Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Jenerali wa jeshi nchini Sudan awalaumu wanasiasa kwa jaribio la mapinduzi

  Jenerali Mohamed Hamdan Dagolo amesema kuwa vikosi vyake vimezuia mapinduzi tangu kuondolewa kwa kiongozi wa zamani

  Makamu wa rais wa baraza la utawala wa nchi hiyo amesema kwamba wanasiasa ndio wa kulaumiwa kwa jaribio la mapinduzi la siku ya Jumanne.

  ‘’Wanasiasa ndio sababu kuu ya kutokea kwa mapinduzi kwasababu wamewasahau raia na lengo lao kuu ni kuzidi kusalia madarakani’’ , alisema Jenerali Mohammed Hamdan Dagolo kwa jina maarufu Hemeti , alinukuliwa na vyombo vya habari akisema.

  ‘’Hali imesababisha switofahamu miongoni mwa raia’’ , aliongezea. Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alisema kwamba wale waliohusika katika kumuondoa madarakani rais Omar al- Bashir ndio waliohusika na jarbio hilo.

  Waziri wa masuala ya kigeni Mariam al- Sadiq aliambia BBC kwamba jeshi liliwazuia maafisa wa ngazi za chini kutochukua mamlaka na kwamba hiyo ilikuwa ishara ya kujitolea kwa jeshi hilo kuhakikisha kuwa kuna kipindi cha serikali ya mpito.

  Alisema kwamba waliopanga njama za mapinduzi hayo walichukua udhibiti wa maeneo muhimu na kwamba walikuwa wamekaribia kutangaza mapinduzi hayo.

  Aliongezea kwamba walijaribu kutafuta mafundi wa mitambo katika kituo kikuu cha habari cha serikali ili kutangaza taarifa yao pamoja na muziki wa kijeshi. Jenerali Dagolo , ambaye anaongoza jeshi la Rapid Support , ni mshirika wa karibu wa rais Bashir.

  Vikosi hivyo vimeshutumiwa kwa kutekeleza mashambulizi katika jimbo la Magharibi la Darfur. Alisema kwamba wanajeshi wake walitibua majaribio kadhaa ya mapinduzi tangu Bashir alipoondolewa madarakani.

  Mapinduzi Mali: Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?

  Nchi sita za Kiarabu: Wote walikuwa wanajeshi na walipoingia madarakani hawakutaka kuondoka hadi vita vikawatimua

 2. Kiongozi wa waasi ahukumiwa kifungo cha maisha DRC

  Kiongozi wa waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amehukumiwa kifungo cha maisha kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

  Chance Mihonya, muasi wa jeshi, alianzisha kikundi cha waasi mnamo 2017 katika Hifadhi ya Kitaifa ya Kahuzi Biega,alikamatwa mwaka jana.

  Mahakama ya jeshi inayotembea iliyowekwa karibu na mji wa Bukavu ilimpata na hatia ya utekaji nyara na kutesa makumi ya watu kutoka vijiji kadhaa katika bustani.

  Pia alihukumiwa kwa kuajiri watoto kwenye jeshi na kutumia akiba ya madini nchini.

  Vikundi vya haki vinasema zaidi ya vikundi mia moja vyenye silaha vinafanya kazi mashariki mwa Congo D ambapo UN inasema zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kukimbia makazi yao mwaka huu kwasababu ya vurugu.

  Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?

  Namna ambavyo waasi wa Uganda walikuwa washirika wa IS nchini DRC

 3. Mary Keitany: Mkenya anayeshikilia rekodi ya dunia ya Marathon astaafu

  Mary Keitany set a world record for a women-only race at the 2017 London Marathon

  Mwanariadha wa Kenya wa mbio za marathon upande wa wanawake Mary Keitany ametangaza kustaafu akiwa na miaka 39 baada ya kuumia mgongo.

  Bado anashikilia rekodi ya dunia ya marathon ya wanawake pekee aliyokimbia kwa muda wa saa mbili na dakika 17 na sekunde moja, amabyo aliweka katika ushindi wake wa tatu wa London Marathon 2017.

  Pia alishinda New York Marathon mara nne.

  "Sasa ni wakati wa kusema kwaheri - ikiwa tu kama mkimbiaji wa mtaalamu- kwenye mchezo ninaupenda sana, "alisema.

  "Baada ya ufanisi wangu wa mwaka 2019, wakati nilipoandikisha matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kuwa nafasi ya pili mjini New York, Nilikuwa na matumaini kuwa bado ninaweza kuwa na mshindani mkubwa kimataifa kwa miaka kadhaa zaidi ingawa nina miaka zaidi 30, "Keitany aliongeza katika taarifa yake.

