Kufikia hapo tunafika tamati ya habari zetu hii leo, tukutane kesho
wanaume milioni 1.5 kutahiriwa Sudan katika kampeni dhidi ya HIV
AFPCopyright: AFP
Wanaume wanaotarajiwa kutahiriwa ni wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 49Image caption: Wanaume wanaotarajiwa kutahiriwa ni wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 49
Mradi wa kuwatahiri wanaume milioni 1.5 wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi
49 Suimeanzishwa nchini Sudan Kusini ili
kupunguza uwezekano wa kuambukiza virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi.
Utafiti unaonesha kuwa wanaume waliotahiriwa wana hatari ya
chini ya kuambukizwa virusi vya HIV kuliko wanaume ambao hawajatahiriwa
wanafanya tendo la ngono na mtu wa jinsia tofautimwenye virusi hivyo.
Shirika lisilo la kiserikali la Human Appeal Associates, kwa ushirikiano na
wizara ya afya ya nchi hiyo, watawatafuta wanaume watakaojitolea kutahiriwa kwa
kipindi cha miaka mitano ijayo.
Majimbo matatu pekee kati ya 10 ndio yenye utamaduni wa
kutahiri, nan je ya majimbo hayo kutahiri ni mwiko.
Serikali imeelezea viwango vya chini vya kutahiri kama hofu
kuu ya afya ya umma inapokuja katika suala la kukabiliana na HIV nchini Sudan
Kusini.
“Viwango vya wanaohitaji kutahiriwa katika mji mkuu Juba
pekee ni vya juu sana," Robert Matthew Uku, kutoka shirika la from Human
Appeal Associates, ameiambia BBC.
Wabunge wa upinzani Uganda wahojiwa kuhusu mauaji ya kikatili
Daily MonitorCopyright: Daily Monitor
Msemaji wa polisi Fred Enanga aliambia vyombo vya habari kwamba wanasiasa hao wawili ndio waliopanga mashambuliziImage caption: Msemaji wa polisi Fred Enanga aliambia vyombo vya habari kwamba wanasiasa hao wawili ndio waliopanga mashambulizi
Wabunge wawili wa Uganda kutoka chama
cha upinzani cha National Unity Platform leo wamefika mbele ya idara ya
uchunguzi wa jinai ili kujibu maswali, kuhusu wimbi la hivi karibuni la mauaji
katika jimbo la kati la masaka.
Maafisa wa polisi walikizunguka kituo
cha polisi ambacho viongozi hao walikuwa wanahojiwa. Wawili hao waliombwa
mbele kufika mbele ya maafisa wa polisi wiki iliopita.
Msemaji wa polisi Fred Enanga aliambia vyombo
vya habari kwamba wanasiasa hao wawili ndio waliopanga mashambulizi
na kufanya mikutano na vijana waliowasajili nje ya mji mkuu wa Kampala.
Bw Enanga aliongeza kuwa washambuliaji
waliahidiwa kulipwa pesa kufanya mashambulio.
Washukiwa kumi na waili wamekamatwa na
kushitakiwa kwa mauaji, huku wengine kumi na mmoja wakutarajiwa kufikishwa
mahamani baadaye wiki hii.
Aidha Bw Enanga alisema kuwa baadhi ya
washukiwa wamekiri kufanya mauaji na wanaisaidia polisi katika kuandaa mashitaka ya uhalifu.
Takriban watu 26 waliuawa na wengine
kujeruhiwa katika mashambulio yaliyofanywa na watu wenye mipanga tangu mwezi wa
Julai. Baadhi yao, ambao walikuwa ni wazee, wali katwa katwa katika nyumba zao majira yasaa mbili za asubuhi.
Eneo hilo limekuwa na wimbi la
mashambulio ya aina hiyo mara mbili katika kipindi cha muongo uliopita.
Kiongozi wa mapinduzi Guinea kuunda serikali mpya wiki zijazo
EPACopyright: EPA
Rais Apha Condé alikamatwa siku ya JumapiliImage caption: Rais Apha Condé alikamatwa siku ya Jumapili
Kiongozi wa mapinduzi yaliomuondoa mamlakani Rais wa Guinea Alpha Condé amesema kuwa serikali mpya ya ‘’Umoja’’
itaundwa katika kipindi cha wiki kadhaa.
Kanali Mamady Doumbouya amewaambia
mawaziri waliohudumu katika serikali ya Bw Condé's kwamba hakutakuwa na uonevu dhidi ya
maafisa wa zamani.
Rais Conde bado yumo kizuizini, lakini hatma
yake haijulikani.
Umoja wa Mataifa, Muungano
wa Afrika, na Jumuiya ya kikanda ya
Ecowas wamelaani mapinduzi na kutoa wito
wa kurejea kwa utawala wa kiraia.
"Ninalaani vikali
kuchukuliwa kokote kwa serikali kwa nguvu ya bunduki na kutoa wito wa
kuachiliwa mara moja kwa Rais Condé," ujumbe wa Twitter wa Katibumkuu wa Umoja wa mataifaAntonio Guterres ulieleza.
Baada ya saa kadhaa za
milio ya risasi Jumapili, mitaa ya mkji mkuu, Conakry,inaripotiwa kuwa kimya,
lakini bado haijajulikana iwapo kambi zote za kijeshi zinaunga mkono mapinduzi.
Kanali Doumbouya, ambaye anaongoza kikosi maalum cha jeshi, hakusema Jumatatu
ni lini serilai mpya itatangazwa.
" Mazungumzo
yataanzishwa ili kuandaa kwa mapana vigezo vya mpito, na halafu serikali ya
umoja itaanzishwa," alisema katika taarifa.Aliwaambia mawaziri wa zamani kuwa wasingeweza
kuondoka nchini na walilazimika kukabidhi magari yao ya kazi kwa jeshi.
AFPCopyright: AFP
Vijana walisherehekea mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea JumapiliImage caption: Vijana walisherehekea mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea Jumapili
Kanali Doumbouya pia ameyataka makampuni ya uchimbaji madini kuendelea na shuguli zao nchini, akiongeza kuwa wataruhusiwa kufanya kazi katika kipindi cha amri ya kutotoka nje usiku iliyowekwa kote nchini humo baada ya mapinduzi.
Guinea ni moja ya nchi zinazouza madini ya Boksiti, ambayo ni kiungo muhimu cha aluminiam. Kufuatia mapinduzi, bei za alminiam zilipanga kwa viwango vya juu kuwahi kushuhudiwa kwa muongo kutokana na hofu juu ya upatikanaji wake.
Mchezaji afariki baada ya kuwa katika koma kwa miaka 39
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Jean Pierre Adams aliichezea Ufaransa mara 22Image caption: Jean Pierre Adams aliichezea Ufaransa mara 22
Mchezaji wa zamani wa ufaransa Jean Pierre Adams , ambaye
alikuwa katika koma kwa miaka 39 amefariki akiwa na umri 73.
