Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Ripoti kuhusu afisa wa polisi kuwa na ushirika na 'tapeli' wa Nigeria yatolewa

  Naibu Kamishna wa Polisi Abba Kyari

  Mkuu wa polisi wa Nigeria amepokea ripoti ya uchunguzi kuhusu afisa wa juu aliyesimamishwa kazi Abba Kyari, ambaye anatafutwa kwa madai ya kuwa na ushirikiano na tapeli wa mtandao wa Instagram Hushpuppi.

  Bw Kyari alisimamishwa kazi kama naibu kamishna wa polisi kufuatia kushtakiwa kwake na mamlaka ya Marekani kwa madai kwamba aliwezesha malipo kwa wafanyakazi wa polisi wa Nigeria kutoka kwa Hushpuppi, ambaye jina lake halisi ni Ramon Abbas.

  Hushpuppi

  Polisi wa Nigeria waliunda jopo la kufanya ukaguzi wa ndani wa madai hayo baada ya mashtaka ya Marekani Bw Kyari anakanusha madai hayo yote.

  Siku ya Alhamisi, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Joseph Egbunike aliwasilisha ripoti ya jopo hilo kwa mkuu wa polisi Usman Baba, bila kufichua maelezo ya matokeo yao.

  Bwana Egbunike alisema ripoti hiyo ni matokeo "ya mchakato wa uchunguzi wenye bidii, wazi na kamili". Mkuu wa polisi alitaja kujitolea kwake kwa haki na akasema timu ya usimamizi wa polisi itapitia mapendekezo hayo na kuwasilisha kwa "hatua muhimu".

  Abba Kyari: Kachero wa Nigeria anayesakwa na Marekani

 2. Waziri wa zamani wa Malawi akamatwa kwa kulipa gharama za fungate kwa fedha za Umma

  Waziri wa zamani wa Malawi amekamatwa kwa kwa madai ya kulipa gharama za fungate kwa kutumia pesa za Umma.

  Charles Mchacha, aliyekuwa waziri wa umwagiliaji wakati wa utawala wa Rais wa zamani Peter Mutharika, anadaiwa kutumia fedha za wizara kwa ajili ya kugharamia hoteli ya hadhi ya juu kwa ajili yake na mkewe baada ya harusi mjini Blantyre.

  Gazeti la Nation la Malawi liliandika kwenye ukurasa wa twitter kuwa maafisa wengine wawili wa serikali pia wamekamatwa na taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo.

  View more on twitter

  Taasisi hiyo ya ACB imesema watu wote watatu watashtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya ofisi, uzembe na wizi.

  Wote wamekana shutuma hizo dhidi yao.

 3. Nchi mbalimbali zatamatisha operesheni za kuondoa raia wao Afghanistan

  Wakati Uingereza ikiingia katika hatua ya mwisho za kuondoka, tutazame nchi nyingine wakati operesheni zao zikifikia tamati:

  Marekani itakuwepo mpaka tarehe 31 Agosti ikiwa itahitajika, idara ya ulinzi imeeleza.

  Kwa jumla, karibu watu 12,500 waliondolewa siku ya Alhamisi, na kuongeza idadi ya walioondolewa tangu udhibiti wa Taliban tarehe 14 Agosti kufikia karibu 105,000, Ikulu ilisema Ijumaa.

  Uhispania imemaliza operesheni ya kuwaondoa raia wake, serikali imesema.

  Ndege mbili za jeshi zilizobeba Wahispania wa mwisho 81 kuwatoa mjini Kabul waliwasili Dubai mapema Ijumaa.

  Ndege pia ziliwabeba wanajeshi wa Kireno wanne na raia 83 wa Afghanistan ambao walifanya kazi na nchi za Nato, serikali imeeleza.

  Ujerumani walitamatisha zoezi la kuwaondoa watu siku ya Alhamisi.

  Jeshi la Ujerumani limewaondoa watu 5,347, wakiwemo raia zaidi ya 4,100 wa Afghanistan.

  Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imesema, mpaka Alhamisi jioni,zaidi ya raia 100 wa Ufaransa na zaidi ya raia 2,500 wa Afghanistan wamewasili kwenye ardhi ya Ufaransa baada ya kuondoka mjini Kabul.

  Ufaransa haitaweza kuwaondoa watu zaidi baada ya siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu Jean Castex ameiambia radio moja nchini humo.

