu wakekwa kutumia kiashiria cha makusanyo ya mapato ya ndani.
Kwa mujibu wa tathimini ya
uhilimivu wa deni imeonesha kuwa deni la serikali ni himilivukatika kipindi cha
muda mfupi , wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo unaokubalika kimataifa kwa
viashiria vyote muhimu.
Kamati ya Kudumu ya Bunge na
Bajeti imeishauri katika maoni ya jumla kutafuta njia ya kupunguza kukopa katika soko la fedha la ndani ili
kuziba nakisi ya bajeti kwa kupitia dhamana ya serikali na hati fungani.
Badala yake, serikali ijikite
zaidi katika kuongeza matumizi ya mikopo inayojidhamini ni yenyewe.
Bobi Wine awasilisha ushahidi zaidi mahakamani dhidi ya ushindi wa Rais Museveni
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Mawakili wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi , maarufu Bobi Wine wamewasilisha ushahidi zaidi katika mahakama ya juu zaidi nchini humo dhidi ya matokeo ya uchaguzi uliomrejesha tena madarakani Rais yoweri Museveni.
Jopo la majaji likiongozwa na Jaji mkuu Alfonce Owiny Doro, linasikiliza ombi hilo katika Mahakama ya juu zaidi hivi sasa.
Hii inakuja baada ya mawakili wa upande wa Bobi Wine kuiomba mahakama waongeze ushahidi zaidi kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika mwezi Januari.
Rais Museveni alipata ushindi wa asilimia
58.08 huku Robert Chagulanyi akipata asilimia zaidi ya 35, matokeo yanayopingwa vikali na Bw Wine.
Upande wa mawakili wa Rais Museveni umeshapokea nakala ya mashtaka
na siku ya Alhamisi wiki hii wanatarajia kufika katika mahakama ya juu kupanga siku
ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, katika kipindi cha siku 45 kulingana sheria ya
uchaguzi nchini humo.
Wataalamu DRC waanza kuwafuatilia waliokutana na mgonjwa wa Ebola
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Maafisa wa Afya nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameanza kuwafuatilia watu waliokuwa pamoja na mgonjwa aliyefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Mwanamke mwenye miaka 42 alifariki siku ya Jumatano juma lililopita jimbo la Kivu Kaskazini siku mbili tu baada ya kuonesha dalili za ugnjwa huo.
Timu ya wataalamu inafanya uchunguzi na mamlaka zimetangaza kuwa zoezi la kutokomeza vimelea vya ugonjwa kwenye maeneo ambayo mgonjwa alitembelea liko njiani kuanza.
Miezi mitatu iliyopita DRC ilitangazwa kuwa imefanikiwa kuutokomeza mlipuko wa 11 wa Ebola uliogharimu maisha ya watu 55.
Waziri wa Afya, Eteni Longodo, amesema madaktari wanachunguza kama maambukizi mapya yanatokana na mlipuko mpya wa ugonjwa huo.
Amezitaka jumuia zinazoishi katika maeneo ya waliothirika kuwa watulivu.
Ugonjwa wa 10 wa Ebola, ni mbaya zaidi kuikumba nchi hiyo, uliua zaidi ya watu 2,200 kati ya Agosti 2018 na Juni 2020.
ICC yaahirisha kesi dhidi ya viongozi wa waasi wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Kesi ya viongozi wa waasi wa Jamuhuri ya Afrika ya kati , iliyotarajiwa kuanza hii leo katika Mahakama ya Kimataifa (ICC) , imeahirishwa mpaka tarehe 16 mwezi Februari.
Alfred Yékatom na Patrice-Edouard Ngaïssona wanakabiliwa na makosa 21 na 32 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu
Uhalifu unaodaiwa ni pamoja na kuongoza shambulio dhidi ya raia kwa makusudi.
Watashtakiwa kwa pamoja kwani mashtaka yanahusiana na mashambulio hayo hayo.