Adams alikuwa amelazwa hospitalini kufanyiwa upasuaji wa
goti lakemwezi machi 1982 lakini
hakupata tena ufahamubaada ya makosa ya
daktari aliyemdunga sindano ya kulała.
Akiwa mzaliwa wa Senegal , beki huyo alishiriki zaidi ya mechi
a140 akiicheze klabu ya Nicena pia
aliichezea klabu ya Paris St- Germain.
Katika Taarifa , PSG ilisema kwamba mchezo wa mchezaji huyo
unafaa kuheshimiwa.
Nice ilisema kwamba itamuomboleza Adams – ambaye aliichezea
Ufaransa mechi 22kati ya mwaka 1972
-1976 kabla mechi iliotarajiwa dhidi ya Monaco Novemba 19.
Adams pia aliichezea klabu ya Nimes 84 , ambayo ilisema
kwamba inatuma risala za rambirambikwa
familia ya mchezaji huyo.
Siku ambayo Adams alifanyiwa upasuaji baada ya kupata
jereha la goti lake – ambalo alipata wakati alipokuwa katika mazoezi – ambapo wafanyakazi
wengi wa hospitali katika klabu jiyo walikuwa katika mgomo.
Upasuaji wake ulifanyikahuku daktari anayehusika na kudunga sindano ya ganzi akihudumia wagonjwa
wengine watu wanane , ikiwemo Adams wakati huo mmoja.
Adams alisimamiwa na daktari aliyekuwa akijifunza ,
ambaye baadaye alisema: Sikuweza kazi niliopatiwa. Kati ya daktari huyo na mwanafunzi
wake , makosa kadhaa yalifanyika , na kumfanya Adams kupata mshtuko wa moyo na
kuharibika ubongo.
Ni hadi katikati ya mwaka 1990 ndiposa daktari wa sindano
za ganzi na mwanafunzi wake waliadhibiwa – wakisimamishwa kazi kwa mwezi mmoja
na kupigwa faini
Ya Yuro 750 .
Adams
alitolewa katika hospitali hiyo baada ya miezi 15 na alikuwa akiangaliwa
nyumbani Nimes na mkewe , Bernadettetangu wakati huo.
Rwanda yadai kutotumia fedha za Ufaransa katika Operesheni zake Msumbiji
ReutersCopyright: Reuters
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema taifa lake linajifadhili lenyewe katika operesheni zake za kijeshi nchini Msumbiji na kukanusha kufadhiliwa na Ufaransa au kampuni ya mafuta ya TotalEnergies.
Mwezi uliopita , askari wa Rwanda walilisaidia jeshi la Msumbiji kupambana na wanamgambo wa kiislamu katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.
“Tuna rasilimali nzuri ambazo tuko tayari kushirikiana na wengine. Hakuna ufadhili tunaopata sisi,” Rais Kagame alisema kwenye mahojiano na televisheni ya Rwandan Broadcasting Agency.
Akiwa anajibu swali kuhusu fedha alizowekeza katika miradi mikubwa ya gesi asilia katika maeneo yalioathiriwa ya Mkoa wa Cabo Delgado.
Rais Kagame amejibu pia kuhusu hatua za haraka zilizochukuliwa na Rwanda katika kupeleka vikundi vya kijeshi mapema kabla ya umoja wa nchi za kusini mwa Afrika-Sadc.
“Pale unapoona nyumba ya jirani inawaka moto yule anayeenda wa kwanza anaulizwa kwanini unaharakisha kwenda hii sehemu moto ukitokea?”
Amesema mpango wa kupeleka majeshi hauna uhusiano wowote na rasilimali zilizopo “ Ila ni kuhakikisha eneo lipo salama” na kuisaidia Msumbiji.
Ethiopian Airlines yajitetea dhidi ya tuhuma za usafirishaji silaha Sudan
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Shirika la ndege la Ethiopia limejitetea kuhusu tuhuma ya usafirishaji wa silaha nchini Sudan.
Shirika hilo la Ethiopia Airlines limesema kuwa shehena za silaha zilizosafirishwa nchini Sudan ni halali.
Shirika hilo limeijibu shirika la habari la nchini Sudan (Suna) baada ya kutoa taarifa ya kwamba mamlaka za Khartoum zimeanza kufanyia uchunguzi wa ujio wa masanduku 72 yaliokuwa yamehifadhi silaha na kusafirishwa na shirika la ndege la Ethiopia.
Masanduku hayo yameripotiwa kubeba silaha nzito za kivita pamoja na miwani ambayo hutumika zaidi usiku.
Taarifa iliyotolewa na shirika hilo inasema kuwa silaha walizosafirisha zilikuwa zinaenda kutumika kwa kazi ya uwindaji.
“Tunakila vithibitisho vya kuonesha kuwa silaha tulizosafirisha kuwa ni halali, ikiwemo barua kutoka kwenye Wizara ya mambo ya nchini Sudani.”
Kiongozi wa mapinduzi Guinea aahaidi serikali ya umoja
Kiongozi wa Guinea, Kanali Mahamady Doumbouya,amezungumza juu ya uelekeo wa taifa hilo mara baada ya kukutana na mawaziri wa serikali ya Rais Alpha.
Alisema:
Serikali ya umoja wa kitaifa itaundwa ndani ya wiki chache
Waziri yeyote wa serikali ya bwana Condé hatoruhusiwa kuondoka nchini humo na lazima wasalimishe hati zao za kusafiria
Kampuni za madini zinapaswa kuendelea na kazi na marufuku ya kutoka nje yameondolewa katika eneo lao la kazi
Hakutakuwa na kufuatilia mawaziri wa zamani na haki itatendeka
Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa na aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 inayomkabili Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe na wenzake watatu amejitoa kusikikiza kesi hiyo.
Mapema leo jijini Dar es Salaam, Mbowe akiwawakilisha wenzake watatu alimuomba Jaji Luvanda aliyekuwa akiendesha kesi hiyo ya ugaidi kujitoa kwa madai kuwa hawana imani naye na kwamba hatotenda haki.
Hata hivyo Jaji Luvanda alitangaza kujitoa kuisikiliza na kesi hiyo kuahirishwa ikisubiri jaji mwingine apangiwe.
Mbowe na wenzake walipofikishwa mahakamani leo, hatma ya mapingamizi yao dhidi ya hati ya mashtaka iliyotumika kuwafungulia kesi ya kula njama za kufanya ugaidi ilipata majibu huku ombi la moja likikataliwa.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alisema, “Mahakama imekataa pingamizi moja, na lingine wamelikubali kwa kiasi fulani na kusema kuwa upande wa mashataka wanapaswa kurekebishe kasoro.Hata hivyo hatujafurahi kwa sababu tulitaka mashtaka hayo yafutwe.”
Mbowe na wenzake watatu wanashikiliwa tangu Julai 21, wakikabiliwa na kesi ya ugaidi.
Awali serikali ya Ethiopia ilikanusha kuzuia misaada kuingia.
