Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wetu wa BBC Swahili, Shukrani na karibu tena hapo kesho.
Jimbo la Nigeria lapanga kuwapa silaha walinzi
EPACopyright: EPA
Maafisa wa Jimbo la Niger wanasema lengo ni kuimarisha usalama wa eneo hiloImage caption: Maafisa wa Jimbo la Niger wanasema lengo ni kuimarisha usalama wa eneo hilo
Maafisa katika Jimbo la Niger nchini Nigeria, wametangaza kwamba watayahami kwa bunduki makundi ya ulinzi.
Hatua hiyo wanasema inalenga kuimarisha usalama katika jimbo hilo ambalo mashambulio kutoka majambazi waliojihami kwa bunduki aina ya AK-47 yameongezeka
Hakuna uwepo wa polisi katika sehemu kubwa ya jimbo hilo, kwa hivyo makundi ya ulinzi yanatarajia kujaza pengo hilo, lakini kuna hofu hatua hiyo huenda ikachangia ongezeko la ghasia.
"Mahasimu wao wanatumia bunduki aina ya AK-47, GMPGS na hivi karibuni RPG alafu sisi tunatuma watu walio na bunduki zilizo na uwezo mara mbili kwenda kukabiliana nao...silaha hizo haziendani na huenda zikafanya hali ya usalama kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyo sasa," Nnamdi Obasi,mshauri mkuu wa shirika la kimataifa la kushughulikia mizozo aliiambia BBC.
Alitaja "ukosefu wa ushirikiano kati ya serikali kuu na serikali ya majimbo katika juhudi za kuimarisha usalama", hali ambayo imefanya mamlaka hizo kushughulikia masuala ya usalama "kwani serikali kuu haijawajiibika."
Uwanja maarufu wa Maracana Brazil kupewa jina la Pele
BBC SportCopyright: BBC Sport
Uwanja maarufu wa Maracana nchini Brazil unatarajiwa kubadilishwa jina kwa heshima ya mchezaji nguli wa soka, Pele.
Hii ni baada ya wabunge wa Jimbo la Rio de Janeiro, kupiga kura ya uwanja huo kubadilishwa jina kuwa Uwanja wa Edson Arantes do Nascimento - Rei Pele.
Edson Arantes do Nascimento ni jina halisi la mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 80, na jina Rei linamaanisha mfalme kwa Kireno.
Gavana wa Jimbo la Rio de Janeiro lazima aidhinishe hatua hiyo kabla ya jina la uwanja huo kubadilishwa rasmi.
Pele, ambaye aliongoza Brazil kushinda Kombe la Dunia mara tatu, alifunga bao lake la 1,000 katika uwanja huo mwaka 1969 wakati wa mchuano kati ya timu yake ya Santos na Vasco da Gama.
Uwanja wa Maracana uliandaa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1950 na 2014, na hali kadhalika sherehe ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki mwaka 2016.
Zaidi ya mashabiki 200,000 waliripotiwa kufiks katika uwanja huo kutazama fainali ya mwaka 1950, ambapo Uruguay ilishinda Brazil, japo uwanja huo sasa una uweza kuwahimili watu 78,838.
Uwanja huo ulipewa
jina Mario Filho, mwandishi wa hambari
aliyeshinikiza ujenzi wake miaka ya 1940,
lakini unajulikana kama Maracana jina la eneo ulipojengwa.
China na Urusi kujenga kituo cha anga za mbali mwezini
EPACopyright: EPA
Shirika la anga za mbali la Urusi Roscosmos limesema kuwa limesaini makubaliano na kituo cha taifa la China cha utawala wa anga za mbali ili kutengeneza vifaa vitakavyosaidia kufanya utafiti wa sakafu ya mwezi, kwenye uzio (orbit) au eneo lote la mwezi.
Balozi wa Marekani nchini Ethiopia kuzuru jimbo la Tigray
BBCCopyright: BBC
Balozi wa Marekani nchini Ethiopia anatarajiwa kuzuru kaskazini mwa jimbo la Tigray ambako oparesheni ya kijeshi iliyoongozwa na serikali dhidi ya vikosi vya People's Liberation Front (TPLF), ilisababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu ya wengine kukimbia makwao.
