Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

  1. Na hadi hapo tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja hivi leo.Hadi hapo kesho panapo majaaliwa

  2. Wito watolewa kutambua miili iliyotolewa kutoka mtoni, Kenya

    Mto Tana uko kaskazini mashariki mwa Kenya
    Image caption: Mto Tana uko kaskazini mashariki mwa Kenya

    Kikundi cha kutetea haki za binadamu nchini Kenya kimehimiza serikali kusaidia kutambua miili 16 iliyoopolewa kutoka Mto Tana katika mkoa wa kaskazini mashariki katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

    "Baadhi ya familia zinaweza kukosa rasilimali ya kuwasafirisha huko kwa zoezi la utambuzi wa mwili," Hussein Khalid, mkurugenzi mtendaji wa Haki Africa, aliambia BBC.

    Alikuwa akijibu mwito wa polisi kwa wale wanaotafuta jamaa waliopotea kutembelea chumba cha kuhifadhi maiti katika kaunti ya Garissa.

    Miili iliyopatikana imeoza sana, wengine walikuwa wamefungwa kamba mikononi na miguuni, wengine walikuwa wamefungwa mawe kwa kuzunguka, ripoti ya vyombo vya habari nchini humo zimesema.

    Hakuna miili yoyote iliyokuwa na aina yoyote ya hati za kitambulisho juu yao.

    Polisi wanasema waathiriwa waliuawa na miili yao kutupwa mtoni, kituo cha runinga ya eneo ya Citizen TV.

    View more on twitter

    Familia zingine zinazotafuta jamaa wao waliopotea huku wakiwa na wasiwasi, walitembelea chumba cha kuhifadhia maiti huko Garissa Jumatatu lakini wakaondoka wakiwa wamevunjika moyo.

    Sampuli kutoka kwa miili hiyo sasa imepelekwa katika maabara ya serikali kwa uchunguzi.

  3. Wachezaji wa Judo wapigwa marufuku kushiriki Olympiki kwa kukataa kucheza na Muisraeli

    Fethi Nourine alijiondoa katika michuano ya Olympiki muda mfupi kabla ya  mchezo kuanza
    Image caption: Fethi Nourine alijiondoa katika michuano ya Olympiki muda mfupi kabla ya mchezo kuanza

    Shirikisho la kimataifa la mchezo wa Judo (IJF) limewawekea marufuku ya miaka 10 mchezaji wa Algerian plapamoja na mkufunzi wake kwasbabu walijiondoa kwenye michuano ya Olympiki ili kuepuka mechi na Muisraeli.

    IJF lilisema kuwa Fethi Nourine na Amar Benikhlef walitumia mechi za Tokyo kama jukwa la kupinga na kuendeleza propaganda.

    Mchezaji wa Algeria alisema uungaji mkono wake kwa Wapalestina ulimfanya asiweze kushindana na Muisraeli.

  4. Zaidi ya 80 wafariki kutokana na mafuriko Sudan

    Nyumba za kuishi na majengo mengine yamezama ndani ya maji ya mafuriko
    Image caption: Baadhi ya nyumba za kuishi na majengo mengine yamezama ndani ya maji ya mafuriko

    Zaidi ya watu 80 wamefariki kutokana na mafuriko nchini Sudan tangu msimu wa mvua uipoanza mwezi Julai, maafisa wanasema.

    Msemaji wa Baraza la kitaifa la ulinzi wa raia alisema Jumatatu kuwa watu 84 wamekufa na wengine 67 walijeruhiwa.

    Mvua za kubwa iliyonyesha imeathiri takriban majimbo 14 kati ya 18 nchini humo, huku nyumba zaidi ya 30,000 zikiangamia au kuharibika.

    Mazao na miundo mbinu ya umma pia vimeathiriwa.

    Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa walau watu 102,000 wameathiriwa na mvua kubwa na mafuriko kote nchini Sudan.