Wakala wa misaada ya kibinadamu wa Marekani alisema jeshi la Tigray liliweka uzio katika mji wa jirani wa Amhara.
Jasusi aliyetoweka azua mgawanyiko wa uongozi Somalia
SOCIAL MEDIACopyright: SOCIAL MEDIA
Kupotea kwa ajenti wa shirika la Kitaifa la Ujasusi na Usalama (Nisa) nchini Somalia mnamo Juni limesababisha mgawnayiko
ndani ya serikali baada ya rais na
waziri mkuu kutoa amri zinazokinzana.
Nisa ilisema wiki iliyopita kwamba Ikran Tahlil, ambaye alifanya kazi
katika idara ya usalama ya mtandao wa shirika hilo, aliuawa na kundi la
wanamgambo wa al-Shabab baada ya kumteka nyara kutoka mji mkuu Mogadishu.
Walakini, al-Shabab ilikana kuhusika katika
kutoweka kwa Tahlil na madai ya kumuua .
Waziri Mkuu Mohamed Roble alitoa taarifa ya
video mnamo 4 Septemba kusema kwamba maelezo ya shirika hilo la ujasusi juu ya
mwanamke huyo aliyepotea hayakuwa
"ya kuridhisha".
Siku moja baadaye, alitangaza kufutwa kazi
kwa mkurugenzi wa Nisa, Fahad Yasin, na kumteua Luteni Jenerali Bashir Mohamed
Jama'a kama mbadala wa muda.
Lakini Rais Mohamed Abdullahi Farmajo
alitupilia mbali agizo la waziri mkuu, akimwamuru mkuu wa upelelezi kubaki
ofisini, iliripoti Televisheni ya serikali.
Kesi ya ajenti huyo wa Nisa imeibua dhoruba la kisiasa nchini Somalia, huku wanasiasa wakilifanya
suala la kampeni katika uchaguzi unaoendelea na habari za kutoweka kwake
kusambaa sana kwenye mitandao ya kijamii
Wanajeshi wazidisha udhibiti wa madaraka baada ya kumtimua Alpha Condé
EPACopyright: EPA
Kikundi cha wanajeshi waliomwondoa Rais wa
Guinea Alpha Condé mamlakani Jumapili wameamuru baraza la mawaziri la nchi hiyo
kuhudhuria mkutano wa lazima Jumatatu.
Wale ambao wanakataa kuhudhuria mkutano huo
wa 11:00 GMT watachukuliwa kuwa waasi,
taarifa kwenye Televisheni ya serikali ilisema.
Rais Condé bado anazuiliwa, lakini hatima
yake haijulikani.
Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na
shirika la kikanda la Ecowas wamelaani mapinduzi hayo na kutoa wito wa
kurejeshwa kwa utawala wa raia.
"Ninalaani vikali kuchukuliwa kwa
serikali kwa nguvu ya bunduki na nataka kuachiliwa mara moja kwa Rais Alpha
Conde," katibu mkuu wa UN António Guterres alisema kupitia twitter
Askari walitangaza kuvunjwa kwa katiba,
kufungwa kwa mipaka na amri ya kutotoka nje nchi nzima.
Katika matangazo kwenye Televisheni ya
serikali Jumapili usiku, walisema magavana wa mikoa walikuwa wamebadilishwa na
nafasi zao kuchukuliwa na makamanda wa
jeshi, na rais aliye na umri wa miaka 83
aliyeondolewa madarakani alikuwa salama
lakini amezuiliwa
Mkuu wa vikosi maalum vya nchi hiyo, Kanali
Mamady Doumbouya, alisema wanajeshi wake wamechukua madaraka kwa sababu
wanataka kumaliza ufisadi uliokithiri na usimamizi mbaya.
Rais Condé alichaguliwa tena kwa kipindi
cha tatu kwa njia ya utata katika hatua iliyozua maandamano mwaka jana .
Kiongozi huyo mkongwe wa upinzani
alichaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo 2010 . Licha ya kusimamia maendeleo
kadhaa ya kiuchumi, amekuwa akituhumiwa kwa kusimamia ukiukwaji mwingi wa haki
za binadamu na unyanyasaji wa wakosoaji wake.
Marekani yalaani kuondolewa madarakani kwa rais Guinea
Marekani imetoa taarifa ya kulaani vikali mapinduzi yaliyotokea Guinea.
Taarifa hiyo imevitaka vyama vya siasa kuacha ghasia na kufuata sheria.
Marekani imesema kuwa ghasia na hatua zozote zile zilizopo nje ya katiba zitaathiri ustawi wa Guinea, amani na utulivu.
Aidha wamesisitiza kuwa midahalo ya kitaifa inapaswa kuwa ya wazi na inayolenga kupata suluhu ya demokrasia na amani.
Taarifa hiyo imekuja na taarifa nyingine za kimataifa kukemea kupinduliwa kwa rais Alpha Condé.
Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi, Ecowas, ililaani "jaribio la mapinduzi" na ikathibitisha "kutokubali mabadiliko yoyote ya kisiasa yanayopingana na katiba".
Imetaka rais Condé aheshimiwe na wale wote waliokamatwa pamoja naye waachiwe huru.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Umoja wa Afrika tayari wameshutumu mapinduzi hayo na kutaka Rais Condé aachiwe huru.
Hatima ya rais huyo bado haijawekwa wazi baada ya video ambayo haijathibitishwa kuonesha Rais akiwa amezungukwa na askari ambao wanadai wamechukua mamlaka ya nchi.
Hata hivyo wizara ya usalama ilisema jaribio hilo la mapinduzi
‘Tutarejea Afghanistan’ Seneta wa Marekani Lindsey Graham
ReutersCopyright: Reuters
Seneta wa chama cha Republican nchini Marekani Lindsey Graham ameambia BBC kwamba anaamini
wanajeshi wa Marekani "watarudi
Afghanistan" katika siku zijazo.
Akiongea kwenye HARDtalk, alisema:
"Itabidi kwa sababu tishio [la ugaidi] litakuwa kubwa sana."
Vikosi vya mwisho vya Marekani viliondoka
Afghanistan wiki moja iliyopita baada ya miaka 20 nchini humo .
Hata hivyo kauli yake hiyo inakinzana na
msimamo wa rais Joe Biden aliyesema kwamba wakati ulikuwa umewadia kwa Marekani
na washirika wake kuondoka Afghanistan .
Uamuzi wa kuyandoa majeshi ya nchi hiyo
katikia taifa hilo umepokelewa kwa hisia mseto hasa baada ya kundi la Taliban
kuizidi nguvu serikali iliyokuwa ikiungwa mkono na nchi za Magharini na kuingia
Kabul tarehe 15 Agosti na inatarajiwa kuunda serikali mpya .
Marekani pia ilikamilisha oparesheni ya
kuwaondoa raia wake na raia wa afghani walioshirikiana na vikosi vyake ingawaje
wengine maelfu waliachwa nyuma na kuna hofu wataadhibiwa na kundi la Taliban
Mtoto wa miaka mitatu aliyepotea porini apatikana baada ya siku nne
Mtoto wa miaka mitatu ambaye alipotea porini nchini Australia amepatikana akiwa mzima baada ya kutafutwa kwa kipindi cha siku nne.