 4. Anayeshukiwa kupanga kujilipua kwenye mazishi akamatwa Uganda

  Paul Lokech anasifiwa kumtimua al-Shabab kutoka mji mkuu wa Somalia, Mogadishu Picha ya picha: Paul Lokech anasifiwa kwa kuwatimua al-Shabab kutoka mji mkuu wa Somalia, Mogadishu

  Mshambuliaji anayeshukiwa kuwa wa kujitoa muhanga amekamatwa nchini Uganda kwa kupanga kujilipua katika mazishi ya kamanda wa jeshi anayefahamika kama ‘they lion of Mogadishu’’.

  Meja Jenerali Paul Lockech alipewa jina hilo la bandia tangu wakati alipokuwa Mkuu wa kikosi cha Muugano wa Afrika kilichopo nchini Somalia (Amisom) kuanzia mwaka 2000.

  Alisifika kwa kuwaondosha wanamgambo wa al-Shabab katika mji mkuu Mogadishu.

  Amisom kilisema kuwa itamkumbuka kama “ mnara wa ishara ya heshima katika mapigano dhidi ya wanamgambo wenye silaha” , na kwamba atakumbukwa kama urithi ambao hauwezi kusahaulika.

  Meja Jenerali Lokech mwenye umri wa miaka 55, ambaye alikuwa anafanya kazi akiwa Inspekta Jenerali wa polisi alifariki kutokana na ugonjwa wa kuganda kwa damu nyumbani kwake siku ya Jumamosi.

  Rais Yoweri Museveni amekuwa akitarajiwa kuhudhiria mazishi yake katika wilaya ya kaskani Mwa nchi hiyo ya Pader.

  Mshukiwa alikamatwa Alhamisi mchana katika operesheni ya pamoja baina ya maafisa mbalimbali wa usalama.

  Msemaji wa jeshi Flavia Byekwaso amesema kuwa alipatikana na zana za kutengeneza mabomu, ikiwa ni pamoja na mabegi ya mabomu, fulana za mabomu ya kujitoa muhanga, na kifaa cha kukata waya wa kulipua mabomu.

  Washukiwa wenzake pia wametambuliwa na operesheni bado inaendelea ili kuwapata, alisema.

 5. Rais wa Zambia kuanza kuunda baraza la mawaziri

  Rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema amesema ataanza kutangaza mawaziri wake siku ya Alhamisi.

  Rais huyo ameandika ujumbe kwenye kurasa wake wa Twitter, kuwa mtu wa kwanza kuteuliwa atakuwa waziri wa fedha:

  View more on twitter

  Bwana Hichilema alichaguliwa kuwa rais mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kumshinda mpinzani wake aliyekuwa rais wa taifa hilo Edgar Lungu, kwa mamilioni ya kura.

  Rais huyo amehaidi raia wa Zambia kuboresha uchumi ambao ulikuwa umeshuka.

 6. Wanafunzi waliotekwa Nigeria waachiwa huru baada ya mamilioni ya fedha kulipwa kama kikombozi

  shule

  Maofisa nchini Nigeria wamesema madaktari wamewafanyia uchunguzi wa kiafya zaidi ya wanafunzi mia moja waliotekwa na watu wenye silaha miezi mitatu iliyopita.

  Wanafunzi hao walitekwa katika moja ya shule ya kiislamu iliyopo mjini Tegina katikati ya jimbo la Niger nchini Nigeria wakati wa shambulio.

  Taarifa zinasema takribani dola laki moja na nusu zililipwa ili kuweza kuachiwa huru.

  Watoto hao walisafirishwa na mabasi kutoka eneo lililo karibu na pori ambalo walikuwa wametekwa.

  Mwalimu mkuu wa shule ameiambia BBC kuwa wanafunzi walioachiwa huru walikuwa wanaonekana kuwa dhaifu kiafya na walikuwa wamechoka sana.

  Walipelekwa katika kituo cha afya kabla ya kuwakutanisha na familia zao. Mamlaka ya shule na wazazi waliweza kupata maelfu ya dola kuwapa watekaji hao ili waweze kuwaachia huru wanafunzi hao kwa kuuza sehemu ya ardhi ya shule na wazazi kuchangishana.

  Maofisa wa shule wamesema pikipiki kadhaa zilipelekwa kwa watu wale wenye silaha ili kufikia makubaliano yao.

  Wazazi ambao hawajakutana na watoto wao kwa kipindi cha miezi mitatu wana shauku kubwa ya kukutana nao tena .

  Mamlaka ya Nigeria inakabiliwa na ongezeko kubwa la magenge ya wahalifu kufanya matukio ya utekaji na kutaka kupewa fedha ili wawaachie huru waliowateka.