Bw.Ngaïssona awali alikana mashtaka yote dhidi yake.
CAR ilitumbukia katika machafuko mwaka 2013 wakati waasi wengi wa Kiislamu kutoka kundi la Seleka walipochukua madaraka katika nchi yenye jamii kubwa ya Wakristo.
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Kisha kundi lenye wanamgambo wengi wa Kikristo, lililoitwa anti-Balaka liliibuka ili kukabiliana na Seleka baada ya Rais François Bozizé kuondolewa madarakani.
Maelfu walipoteza maisha katika mapigano na Umoja wa Mataifa (UN) ulisema zaidi ya watu milioni moja walilazimika kukimbia makazi yao.
Bwana Ngaïssona alikuwa mratibu wa kisiasa aliyejitangaza mwenyewe wa vikosi vya anti-Balaka.
Katika jukumu hilo, ICC imesema alifanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ikiwa ni pamoja na mauaji, kutesa na kuajiri watoto jeshini.
Kesi ya Bw Ngaïssona na Bw Yékatom itaanza wiki chache baada ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati kumkabidhi Mahamat Said Abdel Kani, kiongozi wa kikundi cha Seleka, kwa ICC kwa madai ya uhalifu uliofanywa katika mji mkuu, Bangui, mnamo 2013.
Zanzibar inavyoshamiri katika sekta ya utalii wakati dunia ikikabiliana na corona
Salim Kikeke
BBC Swahili presenter
Unapokuwa angani ukikarbia kutua kwenye uwanja wa ndege wa
kimataiifa wa Amani Abedi Karume Zanzibar, utaona jinsi eneo la kuegesha ndege
liliivyojaa. Na unapotua unagundua kuwa ni ndege za kukodi za watalii pamoja na
nyigine kadhaa za abiria.
Wanapowasili Zanzibar, watalii wanatakiwa kuvaa barakoa na
kutumia viitakasa mikono kabla ya kuanza kujaza fomu za kungia visiwani humo. Je ni ipi siri ya mafanikio ya utalii Zanzibar. Ungana nami nikusimulie katika video ifuatayo
Video content
Video caption: Soko jipya la utalii Zanzibar laibuka baada ya marufuku ya kutoka njeSoko jipya la utalii Zanzibar laibuka baada ya marufuku ya kutoka nje
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ‘kujadili mgogoro wa Somalia
Getty ImagesCopyright: Getty Images
muhula wa Rais Mohamed Abdullahi Farmajo ulimalizika JumatatuImage caption: muhula wa Rais Mohamed Abdullahi Farmajo ulimalizika Jumatatu
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa litakutana siku ya Jumanne
kujadili changamoto za kisiasa nchini Somalia, Shirika la habari la Ufaransa,
AFP limeripoti likinukuu vyanzo vya kidiplomasia.
Upinzani nchini Somalia umeapa kutomtambua Rais Mohamed
Abdullahi Farmajo, ambaye muhula wake ulimalizika siku ya Jumatatu.
Bado haijajulikana uchaguzi utafanyika
lini.
Mazungumzo kati ya serikali na majimbo
kuhusu namna gani ya kufanya uchaguzi yalivunjika tarehe 5 mwezi Februari.
Kuepuka ombwe la madaraka, bunge
lilipitisha azimio mwaka jana kumruhusu rais na bunge kuendelea na nafasi zao
mpaka warithi watakapochaguliwa.
Umoja wa Mataifa umetaka viongozi wa nchi
hiyo wafanye mazungumzo.
Nchi hiyo tayari ilikuwa kufanya uchaguzi wa bunge mwezi
Desemba 2020 kwa sababu ya mizozo inayoendelea kati ya serikali na tawala
zingine za mikoa.
Waziri Mkuu wa Sudan ateua viongozi wa waasi kwenye serikali
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla
Hamdok amelitaja baraza jipya la mawaziri ambalo linahusisha viongozi wa zamani
wa waasi ambao walikuwa sehemu ya mkataba wa Amani uliosainiwa mwezi Oktoba.