Anthony "AJ" Elfalak alionekana na helikopta ya polisi siku ya Jumatatu , akiwa anakunywa maji katika kijito kidogo ndani ya shamba la familia yake lililopo kijijini huko New South Wales.
Mtoto huyo mdogo wa kiume, ambaye ana matatizo ya usonji na hawezi kuongea alikuwa amepotea nyumbani kwao tangu Ijumaa.
Wazazi wake walikuwa wanahofia labda alikuwa ametekwa.
Lakini timu ya uokoaji ilimkuta AJ katika mkondo wa mto ambao uko mita 500 kutoka nyumbani kwao.
Video iliyosambaa mtandaoni inasikika polisi wakisema wamempata mtoto/
Mamlaka imesema AJ ana majeraha kidogo mguuni ila ana afya njema.
Baba yake , Anthony Elfalak, ameita jambo hilo kuwa muujiza.
Kenya yapokea zaidi ya dozi laki 8 za Moderna
BBCCopyright: BBC
Kenya imepokea dozi nyingine 880,320 za chanjo ya Moderna.
Hii ni awamu ya pili ya dozi milioni 1.76 zilizotolewa na serikali ya Marekani nchini Kenya , kupitia kituo cha Covax.
Chanjo hizo zimewasili nchini Kenya Jumatatu asubuhi.
"Kundi la 2 la dozi 880,320 za chanjo ya Moderna # COVID19 imewasili Kenya leo asubuhi. Msaada wa Serikali ya Marekani kupitia #COVAX," WHO Kenya iliandika ujumbe kwenye tweeter.
Kundi la kwanza la chanjo 880,460 za Moderna ziliwasili nchini Jumatatu, Agosti 23, 2021.
Hatua hii inakuja kama kichocheo katika kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.
Kenya sasa ina kipimo cha chanjo 2,284, 292 ambazo zinapatikana kwa matibabu.
Ijumaa ya wiki iliyopita, Kenya ilipokea kundi la kwanza la chanjo moja ya Johnson Johnson Covid-19.
Daktari asimamishwa kazi kwa kumfumua mgonjwa nyuzi
Munira Hussein
BBC Africa
BBCCopyright: BBC
Daktari mmoja nchini Tanzania amesimamishwa kazi kwa kumfumua nyuzi mgonjwa kisa alishindwa kulipia matibabu.
Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii imemuonesha daktari mmoja akilalamikiwa na kiongozi wa Kijiji kwa kumfumua nyuzi mgonjwa mara baada ya kumshona, kisa mgonjwa huyo alishindwa kulipa gharama za matibabu hayo.
Baadaye daktari huyo alitambuliwa kama Jackson Meli kutoka katika kituo cha afya Kerenge, Mkoani Tanga.
Awali mamlaka nchini Tanzania iliomba taarifa za kuweza kumtambua daktari huyo kupitia mitandao ya kijamii.
Mgonjwa ambaye anaoenakana kwenye video hiyo alikuwa ameshonwa katika upande wa juu wa mkono na baadaye kufumuliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi alikemea kitendo hicho na kusema kuwa tayari hatua za kinidhamu zimechukuliwa na taarifa zake zimefikishwa kwenye baraza la matabibu.
‘’Jambo hili lilitokea toka tarehe 28 mwezi wa saba na alikamatwa mara moja na kuwekwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, na alisimamishwa kazi na halmashauri na taarifa zake zimewasilishwa kwenye baraza la matabibu la Tanzania’’ anasema Mwanukuzi.
Chama cha madkatari Tanzania kimekemea pia tukio hilo, katika taarifa iliyotolewa leo na kusisitiza hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.
Mtoto wa Gaddafi aachiwa huru
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Mtoto wa tatu wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, ameachiwa huru kutoka jela ya mji mkuu wa Tripoli, ambako alikuwa amefungwa tangu mwaka 2014.
Sa'adi Gaddafi alikuwa kamanda wa kikosi maalum cha Libya lakini pia alikuwa maarufu katika uchezaji wa kandanda nchini Italia.
Alikimbilia Niger wakati baba yake alivyopinduliwa na kuuliwa mwaka 2011 lakini alirudishwa Libya ambako alikutwa hana hatia dhidi ya kesi zote zilizomkabili yakiwemo madai ya mauaji.
Muda mfupi baada ya kuachiwa huru bwana Gaddafi alikodisha ndege binafsi na kwenda Istanbul.
Serikali ya Libya imetoa taarifa kuwa walikuwa wana matumaini kuwa kuachiwa kwake kutaweza kusaidia taifa hilo kufikia katika makubaliano.
Bondia wa Tanzania Mwakinyo apanda ngazi ya ubora duniani
Munira Hussein
BBC Africa
Mwakinyo -TwitterCopyright: Mwakinyo -Twitter
Bondia wa Tanzania Hythani Hamza Halfan ama maarufu kama Hassan Mwakinyo wa uzito wa Super Welter amepanda kutoka nafasi ya 24 hadi nafasi ya 13 katika viwango vya ubora duniani huku akiwa namba moja Afrika.
Mwakinyo anashikilia ubingwa wa Afrika (ABU) kwa uzito wa super welter.
Mwishoni mwa juma alitetea ubingwa wake kwa kumpiga Julius Indongo kutoka Namibia.
Twitter-MwakinyoCopyright: Twitter-Mwakinyo
'Alhamdulillah, Tumepanda tena. Nimepanda hadi nafasi ya 13 kwenye viwango vya ubora duniani kutoka nafasi ya 24.
Na Nimeendelea kuwa Bingwa Wa ABU Na Bondia Namba 1 Africa’’ aliandika Mwakinyo katika ukurasa wake wa Twitter. Hassan Mwakinyo alijosa katika ulingo wa ngumi za kulipwa tangu mwaka 2015, na amewahi kushikilia mikanda kadhaa ya ubingwa ikiwemo ubingwa wa WBA pan African.
Taliban yadai kudhibiti Bonde la Panjshir
ReutersCopyright: Reuters
Taliban inadai sasa inadhibiti kabisa jimbo
la Panjshir la Afghanistan, sehemu ya mwisho kupinga utawala wake.
Kumekuwa na mapigano makali katika eneo
hilo kaskazini mwa mji mkuu Kabul, na kundi
la (NRF) limekuwa mstari wa mbele kupinga utawala wa Taliban.
"Pamoja na ushindi huu, nchi yetu
imeondolewa kabisa kwenye tishio la vita," msemaji wa Taliban alisema.
Hata hivyo , NRF imekana kushindwa na
Taliban
"Sio kweli, Taliban hawajadhibiti Panjshir
ninakataa madai ya Taliban," msemaji wa NRF Ali Maisam aliambia BBC.