Ziara hiyo inakuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, wiki iliyopita kutoa wito kwa Ethiopia kuruhusu uchunguzi wa kimataifa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu uliotekelezwa katika eneo hilo.
Haijafahamika Balozi Geeta Pasi,ataruhusiwa kufika sehemu gani ya Tigray, lakini ubalozi umesema katika Twitter yake kwamba, Marekani "imejitolea kutoa msaada wa kuokoa maisha ya watu walio hatarini nchini Ethiopia".
Jimbo la Tigray lilitumbukia kwenye mgogoro Novemba 4, mwaka 2020 wakati serikali ilipoanzisha oparesheni ya kijeshi ya kuondoa madarakani chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) baada ya wapiganaji wake kuvamia kambi ya majeshi wa muungano katika jimbo la Tigray.
Madai ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu yameibuka, huku kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akitoa wito kwa Ethiopia kuruhusu wataalam huru katika eneo hilo.
Waokoaji wameopoa miili 12 ya watoto
waliozama katika ufukwe maarufu kusini mwa Ghana.
Watoto hao walio na umri kati ya miaka 14 na 17 walikua wameenda kuogelea siku ya Jumapili mjini Apam.
Wazazi wa watoto hao na wakazi wamekusanyika katika ufukwe huo kusubiri taarifa
kuhusu wale ambao bado hawajapatikana.
"Nilimtafuta JumapiIi jioni lakini
sikumpata, Usiku huo sikupata lepe la usingizi niliposikia kuna watoto
waliokufa maji na miili yao imeopolewa. Nilienda
eneo hilo nikapata alikua mmoja wao," mzazi mmoja aliniambia.
Baadhi ya miili iliopolewa majini siku ya
Jumatatu na Jumanne, mmoja wa maafisa
aliambia BBC.
Fukwe za Ghana zimefungwa kuzuia kuenea kwa
virusi vya corona lakini watoto wanadaiwa kutumia njia za mkato kuepuka wasizuiwe
kwenda kuogelea.
Afisa mwingine kutoka mamlaka ya utalii nchini Ghana amesema ni vigumu
kudhibiti watu kuogelea kwenye fukwe za nchi hiyo.
Unyanyasaji dhidi ya wanawake waongezeka Afrika
AFPCopyright: AFP
Ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imefichua kwamba thuluthi tatu ya wanawake hukumbana na unyanyasaji wa kijinsia na kingono wakati mmoja maishani mwao.
Ripoti hiyo ni moja ya utafiti mkubwa zaidi kufanywa kuhusu unyanyasaji dhidi ya wanawake na inajumuisha data kati ya mwaka 2000-2018.
WHO linasema janga la corona limechangia kuongezeka kwa visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake. Linaripoti visa vya wanawake kushambuliwa na wenzi wao kuongezeka zaidi.
Hali hiyo inawaathiri zaidi ya wanawake milioni 640 kote duniani.
Asia Kusini, Kusini mwa Jangwa la Sahara, na Oceania zina viwango vya juu vya unyanyasaji wa wenzi.
Robo ya wanawake walio na umri kati ya miaka 15 -24 tayari wamekabiliwa unyanyasaji kutoka kwa wenzi wao.
Watu 35 wafariki baada ya kula 'mimea ya porini' Msumbiji
BBCCopyright: BBC
Watu 25 wa familia moja ni miongoni mwa watu 35 waliofariki kaskazini mwa Msumbiji baada ya kuripotiwa kula mimea na matunda ya mwituni, mamlaka zinasema.
Maafisa wanasema hivi karibuni kumeripotiwa visa vya watu katika eneo hilo kula matunda ya mwituni, mizizi na hata nyasi.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na televisheni ya kitaifa , TVM, wakazi wamekua wakisaga nyasi kupika xima – uji wa kienyweji wa Msumbiji, ambao hutengenezwa kutokana na unga wa mahindi.
Uhaba wa chakula katika mkoa wa Nampula umechangiwa na ukosefu wa mvua.
