Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Abdalla Seif Dzungu na Lizzy Masinga

time_stated_uk

 1. Na hadi kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo ya moja kwa moja kwa hii leo. Kwaheri.

 2. ‘Samia Suluhu chachu ya wasichana wadogo Afrika’

  Samia Suluhu Hassan

  Jumuiya ya wanawake wa chama cha upinzani cha Orage Deocratic Movement (ODM) nchini Kenya, imemetuma rambirambi kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na wanawake wote waTanzania, kufuatia kifo cha hayati Rais John Pombe Magufuli.

  Pia wamebainisha mshikamano wao, pamoja na kutuma ujumbe wa heri njema kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kuapishwa kwake kwa kihistoria kama Rais wa kwanza mwanamke katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kundi hilo la wanawake wa ODM Kenya, limesema:

  ''Tunaungana na umma wote wa kike katika kanda ya Afrika Mashariki kubainisha imani yetu juu ya sifa za uongozi wa Mama Suluhu na uwezo wake wa kuongoza Tanzania katika kipindi hiki kipya kutoka pale ambapo mpendwa hayati Rais Magufuli alipoacha''.

  Wanawake hao wamesema kuingia mamlakani kwa Rais Suluhu katika ofisi kuu zaidi nchini Tanzania ‘’kutachangia pakubwa kuwapa moyo wasichana wadogo kote barani Afrika’’.

  Wameongeza kuwa ni matarajio yao kwamba Bi. Suluhu atavunja vikwazo vinavyowakabili wanawake na kuwahamasisha wale watakaokuja nyuma yake ili kujiunga na kazi za huduma ya umma pamoja na kujitolea kuchukua madaraka ya uongozi.

  Wanawake hao wameendelea kusema kuwa Tanzania inaonesha wazi usawa wa jinsia na uwakilishaji wa wanawake katika uongozi wa kisiasa na uteuzi katika serikali.

  ‘’Raia wake wanaweza kuuonea fahari uongozi thabiti alioacha hayati Rais Magufuli, hasa wa kuwa na imani kwa mwanamke kiasi cha kumteua kuchukua nafasi ya Ofisi ya Makamu wa Rais’’, kundi la wanawake wa ODM Kenya limesema.

  Na pia wamemuombea Samia Suluhu Hassan mafanikio katika majukumu yake mapya.

 3. Kenya yaagiza kufungwa kwa kambi kubwa ya wakimbizi

  Kambi ya Dadaab
  Image caption: Kambi ya Dadaab

  Kenya imeagiza kufungwa kwa kambi kubwa nchini humo na kutoa siku 14 kwa Umoja wa Mataifa kutatua njia ya kukabiliana na hatua hiyo.

  Karibu nusu milioni ya wakimbizi sasa hivi wanaishi katika kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma, wengi wao wakiwa kutoka Kusini mwa Sudan na Somalia, nchi ambazo bado haziko thabiti.

  Kenya iliwahi kutishia kufunga kambi hizo siku za nyuma. Lakini leo hii, Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiangí ameliambia shirika la Umoja wa Mataifa kwamba hakuna tena nafasi ya kufanya majadiliano.

  Bwana Matiangí inasemekana kwamba amerejelea vitisho vya mashambulizi ya kigaidi kutoka kambini na pia ametaja uhusiano wa kidiplomasia ambao umezorota kati yake na Somalia.

  Kambi ya Daadab

  Zaidi ya nusu ya wakimbizi nchini Kenya 500,000 ni kutoka Somalia.

  Shirika la Wakambizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema kuwa muda uliotolewa ni mchache mno na kuonya kwamba uamuzi huo huenda ukaathiri ulinzi wa wakimbizi nchini Kenya, hasa ukizingatia janga la virusi vya corona.

  Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya ni makazi kwa karibu wakimbizi 218,000 wengi wao wakiwa raia wa Somali, huku kambi ya wakimbizi ya Kakuma ikiwahifadhi wakimbizi takriban 200,000 waliosajiliwa wengi wao wakiwa kutoka nchi ya Sudan Kusini iliyoathirika na vita.

 4. Mwili wa Hayati Magufuli wawasili Chato

  Kivulo kilichobeba msafara

  Msafara wa viongozi wanaosindikiza mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Machi, 2021 umevuka katika kivuko cha Kigongo-Busisi na kuelekea Chato mkoani Geita mara tu baada ya wananchi wa Mwanza kupata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho.

  Kivuko cha MV Mwanza
  Raia waliofika kuuaga mwili wa Hayati magufuli wakipunga mkono
  Msafara uliobeba mwili wa Hayati John Magufuli
  Watanzania wamejitokeza kwa wingi kumuaga mpendwa wao
  Wanajeshi wakiwa kwenye gari lililobeba mwili wa Hayati Magufuli
 5. Mahakama ya Rwanda yaamua kuendelea na kesi bila Rusesabagina

  Paul Rusesabagina

  Mahakama ya juu mjini Kigali imeamua kuendelea na kesiwakati ambapo Paul Rusesabagina akisema kuwa hatafika tena mahakamani.