Taliban ilichukua udhibiti wa Afghanistan
yote wiki tatu zilizopita, ikichukua mamlaka huko Kabul mnamo Agosti 15
kufuatia kuanguka kwa serikali inayoungwa mkono na nchi za Magharibi.
Habari za moja kwa moja
time_stated_uk
Kufikia hapo tunafika tamati ya habari zetu hii leo, tukutane kesho
wanaume milioni 1.5 kutahiriwa Sudan katika kampeni dhidi ya HIV
Mradi wa kuwatahiri wanaume milioni 1.5 wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 49 Suimeanzishwa nchini Sudan Kusini ili kupunguza uwezekano wa kuambukiza virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi.
Utafiti unaonesha kuwa wanaume waliotahiriwa wana hatari ya chini ya kuambukizwa virusi vya HIV kuliko wanaume ambao hawajatahiriwa wanafanya tendo la ngono na mtu wa jinsia tofautimwenye virusi hivyo.
Shirika lisilo la kiserikali la Human Appeal Associates, kwa ushirikiano na wizara ya afya ya nchi hiyo, watawatafuta wanaume watakaojitolea kutahiriwa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Majimbo matatu pekee kati ya 10 ndio yenye utamaduni wa kutahiri, nan je ya majimbo hayo kutahiri ni mwiko.
Serikali imeelezea viwango vya chini vya kutahiri kama hofu kuu ya afya ya umma inapokuja katika suala la kukabiliana na HIV nchini Sudan Kusini.
“Viwango vya wanaohitaji kutahiriwa katika mji mkuu Juba pekee ni vya juu sana," Robert Matthew Uku, kutoka shirika la from Human Appeal Associates, ameiambia BBC.
Wabunge wa upinzani Uganda wahojiwa kuhusu mauaji ya kikatili
Wabunge wawili wa Uganda kutoka chama cha upinzani cha National Unity Platform leo wamefika mbele ya idara ya uchunguzi wa jinai ili kujibu maswali, kuhusu wimbi la hivi karibuni la mauaji katika jimbo la kati la masaka.
Maafisa wa polisi walikizunguka kituo cha polisi ambacho viongozi hao walikuwa wanahojiwa. Wawili hao waliombwa mbele kufika mbele ya maafisa wa polisi wiki iliopita.
Msemaji wa polisi Fred Enanga aliambia vyombo vya habari kwamba wanasiasa hao wawili ndio waliopanga mashambulizi na kufanya mikutano na vijana waliowasajili nje ya mji mkuu wa Kampala.
Bw Enanga aliongeza kuwa washambuliaji waliahidiwa kulipwa pesa kufanya mashambulio.
Washukiwa kumi na waili wamekamatwa na kushitakiwa kwa mauaji, huku wengine kumi na mmoja wakutarajiwa kufikishwa mahamani baadaye wiki hii.
Aidha Bw Enanga alisema kuwa baadhi ya washukiwa wamekiri kufanya mauaji na wanaisaidia polisi katika kuandaa mashitaka ya uhalifu.
Takriban watu 26 waliuawa na wengine kujeruhiwa katika mashambulio yaliyofanywa na watu wenye mipanga tangu mwezi wa Julai. Baadhi yao, ambao walikuwa ni wazee, wali katwa katwa katika nyumba zao majira yasaa mbili za asubuhi.
Eneo hilo limekuwa na wimbi la mashambulio ya aina hiyo mara mbili katika kipindi cha muongo uliopita.
Kiongozi wa mapinduzi Guinea kuunda serikali mpya wiki zijazo
Kiongozi wa mapinduzi yaliomuondoa mamlakani Rais wa Guinea Alpha Condé amesema kuwa serikali mpya ya ‘’Umoja’’ itaundwa katika kipindi cha wiki kadhaa.
Kanali Mamady Doumbouya amewaambia mawaziri waliohudumu katika serikali ya Bw Condé's kwamba hakutakuwa na uonevu dhidi ya maafisa wa zamani.
Rais Conde bado yumo kizuizini, lakini hatma yake haijulikani.
Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, na Jumuiya ya kikanda ya Ecowas wamelaani mapinduzi na kutoa wito wa kurejea kwa utawala wa kiraia.
"Ninalaani vikali kuchukuliwa kokote kwa serikali kwa nguvu ya bunduki na kutoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa Rais Condé," ujumbe wa Twitter wa Katibumkuu wa Umoja wa mataifaAntonio Guterres ulieleza.
Baada ya saa kadhaa za milio ya risasi Jumapili, mitaa ya mkji mkuu, Conakry,inaripotiwa kuwa kimya, lakini bado haijajulikana iwapo kambi zote za kijeshi zinaunga mkono mapinduzi.
Kanali Doumbouya, ambaye anaongoza kikosi maalum cha jeshi, hakusema Jumatatu ni lini serilai mpya itatangazwa.
" Mazungumzo yataanzishwa ili kuandaa kwa mapana vigezo vya mpito, na halafu serikali ya umoja itaanzishwa," alisema katika taarifa.Aliwaambia mawaziri wa zamani kuwa wasingeweza kuondoka nchini na walilazimika kukabidhi magari yao ya kazi kwa jeshi.
Kanali Doumbouya pia ameyataka makampuni ya uchimbaji madini kuendelea na shuguli zao nchini, akiongeza kuwa wataruhusiwa kufanya kazi katika kipindi cha amri ya kutotoka nje usiku iliyowekwa kote nchini humo baada ya mapinduzi.
Guinea ni moja ya nchi zinazouza madini ya Boksiti, ambayo ni kiungo muhimu cha aluminiam. Kufuatia mapinduzi, bei za alminiam zilipanga kwa viwango vya juu kuwahi kushuhudiwa kwa muongo kutokana na hofu juu ya upatikanaji wake.
Mchezaji afariki baada ya kuwa katika koma kwa miaka 39
Mchezaji wa zamani wa ufaransa Jean Pierre Adams , ambaye alikuwa katika koma kwa miaka 39 amefariki akiwa na umri 73.
Adams alikuwa amelazwa hospitalini kufanyiwa upasuaji wa goti lakemwezi machi 1982 lakini hakupata tena ufahamubaada ya makosa ya daktari aliyemdunga sindano ya kulała.
Akiwa mzaliwa wa Senegal , beki huyo alishiriki zaidi ya mechi a140 akiicheze klabu ya Nicena pia aliichezea klabu ya Paris St- Germain.
Katika Taarifa , PSG ilisema kwamba mchezo wa mchezaji huyo unafaa kuheshimiwa.
Nice ilisema kwamba itamuomboleza Adams – ambaye aliichezea Ufaransa mechi 22kati ya mwaka 1972 -1976 kabla mechi iliotarajiwa dhidi ya Monaco Novemba 19.
Adams pia aliichezea klabu ya Nimes 84 , ambayo ilisema kwamba inatuma risala za rambirambikwa familia ya mchezaji huyo.