Waridi wa BBC: 'Nilimchukia mtoto alipozaliwa bila kujua sababu'
SUZZY KAHEMACopyright: SUZZY KAHEMA
Suzzy Kahema aliishi maisha ya kawaida yenye matumaini tele akiwa mdogo, lakini katika ujana wake alipitia matukio ambayo karibu yasambaratishe maisha yake....Maelezo zaidi
Utafiti wa Umoja wa Mataifa waonesha watu 131,000 wamefurushwa Tigray
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linasema kwamba watu zaidi
ya 131,000 walitoroka makazi yao katika maeneo
39 ya jimbo la Tigray nchini Ethiopia na kukimbilia majimbo jirani ya Afar
na Amhara, kwa mujibu wa utafiti.
IOM limebaini watu katika
nyumba 30,383 wametoroka makwao.
Baadhi ya waliohamishwa, ni pamoja na wanawake na watoto, ambao wanahitaji kwa dharura makai, chakula na maji safi na salama ya kunywa.
Kulingana na IOM, "data hii sio viashiria vya jumla ya idadi ya watu waliotoroka kutokana na vita lakini inawakilisha tu idadi ya wakimbizi wa ndani waliorodheshwa katika tovuti zilizounganishwa na mfumo wa DTM."
Burundi yapiga marufuku uagizaji wa mahindi kwa miezi sita
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Wizara ya biashara ya Burundi imepiga marufuku uagizaji mahindi
kutoka nje kwa miezi sita kuanzia tarehe 8 Machi.
Katika taarifa wizara
hiyo imesema mahindi yaliyoingizwa nchini humo hivi karibuni ''hayakua mazuri'' na huenda yakadhuru afya ya watu.
Haikubainisha
mahindi hayo yaliagizwa kutoka nchi gani.
''Wakati nafaka hii na unga inakataliwa na nchi jirani… tunahitaji
kuhakikisha hayaingizwi nchini'', alisema Jeremie Banigwaninzigo, katibu wa
kudumu wa wizara ya biashara na utalii wa Burundi.
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Hatua hii inakuja baada ya Kenya kupiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka Uganda na Tanzania kutokana na hofu ya usalama ya nafaka hiyo.
Uagizaji mwingi wa mahindi wa Burundi unatoka Uganda na Zambia - lakini haijulikani ni kwa kiwango gani nchi hiyo inategemea uagizaji ili kukidhi mahitaji yake.
Habari za moja kwa moja
Na Ambia Hirsi
time_stated_uk
Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wetu wa BBC Swahili, Shukrani na karibu tena hapo kesho.
Jimbo la Nigeria lapanga kuwapa silaha walinzi
Maafisa katika Jimbo la Niger nchini Nigeria, wametangaza kwamba watayahami kwa bunduki makundi ya ulinzi.
Hatua hiyo wanasema inalenga kuimarisha usalama katika jimbo hilo ambalo mashambulio kutoka majambazi waliojihami kwa bunduki aina ya AK-47 yameongezeka
Hakuna uwepo wa polisi katika sehemu kubwa ya jimbo hilo, kwa hivyo makundi ya ulinzi yanatarajia kujaza pengo hilo, lakini kuna hofu hatua hiyo huenda ikachangia ongezeko la ghasia.
"Mahasimu wao wanatumia bunduki aina ya AK-47, GMPGS na hivi karibuni RPG alafu sisi tunatuma watu walio na bunduki zilizo na uwezo mara mbili kwenda kukabiliana nao...silaha hizo haziendani na huenda zikafanya hali ya usalama kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyo sasa," Nnamdi Obasi,mshauri mkuu wa shirika la kimataifa la kushughulikia mizozo aliiambia BBC.
Alitaja "ukosefu wa ushirikiano kati ya serikali kuu na serikali ya majimbo katika juhudi za kuimarisha usalama", hali ambayo imefanya mamlaka hizo kushughulikia masuala ya usalama "kwani serikali kuu haijawajiibika."
Uwanja maarufu wa Maracana Brazil kupewa jina la Pele
Uwanja maarufu wa Maracana nchini Brazil unatarajiwa kubadilishwa jina kwa heshima ya mchezaji nguli wa soka, Pele.
Hii ni baada ya wabunge wa Jimbo la Rio de Janeiro, kupiga kura ya uwanja huo kubadilishwa jina kuwa Uwanja wa Edson Arantes do Nascimento - Rei Pele.