    Mwaka jana, Sudan ilitangaza hali ya tahadhari kitaifa kwa miezi mitatu kutokana na mafuriko ambayo yaliwauwa watu wapatao 100 na kuwaathiri wengine zaidi ya 600,000, na kuharibu zaidi ya nyuma 100,000.

  5. Familia ya jasusi wa Somalia yakataa tume ya rais

    Tahril alitoweka mwezi Juni
    Image caption: Bi Ikran Tahlil alitoweka mwezi Juni

    Familia yaafisa wa ujasusi wa Somalia aliyepotea, Ikran Tahlil, imeikataa tume ya uchunguzi iliyoundwa na Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed kwa ajili ya kuchunguza kutoweka kwake mwezi Juni.

    Rais Farmajo alituma ujumbe kwenye Twitter kwamba jopo hilo la watu watano la uchunguzi lingepewa ‘’jukumu la taasisi ya kisheria kwa ajili ya utekelezaji wa haki".

    Hatahivyo, familia ya Bi Tahlil imepinga uteuzi wa tume ya uchunguzi na wamesema kuwa wanaamini mahakama ya kijeshi tu jeshi tu ndiyo inayoweza kushugulikia kesi hiyo.

    "Hatuna imani na hatutaikubali tume ya uchunguzi ambayo imeteuliwa na rais kuchunguza kesi ya Ikran. Tunaimani tu na mahakama ya jeshi, na ndio maana tuliwasilisha kesi huko ," Qali Mohamud, mama yake Bi Tahlil, aliiambia Universal TV.

    Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble, ambaye ametofautiana na RaisFarmajo kuhusu kezi hiyo, bado hajasema lolote kuhusiana na uundwaji wa tume hiyo.

    Tarehe 2 Septemba, Shirika la ujasusi na usalama nchini humo (Nisa) lilisema kuwa Bi Tahlil, ambaye alifanya kazi katika idara yake ya usalama wa mtandao, aliuawa na al-Shabab baada ya kutekwa nyara mjini Mogadishu.

    Hatahivyo, al-Shabab ilikanusha kuhusika na kutoweka kwa Bi Tahlil na madai ya kifo chake.

  6. R. Kelly alimdhulumu kingono Aaliyah alipokuwa na umri wa miaka 13 au 14, korti yaambiwa

    at

    R. Kelly alimnyanyasa kingono mwimbaji wa zamani wa R&B marehemu Aaliyah wakati alipokuwa na umri wa miaka 13 au 14, mmoja wa wacheza densi wake wa zamani ameiambia korti.

    Mwanamke huyo, ambaye alitoa ushahidi chini ya jina Angela, aliiambia korti kwamba alikuwa ameona nyota huyo akifanya tendo la ngono kwa Aaliyah kwenye basi la usafiri

    Tukio hilo linadaiwa kutokea mwaka mmoja kabla ya Bwana Kelly kuoa mwimbaji huyo kinyume cha sheria, akiwa na miaka 15.

    Bwana Kelly, 54, anakanusha mashtaka yote dhidi yake.

    Ni pamoja na shtaka moja la udanganyifu - ambalo linamtaja kama mkuu kundi lenye hila la "kuwateka wasichana na vijana" kwa malengo ya ngono’. Ameshtakiwa pia kwa mashtaka manane ya kukiuka sheria za kuzuia ngono kati ya majimbo

    t

    Mwimbaji huyo, ambaye jina lake kamili ni Robert Kelly, hakushtakiwa kwa kubaka au kushambulia, lakini waendesha mashtaka wanaruhusiwa kutoa ushahidi wa uhalifu unaowezekana unaohusiana na mashtaka ya ujambazi, bila kujali ni lini yalitokea.

    Ushuhuda wa Angela ulikuja siku ya 15 ya kesi, huko Brooklyn, New York.

    Alikuwa mtu wa 10 anayetuhumu R Kelly kusimama kortini kutoa ushahidi na akasimulia kisa cha unyanyasaji wa kijinsia wa waathiriwa waliokuwa na umri mdogo .