  "Walakini, nina huzuni kusema, jeraha la mgongo ambalo nilipata mwishoni mwa 2019 lilichangia uamuzi kuhusu kustaafu kwangu.

  "Sikuweza kupata matibabu niliyotaka Ulaya kwa sababu ya vizuizi vya usafiri vinavyohusiana na janga la corona mwaka jana na kila wakati nilifpoikiri nimepata nafuu na kuanza mazoezi kwa bidii, nakabiliwa na shida hiyo tena.

  Mafanikio ya kwanza ya Keitany ulimwenguni yalikuja mnamo 2007 wakati aliposhinda nishani ya fedha ya kibinafsi na tuzo ya dhahabu ya tumi kwenye Mashindano ya Nusu ya Marathon ya Dunia.

  Kwa nini Mkenya Mary Keitany aliwatumia wanaume kufanya mazoezi ya mbion za London Marathon

 4. DRC: Mwandishi wa kibinafsi wa AFP bado anazuiliwa

  Kwa zaidi ya saa 24 sasa, mwandishi wa kibinafsi wa AFP nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jam Pierre Sosthène Kambidi, bado anasemekana kuzuiliwa katika gerza la kijeshi,tangu siku ya Jumatatu.

  Mwandishi huyo mpekuzi pia anachangia mada katika tuvuti ya Actualité.cd, chombo cha habari mtandaoni DRC.

  Chombo cha habari anachofanyia kazi, kiliandika kikinukuu chanzo kutoka mahakama ya kijeshi kwamba Pièrre Sosthene Kambidi anahojiwa kwa kuwa mtu wa kwanza kuwa na video inayoashiria kuua kwa wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa ambao walitekwa na wanaume waliojihami mnamo March 12, 2017, kati kati ya DRC.

  Raia wa Marekani Michael Sharp na Zaida Catalan, wa Uswidi walikuwa sehemu ya kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa nchini DR- Congo. Walikuwa wakichunguza mazo katika eneo la Kasaï.

  Zaidi ya vikao 100 vya mahakama vimefanywa tangu kesi hiyo ilipoanza kusikizwa Juni 15, 2017 dhidi ya watu 30 wanaotuhumiwa kwa mauaji ya wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa.

  Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?

  Mzozo wa DRC: Rais Felix Tshisekedi awateua wanajeshi kuwa magavana wa Ituri na Kivu Kaskazini

 5. Juhudi za kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi zitasaidia kukabiliana na kiangazi na baa la njaa

  Video content

  Video caption: Mabadiliko ya tabia nchi yanachangia janga la nja na kiangazi

  Kuna haja ya kushughulikiakwa dharurahatua za kuzuia au kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kuepuka tatizo la mara kwa mara la baa la njaa na kiangazikatika sehemu nyingi za kenya na upembe wa Afrika .

  Mkurugenzi wa shirika la Save the Children nchini Kenya na Madagascar Yvonne Arunga anasema kiangazi na athari zake kimesababisha mahangaiko kwa maelfu ya watu katika sehemu zilizoathiriwa na suluhisho la kudumu ni kuangazia njia za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na uwekezaji Zaidi kwa jamii zilizoathiriwa ili ziweze kustahimili makali yanayotokana na mageuzi ya hali ya anga .

  kiangazi

  Nchini Kenya ,maelfu ya watu wanakabiliwa na baa la njaa na tayari serikali imetangaza tatizo hilo kuwa janga la kitaifa

  Kaunti za Pwani mwa Kenya na kaskazini mashariki ndizo zilizoathiriwa sana .

  Uhaba wa maji na chakula unawatia hatarini zaidi wanawake na watoto katika maeneo hayo .

  Kenyatta atangaza ukame kuwa janga la kitaifa

  Zaidi ya wakazi laki nne wa Pwani ya Kenya wanakabiliwa na baa la njaa

  Makali ya njaa yavuruga maisha ya maelfu ya watu Pwani mwa Kenya

  Maisha katika nyuzijoto 50: Athari za mabadiliko ya hali ya hewa ,ndani ya maisha ya Waaustralia

  Mabadiliko ya tabia nchi : Sasa dunia inashuhudia mara dufu idadi ya siku ambazo nyuzijoto ni zaidi ya 50

 6. Kenya na Uingereza 'zinafanyia kazi' mpango wa usafiri wa Covid

  The WHO has been opposing vaccine passports for international travel

  Serikali za Kenya na Uingereza zinasema kuwa zinafanyia kazi mfumo wa kutambua vyeti vya chanjo ya Covid vinavyotolewa katika nchi zote mbili , ili kuwezesha usafiri kati yao.