  Wakati wa kesi siku ya Jumatano, ‘shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda, hakutokea kwenye chumba cha mahakama iliposikilizwa mara ya mwisho tarehe 12 Machi, alisema ‘hatarajii haki katika mahakama hiyo’.

  Leo,mahakama imesema ni‘’haki kwa washtakiwa kufika mahakamani,’’ lakini kesi itaendelea ‘’iwapo mtu hatatokea bila sababu za msingi’’.

  Rusesabagina, 66, na washukiwa wengine 20 wanatuhumiwa kujihusisha na ugaidikutokana na shambulio la waasi wa FNL dhidi ya Rwanda mwaka 2018-2019.

  Rusesabagina ambaye ambaye amesisitiza kuwa yeye si Mnyarwanda na ambaye alisema alitekwa nyara na kufikishwa Rwanda hajakiri mashtaka dhidi yake, ingawa alikubali kuwa aliwapa fedha waasi.

  Maelezo zaidi:

 6. Wahalifu, walawiti watumia mtindo wa kulaghai kushiriki unyanyasaji wa kingono

  Wahalifu, walawiti watumia mtindo wa kuwalaghai kushiriki unyanyasaji wa kingono

  Wahalifu na walawiti wa watoto wanajaribu kuwalaghai na kuwatumia vibaya watoto kama sehemu ya unyanyasaji wa kingono unaoibukia na kusambaa kwenye intaneti duniani, wataalamu wanasema.

  Shirika linalofuatilia uhalifu wa aina hiyo kwenye mtandao - Internet Watch Foundation(IWF) limesema kuwa waathiriwa ni watoto wavulana wenye umri wa kati ya miaka 3 na 16, huku baadhi wakiandaliwa kunakili ponografia ya watu wazima.

  Wakfu huo ulibaini mifano 511 ya watoto ndugu waliojaribiwa kuingizwa kwenye mtandao huo baina ya miezi ya Septemba na Disemba.

  Karibu tukio moja kati ya matukio 30 yote "ya maudhui yalitengenezwa binafsi " katika wakati ule.

  Wanaharakati wa matangazo ya moja kwa moja ya mtandaoni (livestreaming )wanasema huduma hiyo inahitaji kufanya juhudi zaidi katika kuwalinda watoto.

  IWF, ambao inafanya kazi kwa ushirikiano na polisi na mitandao mbali mbali, inasema janga la Covid-19 lilipunguza maudhui yenye madhara" kwa unyanyasaji.

  Mkurugenzi mtendaji wake, Susie Hargreaves, amesema kumekuwa na:

  .Kiwango kikubwa cha uhitaji wa maudhui ya unyanyasaji

  .Ongezeko la muda unaotumiwa kwenye mtandao na watoto

  .Ongezeko katika matumizi ya majukwaa ya matangazo ya moja kwa moja ya mtandao-livestreaming

  Mara nyingi tukio hilo huanza kwenye majukwaa yamitandao yakijamii na michezo(game) ya intaneti, kabla ya wahalifu hao kuwashawishi watoto kujiunga na huduma ya mazungumzo kwa njia ya video au ya matangazo ya moja kwa moja, ambako unanyasaji unaanza kufanyika.

  Unyanyasaji huu ulikuwa ni kitu kilichozoeleka katika nchi masikini zaidi awali miongoni mwa nchi masikini- lakini video ya IWF inaonesha pia watoto kutoka mataifa ya magharibi, ikiwa ni pamoja na Marekani, Uingereza na mataifa ya Ulaya wakinyanyaswa.

 7. Watu 18 walioshikiliwa na vikosi vya usalama Uganda waachiwa

  Wanaume 18 walioaminika kushikiliwa na vikosi vya usalama vya Uganda wameachiwa na kuruhusiwa kurejea kwenye kijiji walichotoka

  Watu hao waliokamatwa wakati wa uchaguzi mwezi Januariwamesema hawajui walikuwa wakishikiliwa wapi.

  Baada ya kuachiwa kwao , baadhi yao wameiambia BBC kuwa walitupwa kwenye idara ya usalama katika maeneo mblimbali ya wilaya ya Kyotera, Kusini mwa jiji la Kampala, Jumatatu usiku.

  Mmoja wao, John Kiwanuka, alidhaniwa kuwa amekufa, baada ya kupatikana damu nyingi kwenye chumba chake cha kulala baada ya kukamatwa mwezi Januari.

  Serikali imekiri kuwa inawashikilia watu 200, kwa shutuma za kushiriki maandamano au kwa madai ya kukutwa na mali za jeshi.

  Lakini takwimu za serikali hazihusishi kundi la wanaume 18 walioachiwa siku ya Jumatatu.