Bw.Hamdok alivunja baraza
lililopita siku ya Jumapili kwa ajili ya kuunda serikali ya umoja.
Mawaziri wawili walichaguliwa kutoka kwenye jeshi. Wengi kutoka kwenye vikosi vya Uhuru na mabadiliko vilivyoongoza maandamano
yaliyomuondoa Omar al-Bashir madarakani.
Waziri Mkuu amemteua kiongozi wa zamani wa waasi na mwanauchumi Gibril
Ibrahim kuwa Waziri wa fedha.
Hatua hii imekuja wakati ambapo kuna upungufu wa
chakula na mafutakupanda na mfumuko wa bei.
Kuwa waziri wa mambo ya nje wa Sudan katika eneo lenye hali tete pia
itakuwa mtihani mkubwa. Kazi hiyo ilikwenda kwa Mariam al-Sadiqal-Mahdi- binti
wa waziri mkuu wa mwisho wa aliyechaguliwa kidemokrasia, Sadiqal-Mahdi.
Bado kuna wanajeshi katika baraza la mawaziri la Bwana Hamdok - ukumbusho wa
ndoa ngumu kati ya wanajeshi na raia wakati Sudan inaendelea na kipindi cha
mpito kuelekea demokrasia.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumanne tarehe 09.02.2021
Habari za moja kwa moja
Na Lizzy Masinga, Dinah Gahamanyi na Asha Juma
time_stated_uk
Na hadi kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa hii leo. Kwaheri.
Mkuu mpya wa jeshi nchini Msumbiji afariki dunia kwa corona
Mkuu wa jeshi nchini Msumbiji aliyeteuliwa hivi karibuni, Eugénio Ussene Mussa, amefariki dunia Jumatatu baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Aliaga dunia wakati anapata matibabu katika moja ya hospitali kubwa nchini Msumbiji, kwa jina Maputo Central Hospital.
Ni chini ya mwezi mmoja tangu alipoapishwa kama Mkuu wa jeshi Januari 20 na kuchukua usukani.
Kabla ya kushika hatamu alikuwa anahusika na oparesheni za kubabiliana na wanamgambo wa Kiislamu katika eneo lenye utajiri mkubwa wa gesi mkoa wa Cabo Delgado.
Mwezi uliopita, aliwaambia wanajeshi waliokuwa wamekusanyika kwamba 2021 utakuwa mwaka muhimu katika kukabiliana na ugaidi.
Mjumbe wa kibinafsi wa Umoja wa Mataifa nchini Msumbiji, Mirko Manzoni, ametuma risala za rambirambi kwa Rais Filipe Nyusi na watu wa msumbiji.
Virusi vya Corona: Chuo Kikuu Huria Tanzania chatahadharisha wanafunzi, wafanyakazi
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimetoa tahadhari kwa wanafunzi na wafanyakazi wake juu ya hatari ya maambukizi ya virusi vya corona na kuwataka kuchukua hatua zote za kujilinda.
Tahadhari hiyo imetolewa kupitia waraka wa Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Elifas Tozo Bisanda wa jana Februari 8, 2020. Waraka amabao hii leo umekuwa ukisambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Tanzania.
Awali BBC ilizungumza na Profesa Tozo ambaye amesisitiza kuwa: "taarifa hii ni ya ndani kwa wafanyakazi pamoja na wanafunzi...wengine haiwahusu."
Waraka huo unawataka wanafunzi na wafanyakazi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kuwa tishio la maambukizi "linashamiri".
"Kwa upande wa wanafunzi tunasisitiza wakae nyumbani na kusoma kwa njia ya mtandao, hatutaruhusu wanafunzi na wageni kuingia kwenye kampasi zetu bila sababu maalumu’’ inasema taarifa hiyo.
Kwa upande wa wafanyakazi wao wataendesha mikutano yao kwa njia ya mtandao.