  Haya yanajiri baada ya Uingereza kubadili mfumo wao tata wa usafiri wa kimataifa ili kuwarahisishia wasafiri kuingia nchini humo.

  Licha ya kuondolewa katika orodha nyekundu ya Uingereza, Wakenya wanaonuia kusafiri huko bado watahitajika kufanyiwa vipimo vya corona siku tatu kabla ya safari, kukaaa karantini kwa siku 10 wanapowasili pamoja na kulipia gharama ya vipimo na kutengwa.

  Chini ya sheria mpya za Uingereza kuanzia tarehe 4 Oktoba, watu waliopewa chanjo kamili kutoka nchi ambazo hazimo kwenye orodha nyekundu watasamehewa kukaaa karantini ya lazima.

  Lakini taarifa ya pamoja ya siku ya Jumanne iliyotolewa na Balozi wa Uingereza nchini Kenya na Wizara ya Afya ya Kenya inaonesha jinsi suala hilo bado linakabiliwa na utata na huenda lisitatuliwe hivi karibuni.

  Cheti hicho kilianza kutumika rasmi Julai mosi kwa awamu ya kipindi cha wiki sita

  "Kuanzisha mfumo wa kutambua vyeti vya chanjo ya kila mmoja kwa mpango wa pasipoti ya chanjo kwa kusafiri huchukua muda haswa katika janga lisilokuwa la kawaida," taarifa hiyo inasema.

  Wataalam wa afya nchini Kenya wanasema tangazo la hivi karibuni kutoka Uingereza litakuwa na athari katika utumiaji wa chanjo za Covid-19 nchini.

  Watu kutoka nchi zingine za Kiafrika ambao wamebaki katika orodha nyekundu ya Uingereza wamekosoa sheria hizo mpya za usafiri wakisema ni za kibaguzi.

  Shirika la Afya Ulimwenguni limekuwa likipinga pasipoti za chanjo kwa safari ya kimataifa kwa sababu ya kupatikana kwa usawa wa chanjo za Covid-19 ulimwenguni.

  Chanjo ya pasipoti: Cheti cha kidijitali cha Covid Muungano wa Ulaya na jinsi kitakavyowaathiri wasafiri

 7. Tundu Lissu afutiwa kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili

  Eagan Salla

  BBC Swahili, Dar es Salaam

  Tundu Lissu

  Kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu pamoja na mwandishi wa habari mwandamizi Jabir Idrisa na wenzao wawili imefutwa na mahakama ya hakimu mkazi kisitu jijini Dar es salaam baada ya upande wa serikali kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo.

  Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti hilo la Mawio Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa kampuni ya Jaman Ismail Mehboob.

  Lissu na wenzake walishtakiwa kwa makosa matano ikiwa ni pamoja na kuandika na kuchapisha habari ya uchochezi iliyokuwa na kichwa cha habari ‘’Machafuko yaja Zanzibar’’ kwenye gazeti la Mawio kinyume cha sheria ya magaezeti ya mwaka 2002.

  Kati ya Januari 12 hadi 14 mwaka 2016 jijini Dar es salaam washtakiwa Jabir Mkina na Lissu waliandika taarifa hiyo ya uchochezi.

  Katika shitaka la pili walidaiwa januari 14 mwaka 2016 walichapisha habari hizo za kuleta chuki visiwani Zanziabar.

  Katika shitaka jingine mshtakiwa Mehboob alidaiwa kuchapisha gazeti hilo Januari 13 mwaka 2016 katika jengo la Jamana jijini Dar es salaam bila kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa msajili wa magazeti.

  Kesi hiyo ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka mitano imefutwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) Sylvester Mwakitalu chini ya sheria kifungu cha 91 cha sheria ya makosa ya jinai ambapo ameieleza mahakama upande wa jamhuri hauna nia ya kuendela na shauri hilo.

  Washitakiwa wote wako huru.

  Tundu Lissu: Mambo sita anayotaka ahakikishiwe utekelezaji wake kabla ya kurejea nyumbani kutoka uhamishoni

  Je, Tundu Lissu ni 'adui' wa Tanzania?