  Mamia ya wafuasi wa upinzani wanaaminika kukamatwa nchi nzima wakati na baada ya uchaguzi uliopingwa mwezi Januari.

  Katika kipindi cha majuma kadhaa ya hivi karibuni BBC imekuwa ikikusanya ushuhuda kutoka kwa familia zilizokuwa zikihitaji taarifa kuhusu wapendwa wao waliopotea.

  Baadhi ya waliokamatwa na kuachiwa baadae walisema walipitia mateso wakiwa huko.

  Serikali haijsema lolote kuhusu madai hayo.

  Je, hatua ya Bobi Wine kuondoa shauri la kupinga ushindi wa Museveni ina maana gani kwa Tume ya Uchaguzi, Mahakama na wafuasi wake?

  ‘Red, red wine': Maana ya alama za uchaguzi Afrika

 8. Watu watatu wauawa katika shambulio la bomu la kutegwa Kenya

  Inaaminiwa kuwa kundi la alshabab ndilo lililohusika na shambulio hilo

  Takribani watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati basi walilokuwa wakisafiria lilipopigwa na bomu lililotegwa katika barabara ya Arabia katika Kaunty ya Mandera nchini Kenya.

  Basi hilo lilikuwa njiani kuelekea katika mji wa Mandera uliopo mpakani mwa Kenya na Somalia Jumatano asubuhi lilipopigwa na kilipuzi kilichotegwa.

  Walioshuhudia tukio hilo wanasema basi hilo liliharibika vibaya baada ya kulipuka.

  Picha zilizochukuliwa kutoka kwenye eneo la tukio zinaonesha basi hilo likiwa limepasuka vipande huku waathiriwa wakiwa wamelala chini.

  Polisi imesema kuwa inahofia idadi ya majeruhi inaweza kuongezeka. Gavana wa ManderaAli Roba pia amethibitisha idadi ya vifo.

  Shambulio hili linakuja siku moja tu baada ya maafisa wa usalama kuzima jaribio la wanamgambo wa al-Shabaablakushambulia kambiya polisi iliyopo katika eneo laLafey, katika Kaunty ya Mandera.

  Inaaminiwa kuwa kundi hilohilo ndilo lililohusika na shambulio hili.

  Wanamgambo wa Al-Shabab wavamia hoteli Mogadishu, Somalia

 9. Mo Salah, kikosi cha Misri wawasili Kenya kucheza dhidi ya Harambee stars

  Misri na Mo Salah wawasili jijini Nairobi kuchuana Harambee Stars

  Misri na Mo Salah wamewasili jijini Nairobi Jumanne kwa ajili ya mchezo kati ya Mafarao hao na Harambee Stars, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa michezo wa kimataifa, Kasarani Alhamisi.

  Ushindi wa Misri utawahakikishia wanafuzu katika kinyang'anyiro hicho cha Afrika kitachofanyika nchini Cameroon mwaka ujao.

  Kenya pia inauhitaji sana ushindi huu ili kujiongezea nafasi ya kufuzu.

  Katika hatua nyingine, Mo Salah ameripotiwa na gazeti la Independent la Misri kuwa ameomba kujitenga na wenzake, lakini haijafahamika kama ombi lake limetekelezwa.

  Uamuzi wa Salah wa kuishi tofauti na wenzake unaaminika kuwa jitihada za kujitenga.

  Salah alikutwa na virusi vya Covi-19 wakati wa safari ya hivi karibuni barani Afrika kwa ajili ya majukumu yake ya kimichezo mwaka jana, pia mchezaji mwenzake Mohamed Elneny, anayekipiga katika klabu ya Arsenal.

  Elneny pia yuko kwenye kikosi kitakachopepetana na Kenya.

 10. Habari za hivi pundeMwili wa John Pombe Magufuli wawasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza

  Video content

  Video caption: Kifoi cha Rais Mgufuli: Mwili wa kiongozi huyo ukiwasili Mwanza
 11. Rastafari wa Mwanza wamfanyia ibada maalum rais John Pombe Magufuli

  Rastafari wa Mwanza wenye itikadi za kipekee wamefanya ibada maalumu ya kumuombea hayati Rais John Pombe Magufuli wakisisitiza alikuwa ni shujaa

  ilevile wamemuombea Rais Mpya Samia Suluhu Hassani hekima ya kutimiza kwa ukamilifu na uadilifu majukumu yake na kuendeleza mema yote yaliyo achwa na mtangulizi wake.

  Video content

  Video caption: Kifo cha Rais Magufuli: Rastafari wa Mwanza wamfanyia ibada kiongozi huyo wa Tanzania
 12. Habari za hivi pundeWakazi wa Mwanza wakisubiri mwili wa Magufuli uwanja wa ndege

  Video content

  Video caption: Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Jinsi hali Ilivyo Mwanza
 13. Natumai Hujambo. Ni siku nyengine ambapo tunaendelea kukupasha yanayojiri kuhusu kifo cha rais John Pombe Magufuli