  Zaidi ya wanafunzi 1000 wametekwa wakiwa shuleni au vyuoni tangu mwezi Disemba mwaka jana na wameachiwa huru baada ya fedha kutolewa

  Nigeria:Wanajeshi Wanawake wana jukumu gani katika usalama wa Nigeria?

  Mizozo Nigeria: Fahamu vitisho vitano vya usalama vinavyoikabili Nigeria

 7. Lisa Shaw: Kifo cha Mtangazaji kilisababishwa na matatizo ya chanjo ya Covid

  Lisa Shaw

  Kifo cha Mtangazaji mmoja wa radio kilisababishwa na matatizo ya kiafya yaliyochangiwa na chanjo ya Covid-19 aina ya AstraZeneca, uchunguzi kuhusu kifo chake umebaini.

  Lisa Shaw, aliyekuwa mfanyakazi wa BBC Radio Newcastle, alifariki mwezi Mei akiwa na umri wa miaka 44 kutokana na kuumwa na kichwa baada ya kuchomwa chanjo ya kwanza.

  Afisa wa Mahakama ya Newcastle Karen Dilks alifahamishwa kuwa Bi. Shaw alipata mgando wa damu kwenye ubongo ambao ulisababisha kifo chake.

  Wachunguzi walifahamishwa kuwa hali hiyo inayohusishwa na chanjo ya Oxford-AstraZeneca ilikuwa nadra sana.

  Bi Dilks alisema Shaw alikuwa mzima na buheri wa afya na kuhitimisha "wazi" kuwa kifo chake kilitokana na hali isiyokuwa ya kawaida inayofahamika kama"thrombotic thrombocytopenia ", inayofanya ubongo kuvimba na kutokwa na damu.

  Soma zaidi:

 8. Waziri Mkuu wa zamani wa Mali amekamatwa kwa madai ya rushwa

  Mali
  Image caption: Waziri mkuu wa zamani wa Mali

  Waziri mkuu wa zamani wa Mali Boubèye Maïga amekamatwa kwa madai ya rushwa katika matumizi ya ndege ya rais miaka saba iliyopita.

  Wakili wake Kassoum Tapo alisema taarifa juu ya kukamatwa kwake Alhamisi hii bado haijawekwa wazi.

  Bwana Maïga amekuwa akishutumiwa kwa madai ya kuongeza gharama ya malipo ya ndege ya Rais wa zamani Ibrahim Keïta.

  Alikuwa waziri wa ulinzi wakati akifanya gharama hizo mwaka 2014.

  Ndege hiyo ya rais ilinunuliwa kwa dola milioni 40 (£29m), kiwango cha fedha ambacho kilikosolewa vikali kuwa ni gharama kubwa sana.

  Bwana Maïga alikuwa waziri mkuu kati ya mwaka 2017 na 2019 wakati alipojiuzuru baada ya kuibuka kwa ghasia nchini kwake.

  Boubou Cissé alichukua wadhifa huo wakati alipoondolewa madarakani pamoja na Rais Keïta mnamo Agosti 2020.

 9. Raila akariri wito wa rais Uhuru Kenyatta kwa naibu wa rais William Ruto kujiuzulu kutoka serikalini

  ra

  Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya na Kiongozi Upinzani nchini humo Raila Odinga ameunga mkono wito wa Rais wa taifa hilo Uhuru Kenyatta kuwa naibu wake William Ruto kujiuzulu kutoka serikalini iwapo hajaridhika na jinsi serikali inavyoendeshwa.

  Odinga amesema hatua ya kuondoka serikalini kwa Ruto na wabaunge wanaomuunga mkono pamoja na chama cha UDA ndio jambo la ‘heshima’ kufanya kwa sasa.

  “Iwapo unaona mambo hayako sawa na wewe ni mtu mwenye msimamo wako basi sema mambo sio mazuri na ujiuzulu’ Raila amesema.

  ''Kuna wabunge wanaosema kuwa wapo UDA ilihali wangali wanapokea mashahar akupitia chama cha Jubilee,wanafaa kujiuzulu na kuvitetea viti vyao kupitia chama kipya'' Aliongeza.

  Kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu Rais Uhuru Kenyatta kupitia mahojiano ya runinga alimtaka naibu wake kuondoka serikalini badala ya kuikosoa kila mara.

  Rais alisema Ruto anafaa kuzingatia kuendeleza kampeni zake za uchaguzi mkuu wa mwaka ujao akiwa nje ya serikali iwapo hajapendezwa na utawala wake.