 8. Waasi wa Ethiopia watuhumiwa kuharibu vituo vya afya

  Mzozo kaskazini mwa Ethiopia ulianza miezi 10 iliyopita
  Image caption: Mzozo kaskazini mwa Ethiopia ulianza miezi 10 iliyopita

  Serikali ya Ethiopia inasema waasi wameharibu maelfu ya vituo vya afya latika eneo la kaskazini mwa nchi.

  Zaidi ya watu milioni 1.9 katika majimbo ya Amhara na Afar nchini Ethiopia hawwezi kupata huduma za afya baada ya waasi watiifu kwa Tigray People’s Liberation Front (TPLF)kuripotiwa kupora vituo vya afya.

  Waasi hawajatoa tamko lolote kuhusuana na tuhuma hizo za hivi punde dhidi yao.

  Waziri wa Afya Lia Tadesse amewaambia wanahabaru siku ya Jumanne kwamba waasi waliharibu hopsitali 20 na vituo vya afya, 277 na zahanati 1,162 katika eneo la Amhara.

  Aliongeza kuwa hospitali mojaa, zahanati 10 na vituo 38 vya afya zimeharibiwa katika eneo la Afar.

  Mnamo Agosti 30, Waziri wa Elimu Getahun Mekuria alisema waasi wameharibu zaidi ya shule 7,000 kaskazini mwa Ethiopia, zikiwemo 445 katika jimbo la Afar nza zaidi ya 140 katika jimbo la Amhara.

  Mapigano kati ya waasi wa Tigray na vikosi vya muungano vya Ethiopia yalizuka katika jimbo la Tigray Novemba 2020, lakini mapigano hayo sasa yamesambaaa hadi maeneo jirani ya Amhara na Afar.

  Maelezo zaidi:

  Uchumi wa Ethiopia waathiriwa na mzozo wa Tigray

  Mgogoro wa Tigray-Ethiopia: Baa la njaa lililosababishwa na binadamu

  Ushahidi unaoonesha jinsi jeshi la Ethiopia lilivyofanya mauaji Tigray

 9. Tanzania: Maafisa saba wa polisi wafutwa kazi kwa kuingia nchini Malawi

  Maafisa saba wa polisi nchini Tanzania wamefutwa kazi baada ya kupatikana na na hatia ya kuvuka mpaka wa tazania nakuingia Malawi wakiwa wamevalia sare za jeshi na silaha kinyumw cha sheria, Gazeti la Mwananchi linaripoti.

  Mwananchi linamnukuu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Janneth Magomi akisema hatua hiyo imefikiwa baada ya askari hao kufikishwa katika Mahakama ya Kijeshi Septemba 20, 2021 na kuwakutwa na hatia.

  Maafisa hao wa polisi yasemekana walikuwa wakitumia gari la polisi na wakati wakitekeleza majukumu yao walifika eneo la Kijiji cha Ikumbilo wilayani humo.

  Bw. Magomi alisema maafisa hao walikutana na mwendesha pikipiki mmoja katika kijiji hicho ambaye walimshuku kupakia mzigo wa magendo na ndipo walipoanza kumfukuzia kabla mtu huyo hajakimbia na kuvuka mpaka kuingia nchi jirani ya Malawi.

  Alisema wakati wanamfukuza mwendesha bodaboda huyo, askari hao walikutana na kundi la wananchi wa Malawi ambao walianza kuwashambulia kwa mawe.

  Purukushani lilizuka lakini askari hao walijitetea kwa kupiga risasi hewani ili kuwatawanya wananchi hao wasiwadhuru.

  Askari wa Malawi walifika eneo la tukio na kutuliza ghasia hizo ambapo skari wanne kati yao walikamatwa, huku wenzao watatu wakitoroka.

  Uhusiano kati ya Tanzania na Malawi umekuwa ukigubikwa na mambo makubwa matatu katika kipindi cha miaka 50 iliyopita

 10. Kenya na Tanzania zaongoza katika ubunifu kusini mwa jangwa la sahara

  keTZ

  Nchi za Kenyana Tanzania zinashikilia nafasi za pili na tatu mtawalia katika ubunifu kwa mujibu wautafiti uliofanywa chini ya Global innovation index. AfrikaKusini ndio inayoongoza katika kanda hiyo

  . Duniani koteKenya inashikilia nafasi ya 85 ilhali Tanzania ni ya 90 na kuzifanya nchi hizo za Afrika mashariki kuwa katika orodha ya 100 bora duniani kwa ubunifu .

  Marekani inaongoza katika viashiria kadhaa muhimu vya uvumbuzi.