    Alisema alianza kufanya mapenzi na Bwana Kelly mnamo 1991, wakati bado alikuwa shuleni.

    Kesi hiyo inaendelea

  7. Mwanamke anayetumia maelfu ya pauni kuhakikisha njiwa wake wanapendeza kwa mitindo

    Their rooms are reserved for private use
    Image caption: Wametengewa chumba chao kwa matumizi ya kibinafsi

    Huenda umewahi kusikua kuwa kuhusu watu wanaotumia pesa nyingi sana kugarimia maisha ya mbwa wao.

    Lakini mara hii mambo sio mbwa tena. Mwanamke mmoja kwa jina amekuwa akitumia kitita cha Pauni4,000 kila mwaka kuwapendezesha njiwa wake wawili aliowaasili ambao kwa sasa wana chumba , kabati lao la nguo na hata kutembezwa ndani ya baiskeli ya watoto wachanga.

    Meggy Johnson, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Lincolnshire, aliwanusuru ndege hao aina ya njiwa kwa majina Sky na Moose, baada ya kupatikana wakiwa wametupwa walipokuwa bado vifaranga

    Hutumia kiti hiki cha magurudumu  ambacho kwa kawaida hutumiwa kwa watoto kuwatembeza njiwa wake kuwafurahisha
    Image caption: Hutumia kiti hiki cha magurudumu ambacho kwa kawaida hutumiwa kwa watoto kuwatembeza njiwa wake kuwafurahisha

    Bi Meggy Johnson aliwatunza na kuhakikisha kuwa wanarejea katika hali nzuri ya afya kwa kuwalisha kwa mikono yake kwa kipindi cha wiki sita- na katika kipindi hiki alitokea kujenga uhusiano wa karibu nao na kuwapenda sana.

    Kwa sasa, njiwa hao wanaishi “maisha ya anasa” huku wakifanyiwa sherehe za siku ya kuzaliwa, wakipewa wanasesele laini na kutembezwa.

    Licha ya huduma yake ya upendo, Meggy, mara nyingi hupata kauli za matusi kutoka kwa watu wasiojulikana ambao humuita“panya wa kuruka ”,lakini anasema ni marafiki zake wazuri na “wanastahili fursa”, ya kupewa matunzo bora.

    Licha ya huduma yake ya upendo, Meggy, mara nyingi hupata kauli za matusi kutoka kwa watu wasiojulikana
    Image caption: Licha ya huduma yake ya upendo, Meggy, mara nyingi hupata kauli za matusi kutoka kwa watu wasiojulikana

    Mpenzi huyu wa wanyama hutumia pauni 400 kila mwezi kuwafurahisha njiwa hao pamoja na ndege wengine wawili aliowaokoa.

  8. Met Gala 2021: Watu maarufu walivyoonyesha mavazi yao ya kifahari kwenye zulia jekundu

    Mwanamuziki Billie Eilish, ambaye alikuwa mshereheshaji mwenza wa tukio, alifananishwa na Marilyn Monr
    Image caption: Mwanamuziki Billie Eilish, ambaye alikuwa mshereheshaji mwenza wa tukio, alifananishwa na Marilyn Monr

    The Met Gala - ni mojawapo ya maonyesho makubwa zaidi ya mitindo ya mavazi na matukio yanayowakutanisha nyota wa fani za filamu na mitindo ya mavazi duniani. Nyota hao walipita kwenye zulia jekundu jijini New York kuonyesha na kunadi mavazi yao yaliyobuniwa na nembo kubwa za mavazi. Washiriki ni baadhi ya watu maarufu zaidi duniani.

    Likifanyika kwa madhumuni ya kuchangisha pesa kwa ajili ya jumba la Makumbusho taasisi ya - Metropolitan Museum of Art's Costume Institute.

    Onyesho la Gala limerejea baada ya kuahirishwa mwaka jana kutokana na janga la corona.