Aidha taarifa hiyo pia imesisitiza umuhimu wa kujifukiza na kutumia dawa asili, lakini pia kujilinda kwa kuvaa barakoa na kuepuka misongamano.
"Inakua ngumu sana kuepuka maambukizi kama hatuzingatii masharti ya kujikinga. Hata hivyo imethibitishwa kuwa taratibu za kujifukiza (Nyungu) zinaleta ahueni lakini haimaiinishi kwamba virusi vile vitakufa’’ inasema taarifa hiyo.
Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) halijathibitisha dawa yeyote ya mitishamba kutibu virusi vya corona na pia imetahadharisha juu ya kujifukiza.
Mwezi uliopita Kanisa Katoliki nchini Tanzania lilitoa tahadhari juu ya wimbi jipya la maambukizi ya corona na kuwataka wananchi kuchukua hatua zote za kujikinga.
Tahadhari hiyo ilitolewa kupitia waraka ulioandikwa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas Nyaisonga.
Hata hivyo Wizara ya afya nchini humo bado haijathibitisha taarifa za uwepo wa wagonjwa au vifo vinavyo sababishwa na wimbi jipya la virusi vya corona.
Mara ya mwisho kutolewa kwa taarifa za mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona ilikua mwezi Aprili mwaka jana.
Ethiopia yapanga kufunga kambi za wakimbizi Tigray
Ethiopia inapanga kufunga kambi mbili za wakimbizi zilizopio kaskazini mwa jimbo la Tigray ambalo lilikumbwa na vita kati ya waliokuwa watawala (TPLF) na serikali kuu, kwa mujibu wa shirika la wakimbizi nchini humo.
Akizungumza na wanahabari Jumanne, mkuu wa Shirika la Wakimbizi na Wanaorejea nchini Ethiopia, Tesfaye Gobezay, amesema ukaribu na mipaka ya Eritrea na hali mbaya ya kijiographia ndizo sababu zilizopeekea kufungwa kwa kambi hizo.
Karibu wakimbizi 100,000 kutoka Eritrea walikuwa wanaishi kambini huko Tigray kabla ya kuanza kwa mapigano mapema mwezi Novemba.
Kambi mbili - Shimbela na Hitsats – ambazo zilikuwa na zaidi ya wakimbizi 20,000 hazijaweza kufikiwa kwa ajili ya kupewa misaada siku za hivi karibuni.
Bwana Tesfaye aliongeza kuwa wakimbizi watapelekwa katika kambi zingine au kurejeshwa wenye jamii.
Hivi karibuni, shirika la UN lilisema kwamba karibu wakimbizi 20,000 wa Eritrea hawajulikani walipo.
Kulingana na Bwana Tesfaye kumekuwa na majaribio ya awali ya kufunga kambi za Hitsats, lakini juhudi hizo zikashindikana kwasababu chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kilipinga mpango huo na pia janga la corona likachangia.
“Kulikuwa na mapigano haswa katika kambi hizo” na wakimbizi “walijikuta katika njia panda”,Bwana Tesfaye alisema.
Hata hivyo uchunguzi zaidi unahitajika kubaini taarifa za kina na ikiwa kuna waliopoteza maisha yao.
WHO yaonya kuhusu kusitishwa kwa chanjo ya corona Afrika Kusini
Shirika la Afya Dunia (WHO) limeonya dhidi ya maamuzi ya haraka kuhusu ufanisi wa chanjo ya kukabiliana na virusi vya corona.
Hii ni baada ya utafiti uliofanywa Afrika Kusini kuonesha kuwa chanjo ya AstraZeneca haitakuwa na ufanisi mkubwa dhidi ya virusi vipya vya corona vilivyokumba nchi hiyo.
Lakini wataalamu wana matumaini kuwa chanjo hiyo bado itakuwa na ufanisi katika kuzuia maambukizi makali.
Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kuwa data iliyotumiwa kwenye utafiti huo, ilikuwa ni "majaribio ya watu kidogo tu" na walioshirikishwa walikuwa "vijana wenye afya zao".
"Ni muhimu kubaini ikiwa chanjo hiyo ina ufanisi au la katika kuzuia watu kuwa wagonjwa zaidi," amesema katika taarifa.
Lakini pia ametambua kuwa watengenezaji wa chanjo watahitajika kuiboresha ili kukabiliana na virusi hivyo.
"Ni wazi kwamba watengenezaji wa chanjo watalazimika kuiimarisha zaidi ili kwendana na virusi vipya, hasa uzingatia virusi vya sasa kwa ajili ya siku za baadaye.
"Tunajua virusi hubadilika na tunajua tunastahili kuwa tayari kuboresha chanjo ili ziendelee kuwa na ufanisi," amesema.
Polepole: Magufuli hana mpango wa kuongeza muhula mwingine
Munira Hussein
BBC Africa
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole amesema kuwa Rais wa Tanzania John Magufuli hana mpango wa kuongeza muda wa kukaa madarakani.
Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji kupitia chama cha ACT-Wazalendo bungeni leo aliibua suala hilo akikosoa wabunge wawili wa CCM ambao walitoa hoja ya kutaka Rais Magufuli kuongezewa muda na Polepole kujibu hoja zao.
Akitoa taarifa kwa mbunge huyo wa ACT, Polepole amesema kuwa Rais hataongeza muda wowote.
“Masuala ya Chama cha mapinduzi hujadiliwa kwenye vikao vya chama , hapa bungeni wabunge wana uhuru wa kuzungumza lakini kinachozungumzwa humu ndani hakiathiri msimamo wa Chama cha Mapinduzi ambao tumeshautoa, Rais hataongeza muda,” ameeleza Polepole.
Mjadala wa kuongeza muda wa rais madarakani umerejea tena hivi karibuni baada ya wabunge wawili wa CCM kuchangia Bungeni.
Awali, katika muhula wake wa kwanza, Rais Magufuli alipuuzia mapendekezo hayo kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge lililopita akiahidi kutoongeza hata dakika moja muda wake wa kuondoka madarakani utakapofika.
Tanzania:Deni la Taifa laongezeka kwa asilimia 7.6
Ongezeko la deni la Taifa nchini Tanzania limefikia kiasi cha trilioni 59 hadi kufikia mwaka 2020 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 7.6 ikilinganishwa na shilingi trilioni 54.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2019, huku Bunge likitoa ushauri liwe himilivu.
Kati ya kiasi hicho deni la ndani limefikia sh trilioni 16.2 na deni la nje sh. Trilioni 42.8.
Ongezeko la deni limetokana na ukopaji kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. Gazeti la Nipashe nchini Tanzania limeripoti
Hayo yamebainishwa na Sillo Baran Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti alipokuwa akiwasilisha taarifa kuhusu tathimini ya utekelezajiwa mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2017 mpaka 2020/2021.
Ingawa deni hilo ni himilivu kwa viashiria vyote muhimu serikali imeshauriwa ione haja ya kujipima uhimilivu wakekwa kutumia kiashiria cha makusanyo ya mapato ya ndani.
Kwa mujibu wa tathimini ya uhilimivu wa deni imeonesha kuwa deni la serikali ni himilivukatika kipindi cha muda mfupi , wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo unaokubalika kimataifa kwa viashiria vyote muhimu.
Kamati ya Kudumu ya Bunge na Bajeti imeishauri katika maoni ya jumla kutafuta njia ya kupunguza kukopa katika soko la fedha la ndani ili kuziba nakisi ya bajeti kwa kupitia dhamana ya serikali na hati fungani.
Badala yake, serikali ijikite zaidi katika kuongeza matumizi ya mikopo inayojidhamini ni yenyewe.