Edson Arantes do Nascimento ni jina halisi la mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 80, na jina Rei linamaanisha mfalme kwa Kireno.
Gavana wa Jimbo la Rio de Janeiro lazima aidhinishe hatua hiyo kabla ya jina la uwanja huo kubadilishwa rasmi.
Pele, ambaye aliongoza Brazil kushinda Kombe la Dunia mara tatu, alifunga bao lake la 1,000 katika uwanja huo mwaka 1969 wakati wa mchuano kati ya timu yake ya Santos na Vasco da Gama.
Uwanja wa Maracana uliandaa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1950 na 2014, na hali kadhalika sherehe ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki mwaka 2016.
Zaidi ya mashabiki 200,000 waliripotiwa kufiks katika uwanja huo kutazama fainali ya mwaka 1950, ambapo Uruguay ilishinda Brazil, japo uwanja huo sasa una uweza kuwahimili watu 78,838.
Uwanja huo ulipewa jina Mario Filho, mwandishi wa hambari aliyeshinikiza ujenzi wake miaka ya 1940, lakini unajulikana kama Maracana jina la eneo ulipojengwa.
China na Urusi kujenga kituo cha anga za mbali mwezini
Shirika la anga za mbali la Urusi Roscosmos limesema kuwa limesaini makubaliano na kituo cha taifa la China cha utawala wa anga za mbali ili kutengeneza vifaa vitakavyosaidia kufanya utafiti wa sakafu ya mwezi, kwenye uzio (orbit) au eneo lote la mwezi.
Maelezo zaidi
Balozi wa Marekani nchini Ethiopia kuzuru jimbo la Tigray
Balozi wa Marekani nchini Ethiopia anatarajiwa kuzuru kaskazini mwa jimbo la Tigray ambako oparesheni ya kijeshi iliyoongozwa na serikali dhidi ya vikosi vya People's Liberation Front (TPLF), ilisababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu ya wengine kukimbia makwao.
Ziara hiyo inakuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, wiki iliyopita kutoa wito kwa Ethiopia kuruhusu uchunguzi wa kimataifa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu uliotekelezwa katika eneo hilo.
Haijafahamika Balozi Geeta Pasi,ataruhusiwa kufika sehemu gani ya Tigray, lakini ubalozi umesema katika Twitter yake kwamba, Marekani "imejitolea kutoa msaada wa kuokoa maisha ya watu walio hatarini nchini Ethiopia".
Jimbo la Tigray lilitumbukia kwenye mgogoro Novemba 4, mwaka 2020 wakati serikali ilipoanzisha oparesheni ya kijeshi ya kuondoa madarakani chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) baada ya wapiganaji wake kuvamia kambi ya majeshi wa muungano katika jimbo la Tigray.
Madai ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu yameibuka, huku kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akitoa wito kwa Ethiopia kuruhusu wataalam huru katika eneo hilo.
Soma zaidi:
Waghana waomboleza vijana waliokufa maji
Waokoaji wameopoa miili 12 ya watoto waliozama katika ufukwe maarufu kusini mwa Ghana.
Watoto hao walio na umri kati ya miaka 14 na 17 walikua wameenda kuogelea siku ya Jumapili mjini Apam.
Wazazi wa watoto hao na wakazi wamekusanyika katika ufukwe huo kusubiri taarifa kuhusu wale ambao bado hawajapatikana.
"Nilimtafuta JumapiIi jioni lakini sikumpata, Usiku huo sikupata lepe la usingizi niliposikia kuna watoto waliokufa maji na miili yao imeopolewa. Nilienda eneo hilo nikapata alikua mmoja wao," mzazi mmoja aliniambia.
Baadhi ya miili iliopolewa majini siku ya Jumatatu na Jumanne, mmoja wa maafisa aliambia BBC.
Fukwe za Ghana zimefungwa kuzuia kuenea kwa virusi vya corona lakini watoto wanadaiwa kutumia njia za mkato kuepuka wasizuiwe kwenda kuogelea.
Afisa mwingine kutoka mamlaka ya utalii nchini Ghana amesema ni vigumu kudhibiti watu kuogelea kwenye fukwe za nchi hiyo.