  Hong Kong (China), Israeli na Singapore zinafuata kwa chumi za juu ulimwenguni zinazoongoza katika viashiria muhimu vya uvumbuzi.

  Mwaka huu, Marekani inachukua uongozi kamili katika suala hili;kushika nafasi ya kwanza katika viashiria 13 kati ya 81 vilivyotumika,

  pamoja na metriki kama R & D ya ushirika wa Ulimwenguni,wawekezaji, mikataba ya mitaji iliyopatikana, ubora wa vyuo vikuu vyake, ubora na athari za kisayansi

  machapisho (H-index), idadi ya hati miliki kwa asili,na ushirikiano kupitia njia za kilektroniki na mitandaoni .

  Orodha hiyo ya kila mwaka hutolewa na Shirika la Mali Miliki Ulimwenguni (WIPO) na huangazia viasharia mbali mbali vinavyofanikisha ustawi wa sekta mbali mbali zinazofanikisha uwezekani,ustawi wa leba,uboreshaji wa hali ya maisha na urahisi wa kufanya biashara na kazi .

  Tanzania:Uchumi wa Tanzania umestahimili vipi athari za corona?

  Rais Samia na Kenyatta wakubaliana kutatua vikwazo vya kibiashara baina ya Tanzania na Kenya

 11. Mhakama yawafunga wabunge wawili wa Tunisia

  Wabunge wawili wa Tunisia wamefungwa jela na mahakama ya kijeshi huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo.

  Wabunge hao wawili ni wa chama cha Karama.

  Wabunge watano wamefungwa kufikia sasa tangu mwezi Julai wakati Rais Kais Saied alipoingia madarakani.

  Nidal Saudi alituhumiwa kumtukana afisa wa usalama wa uwanja wa ndege miezi kadhaa iliyopita.

  Mbunge mwingine Saif Eddine Makhlouf, alituhumiwa kwa kuwatishia majaji na kuwatuhumu kwa kuhusika na mapinduzi wakati alipozuiliwa nafasi ya kumwakilisha Bw. Saudi kama wakili wake.

  Bwana Makhlouf amekuwa mkosoaji wa rais.

  Mnamo mwezi Julai, Rais Saied alifanya mabadiliko serikalini, kusitisha bunge na kuchukua udhibiti wa nchi.

  Wapinzani wake walimshtaki kwa kufanya mapinduzi lakini hatua yake ilipokelewa vyema na raia wa Tunisia.

  Utawala wa Zine al-Abidine Ben Ali Tunisia, anakumbukwa vipi?

 12. Hali ilivyo Laikipia nchini Kenya baada Machafuko yaliyotokea(picha)

  Mama ameamua kulalia kiti chake
  Image caption: Baada ya kutokea kwa machafuko sasa hakuna pa kulala na mama huyo ameamua kulalia kiti chake

  Baada ya mashabulizi yaliyofanywa na majangili katikta eneo la Ol-Morani, kaunti ya Laikipia nchini Kenya baadhi ya wenyeji walikimbilia sehemu za makanisa ili kujinusuru . Je ,maisha yako vipi tangu kutokea kwa machafuko hayo? Tazama kupitia picha hizi;

  Baadhi ya waadhiliwa walio-amua kurundi makwao
  Image caption: Baadhi ya waadhiliwa walioamua kurundi makwao
  Mama mjamzito akiwa katika boma la kanisani akiwaza
  Image caption: Mama mjamzito akiwa katika boma la kanisani akiwaza
  Waathiriwa wakiwa katika kanisani Katoliki.
  Image caption: Waathiriwa wakiwa katika kanisani Katoliki
  Walinda usalama wakishika doria
  Image caption: Walinda usalama wakishika doria
  Walinda usalama wakishika doria
  Image caption: Walinda usalama wakishika doria
  Usalama ukiimarishwa katika eneo lililoathirika
  Image caption: Usalama ukiimarishwa katika eneo lililoathirika

  Wanafunzi wakisindikizwa na maafisa wa usalama kwenda shuleni na kurejea nyumbani

  Wanafunzi wakiongozana na maafisa wa usalama
  Image caption: Wanafunzi wakiongozana na maafisa wa usalama

  Mifugo walionaswa kwa kuvamia mashamba, hapa ni kituo cha polisi cha Rumuruti

  Mifugo walionaswa kwa kuvamia mashamba
  Image caption: Mifugo walionaswa kwa kuvamia mashamba

  Soma zaidi:

  Wanajeshi kushirikiana na Polisi kuwaondoa wavamizi Laikipia Kenya

 13. Baba akamatwa kwa kuyachoma 'matiti' ya binti yake Nigeria

  Nigeria

  Polisi katika jimbo la Nigeria la Lagos wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwenye umri wa miaka minane kwa kutumia jiwe la moto.