Siku ambayo Adams alifanyiwa upasuaji baada ya kupata jereha la goti lake – ambalo alipata wakati alipokuwa katika mazoezi – ambapo wafanyakazi wengi wa hospitali katika klabu jiyo walikuwa katika mgomo.
Upasuaji wake ulifanyikahuku daktari anayehusika na kudunga sindano ya ganzi akihudumia wagonjwa wengine watu wanane , ikiwemo Adams wakati huo mmoja.
Adams alisimamiwa na daktari aliyekuwa akijifunza , ambaye baadaye alisema: Sikuweza kazi niliopatiwa. Kati ya daktari huyo na mwanafunzi wake , makosa kadhaa yalifanyika , na kumfanya Adams kupata mshtuko wa moyo na kuharibika ubongo.
Ni hadi katikati ya mwaka 1990 ndiposa daktari wa sindano za ganzi na mwanafunzi wake waliadhibiwa – wakisimamishwa kazi kwa mwezi mmoja na kupigwa faini
Ya Yuro 750 .
Adams alitolewa katika hospitali hiyo baada ya miezi 15 na alikuwa akiangaliwa nyumbani Nimes na mkewe , Bernadettetangu wakati huo.
Rwanda yadai kutotumia fedha za Ufaransa katika Operesheni zake Msumbiji
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema taifa lake linajifadhili lenyewe katika operesheni zake za kijeshi nchini Msumbiji na kukanusha kufadhiliwa na Ufaransa au kampuni ya mafuta ya TotalEnergies.
Mwezi uliopita , askari wa Rwanda walilisaidia jeshi la Msumbiji kupambana na wanamgambo wa kiislamu katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.
“Tuna rasilimali nzuri ambazo tuko tayari kushirikiana na wengine. Hakuna ufadhili tunaopata sisi,” Rais Kagame alisema kwenye mahojiano na televisheni ya Rwandan Broadcasting Agency.
Akiwa anajibu swali kuhusu fedha alizowekeza katika miradi mikubwa ya gesi asilia katika maeneo yalioathiriwa ya Mkoa wa Cabo Delgado.
Rais Kagame amejibu pia kuhusu hatua za haraka zilizochukuliwa na Rwanda katika kupeleka vikundi vya kijeshi mapema kabla ya umoja wa nchi za kusini mwa Afrika-Sadc.
“Pale unapoona nyumba ya jirani inawaka moto yule anayeenda wa kwanza anaulizwa kwanini unaharakisha kwenda hii sehemu moto ukitokea?”
Amesema mpango wa kupeleka majeshi hauna uhusiano wowote na rasilimali zilizopo “ Ila ni kuhakikisha eneo lipo salama” na kuisaidia Msumbiji.
Ethiopian Airlines yajitetea dhidi ya tuhuma za usafirishaji silaha Sudan
Shirika la ndege la Ethiopia limejitetea kuhusu tuhuma ya usafirishaji wa silaha nchini Sudan.
Shirika hilo la Ethiopia Airlines limesema kuwa shehena za silaha zilizosafirishwa nchini Sudan ni halali.
Shirika hilo limeijibu shirika la habari la nchini Sudan (Suna) baada ya kutoa taarifa ya kwamba mamlaka za Khartoum zimeanza kufanyia uchunguzi wa ujio wa masanduku 72 yaliokuwa yamehifadhi silaha na kusafirishwa na shirika la ndege la Ethiopia.
Masanduku hayo yameripotiwa kubeba silaha nzito za kivita pamoja na miwani ambayo hutumika zaidi usiku.
Taarifa iliyotolewa na shirika hilo inasema kuwa silaha walizosafirisha zilikuwa zinaenda kutumika kwa kazi ya uwindaji.
“Tunakila vithibitisho vya kuonesha kuwa silaha tulizosafirisha kuwa ni halali, ikiwemo barua kutoka kwenye Wizara ya mambo ya nchini Sudani.”
Kiongozi wa mapinduzi Guinea aahaidi serikali ya umoja
Kiongozi wa Guinea, Kanali Mahamady Doumbouya,amezungumza juu ya uelekeo wa taifa hilo mara baada ya kukutana na mawaziri wa serikali ya Rais Alpha.
Alisema:
Mapinduzi ya Guinea:Rais Alpha Condé akamatwa na jeshi linalodai kuchukua madaraka
Jaji ajiondoa kesi ya Mbowe
Alfred Lasteck
BBC News, Dar es Salaam
Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa na aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 inayomkabili Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe na wenzake watatu amejitoa kusikikiza kesi hiyo.
Mapema leo jijini Dar es Salaam, Mbowe akiwawakilisha wenzake watatu alimuomba Jaji Luvanda aliyekuwa akiendesha kesi hiyo ya ugaidi kujitoa kwa madai kuwa hawana imani naye na kwamba hatotenda haki.
Hata hivyo Jaji Luvanda alitangaza kujitoa kuisikiliza na kesi hiyo kuahirishwa ikisubiri jaji mwingine apangiwe.
Mbowe na wenzake walipofikishwa mahakamani leo, hatma ya mapingamizi yao dhidi ya hati ya mashtaka iliyotumika kuwafungulia kesi ya kula njama za kufanya ugaidi ilipata majibu huku ombi la moja likikataliwa.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alisema, “Mahakama imekataa pingamizi moja, na lingine wamelikubali kwa kiasi fulani na kusema kuwa upande wa mashataka wanapaswa kurekebishe kasoro.Hata hivyo hatujafurahi kwa sababu tulitaka mashtaka hayo yafutwe.” Mbowe na wenzake watatu wanashikiliwa tangu Julai 21, wakikabiliwa na kesi ya ugaidi.
Hatimaye msaada wa vyakula wa UN umeweza kuwasili Tigray
Zaidi ya maroli 100 ya chakula yamewasili Ethiopia, eneo la Tigray baada ya wiki kadhaa za kufungiwa kuingia,Shirika la Chakula Duniani (WFP).
Kulikuwa na ugumu kwa misaada kuingia katika eneo hilo.
Tigray imekuwa katika mgogoro kwa kipindi cha miezi 10-na serikali ya shirikisho.
WFP imeweka video kwenye tweeter kuonesha jinsi misaada inavyoingia katika mji mkuu wa Tigray, Mekelle;
Awali serikali ya Ethiopia ilikanusha kuzuia misaada kuingia.
Wakala wa misaada ya kibinadamu wa Marekani alisema jeshi la Tigray liliweka uzio katika mji wa jirani wa Amhara.
Jasusi aliyetoweka azua mgawanyiko wa uongozi Somalia
Kupotea kwa ajenti wa shirika la Kitaifa la Ujasusi na Usalama (Nisa) nchini Somalia mnamo Juni limesababisha mgawnayiko ndani ya serikali baada ya rais na waziri mkuu kutoa amri zinazokinzana.
Nisa ilisema wiki iliyopita kwamba Ikran Tahlil, ambaye alifanya kazi katika idara ya usalama ya mtandao wa shirika hilo, aliuawa na kundi la wanamgambo wa al-Shabab baada ya kumteka nyara kutoka mji mkuu Mogadishu.