    Hawa ni baadhi ya watu maarufu na jinsi walivyojinadi kwenye zulia jekundu:

    Co-host Naomi Osaka showed off a colourful Louis Vuitton dress and elaborate hairstyle - said to be a nod to her Haitian and Japanese heritage
    Image caption: Mshereheshaji mwenza wa tuki mchezaji tenisi maarufu Naomi Osaka alionyesha gauni lake la rangi za kupendeza la nembo ya Louis Vuitton na mtindo wake wa kipekee wa nywele -ambao unasemekana una asili yake ya Haiti na Japan
    Mwanamashairi  Amanda Gorman
    Image caption: Mwanamashairi Amanda Gorman, ambaye allisoma ushairi wake katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Marekani Joe Biden , alikuwa pia mshereheshaji mwenza. Alichagua kuvaa gauli lake la nembo ya Vera Wang na kitambaa cha kichwani cha channel "a re-imagined Statue of Liberty"
    Kim Kardashian's look spawned a series of memes on social media
    Image caption: Muonekano wa Kim Kardashian uliibua msururu picha za watu na vibonzo vya kuigiza vazi hili kwenye mitandao ya kijamii
    A$AP Rocky na mpenzi wake Rihanna waliwasili kuchelewa kimtindo, huku wakiwa wamevalia mavazi yanayoshabihiana
    Image caption: A$AP Rocky na mpenzi wake Rihanna waliwasili kuchelewa kimtindo, huku wakiwa wamevalia mavazi yanayoshabihiana
    Serena Williams aliwavutia wengi kwa vazi lake lililofunika mwili la nembo ya  Gucci bodysuit  ambalo lilishuka hadi mguuni lilinoonekana mithili ya manyoya ya ndege
    Image caption: Mchezaji nyota wa tenisi Serena Williams aliwavutia wengi kwa vazi lake lililofunika mwili la nembo ya Gucci bodysuit ambalo lilishuka hadi mguuni lilinoonekana mithili ya manyoya ya ndege
    Eilish was accompanied by her brother, Finneas O'Connell, who chose an all-red suit and sequined face covering
    Image caption: Eilish alisindikizwa na kaka yake, Finneas O'Connell, ambaye aliamua kuchagua kuvaa suti kiatu na barakoa vya rangi nyekundu
    Frank Ocean aliwasili kwenye tukio akiwa na mwanasesere wa robot wa rangi ya kijani
    Image caption: Frank Ocean aliwasili kwenye tukio akiwa na mwanasesere wa robot wa rangi ya kijani
    Rapper Lil Nas X kwanza aliingia na vazi hili ...ambalo lilificha vazi la suti la Versace armour ambalo baadaye alilifichua
    Image caption: Rapper Lil Nas X kwanza aliingia na vazi hili ...ambalo lilificha vazi la suti la Versace armour ambalo baadaye alilifichua
  9. Mama yake Waziri mkuu wa Uingereza Charlotte Johnson Wahl afariki

    Waziri mkuu pamoja na mama yake, Charlotte Johnson Wahl, na dada yake Rachel mwaka 2004
    Image caption: Waziri mkuu Boris Johnson pamoja na mama yake, Charlotte Johnson Wahl, na dada yake Rachel mwaka 2004

    Mama yake Waziri mkuu wa Uingereza Charlotte Johnson Wahl amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.

    Taarifa iliyochapishwa katika gazeti la Times nchini Uingereza inasema amefariki kifo cha "ghafla na cha amani" katika hospitali ya St Mary magharibi mwa London.

    Boris Johnson wakati mmoja alimuelezea mama yake, ambaye alikuwa mchoraji kama mwenye "mamlaka ya juu zaidi " katika familia.

    Watu maarufu kutoka vyama vyote vya kisiasa, akiwemo kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer, wametuma salamu za rambirambi kwa Bw Johnson.

    Katika ujumbe wake wa Twitter Sir Keir aliandika : "Pole sana, nimepata taarifa ya waziri mkuu kumpoteza mama yake. Natoa rambirambi kwake binafsi na kwa familia yake."