  Rekodi ya polisi inasema kuwa baba huyo alitekeleza maasi dhidi ya binti yake, kwasababu matiti yake yalikuwa yameanza kuonyesha 'chuchu', ambazo ni ishara za kwanza za kubalehe.

  Kwa sasa msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu, huku ripoti zikisema kuwa yuko katika hali mahututi, kutokana na majeraha aliyosababishiwa na baba yake mzazi Bw Banjo.

  Baba yake msichana huyo aliripotiwa polisi na kikundi cha kutetea haki za watoto, na Msemaji wa polisi wa jimbo la Lagos DSP Asijebotu amethibitisha madai hayo, akisema kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

  Kulingana na taarifa nchini Nigeria, wazazi wa msichana huyo kwa sasa wanashikiliwa na polisi katika jimbo la Lagos.

  Mkuu wa kikundi cha kutetea haki za watoto Comrade Ebenezer Omejalile, ambacho kilimshitaki baba huyo, ameiambia BBC kwamba Bw Banjo , anayefahamika kama Panel, "Aliyabana na kisha kuyachoma matiti ya binti yake ."

  "Baba wa msichana huyo alitumia jiwe la moto alilolifunga ndani ya nguo na kumchoma hadi alipohakikisha kuwa ameyaharibu kabisa matiti ya binti yake," alisema.

  Alisema pia kwamba baba huyo alielezea kutoridhishwa kwake na jinsi binti yake alivyokuwa ameanza kuonyesha dalili za saratani ya matiti kwenye matiti yake, na ndio maana alitaka kuyazuia yasiote.

  Mama yake msichana huyo alisema kuwa Bw Banjo amekuwa akimpiga binti yake mara kwa mara.

  Comrade Ebenezer alisema kuwa alimwambia baba yake msichana huyo kuwa alifanya uhalifu.

  La kusahangaza zaidi ni kwamba, kulingana na Comrade Ebenerzer, ni jinsi baba huyo alivyosema amekuwa kimuogesha binti yake wa miaka 8 kila siku.

  Mila na utamaduni: Tanzania wanakozikwa watu wakiwa wameketi hadi Cameroon wanakopiga matiti pasi angalia tamaduni za kiajabu Afrika

 14. Mwanaspoti wa Burkina Fasso aliyevunja rekodi ya dunia ya unyanyuaji uzani apokelewa kama shujaa

  Iron Biby (pictured) cartwheeled after his historic lift

  Mwanaspoti wa Burkina Faso aliyevunja rekodi ya unyanyuaji uzani siku ya Jumamosi amepokelewa kama shujaa katika uwanja wa ndege Ouagadougou siku ya Jumatatau,kulinngana na kituo cha Radio ya Ufaransa RFI.

  Cheick Ahmed al-Hassan Sanou - maarufu Iron Biby - alinyanyua mbao ya uzani wa kilo 229 juu ya kichwa chake katika fainali ya the Giants Live World Tour huko Scotland na kuvunja rekodi ya zamani ya ya dunia ya kilo 228.

  Iron Biby aliyekuwa na tabasamu alipokea kombe hilo kwa heshma ya Burkina Faso, na kunukuliwa na RFI akisema ushindi wake unatuma ujumbe wa matumaini.

  “Ni kitu kikubwa kwangu, kwa sababu tangu mwaka 2018 nimekuwa nikijaribu kuvunja rekodi ya dunia.”

  RFI pia imeripoti matamshi sawia na hayo kutoka kwa Waziri wa michezo Dominique Nana.

  "Bendera ya Burkina Faso imeshinda.

 15. Gabby Petito: Mwili uliopatikana Wyoming ni wa mwanablogu wa 'van life' aliyetoweka

  Familia Gabby Petito iliripoti kupotea kwake Septemba 11
  Image caption: Familia Gabby Petito iliripoti kupotea kwake Septemba 11

  Shirika la upelelezi la Marekani(FBI) limethibitisha kwamba mwili uliopatikanandani ya mbuga ya Wyoming siku ya Jumapili ni wa mwanablogu wa "van life" Gabby Petito.

  Mtaalam aligundua mwanzoni kwamba kifo chake kilikuwa mauaji lakini hakutoa ishara ya jinsi alivyokufa.