Walakini, al-Shabab ilikana kuhusika katika kutoweka kwa Tahlil na madai ya kumuua .
Waziri Mkuu Mohamed Roble alitoa taarifa ya video mnamo 4 Septemba kusema kwamba maelezo ya shirika hilo la ujasusi juu ya mwanamke huyo aliyepotea hayakuwa "ya kuridhisha".
Siku moja baadaye, alitangaza kufutwa kazi kwa mkurugenzi wa Nisa, Fahad Yasin, na kumteua Luteni Jenerali Bashir Mohamed Jama'a kama mbadala wa muda.
Lakini Rais Mohamed Abdullahi Farmajo alitupilia mbali agizo la waziri mkuu, akimwamuru mkuu wa upelelezi kubaki ofisini, iliripoti Televisheni ya serikali.
Kesi ya ajenti huyo wa Nisa imeibua dhoruba la kisiasa nchini Somalia, huku wanasiasa wakilifanya suala la kampeni katika uchaguzi unaoendelea na habari za kutoweka kwake kusambaa sana kwenye mitandao ya kijamii
Wanajeshi wazidisha udhibiti wa madaraka baada ya kumtimua Alpha Condé
Kikundi cha wanajeshi waliomwondoa Rais wa Guinea Alpha Condé mamlakani Jumapili wameamuru baraza la mawaziri la nchi hiyo kuhudhuria mkutano wa lazima Jumatatu.
Wale ambao wanakataa kuhudhuria mkutano huo wa 11:00 GMT watachukuliwa kuwa waasi, taarifa kwenye Televisheni ya serikali ilisema.
Rais Condé bado anazuiliwa, lakini hatima yake haijulikani.
Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na shirika la kikanda la Ecowas wamelaani mapinduzi hayo na kutoa wito wa kurejeshwa kwa utawala wa raia.
"Ninalaani vikali kuchukuliwa kwa serikali kwa nguvu ya bunduki na nataka kuachiliwa mara moja kwa Rais Alpha Conde," katibu mkuu wa UN António Guterres alisema kupitia twitter
Askari walitangaza kuvunjwa kwa katiba, kufungwa kwa mipaka na amri ya kutotoka nje nchi nzima.
Katika matangazo kwenye Televisheni ya serikali Jumapili usiku, walisema magavana wa mikoa walikuwa wamebadilishwa na nafasi zao kuchukuliwa na makamanda wa jeshi, na rais aliye na umri wa miaka 83 aliyeondolewa madarakani alikuwa salama lakini amezuiliwa
Mkuu wa vikosi maalum vya nchi hiyo, Kanali Mamady Doumbouya, alisema wanajeshi wake wamechukua madaraka kwa sababu wanataka kumaliza ufisadi uliokithiri na usimamizi mbaya.
Rais Condé alichaguliwa tena kwa kipindi cha tatu kwa njia ya utata katika hatua iliyozua maandamano mwaka jana .
Kiongozi huyo mkongwe wa upinzani alichaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo 2010 . Licha ya kusimamia maendeleo kadhaa ya kiuchumi, amekuwa akituhumiwa kwa kusimamia ukiukwaji mwingi wa haki za binadamu na unyanyasaji wa wakosoaji wake.
Mapinduzi Guinea:Mfahamu Kanali Mamady Doumbouya, kiongozi wa mapinduzi nchini Guinea
Mapinduzi ya Guinea:Rais Alpha Condé akamatwa na jeshi linalodai kuchukua madaraka
Marekani yalaani kuondolewa madarakani kwa rais Guinea
Marekani imetoa taarifa ya kulaani vikali mapinduzi yaliyotokea Guinea.
Taarifa hiyo imevitaka vyama vya siasa kuacha ghasia na kufuata sheria.
Marekani imesema kuwa ghasia na hatua zozote zile zilizopo nje ya katiba zitaathiri ustawi wa Guinea, amani na utulivu.
Aidha wamesisitiza kuwa midahalo ya kitaifa inapaswa kuwa ya wazi na inayolenga kupata suluhu ya demokrasia na amani.
Taarifa hiyo imekuja na taarifa nyingine za kimataifa kukemea kupinduliwa kwa rais Alpha Condé.
Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi, Ecowas, ililaani "jaribio la mapinduzi" na ikathibitisha "kutokubali mabadiliko yoyote ya kisiasa yanayopingana na katiba".
Imetaka rais Condé aheshimiwe na wale wote waliokamatwa pamoja naye waachiwe huru.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Umoja wa Afrika tayari wameshutumu mapinduzi hayo na kutaka Rais Condé aachiwe huru.
Hatima ya rais huyo bado haijawekwa wazi baada ya video ambayo haijathibitishwa kuonesha Rais akiwa amezungukwa na askari ambao wanadai wamechukua mamlaka ya nchi.
Hata hivyo wizara ya usalama ilisema jaribio hilo la mapinduzi
liliweza kuzuiwa na walinzi wa rais.
‘Tutarejea Afghanistan’ Seneta wa Marekani Lindsey Graham
Seneta wa chama cha Republican nchini Marekani Lindsey Graham ameambia BBC kwamba anaamini wanajeshi wa Marekani "watarudi Afghanistan" katika siku zijazo.
Akiongea kwenye HARDtalk, alisema: "Itabidi kwa sababu tishio [la ugaidi] litakuwa kubwa sana."
Vikosi vya mwisho vya Marekani viliondoka Afghanistan wiki moja iliyopita baada ya miaka 20 nchini humo .
Hata hivyo kauli yake hiyo inakinzana na msimamo wa rais Joe Biden aliyesema kwamba wakati ulikuwa umewadia kwa Marekani na washirika wake kuondoka Afghanistan .
Uamuzi wa kuyandoa majeshi ya nchi hiyo katikia taifa hilo umepokelewa kwa hisia mseto hasa baada ya kundi la Taliban kuizidi nguvu serikali iliyokuwa ikiungwa mkono na nchi za Magharini na kuingia Kabul tarehe 15 Agosti na inatarajiwa kuunda serikali mpya .
Marekani pia ilikamilisha oparesheni ya kuwaondoa raia wake na raia wa afghani walioshirikiana na vikosi vyake ingawaje wengine maelfu waliachwa nyuma na kuna hofu wataadhibiwa na kundi la Taliban
Mtoto wa miaka mitatu aliyepotea porini apatikana baada ya siku nne
Mtoto wa miaka mitatu ambaye alipotea porini nchini Australia amepatikana akiwa mzima baada ya kutafutwa kwa kipindi cha siku nne.
Anthony "AJ" Elfalak alionekana na helikopta ya polisi siku ya Jumatatu , akiwa anakunywa maji katika kijito kidogo ndani ya shamba la familia yake lililopo kijijini huko New South Wales.
Mtoto huyo mdogo wa kiume, ambaye ana matatizo ya usonji na hawezi kuongea alikuwa amepotea nyumbani kwao tangu Ijumaa.