    Bi Johnson Wahl, ambaye baba yake alikuwa rais wa Tume ya Ulaya ya haki za binadamu katika miaka ya 1970, aliolewa na Stanley Johnson mwaka 1963 kabla ya kumaliza shahada yake katika Chuo kikuu cha Oxford kama mhitimu wa kwanza wa kike kumaliza masomo ya shahada chuoni hapo akiwa ameolewa.

    Wawili hao walikuwa na watoto wanne - Boris, mwandishi wa habari Rachel, waziri wa zamani wa mazingira Jo na mwanamazingira Leo. Ndoa yao ilivunjika 1979.

    Kama msanii wa uchoraji, Bi Johnson Wahl alitengeneza jina lake kama mchoraji wa picha, ambapo wasanii wa maigizo Joanna Lumley na author Jilly Cooper wakiwa miongoni mwa watu aliowachora.

    Mnamo mwaka 1988, aliolewa na Profesa Mmarekani Nicholas Wahl na akahamia New York – ambapo alianza kuchora michoro ya jiji. Alirejea London baada ya kifo cha mume wake mwaka 1996.

    Akiwa na umri wa miaka 40, alipatwa na maradhi ya ubongo ya Parkinson, lakini aliendelea kuchora, akitembea kwa usaidizi wa kifaa cha kutembea.

  10. Wanawake wa Afghanistan wapinga masharti makali ya mavazi ya wanafunzi wa kike

    Kampeni ya mtandao wa kijamii ilianzishwa na Dkt  Bahar Jalali
    Image caption: Kampeni ya mtandao wa kijamii ilianzishwa na Dkt Bahar Jalali

    Wanawake wa Afghanistan wameanzisha kampeni ya mtandaoni dhidi ya masharti makali ya mavazi ya wanafunzi wa kike.

    Wakitumia Hashtag ya #DoNotTouchMyClothes na #AfghanistanCulture,wengi wanasambaza picha za nguo zao nzuri za kitamaduni. Mwandishi wa BBC Sodaba Haidare alizungumza na mwanamke mmoja aliye kinara wa kampeni hii.

    Andika "Nguo za jadi za Afghanistan" kwenye Google na utashangaa kwa kuona nguo za kitamaduni zenye rangi nyingi. Kila moja ni ya kipekee, na mapambo ya mikono na muundo , nzito, vioo vidogo vilivyowekwa kama nakshi kwa uangalifu kifuani, sketi ndefu na zenye kupendeza. Wanawake wengine huvaa kofia zilizopambwa, wengine huvaa vitambaa kichwani, kulingana na mkoa gani wa Afghanistan wanatoka.

    Toleo la nyuma la nguo kama hizo lilikuwa linavaliwa kila siku na wanawake wanaokwenda chuo kikuu au mahali pao pa kazi katika miaka 20 iliyopita.

    Wakati mwingine suruali ilibadilishwa na suruali ya jeans na vitambaa viliwekwa juu ya vichwa vyao badala ya juu ya mabega.

    Women Afghan students wore all black during a pro-Taliban rally at a university in Kabul
    Image caption: Wanafunzi wa kike wa Afghanistan walivaa nguo nyeusi wakati wa mkutano wa kuunga mkono Taliban aktika chuo kikuu mjini Kabul

    Lakini picha za wanawake walio na nguo ndefu ndefu zilizofunikwa na abaya za rangi nyeusi, kufunika uso na mikono yao, na kukusanyika huko Kabul mwishoni mwa wiki kuunga mkono "agizo la Taliban" zimeonesha toafauti kubwa.

    Katika video moja, wanawake wanaoongoza maandamano ya kuunga mkono Taliban katika mji mkuu walionekana wakisema wanawake wa Afghanistan wanaojipaka urembo na katika nguo za kisasa "hawamukilishi mwanamke wa Kiislamu wa Afghanistan" na "hatutaki haki za wanawake ambazo ni za kigeni na kinyume na sharia "- akimaanisha sheria ya Kiislamu inayoungwa mkono na Taliban.