  Bi. Petito, 22, alikuwa akizuru mbuga ya kitaifa ya Grand Teton akiwa na mchumba wake, Brian Laundrie, 23.

  Polisi kwa sasa wanamtafuta Bw.Laundrie, ambaye hajulikani aliko.

  Anachukuliwa kama "mshukiwa" katika kesi, lakini hajashtakiwa kwa uhalifu wowote.

  Hakuna maelezo kuhusu uchunguzi wa maiti yaliyotolewa.

  Familia ya Bi Petito iliripoti kupotea kwake siku 10 baadaye.

  Wiki kadhaa kabla ya hapo, polisi wa Utah mjini Moab walifahamishwa kuhusu uwezekano wa mzozo wa kinyumbani.

  Kanda za Bodycam ilimuonesha Bi Petito akilia na kulalamika kuhusu hali yake afya ya akili.

  Ripoti ya polisi baadaye ilisema Bw. Laundrie alidai Bi Petito alimpiga wakati wa mabishano.

  Hakuna mashtaka yaliyowasilishwa, na maafisa walipendekeza kwamba wenzi hao wasilalale mahali. Kilichofanyika baadaye hakikubainika.

 16. Raia Kenya na Ethiopia waliochanjwa miongoni mwa walioruhusiwa kuingia Uingereza

  Kenya yaondolewa kwenye orodha ya Uingereza ya vikwazo vya kusafiri
  Image caption: Kenya yaondolewa kwenye orodha ya Uingereza ya vikwazo vya kusafiri

  Nchi nane leo (Jumatano, Septemba 22) zimeondolewa kwenye orodha ya zile zilizopigwa marufuku kuingia Uingereza wakati serikali ya nchi hiyo inapoanza kutekeleza mabadiliko kwenye mfumo wake wenye utata wa usafiri kimataifa.

  Misri na Kenya ni nchi za Afrika ambazo sasa, zitakuwa na wasafiri wanaoruhusiwa kuingia Uingereza.

  Habari hii imepokelewa kama afueni kubwa nchini Kenya ambapo tasnia ya utalii imepata hasara kubwa kufuatia vizuizi vya usafiri kama njia moja ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.

  Uingereza ni ya nne yenye mchango mkubwa zaidi kwa watalii wanaotembelea nchi ya Kenya iliyopo Afrika Mashariki ambayo kwa sasa hivi iko katikati ya msimu wake wa kilele cha utalii ambao unamalizika na uhamiaji wa nyumbu kila mwaka.

  Furaha ya kukaribisha zaidi ya watalii 100 waliowasili katika uwanja wa ndege wa Mombasa, pwani ya Kenya, zimeshuhudiwa kwa mbwembwe na taadhima kuu.

  Wageni waliowasili wakiwa ni kutoka Romania – watalii wapya katika soko hilo nchini Kenya.

  "Tuna furaha kubwa sana kuwa hapa, na tutafurahia ujio wetu kabisa. Ni mara yetu ya kwanza. Watu waje kutembelea, wafurahie," mmoja wa watalii alisema.

  Idadi ya watalii nchini humo imepungua kwa zaidi ya theluthi mbili kutokana na janga la virusi vya corona na katika juhudi za kufufua sekta hiyo kwa hali na mali, sasa imegeukiwa soko la watalii kutoka Asia na Mashariki mwa Ulaya.

  Hata hivyo, watalii hawa wapya wanaokuja ni sehemu ndogo tu ya kile Kenya ilizoea kabla ya janga hilo.

  Sekta hiyo hadi sasa imepoteza mapato ya dola bilioni moja na nusu huku ajira milioni mbili zikitoweka - takwimu ambazo Waziri wa Utalii Najib Balala anasema zitachukua miaka kuimarika.

  "Idadi bado ni ndogo, lakini tumeona polepolea watalii wameanza kujiwekea nafasi zao za kuzuru Kenya majira ya joto. Haifurahishi lakini angalau ni ishara ya nia njema na kuonesha kwamba maisha yanarudi kama kawaida katika utalii, " amesema Waziri wa Utalii Najib Balala.

  Je dhana potofu kwamba chanjo ya corona ina sumaku ilitoka wapi?

 17. Samuel Eto atangaza kugombea urais wa shirikisho la soka Cameroon.

  Samuel Eto'o
  Image caption: Samuel Eto'o alifunga magoli 56 katika michuano 118 kama mchezaji wa Cameroon

  Nyota wa mpira wa soka nchini Cameroon Samuel Eto atangaza kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon.

  Tangazo hilo limetolewa Jumanne katika ukurasa wake rasmi wa Facebook.

