Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu mbashara kwa leo. Eid Mubarak!

 2. Jinsi Eid ilivyosaliwa Jerusalem

  al-Aqsa

  Mamia ya Wapelistina wamejitokeza asubuhi ya leo kusali sala ya Eid katika msikiti mtukufu wa al-Aqsa uliopo Jerusalem.

  al-Aqsa

  Msikiti huo umeshuhudia mwanzo wa ghasia ambazo sasa zimeendelea katika sehemu mbalimbali za Pelestina baina ya waandamanaji na vikosi vya usalama vya Israeli.

  al-Aqsa

  Imamu wa msikiti huo alitangaza kuwa; "Watu wetu wataonesha furaha ya kusali Eid leo licha ya machungu yanayoendelea nchini mwao."

 3. Fainali ya Champions League kuchezwa Porto

  Uwanja wa Porto
  Image caption: Uwanja wa Porto unabeba mashabiki 50,000 lakini idadi katika fainali ya Champions League itakuwa 12,000 tu.

  Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya Chelsea na Manchester City sasa itachezwa nchini Ureno Mei 29 ambapo mashabiki 6,000 kutoka kila timu wataruhusiwa kuingia uwanjani.

  Mchezo huo umehamishwa kutoka Uturuki ambapo ndipo awali ulipangwa ufanyike kutokana hatua za tahadhari za kujikinga na tishio la virusi vya corona. Sasa mchezo huo utarindima katika jiji la Porto.

  Ureno ni moja ya nchi ambazo hazipo katika orodha ya marufuku ya kusafiri ya Uingereza, hivyo mashabiki kutoka England hawatalazimika kukaa karantini watakaporudi nyumbani baada ya mechi.

  Fainali hiyo ilipangwa kuchezwa katika uga wa Olimpiki wa Ataturk katika jiji la Instanbul, lakini Uturuki ipo katika orodha ya nchi ambazo zipo kwenye mstari mwekundu wa Uingereza.

  "Kuwanyima mashabiki fursa ya kuutazama mchezo huo kutokea kiwanjani halikuwa jambo ambalo tunataka litokee. Nina furaha kuwa mpango huu sasa umefanikiwa," ameeleza Rais wa Chama cha Kandanda cha Ulaya, Uefa Aleksander Ceferin.

 4. Kampuni ya Uingereza kuwalipa fidia Watanzania kwa manyanyaso

  George Joseph Bwisige
  Image caption: George Joseph Bwisige amesema alikuwa akisubiri kwa muda mrefu fidia hiyo.

  Kampuni ya kuchimba madini ya Petra Diamonds ya nchini Uingereza imekubali kuwalipa watu ambao walipigwa na kushikiliwa na maafisa katika mgodi wao wa Williamson mkoani Shinyanga, Tanzania.

  Jumla ya dola milioni sita zitalipwa kwa wachimbaji 71 katika mgodi huo ambao haki zao za kibinaadamu zilivunjwa.

  Katika taarifa yake, kampuni ya Petra imesema: "tunatambua kuwa matukio ambayo yalitokea nyuma kwa masikitiko makubwa yalisababisha vifo, majeraha na kunyanyaswa kwa wachimbaji haramu."

  Lakini kama sehemu ya makubaliano, kampuni hiyo haijakiri kufanya makosa.

  Uchunguzi wa matukio hayo ya kuvunjwa kwa haki za binaadamu za wachimbaji ulianzishwa na shirika lisilo la kiserikali la Uingereza la Rights and Accountability in Development (Raid).

  Waathirika wa matukio hayo waliwakilishwa kwenye kesi hiyo na wanasheria wa haki za binadamu kutoka kampuni ya Leigh Day.

  Malipo hayo yatawawezesha waathirika kupata huduma za kiafya wanazozihitaji.

  Mkurugenzi mtendaji wa Raid Anneke Van Woudenberg amesema anaamini makubaliano hayo yatawezesha kutokuvunjwa kwa haki za binaadamu katika siku za usoni.

  Mwanaharakati na mwenyeji wa eneo hilo George Joseph Bwisige amesema alikuwa "akisubiri kwa muda mrefu" kwa jambo hilo kutokea.

 5. Rwanda washeherekea Eid

  Waislamu katika baadhi ya mataifa hii leo wameanza kusherehekea sikukuu ya Eid ul-Fitri. Nchini Rwanda waumini leo asubuhi walijitokeza kusali katika viwanja mbali mbali kama wanavyoonekana katika picha zifuatazo:

  Rwanda Broadcasting Agency
  eid
  eid
  Eid
 6. Mke wa Mugabe ashtakiwa kwa mazishi ‘yasiyofaa’ ya rais Mugabe

  mugabe

  Mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe Grace Mugabe, ameagizwa kufika mbele ya mahakama ya kitamaduni kwa tuhuma za kufanya mazishi “yasiyofaa” ya hayati Rais Robert Mugabe.

  Grace Mugabe anatuhumiwa kwa kuenda kinyume na utamaduni wa jamii yao kwa kumzika mume wake katika boma la familia badala ya kumzika “sehemu iliyochaguliwa na jamaa zake na mama yake".

  Katika waraka kutoka kwa Chifu Zvimba, ambaye ni mkuu wa kitamaduni wa nyumbani kwa kina Mugabe, Mke wake Grace anatakiwa kuufukua mwili wa hayati Rais Mugabe ili uzikwe tena “kulingana na utamaduni wa watu wa Zvimba".