    Taarifa zaidi kuhusu wanawake Afghanistan:

  11. Watu sita wafariki katika shambulio la kuvizia Burkina Faso

    Burkina Faso imekuwa ikikabiloiana na wapiganaji wa Jihad kwa miaka mingi
    Image caption: Burkina Faso imekuwa ikikabiliana na wapiganaji wa Jihad kwa miaka mingi

    Shambulio la kuvizia dhidi ya msafara wa maafisa wa usalama nchini Burkina Faso uliokuwa ukisafirisha malori ya mafuta kutoka kwenye mgodi wa machimbo ya dhahabu, karibu na mpaka wa Niger limewauwa maafisa wa usalama sita, maafisa wanasema.

    Watu saba wamejeruhiwa baada ya kile ambacho serikali ya jimbo mashariki mwa Burkina Faso ilisema lilikuwa ni shambulio la jihadi.

    Miaka miwili iliyopita watu 39 waliuawa wakati msafara wa magari uliokuwa ukitoka eneo hilo hilo kushambuliwa.

    Tukio hilo lilisababisha kufungwa kwa shughuli za uzalishaji kwa takriban mwaka mmoja.

    Tangu mwaka 2015 mashambulio ya makundi yenye uhusiano na Islamic State na al-Qaeda wamewauwa zaidi ya watu 1,500 na kuwalazimisha zaidi ya milioni moja wengine kuyahama makazi yao.

    Fahamu kundi linaloihangaisha Nigeria licha ya kuwa na jeshi kubwa

    Boko Haram: Hizi ndizo sababu sita za serikali ya Nigeria kushindwa kuliangamiza kundi la kigaidi la Boko Haram

  12. Mji wa Kigali Rwanda wanzisha usafiri wa baiskeli ili kuepusha uchafuzi wa hali ya hewa

    Baiskeli za  GuraRide kwa sasa zimewekwa katika maeneo 13 ya jiji la Kigali
    Image caption: Baiskeli za GuraRide kwa sasa zimewekwa katika maeneo 13 ya jiji la Kigali

    Mji wa Kigali umeanzisha aina mpya ya kusafiri mjini humo kwa kutumia baiskeli kama sehemuyajuhudi za Rwandaza kukabiliana na uchafuzi wa mazingira na kupunguza hewa ya kaboni katika miji na vituo vya miji vinavyoongezeka nchini humo.

    Wasafiri wataweza kutumia baiskeli hizo kwa kupokezana katika mji mkuu Kigali kwa bei ya chini ikilinganishwa na usafiri mwingine uliopo mjini humo.

    Kijana akienda kuchukua baiskeli kwa ajili ya kuendesha
    Image caption: Kijana akienda kuchukua baiskeli kwa ajili ya kuendesha

    Mjini Kigali, mtaa wa Remera baiskeli nyingi zenye rangi ya kijani na manjano zimeegeshwa katika kila kona ya barabara.

    Wakazi wa mji huo wanapakua application kwenye play store ya simu zao, ili waweze kutumia baiskeli yetu’’, anaeleza kijana wa kike ambaye amekuwa akitoa maelezo kwa wapita njia wanaoashuhudia jinsi ya matumizi ya maiskeli hizo.

    Kuna vituo 13 vya baiskeli hizi mjini Kigali ambako pia kuna barabara maalumu za kuendeshea baiskeli. Mtaa wa Remera karibu na uwanja wa mpira kuna vituo vingine na baadhi wameanza kutumia baiskeli hizi.

    Barabara za baiskeli zimeandaliwa kando ya barabara kuu
    Image caption: Barabara za baiskeli zimeandaliwa kando ya barabara kuu

    Kwa mjibu wa kampuni ya ‘Gura Ride’ inayosimamia mpango huu anayetaka baiskeli anaichukua katika kituo kilicho karibuna kisha shughuli zake kuiweka kwenye kituo kingine kilicho karibu na mwisho wa safari yake.