Unyanyasaji dhidi ya wanawake waongezeka Afrika
Ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imefichua kwamba thuluthi tatu ya wanawake hukumbana na unyanyasaji wa kijinsia na kingono wakati mmoja maishani mwao.
Ripoti hiyo ni moja ya utafiti mkubwa zaidi kufanywa kuhusu unyanyasaji dhidi ya wanawake na inajumuisha data kati ya mwaka 2000-2018.
WHO linasema janga la corona limechangia kuongezeka kwa visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake. Linaripoti visa vya wanawake kushambuliwa na wenzi wao kuongezeka zaidi.
Hali hiyo inawaathiri zaidi ya wanawake milioni 640 kote duniani.
Asia Kusini, Kusini mwa Jangwa la Sahara, na Oceania zina viwango vya juu vya unyanyasaji wa wenzi.
Robo ya wanawake walio na umri kati ya miaka 15 -24 tayari wamekabiliwa unyanyasaji kutoka kwa wenzi wao.
Watu 35 wafariki baada ya kula 'mimea ya porini' Msumbiji
Watu 25 wa familia moja ni miongoni mwa watu 35 waliofariki kaskazini mwa Msumbiji baada ya kuripotiwa kula mimea na matunda ya mwituni, mamlaka zinasema.
Maafisa wanasema hivi karibuni kumeripotiwa visa vya watu katika eneo hilo kula matunda ya mwituni, mizizi na hata nyasi.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na televisheni ya kitaifa , TVM, wakazi wamekua wakisaga nyasi kupika xima – uji wa kienyweji wa Msumbiji, ambao hutengenezwa kutokana na unga wa mahindi.
Uhaba wa chakula katika mkoa wa Nampula umechangiwa na ukosefu wa mvua.
Waridi wa BBC: 'Nilimchukia mtoto alipozaliwa bila kujua sababu'
Suzzy Kahema aliishi maisha ya kawaida yenye matumaini tele akiwa mdogo, lakini katika ujana wake alipitia matukio ambayo karibu yasambaratishe maisha yake....Maelezo zaidi
Utafiti wa Umoja wa Mataifa waonesha watu 131,000 wamefurushwa Tigray
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linasema kwamba watu zaidi ya 131,000 walitoroka makazi yao katika maeneo 39 ya jimbo la Tigray nchini Ethiopia na kukimbilia majimbo jirani ya Afar na Amhara, kwa mujibu wa utafiti.
IOM limebaini watu katika nyumba 30,383 wametoroka makwao.
Baadhi ya waliohamishwa, ni pamoja na wanawake na watoto, ambao wanahitaji kwa dharura makai, chakula na maji safi na salama ya kunywa.
Kulingana na IOM, "data hii sio viashiria vya jumla ya idadi ya watu waliotoroka kutokana na vita lakini inawakilisha tu idadi ya wakimbizi wa ndani waliorodheshwa katika tovuti zilizounganishwa na mfumo wa DTM."
Burundi yapiga marufuku uagizaji wa mahindi kwa miezi sita
Wizara ya biashara ya Burundi imepiga marufuku uagizaji mahindi kutoka nje kwa miezi sita kuanzia tarehe 8 Machi.
Katika taarifa wizara hiyo imesema mahindi yaliyoingizwa nchini humo hivi karibuni ''hayakua mazuri'' na huenda yakadhuru afya ya watu.
Haikubainisha mahindi hayo yaliagizwa kutoka nchi gani.
''Wakati nafaka hii na unga inakataliwa na nchi jirani… tunahitaji kuhakikisha hayaingizwi nchini'', alisema Jeremie Banigwaninzigo, katibu wa kudumu wa wizara ya biashara na utalii wa Burundi.
Hatua hii inakuja baada ya Kenya kupiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka Uganda na Tanzania kutokana na hofu ya usalama ya nafaka hiyo.
Uagizaji mwingi wa mahindi wa Burundi unatoka Uganda na Zambia - lakini haijulikani ni kwa kiwango gani nchi hiyo inategemea uagizaji ili kukidhi mahitaji yake.
Soma zaidi:
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatano 10.03.2021