  Ruto hata hivyo hajaonyesha nia ya kutaka kuondoka serikalini na siku ya Jumanne alisema hataondoka kwenye serikali ambayo alisaidia kuiunda.

  Ruto na Rais Kenyatta walishirikiana katika chaguzi za 2013 na 2017

  Maelezo zaidi:

 10. Beki wa Manchester City Benjamin Mendy ashitakiwa kwa ubakaji

  M

  Mlinzi wa Manchester City, Benjamin Mendy (27) ameshitakiwa kwa makosa manne ya ubakaji na lingine la unyanyasaji wa kijinsia, kwa mujibu wa Polisi wa Cheshire.

  Makosa hayo yanawahusu walalamikaji watatu walio na umri wa zaidi ya miaka 16 na yanaelezwa kufanyika kati ya Oktoba 2020 na Agosti mwaka huu.

  Mendy, anayeishi eneo la Prestbury, kwa sasa anashikiliwa na polisi kabla ya kufikishwa mahakamani leo katika mkoa ya Chester.

  Mlinzi huyo wa kushoto amekuwa akiwachezea mabingwa hao wa ligi kuu England msimu uliopita tangu mwaka 2017 alipojiunga nao akitokea Monaco kwa ada inayoripotiwa kuwa ni £52m.

  Msemaji wa Polisi alisema: "Polisi Cheshire na kitengo cha mashataka cha Crown wanapenda kuwakumbusha kuwa kesi ya jinai inayomkabili Mendy ipo na ana haki zote za kusikilizwa."

  Manchester City ilisema mlinzi huyo, ambaye pia anachezea timu ya taifa ya Ufaransa , ameondolewa kwenye kikosi hicho mpaka baada ya uchunguzi wa kesi yake hiyo.

  "Suala hilo liko kwenye mchakato ya kisheria kwa hivyo klabu haitaweza kuzungumzia zaidi mpaka litakapokamilika," Klabu hiyo iliongoeza.

  Habari zaidi:

 11. Watu kadhaa wamekamatwa DRC kwa kutumia dawa za kulevya za kienyeji

  mm

  Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewakamata watu wapatao 100 wanaoshukiwa kuwa watumiaji na wauzaji wa dawa mpya za kulevya.

  Rais Felix Tshisekedi ametaka uchunguzi ufanyike kuhusu dawa hizo za kulevya ambazo zinatengenezwa katika bomba la kutoa moshi wa gari.

  Dawa hizo mpya zinazoitwa 'bombe' ni mchanganyiko unga wa dawa mbalimbali.

  Baadhi ya wanaoshukiwa kuwa watumiaji walikamatwa Alhamisi, Shirika la Habari la AFP limeripoti, kuwa walikuwa watu hao hawana hatia ila tu walikuwa katika eneo baya na muda usio rafiki.

  Mkuu wa Polisi katika uhalifu Alphonse Landu amesema wanawafuatilia wauzaji wa dawa hizo za kulevya za kienyeji mjini Kinshasa, tovuti ya Actualite Congo umeripoti.

  Matumizi ya dawa za kulevya DRC ni changamoto kubwa kwa vijana na Wizara ya Afya ina wasiwasi juu ya dawa hizo mpya za kulevya.

 12. TV zote za Samsung zilizoporwa Afrika Kusini zimedhibitiwa

  mm

  Kampuni ya Samsung imeweka zuio kwa TV zote zilizoibiwa Afrika Kusini wakati wa ghasia za uporaji mwezi Julai, na kuzifanya zisiweze kufanya kazi tena.

  Kampuni hiyo imesema imeweka zuio hilo kwa kutengeneza mfumo wa kuzima runinga zote zilizoibiwa kushindwa kutumika.

  TV hizo zinaweza kufanya kazi endapo mtumiaji wa runinga iliyoibiwa anatumia mawasiliano ya intaneti kinyume na sheria, kwa mujibu wa Samsung.

  Mfumo huo umeangalia orodha ya namba za usajili wa TV’ kabla ya kuzuia matumizi yake.

  Afrika Kusini ilikuwa na maandamano ya ghasia na kwa wiki kadhaa mwezi uliopita na yaliyosababisha watu zaidi ya 300 kuuawa na mali zenye zaidi ya thamani ya mamilioni ya randi.

  Baadhi ya vitu ziliripotiwa kuibiwa wakati wa ghasia ni TV za kisasa.