Wazazi wake walikuwa wanahofia labda alikuwa ametekwa.
Lakini timu ya uokoaji ilimkuta AJ katika mkondo wa mto ambao uko mita 500 kutoka nyumbani kwao.
Video iliyosambaa mtandaoni inasikika polisi wakisema wamempata mtoto/
Mamlaka imesema AJ ana majeraha kidogo mguuni ila ana afya njema.
Baba yake , Anthony Elfalak, ameita jambo hilo kuwa muujiza.
Kenya yapokea zaidi ya dozi laki 8 za Moderna
Kenya imepokea dozi nyingine 880,320 za chanjo ya Moderna.
Hii ni awamu ya pili ya dozi milioni 1.76 zilizotolewa na serikali ya Marekani nchini Kenya , kupitia kituo cha Covax.
Chanjo hizo zimewasili nchini Kenya Jumatatu asubuhi. "Kundi la 2 la dozi 880,320 za chanjo ya Moderna # COVID19 imewasili Kenya leo asubuhi. Msaada wa Serikali ya Marekani kupitia #COVAX," WHO Kenya iliandika ujumbe kwenye tweeter.
Kundi la kwanza la chanjo 880,460 za Moderna ziliwasili nchini Jumatatu, Agosti 23, 2021. Hatua hii inakuja kama kichocheo katika kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.
Kenya sasa ina kipimo cha chanjo 2,284, 292 ambazo zinapatikana kwa matibabu.
Ijumaa ya wiki iliyopita, Kenya ilipokea kundi la kwanza la chanjo moja ya Johnson Johnson Covid-19.
Daktari asimamishwa kazi kwa kumfumua mgonjwa nyuzi
Munira Hussein
BBC Africa
Daktari mmoja nchini Tanzania amesimamishwa kazi kwa kumfumua nyuzi mgonjwa kisa alishindwa kulipia matibabu.
Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii imemuonesha daktari mmoja akilalamikiwa na kiongozi wa Kijiji kwa kumfumua nyuzi mgonjwa mara baada ya kumshona, kisa mgonjwa huyo alishindwa kulipa gharama za matibabu hayo.
Baadaye daktari huyo alitambuliwa kama Jackson Meli kutoka katika kituo cha afya Kerenge, Mkoani Tanga.
Awali mamlaka nchini Tanzania iliomba taarifa za kuweza kumtambua daktari huyo kupitia mitandao ya kijamii. Mgonjwa ambaye anaoenakana kwenye video hiyo alikuwa ameshonwa katika upande wa juu wa mkono na baadaye kufumuliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi alikemea kitendo hicho na kusema kuwa tayari hatua za kinidhamu zimechukuliwa na taarifa zake zimefikishwa kwenye baraza la matabibu. ‘’Jambo hili lilitokea toka tarehe 28 mwezi wa saba na alikamatwa mara moja na kuwekwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, na alisimamishwa kazi na halmashauri na taarifa zake zimewasilishwa kwenye baraza la matabibu la Tanzania’’ anasema Mwanukuzi.
Chama cha madkatari Tanzania kimekemea pia tukio hilo, katika taarifa iliyotolewa leo na kusisitiza hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.
Mtoto wa Gaddafi aachiwa huru
Mtoto wa tatu wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, ameachiwa huru kutoka jela ya mji mkuu wa Tripoli, ambako alikuwa amefungwa tangu mwaka 2014.
Sa'adi Gaddafi alikuwa kamanda wa kikosi maalum cha Libya lakini pia alikuwa maarufu katika uchezaji wa kandanda nchini Italia.
Alikimbilia Niger wakati baba yake alivyopinduliwa na kuuliwa mwaka 2011 lakini alirudishwa Libya ambako alikutwa hana hatia dhidi ya kesi zote zilizomkabili yakiwemo madai ya mauaji.
Muda mfupi baada ya kuachiwa huru bwana Gaddafi alikodisha ndege binafsi na kwenda Istanbul.
Serikali ya Libya imetoa taarifa kuwa walikuwa wana matumaini kuwa kuachiwa kwake kutaweza kusaidia taifa hilo kufikia katika makubaliano.
Muammar Gaddafi :Miaka 10 baadaye Walibya wana majuto?
Fahamu ukweli kuhusu kikosi cha wanawake pekee kilichokuwa kikimlinda Muammar Gaddafi
Libya: Mtoto wa Gaddafi Saif al-Islam yuko hai ataka kuongoza Libya
Bondia wa Tanzania Mwakinyo apanda ngazi ya ubora duniani
Munira Hussein
BBC Africa
Bondia wa Tanzania Hythani Hamza Halfan ama maarufu kama Hassan Mwakinyo wa uzito wa Super Welter amepanda kutoka nafasi ya 24 hadi nafasi ya 13 katika viwango vya ubora duniani huku akiwa namba moja Afrika.
Mwakinyo anashikilia ubingwa wa Afrika (ABU) kwa uzito wa super welter.
Mwishoni mwa juma alitetea ubingwa wake kwa kumpiga Julius Indongo kutoka Namibia.
'Alhamdulillah, Tumepanda tena. Nimepanda hadi nafasi ya 13 kwenye viwango vya ubora duniani kutoka nafasi ya 24.
Na Nimeendelea kuwa Bingwa Wa ABU Na Bondia Namba 1 Africa’’ aliandika Mwakinyo katika ukurasa wake wa Twitter. Hassan Mwakinyo alijosa katika ulingo wa ngumi za kulipwa tangu mwaka 2015, na amewahi kushikilia mikanda kadhaa ya ubingwa ikiwemo ubingwa wa WBA pan African.
Taliban yadai kudhibiti Bonde la Panjshir
Taliban inadai sasa inadhibiti kabisa jimbo la Panjshir la Afghanistan, sehemu ya mwisho kupinga utawala wake.
Kumekuwa na mapigano makali katika eneo hilo kaskazini mwa mji mkuu Kabul, na kundi la (NRF) limekuwa mstari wa mbele kupinga utawala wa Taliban.
"Pamoja na ushindi huu, nchi yetu imeondolewa kabisa kwenye tishio la vita," msemaji wa Taliban alisema.
Hata hivyo , NRF imekana kushindwa na Taliban
"Sio kweli, Taliban hawajadhibiti Panjshir ninakataa madai ya Taliban," msemaji wa NRF Ali Maisam aliambia BBC.
Taliban ilichukua udhibiti wa Afghanistan yote wiki tatu zilizopita, ikichukua mamlaka huko Kabul mnamo Agosti 15 kufuatia kuanguka kwa serikali inayoungwa mkono na nchi za Magharibi.
Afghanistan: Taliban washutumiwa kumuua polisi wa kike
Gul Agha Sherjoy: Mfahamu mshirika mkubwa wa Marekani aliyepigana dhidi ya Taliban
Afghanistan: Jinsi Uingereza, Urusi na Marekani zilivyoshindwa na Taliban katika kipindi cha miaka 180 iliyopita