  Pia ameagizwa kulipa faini ya ng’ombe na mbuzi kwa kukiuka utamaduni.

  Mugabe alifariki mwaka 2019 katika hospitali moja nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95.

  Familia yake iliamua afanyiwe mazishi ya faragha kijijini kwao Kutama wilaya ya Zvimba- karibu kilomita 90 sawa na (maili 55) magharibi mwa mji mkuu wa Harare – baada ya mvutano wa wiki kadhaa na serikali.

  Patrick Zhuwao, mpwa wa marehemu rais, siku ya Alhamisi aliiambia televisheni ya Shirika la utangazaji la Afrika Kusini kwamba Mugabe alizikwa kulingana na ombi lake, uamuzi ambao unastahili kuheshimiwa.

  Amesema hakuna mzozo ndani ya familia akiongeza kwamba suala hilo lipo nje ya mamlaka ya chifu.

 7. Panya 'kupima' corona Tanzania

  panya

  Watafiti nchini Tanzania kutoka chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) wamesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa panya kutumika kutambua maambukizi ya virusi vya corona, Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi nchini humo.

  Dkt.Georgies Mgode, mtafiti kutoka SUA ameliambia gazeti hilo kuwa wana imani kuwa panya wanaweza kutambua virusi vya corona kwa ufanisi mkubwa kwa sababu tayari wameona mafanikio ya jinsi panya wanavyoweza kutambua mabomu yaliyojificha ardhini na kutambua vimelea vya kifua kikuu.

  "Vipimo vya virusi vya corona kwa sasa ni ghali na vinatoka nje ya nchi, lakini kwa kutumia panya itakuwa rahisi na itapunguza maumivu kwa wanaopimwa kwa vifaa."

  Vilevile gazeti hilo limemnukuu Dkt.Mgode akisisitiza kuwa kutambua maaambukizi ni jambo muhimu kwani kutasaidi kujilinda na wale watakaokutwa na maambukizi kupata huduma kwa haraka hivyo kupunguza vifo na maambukizi.

  Ameishukuru serikali kwa kuruhusu matumizi ya panya katika hospitali zake kwa makubaliano kuwa majibu yathibitishwe na teknolojia nyingine zinazokubalika kabla majibu hayatumika hospitalini.

 8. Israel-Gaza: Makombora yapiga Israeli baada ya wanamgambo kuuawa

  roket

  Wanamgambo wa Hamas wamerusha makumi ya maroketi upande wa Israel kujibu shambulio la angani la Israel lililowaua makamanda wa ngazi ya juu na kuangusha ghorofa nyingine mjini Gaza.

  Ghasia hizo zilizoanza Jumatatu wiki hii zimeibua mzozo mkubwa nchini kati ya Wayahudi na Waarabu wa Israel.

  Katika visa viwili tofauti, mwanaume wa Kiyahudi mjini Acre alishambuliwa na wanaume wa kiarabu, na Wayahudi walimtoa Mpalestina kwenye gari na kumpiga mjini Bat Yam.

  Karibu wa 67 wameuawa mjini Gaza na wengine Saba kuuawa hook Israel.

  Mapigano yalianza Jumatatu baada ya Hali ya taharuki kuongezeka kati ya Waisrael na Wapalestina Mashariki mwa Jerusalem na kufuatiwa na makabiliano yaliyosababishwa na mvutano wa kupigania eneo linalozozaniwa na Waislamu na Wayahudi.

 9. Kirusi cha India chaendelea kuenea Afrika

  virus

  Mataifa mengine matatu barani Afrika - Algeria, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Nigeria - zimebaini kuwa na watu wenye maambukizi ya virusi vya corona kutoka wimbi la India, Dkt. Ngoy Nsenga, kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO), ameiambia BBC.

  Mpaka sasa mataifa saba ya Afrika yamethibitika kuwa na maambukizi ya aina mpya ya kirusi kutoka India cha B.1.617, ambapo utafiti wa awali unaonesha kuwa aina hiyo ya kirusi kinasambaa haraka kuliko aina nyingine yeyote ya virusi vya corona.

  Dkt Nsenga, ambaye anaratibu shughuli za WHO katika kukabiliana na Covid-19 barani Afrika, amesema taarifa zaidi zitatolewa kuhusu watu walioambukizwa au historia ya watu waliosafiri wakiwa wana virusi hivyo nchini Algeria, DRC na Nigeria, .

  Mataifa manne ya Afrika tayari yamethibitisha kuwa na aina mpya ya virusi vya corona ambayo inahusisha na wasafiri kutoka India. Mataifa hayo ni:

  • Kenya: Ina watu kumi na tano waliopata maambukizi hayo
  • Morocco:Ina watu wawili wenye maambukizi
  • Afrika Kusini : Ina watu wawili wenye maambukizi hayo
  • Uganda: Ina mtu mmoja

  Hivi karibuni WHO imesema, kirusi cha India kilianza kuonekana Oktoba 2020, na kuleta hofu duniani.

  Kuna utafiti unaosema kuwa wimbi jipya la maambukizi ya corona limeongeza idadi ya vifo nchini India, na sasa hospitali zimejaa huku wakikosa maeneo ya kuzika au kuchoma maiti.

 10. Habari...Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kurasa wa BBC Swahili leo ikiwa tarehe 13/05/2021