  "Nimeamua kuchukua uamuzi huu kwasababu ya kuipenda Cameroon na kupenda soka yetu", alielezea Samuel Eto katika taarifa yake.

  Aliandika pia, "ni wakati wa kujenga upya mpira wetu".

  Baada ya uvumi kadhaa, Eto ameamua kuwa mgombea wakati kuna utata juu ya marufuku ya uraia mara mbili nchini Cameroon.

  Samuel Eto alikuwa raia wa Uhispania wakati alikuwa akichezea Uhispania.

  Miongoni mwa masharti yanayotakiwa kuwa mgombea wa urais wa shirikisho la mpira wa miguu la Cameroon, ni marufuku ya kuwa na utaifa wa kigeni.

  Samuel Eto ni kigogo wa tatu wa zamani kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon.

  Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa ugombea wake utathibitishwa.

  Uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 11.

  Pia unaweza kusoma:

  Eto’o apewa kazi ya ukufunzi Uturuki

 18. New York: Taliban yaomba kuzungumza katika Mkutano Mkuu wa UN

  Amir Khan Muttaqi
  Image caption: Waziri wa mambo ya nje wa Taliban Amir Khan Muttaqi alitoa ombi hilo kupitia barua kwa UN Jumatatu

  Taliban wameomba kuhutubia viongozi wa ulimwengu katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wiki hii katika Jiji la New York.

  Waziri wa mambo ya nje wa kundi hilo alitoa ombi hilo kwa barua Jumatatu.

  Kamati ya UN itatoa uamuzi juu ya ombi hilo.

  Taliban pia wamemteua msemaji wao wa Doha, Suhail Shaheen, kuwa balozi wa UN wa Afghanistan.

  Kundi hilo ambalo lilichukua udhibiti wa Afghanistan mwezi uliopita, lilisema mjumbe wa serikali iliyong’olewa madarakani haiwakilisha tena nchi hiyo.

  Ombi la kushiriki katika mjadala wa kiwango cha juu linazingatiwa na kamati ya utambulisho, ambayo wajumbe wake tisa ni pamoja na Marekani, China na Urusi, kulingana na msemaji wa UN.

  Lakini wana uwezekano wa kukutana kabla ya kumalizika kwa kikao cha Mkutano Mkuu Jumatatu ijayo.

  Hadi wakati huo, chini ya sheria za UN, Ghulam Isaczai atabaki kuwa balozi wa Afghanistan katika shirika hilo la ulimwengu.

  Anatarajiwa kutoa hotuba siku ya mwisho ya mkutano tarehe 27 Septemba.

  Hata hivyo, Taliban walisema ujumbe wake "hauwakilishi tena Afghanistan".

  Pia, walisema kwamba nchi kadhaa hazimtambui tena Rais wa zamani Ashraf Ghani kama kiongozi.

  Bwana Ghani aliondoka ghafla nchini Afghanistan wakati wanamgambo wa Taliban walipokuwa wakisonga mbele kuingia mji mkuu, Kabul, mnamo Agosti 15.

  Tangu wakati huo amekimbilia katika Falme za Kiarabu.

  Wakati Taliban inadhibiti Afghanistan mara ya mwisho, kati ya mwaka 1996 na 2001, balozi wa serikali waliyoipindua alibaki kama mwakilishi wa UN, baada ya kamati ya utambulisho kuahirisha uamuzi wake juu ya madai ya kushinikiza kupata nafasi hiyo.

  Katika mkutano wa UN Jumanne, Qatar iliwataka viongozi wa ulimwengu kuendelea kushirikiana na Taliban.

  "Kuwasusia kutasababisha tu ubaguzi na athari zaidi, wakati mazungumzo yanaweza kuzaa matunda," alisema mtawala wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani.

  Qatar imekuwa kiungo muhimu nchini Afghanistan.

  Iliandaa mazungumzo kati ya Taliban na Marekani ambayo yalimalizika kwa makubaliano ya mwaka 2020 ya kuondoa vikosi vya Nato vinavyoongozwa na Marekani.

  Soma zaidi:

  Vita vya Afghanistan:Je! Uhusiano wa Urusi utakuwaje baada ya Taliban kuchukua Afghanistan?

  Afghanistan: Fahamu kwanini Taliban inataka taifa hilo kuwa Emirati ya Kiislamu

  Mullah Abdul Ghani Baradar: Mfahamu kiongozi wa kundi la Taliban

 19. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hivi leo Jumatano tarehe 22 Septemba 2021