  Hatua hiyo ya kuweka zuio la kuweza kuzima matumizi ya TV kwa mbali umesifiwa na watumiaji mitandao na kuweza kuzuia uhalifu huo.

  Mtu mmoja alisema Samsung inalipa kisasi kwa waporaji kwa njia ya kielektoniki na mwingine alisema kulikuwa na sababu zaidi za kutounganisha TV kwenye intaneti".

 13. Ron Jeremy: Nyota wa filamu wa Marekani alishtakiwa kwa uhalifu wa kingono

  Bwana Jeremy

  Nyota wa filamu ya watu wazima nchini Marekani Ron Jeremy ameshtakiwa kwa makosa 34 ya uhalifu wa kingono unaohusisha wanawake 21, kwa zaidi ya miaka 20, waendesha mashtaka wa Los Angeles wanasema.

  Bwana Jeremy, 68, alikana mashtaka hayo Jumatano.

  Ni mmoja wa majina tajika katika filamu ya watu wazima na ameshiriki katika zaidi ya filamu 1,700 tangu mwaka 1979.

  Shtaka la Agosti 19, ambalo lilikuwa limefungwa Jumatano, linamshutumu Bwana Jeremy kwa makosa 12 ya ubakaji, ikiwa ni pamoja na ile ya msichana wa miaka 17 mnamo 2008 na msichana wa miaka 15 mwaka 2004.

  Mashtaka ya hivi karibuni yanayomkabili ni ya Januari mosi 2020, ambapo mwanamke wa miaka 21 anamtuhumu kwa ubakaji na ulawiti.

  Wakili wake siku ya Jumatano alisema Bw. Jeremy anashikilia kuwa mteja wake hana hatia yoyote.

  Bwana Jeremy, ambaye jina lake halisi ni Ronald Jeremy Hyatt, anakaa gerezani kwa dhamana ya $ 6.6m (£ 4.81m).

  Mnamo Juni jmwaka jana, Bwana Jeremy alifikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kubaka wanawake wawili na kuwanyanyasa kingono wengine wawili kati ya 2014 na 2019.

  Wakati huo, wakili wake alikanusha mashtaka hayo, akidai kwamba Bwana Jeremy alikuwa "msaidizi wa wanawake" zaidi ya 4,000 na kwamba "wanawake hujitupa kwake."

  Mchekeshaji Bill Cosby amehukumiwa hadi miaka 10 jela kwa unyanyasaji wa kingono

  Bill Cosby: Wajue watu wengine maarufu waliofungwa na kuachiwa

 14. Spishi mpya ya nyangumi wa kale wenye miguu minne yagunduliwa Misri

  nyangui

  Wanasayansi huko Misri wamegundua spishi mpya ya nyangumi wenye miguu minne ambao waliishi karibu miaka milioni 43 iliyopita.

  Mabaki ya spishi hiyo kwa jina Phiomicetus anubis awali yaligunduliwa katika Jangwa la Magharibi la Misri.

  Fuvu la kichwa chake linafanana na Anubis, mungu wa zamani wa mbwa-mwitu wa Misri wa wafu ambaye aliitwa jina lake.

  Kizazi cha kale cha nyangumi wa kisasa walitengenezwa kutoka kwa wanyama kama kulungu ambao waliishi ardhini kwa kipindi cha miaka milioni 10.

  Akiwa na uzani wa kilo 600 na mita tatu (10ft) kwa urefu, Phiomicetus alikuwa na taya kubwa na ngumu ili kuwakamata mawindo, kulingana na utafiti uliochapishwa na Proceedings of the Royal Society B Jumatano.

  Nyangumi huyo aliweza kutembea ardhini na kuogelea ndani ya maji.

  Mifupa ya sehemu yake ilipatikana katika Fayum Depression nchini Misri na kuchambuliwa na wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Mansoura. Ingawa eneo hilo sasa ni jangwa, wakati mmoja lilikuwa limefunikwa na bahari.

 15. Nigeria:Watu waliojihami wawaachilia watoto wa shule waliokuwa wakishikiliwa mateka

  NG

  Wapiganaji wenye silaha nchini Nigeria wamewaachilia huru wanafunzi waliotekwa nyara kutoka shule moja ya Kiislamu mnamo Mei, kulingana na mwalimu wao mkuu.

  Wanafunzi 136 kutoka shule ya Tegina katika jimbo la Niger, walikamatwa na watu wenye silaha wakidai fidia.

  Maafisa wa shule wanasema wanafunzi 15 walitoroka mnamo Juni na wengine sita walifariki wakiwa mateka

  Utekaji nyara wa watu wengi kwa ajili ya fidia umekuwa jambo la kawaida nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuni.