Bobi Wine awasilisha ushahidi zaidi mahakamani dhidi ya ushindi wa Rais Museveni
Mawakili wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi , maarufu Bobi Wine wamewasilisha ushahidi zaidi katika mahakama ya juu zaidi nchini humo dhidi ya matokeo ya uchaguzi uliomrejesha tena madarakani Rais yoweri Museveni.
Jopo la majaji likiongozwa na Jaji mkuu Alfonce Owiny Doro, linasikiliza ombi hilo katika Mahakama ya juu zaidi hivi sasa.
Hii inakuja baada ya mawakili wa upande wa Bobi Wine kuiomba mahakama waongeze ushahidi zaidi kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika mwezi Januari.
Rais Museveni alipata ushindi wa asilimia 58.08 huku Robert Chagulanyi akipata asilimia zaidi ya 35, matokeo yanayopingwa vikali na Bw Wine.
Upande wa mawakili wa Rais Museveni umeshapokea nakala ya mashtaka na siku ya Alhamisi wiki hii wanatarajia kufika katika mahakama ya juu kupanga siku ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, katika kipindi cha siku 45 kulingana sheria ya uchaguzi nchini humo.
Wataalamu DRC waanza kuwafuatilia waliokutana na mgonjwa wa Ebola
Maafisa wa Afya nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameanza kuwafuatilia watu waliokuwa pamoja na mgonjwa aliyefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Mwanamke mwenye miaka 42 alifariki siku ya Jumatano juma lililopita jimbo la Kivu Kaskazini siku mbili tu baada ya kuonesha dalili za ugnjwa huo.
Timu ya wataalamu inafanya uchunguzi na mamlaka zimetangaza kuwa zoezi la kutokomeza vimelea vya ugonjwa kwenye maeneo ambayo mgonjwa alitembelea liko njiani kuanza.
Miezi mitatu iliyopita DRC ilitangazwa kuwa imefanikiwa kuutokomeza mlipuko wa 11 wa Ebola uliogharimu maisha ya watu 55.
Waziri wa Afya, Eteni Longodo, amesema madaktari wanachunguza kama maambukizi mapya yanatokana na mlipuko mpya wa ugonjwa huo.
Amezitaka jumuia zinazoishi katika maeneo ya waliothirika kuwa watulivu.
Ugonjwa wa 10 wa Ebola, ni mbaya zaidi kuikumba nchi hiyo, uliua zaidi ya watu 2,200 kati ya Agosti 2018 na Juni 2020.
ICC yaahirisha kesi dhidi ya viongozi wa waasi wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati
Kesi ya viongozi wa waasi wa Jamuhuri ya Afrika ya kati , iliyotarajiwa kuanza hii leo katika Mahakama ya Kimataifa (ICC) , imeahirishwa mpaka tarehe 16 mwezi Februari.
Alfred Yékatom na Patrice-Edouard Ngaïssona wanakabiliwa na makosa 21 na 32 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu Uhalifu unaodaiwa ni pamoja na kuongoza shambulio dhidi ya raia kwa makusudi.
Watashtakiwa kwa pamoja kwani mashtaka yanahusiana na mashambulio hayo hayo. Bw.Ngaïssona awali alikana mashtaka yote dhidi yake.
CAR ilitumbukia katika machafuko mwaka 2013 wakati waasi wengi wa Kiislamu kutoka kundi la Seleka walipochukua madaraka katika nchi yenye jamii kubwa ya Wakristo.
Kisha kundi lenye wanamgambo wengi wa Kikristo, lililoitwa anti-Balaka liliibuka ili kukabiliana na Seleka baada ya Rais François Bozizé kuondolewa madarakani.
Maelfu walipoteza maisha katika mapigano na Umoja wa Mataifa (UN) ulisema zaidi ya watu milioni moja walilazimika kukimbia makazi yao.
Bwana Ngaïssona alikuwa mratibu wa kisiasa aliyejitangaza mwenyewe wa vikosi vya anti-Balaka.