    Hatahivyo changamoto iliyopo bado nikwamba bado kuna barabara chache za kuendeshea baiskeli hizi mjini kigali ,pia milima iliyopo mjini Kigali inaweza kuwa kikwazo.

    Barabara ziko maeneo mawili ya jiji  kwa sasa
    Image caption: Barabara ziko maeneo mawili ya jiji kwa sasa

    Lakini wahusika wana majibu kwa changamoto hizo, Jerry Ndayishimiye ni afisa wa GuraRide:

    Meya wa jiji la Kigali Pudence Rubingisa amesema lengo kubwala mradi huuni kukabiliana na uhalibifu wa mazingira:‘’tunataka usafiri unaotusaidia kulinda uchafuzi wa mazingira, kusafiri bila kutumia magari kwani tutakaposafiri kwa kutumia baiskeli itakuwafaidakubwa kwa afya zetu kwa kupata hewa safi’’

    Fahamu miji 10 safi zaidi Afrika

    Hii ni miji 5 duniani yenye gharama ya chini zaidi ya kuishi

  13. Mfanyabiashara Mnyarwanda apigwa risasi na kuuawa Msumbiji

    Revocant Karemangingo alipigwa risasi mita 50 kutoka kwenye makazi yake nchini  Msumbiji
    Image caption: Revocant Karemangingo alipigwa risasi mita 50 kutoka kwenye makazi yake nchini Msumbiji

    Mfanyabiashara Mnyarwanda amepigwa risasi na kuuawa katika mainspaa ya Matola ,kilomita chache kutoka mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.

    Levocat Karemangingo alipigwa risasi karibu mita 50 kutoka kwenye makazi yake yaliyopo katika eneo la Liberdade Jumatatu asubuhi.

    Imedaiwa kuwa uhalifu huo ulifanywa na majambazi waliokuwa katika magari matatu ambao walilizuwia gari lake kabla ya kummiminia risasi.

    Wauaji hao hadi sasa hawajulikana, jambo lililoitikisa jamii ya Wanyarwanda wanaoishi Msumbiji.

    Polisi walikuwa kwenye eneo la tukio kufanya uchunguzi wa mwili wake na baadaye ulipelekwa kwenye hospitali ya jimbo.

    Baadhi ya Wanyarwanda wamewaambia waandishi wa habari kuwa uhalifu huo uliwalenga raia wanaopinga serikali ya sasa ya Rwanda na kudai kuwa watu wengi wanalengwa.

    Wanyarwanda walioko Msumbiji wameiomba serikali kuwapatia ulinzi zaidi.

    Mwaka 2019, Mnyarwanda mwingine, Louis Baziga, aliuawa kwa risasi katika kitongoji cha Maputo baada ya watu wenye gari kuzuia gari lake na kumpiga risasi. Alifahamika kuiunga mkono serikali ya sasa ya Rwanda.

    Taarifa zaidi kuhusu Msumbiji:

  14. Paul Pogba na Burnaboy watumbuiza katika tamasha la muziki England

    View more on twitter

    Kiungo wa kati wa klabu ya Manchester United Paul Pogba aliisaidia klabu yake kuilaza Newcastle4-1siku ya Jumamosikabla ya kujiunga na nyota wa muziki wa Nigeria Burna Boy kuwatumbuiza raia.

    Pogba ambaye familia yake inatoka nchini Guinea , alicheza pamoja na Cristiano Ronaldokatika uwanja wa Old Trafford huku nyota huyo wa Ureno akifunga magoli mawili baada ya kurudi katika timu hiyo kutoka Juventus.

    Mchezaji huyo ambaye ni mshindi mara mbili wa kombe la dunia na Ufaransa , alitoa pasi mbili za magoli kabla ya kwenda katika tamasha la muziki la Parklife music festival mjini Manchester na kushiriki pamoja na Burna Boy, ambaye alikuwa amevalia tishati ya Manchester United.