  Mwalimu mkuu Abubakar Alhassan alisema hangeweza kutoa idadi kamili ya wanafunzi walioachiliwa, lakini "hakuna mwanafunzi aliye aliyeshikiliwa mateka ".

  Aliliambia shirika la habari la AFP kwamba wanafunzi hao walikuwa wakisafirishwa kwenda nyumbani.

  Bado haijafahamika jinsi wanafunzi hao walivyoachiliwa.

  Fati Abdullahi, ambaye binti wakemwenye umri wa miaka 18 na mtoto wake wa kiume wa miaka 15 walichukuliwa na kikundi hicho, alisema watoto wake walikuwa wameachiliwa.

  "Tunatamani kuwaona," alisema.

  Mnamo Mei 30, watu wenye silaha waliokuwa wakitumia pikipiki walivamia mji huo na kufyatuarisasi huku wakimuua mtu mmoja na kumjeruhi mwingine.

  Watu walipokimbia, washambuliaji walikwenda shuleni na kuwakamata watoto hao.

  Mnamo Julai, watekaji nyara walimkamata mtu ambaye alitumwa kupeleka malipo ya fidia ili kuhakikisha kuachiliwa kwa wanafunzi.

  Wazazi na wasimamizi wa shule walikuwa wameuza mali na sehemu ya ardhi ya shule hiyo kulipa fidia. Lakini baadaye walisema malipo hayakutosha .

  Zaidi ya wanafunzi 1,000 wametekwa nyara kutoka shule kaskazini mwa Nigeria tangu Disemba mwaka jana.

  Mamlaka huko zimekosolewa kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama nchini kote ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara

 16. Ya hivi punde unayofaa kujua kuhusu shambilio la bomu katika uwanja wa ndege wa Kabul

  tl

  Jana Alhamisi palitokea shambulio baya katika uwanja wa ndege wa Kabul nchini Afghanistan lililosababisha vifo vya takriban watu 60. Haya ndio ya hivi punde kuhusu shambulio hilo:

  • Tariban watu 60 waliuawa na 140 walijeruhiwa katika milipuko miwili katika uwanja wa ndege wa Kabul - afisa wa afya wa Afghanistan ameiambia BBC
  • Wanajeshi 13 wa Marekani ni miongoni mwa wale waliokufa, Pentagon imethibitisha, katika siku inayoonekana kuwa mbaya zaidi kwa wanajeshi wa Amerika nchini Afghanistan tangu 2011
  • Akijibu shambulio hilo, Rais wa Marekni Joe Biden amewaambia waliohusika : "Tutawasaka na kulipiza"
  • Anaapa pia kumaliza oparesheni ya kuwaokoa watu , lakini amesema kwamba "kumtoa kila mtu nje sio jambo ambalo anaweza kutoa hakikisho "
  • Rais anasema hadi sasa hakuna uthibitisho wa ushirikiano kati ya Taliban na Dola la Kiisilamu, Isis-K ambalo alidai kuwa ndilo lililosababisha shambulio hilo
  • Viongozi wa nchi za Magharibi wamelaani shambulio la Kabul, kwani mataifa kadhaa yanamaliza shughuli zao za uokoaji
  biden

  Hofu ya mashambulio Zaidi

  Makamanda wa Marekani wako macho juu ya hofu ya mashambulio zaidi Kutoka kwa ISIS, pamoja na roketi zinazowezekana au mabomu yanayosafirishwa kwa gari yakilenga uwanja wa ndege wa Kabul, mkuu wa Jeshi la Marekani Frank McKenzie alisema.

  "Tunafanya kila tuwezalo kuwa tayari," Jenerali McKenzie alisema, wakati vikosi vya Marekani vikilenga kumaliza kujiondoa kwao Afghanistan.Marekani inharakisha kukamilisha uokoaji kufikia tarehe ya mwisho - 31 Agosti iliyokubaliwa na Taliban.

  Rais wa Markani Joe Biden hajazidisha muda wa oparesheni hiyo .Alhamisi jioni alisema kuwa juhudi za uokoaji zitaendelea licha ya mashambulio hayo.

  Vita vya Afghanistan: Bonde 'lililoshindikana' lililoko umbali wa saa moja kutoka Kabul

  Afghanistan: Kikosi kipya cha 'Fateh ambacho Taliban inatumia kulinda Kabul

 17. Hujambo na Karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Ijumaa tarehe 27 Agosti .