Katika jukumu hilo, ICC imesema alifanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ikiwa ni pamoja na mauaji, kutesa na kuajiri watoto jeshini.
Kesi ya Bw Ngaïssona na Bw Yékatom itaanza wiki chache baada ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati kumkabidhi Mahamat Said Abdel Kani, kiongozi wa kikundi cha Seleka, kwa ICC kwa madai ya uhalifu uliofanywa katika mji mkuu, Bangui, mnamo 2013.
Zanzibar inavyoshamiri katika sekta ya utalii wakati dunia ikikabiliana na corona
Salim Kikeke
BBC Swahili presenter
Unapokuwa angani ukikarbia kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataiifa wa Amani Abedi Karume Zanzibar, utaona jinsi eneo la kuegesha ndege liliivyojaa. Na unapotua unagundua kuwa ni ndege za kukodi za watalii pamoja na nyigine kadhaa za abiria.
Wanapowasili Zanzibar, watalii wanatakiwa kuvaa barakoa na kutumia viitakasa mikono kabla ya kuanza kujaza fomu za kungia visiwani humo. Je ni ipi siri ya mafanikio ya utalii Zanzibar. Ungana nami nikusimulie katika video ifuatayo
Video content
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ‘kujadili mgogoro wa Somalia
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa litakutana siku ya Jumanne kujadili changamoto za kisiasa nchini Somalia, Shirika la habari la Ufaransa, AFP limeripoti likinukuu vyanzo vya kidiplomasia.
Upinzani nchini Somalia umeapa kutomtambua Rais Mohamed Abdullahi Farmajo, ambaye muhula wake ulimalizika siku ya Jumatatu.
Bado haijajulikana uchaguzi utafanyika lini.
Mazungumzo kati ya serikali na majimbo kuhusu namna gani ya kufanya uchaguzi yalivunjika tarehe 5 mwezi Februari.
Kuepuka ombwe la madaraka, bunge lilipitisha azimio mwaka jana kumruhusu rais na bunge kuendelea na nafasi zao mpaka warithi watakapochaguliwa.
Umoja wa Mataifa umetaka viongozi wa nchi hiyo wafanye mazungumzo.
Nchi hiyo tayari ilikuwa kufanya uchaguzi wa bunge mwezi Desemba 2020 kwa sababu ya mizozo inayoendelea kati ya serikali na tawala zingine za mikoa.
Waziri Mkuu wa Sudan ateua viongozi wa waasi kwenye serikali
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amelitaja baraza jipya la mawaziri ambalo linahusisha viongozi wa zamani wa waasi ambao walikuwa sehemu ya mkataba wa Amani uliosainiwa mwezi Oktoba.
Bw.Hamdok alivunja baraza lililopita siku ya Jumapili kwa ajili ya kuunda serikali ya umoja.
Mawaziri wawili walichaguliwa kutoka kwenye jeshi. Wengi kutoka kwenye vikosi vya Uhuru na mabadiliko vilivyoongoza maandamano yaliyomuondoa Omar al-Bashir madarakani.
Waziri Mkuu amemteua kiongozi wa zamani wa waasi na mwanauchumi Gibril Ibrahim kuwa Waziri wa fedha.
Hatua hii imekuja wakati ambapo kuna upungufu wa chakula na mafutakupanda na mfumuko wa bei.
Kuwa waziri wa mambo ya nje wa Sudan katika eneo lenye hali tete pia itakuwa mtihani mkubwa. Kazi hiyo ilikwenda kwa Mariam al-Sadiqal-Mahdi- binti wa waziri mkuu wa mwisho wa aliyechaguliwa kidemokrasia, Sadiqal-Mahdi.
Bado kuna wanajeshi katika baraza la mawaziri la Bwana Hamdok - ukumbusho wa ndoa ngumu kati ya wanajeshi na raia wakati Sudan inaendelea na kipindi cha mpito kuelekea demokrasia.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumanne tarehe 09.02.2021